Mheshimiwa John Mnyika: What is Plan C

Wanapiga makasia kwa furaha na kasi kuelekea kule ambako maji yanaelekea,.... maskini hawajui ule unaoonekana kuwa wepesi wa makasia na kasi ya maji unatupeleka kwenye maporomoko ya maji ambako kuna mawe na miamba........
 
Naam mkuu ndio maana nikashauri kama tatizo ni hakuna mafuta na baadhi ya mitambo imezimwa.., basi inabidi hata tufahamu gharama ya kuendeshea mitambo hio kwa siku hata moja tu..!! na sisi wanajamiii na wananchi tuchangishe na kuendesha hio mitambo kwa siku moja kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha njia ya kufanya ambapo serikali itaona aibu na hata waheshimiwa wetu itabidi waone aibu kwa kula maposho wakati wananchi tunakopa ili tu, tupate mwanga hata wa siku moja

Mkuu wazo lako liko murua kabisa la at least wananchi kuchangia kwa siku moja kuendesha mitambo ile au kununua mafuta
Ila tatizo lililopo je viongozi wetu wana utashi huo wa kujua kuwa wananchi wanaangamia kwa kukosa nishati ya umeme au wanakisikia kilio cha wananchi wao waliowaweka madarakani kuhusu umeme au ni kile kilio cha samaki machozi yanaenda na maji.

Je viongozi wetu wana utashi kumaliza tatizo au ni kwamba washachukua 10% zao na wanaendeela na shughuli zao maana hawana shida ya umeme kwao?
 
ʞontɹact Sniper;2377613 said:
Wanapiga makasia kwa furaha na kasi kuelekea kule ambako maji yanaelekea,.... maskini hawajui ule unaoonekana kuwa wepesi wa makasia na kasi ya maji unatupeleka kwenye maporomoko ya maji ambako kuna mawe na miamba........

Sniper suluhisho hapa ni nini
Tuendelee kulalamika malalamiko ambayo hayafiki kokote au tuamke na kusema sasa enough is enough hapa tulipofikia panatosha tunahitaji mabadiliko na suluhisho la hapa tulipofika
 
Mkuu wazo lako liko murua kabisa la at least wananchi kuchangia kwa siku moja kuendesha mitambo ile au kununua mafuta
Ila tatizo lililopo je viongozi wetu wana utashi huo wa kujua kuwa wananchi wanaangamia kwa kukosa nishati ya umeme au wanakisikia kilio cha wananchi wao waliowaweka madarakani kuhusu umeme au ni kile kilio cha samaki machozi yanaenda na maji.

Je viongozi wetu wana utashi kumaliza tatizo au ni kwamba washachukua 10% zao na wanaendeela na shughuli zao maana hawana shida ya umeme kwao?

Ni kweli kabisa viongozi wetu hawajali kabisa...!! (ila kama kuna kitu wanachojali ni kuona kwamba huenda wasirudi madarakani baada ya miaka mitano ijayo)... Na viongozi hawa wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwamba hili tatizo haliwezi kupata solution kwamba ni mvua ndio imesababisha na hili ni jambo la kawaida...

Hivyo basi wananchi hata siku moja tukionyesha kwamba hawa jamaa ni wasanii itabidi waanze kufanya kazi yao ukizingatia kwamba nafasi zao zitakuwa mashakani...

Hivyo basi ni nani wa kutuongoza zaidi ya Waziri Kivuli wa hii Wizara!!!??
 
Sniper suluhisho hapa ni nini
Tuendelee kulalamika malalamiko ambayo hayafiki kokote au tuamke na kusema sasa enough is enough hapa tulipofikia panatosha tunahitaji mabadiliko na suluhisho la hapa tulipofika

Kelele zilizopigwa zimetosha sana, na sasa hivi zimezoeleka sana na kwa yote mpaka tulipofika, sasa hivi watanzania tunatabilika sana, ndiyo maana huoni dalili ya respond yeyote ile, I trust no Politician, iliyobaki kwa sasa tujipigania, tuna silaha za kutosha sana, nazo ni kama zifuatazo, vijana wasio na ajira, wananchi waliodhurumiwa (mambo mbalimbali) na sheria ikashindwa kuwapigania, watu wenye vinyongo, na wale ambao wanahisi mapambano haya yatawasidia, pamoja na wataalumu katika nyanja mbalimbali ambao wanauhisi uchungu huu wa watu kudhurumiwa bila ukomo.

Ni furaha yangu kama serikali yetu itabadilika na kuwa na sifa zifuatazo....yaani usikivu na uwajibikaji na kutovumilia uzembe, ufisadi wala kutokuwa na rafiki wa kudumu pale maslahi ta taifa yanapoingiliwa.
Ni sisi wenye jukumu la kuiweka madarakani serikali lakini bahati mbaya sana ni kuwa katika kutafuta fursa wenzetu wanakuwa na ajenda mbili, moja ya kuombea ridhaa, nyingine na kubwa kwa ni malengo yao binafsi.

Lakini kabla ya kutengeneza msimamo au kuchukua au kukubaliana kuchukua hatua stahiki dhidi ya serikali tujiulize kwanza ni kitu gani tumekifanya ambacho tunaweza tukatumia kama silaha na sababu ya kufanya maamuzi...Je binafsi tunawajibika ipaswavyo katika maeneo yetu? Je tu waadilifu kwa kiasi gani? Je dhamira zetu za kimapinduzi ni matokeo ya kimkumbo na kimakundi au ni dhamira za kweli na dhato toka katika mioyo yetu?
Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi
 
Hivi ni kweli maandamo ndio yatakayotuletea umeme....? (labda..) je kama yasipofanikiwa tutafanya nini..?, je ni kweli tutaandamana tena na tena na tena..?

Halafu kumbuka hawa jamaa ni wazee waku-spin mambo tukiandamana kudai maendeleo yetu wenyewe wanasema ni fujo ( na wapo watu wanaoamini uongo huo kwamba maandamano ni fujo)

Hivyo basi Je kweli hatuwezi kutumia njia nyingine ya attack japo kuonyesha kwamba tunapingana nao ila positively...?

Mfano mitambo yote iliyosimama kwa sababu ya kukosa mafuta wananchi kuchanga pesa na kuendesha mitambo hata kwa siku moja tu...!!! ili kuonyesha kwamba Tanzania bila giza inawezekana na viongozi wetu ni wasanii

Mkuu yaani bado unahimiza kuchangishana tena ...no please.Si kubaliani nawe hata kidogo,tunapaswa kuishinikiza serikali kutumia vizuri kodi wanazotunyonya kuhakikisha wanaboresha maisha yetu na si vinginevyo...tuchange!hiyo fedha tutaitoa wapi wajameni...Ebu tuamkae waTANZANIA tunaburuzwa mpaka fikra zetu bah.
 
ʞontɹact Sniper;2377821 said:

Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi
Ni kweli mkuu hii nchi ishapotea na the all system needs to change..., sababu hali ilivyo sasa hata akija malaika kuongoza nchi..., system ni corrupt kiasi ambacho hata yeye anaweza akabadilika na kuwa corrupt.

Lakini hata kabla hatujabadilisha system unakata kuniambia tuendelee na hili tatizo la umeme mpaka system itakapo kaa sawa..., na hizi biashara zetu zinazotegemea umeme tutazipeleka wapi au kuwa mgeni wa nani?

Kama watu kama 50 kila mmoja ananunua ka-generator kake mwenyewe huoni kwamba kuna uwezekano wa kuchanga na kununua kitu kikubwa ambacho kitasaidia hata watu 10,000 kwa gharama ambayo sio tofauti na gharama ambayo watu hawa 50 wanatumia..? (wakati huo tunangojea mvua... au so called system ibadilike) long term plans

My point is kipindi cha kutemegea serikali isiyotegemewa umekwisha inabidi sisi wenyewe wenye nchi yetu tujue cha kufanya
 
Ni kweli kabisa viongozi wetu hawajali kabisa...!! (ila kama kuna kitu wanachojali ni kuona kwamba huenda wasirudi madarakani baada ya miaka mitano ijayo)... Na viongozi hawa wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwamba hili tatizo haliwezi kupata solution kwamba ni mvua ndio imesababisha na hili ni jambo la kawaida...

Hivyo basi wananchi hata siku moja tukionyesha kwamba hawa jamaa ni wasanii itabidi waanze kufanya kazi yao ukizingatia kwamba nafasi zao zitakuwa mashakani...

Hivyo basi ni nani wa kutuongoza zaidi ya Waziri Kivuli wa hii Wizara!!!??

VOR sauti yako ni kama ya mtu aliaye jangwani na inahitaji support kubwa ya umma wa watanzania kuhakikisha kuwa inasikika na wanaielewa
Tumekuwa na viongozi ila naona ni viongozi jina wasiojua wajibu wao ni nini na wasiotekelez amipango yao au majukumu yao
Wamebaki nao ni walalamishi badala ya watendaji, hawaji na suluhisho la matatizo kwa waliowachagua ila wanakuja na matatizo tena kwa wananchi wao.

Tufikie sehemu ya kuwaondoa watu kama hawa madarakani na njia hii ndio itawapa hata wwale wengine watakaochukua madaraka hayo muamko wa kutatua matatizo yao.

Tuchukue mfumo wa Rwanda kama waziri anashindwa kudeliver aondoke ampishe mwenzake, Ifikie mahali cheo cha kuteuliwa kiwe ni cha kuteuliwa sio cha kuzaliwa nacho.

Kama unashindwa kutimiza kile ambacho umepewa dhamana kukifanya ondoka wapishe wengine.
 
Siku tukiacha kuwategemea wanasiasa kwa ajili ya solutions za matatizo yetu, Plan C itakuja automatically.

Until then tutaendelea kupigika
 
<br />
<br />
Mkuu yaani bado unahimiza kuchangishana tena ...no please.Si kubaliani nawe hata kidogo,tunapaswa kuishinikiza serikali kutumia vizuri kodi wanazotunyonya kuhakikisha wanaboresha maisha yetu na si vinginevyo...tuchange!hiyo fedha tutaitoa wapi wajameni...Ebu tuamkae waTANZANIA tunaburuzwa mpaka fikra zetu bah!

Mkuu sisemi kwamba wananchi ndio tubadilike kuwa Tanesco na kuendesha Tanesco...!!! , hapana mkuu bali ni kwamba hata tukiendesha kwa siku moja hii itakuwa symbolic, au wananchi tukichanga tukaleta hata mtambo wa kuzalisha 1MW hii itakuwa symbolic kwamba kama hata sisi masikini tunaweza iweje serikali yenye kodi zetu ishindwe..!!

Sababu kama ni kuishinikiza serikali tumefanya hivyo kwa muda wa miaka kama thelasini..!! au unamaanisha kwamba hii serikali haijawahi kulazimishwa?
 
&#670;ont&#633;act Sniper;2377821 said:
Kelele zilizopigwa zimetosha sana, na sasa hivi zimezoeleka sana na kwa yote mpaka tulipofika, sasa hivi watanzania tunatabilika sana, ndiyo maana huoni dalili ya respond yeyote ile, I trust no Politician, iliyobaki kwa sasa tujipigania, tuna silaha za kutosha sana, nazo ni kama zifuatazo, vijana wasio na ajira, wananchi waliodhurumiwa (mambo mbalimbali) na sheria ikashindwa kuwapigania, watu wenye vinyongo, na wale ambao wanahisi mapambano haya yatawasidia, pamoja na wataalumu katika nyanja mbalimbali ambao wanauhisi uchungu huu wa watu kudhurumiwa bila ukomo.

Ni furaha yangu kama serikali yetu itabadilika na kuwa na sifa zifuatazo....yaani usikivu na uwajibikaji na kutovumilia uzembe, ufisadi wala kutokuwa na rafiki wa kudumu pale maslahi ta taifa yanapoingiliwa.
Ni sisi wenye jukumu la kuiweka madarakani serikali lakini bahati mbaya sana ni kuwa katika kutafuta fursa wenzetu wanakuwa na ajenda mbili, moja ya kuombea ridhaa, nyingine na kubwa kwa ni malengo yao binafsi.

Lakini kabla ya kutengeneza msimamo au kuchukua au kukubaliana kuchukua hatua stahiki dhidi ya serikali tujiulize kwanza ni kitu gani tumekifanya ambacho tunaweza tukatumia kama silaha na sababu ya kufanya maamuzi...Je binafsi tunawajibika ipaswavyo katika maeneo yetu? Je tu waadilifu kwa kiasi gani? Je dhamira zetu za kimapinduzi ni matokeo ya kimkumbo na kimakundi au ni dhamira za kweli na dhato toka katika mioyo yetu?
Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi

Mkuu ukishakuwa na uongozi ambao ni legelege kuanzia juu hata huku chini huwezi pata afadhali yoyote. Kuna uozo mkubwa sana kweney kila sekta na sababu ni kuwa hakuna uwajibikaji kuanzia ngazi za juu mpaka mfagizi wa ofisi.

Ni wale wanaokuja wanasign kitabu cha mahudhurio na kwenda kwenye biashara zao na hili lipo karibu kila ofisi
Wananchi wakihamasishwa na wakiwa wanaona uwajibikaji kuanzia kwa watendaji wakubwa sidhani kama utaona kitu legelege na hili likifanyika mkuu sidhani kama kutakuwa na uzembe.

Mbona Rwanda wanaweza bana sisi tuna nini tushindwe
 
Siku tukiacha kuwategemea wanasiasa kwa ajili ya solutions za matatizo yetu, Plan C itakuja automatically.

Until then tutaendelea kupigika

Ni kweli usemayo lakini watanzania wanahitaji mtu wa kuwa-mobilize na kuwaonyesha ni nini cha ukweli na ni nini cha uongo..., kiongozi anahitajika kuwaongoza watu hata kama akiwa mwanaharakati..., sababu sasa ni wengi wamechoka lakini hawajui ni nini cha kufanya, na haki zao wanadhani ni favor
 
Nasikia Baada ya Wenje kuongea Bungeni umeme umerudi mwanza na hii ni baada ya kama siku 5...!!!!!

Sasa swali ni kwamba huu umeme umetoka wapi?, au mvua ya ghafla imenyesha Mtera
 
Mtumania cha ndugu hufa masikini. Tunaweka matumaini yetu yote kwa wanasiasa, hatuwezi kufika hata siku moja, kwa sababu tunabweteka na kusema Waziri Kivuli yupo atoe solution. Toa wewe mwananchi solution kisha mlazimishe Waziri kivuli na serikali waitekeleze.
 
Nasikia Baada ya Wenje kuongea Bungeni umeme umerudi mwanza na hii ni baada ya kama siku 5...!!!!!

Sasa swali ni kwamba huu umeme umetoka wapi?, au mvua ya ghafla imenyesha Mtera

Mkuu naamini kw anjia moja tuu ya kuingia barabarani na watu kufanya kile ambacho watu wanakiogopa sana kusema wazi kuw atumechoka na kunyanyasika katika nchi yetu haya mambo hayataenda sawa.
Tuwapate watu ambao wako tayari kufanya hilo na wanaokerwa na namna mambo yanavyoenda
 
Mkuu sisemi kwamba wananchi ndio tubadilike kuwa Tanesco na kuendesha Tanesco...!!! , hapana mkuu bali ni kwamba hata tukiendesha kwa siku moja hii itakuwa symbolic, au wananchi tukichanga tukaleta hata mtambo wa kuzalisha 1MW hii itakuwa symbolic kwamba kama hata sisi masikini tunaweza iweje serikali yenye kodi zetu ishindwe..!!

Sababu kama ni kuishinikiza serikali tumefanya hivyo kwa muda wa miaka kama thelasini..!! au unamaanisha kwamba hii serikali haijawahi kulazimishwa?

Sikumbuki kama serikali ilishawahi kushinikizwa huko nyuma,na kama iliwahifanywa hivyo ilikuwa so softly kiasi ambacho haijajifunza chochote.Watanzania tumejitolea sana,ndio maana viongozi wetu 'wanachukulia poa'...

Kufikiria kujitolea tena ni sawa na kuendeleza ukondoo na uzezeta wetu, strategy hii sio muafaka,muda wa kutumia maneno na maandishi tena haupaswi kuongezwa...INATOSHA SASA.kilicho muafaka ni kuunganisha nguvu zetu wanyonge na kuwashikisha adabu,kuwatoa kabisa madarakani,tuanze upya.
 
Mkuu ukishakuwa na uongozi ambao ni legelege kuanzia juu hata huku chini huwezi pata afadhali yoyote. Kuna uozo mkubwa sana kweney kila sekta na sababu ni kuwa hakuna uwajibikaji kuanzia ngazi za juu mpaka mfagizi wa ofisi. Ni wale wanaokuja wanasign kitabu cha mahudhurio na kwenda kwenye biashara zao na hili lipo karibu kila ofisi
Wananchi wakihamasishwa na wakiwa wanaona uwajibikaji kuanzia kwa watendaji wakubwa sidhani kama utaona kitu legelege na hili likifanyika mkuu sidhani kama kutakuwa na uzembe
Mbona Rwanda wanaweza bana sisi tuna nini tushindwe

Kwakweli kwa sasa hivi hatuna la kufanya, wala ushauri wa kutoa, Tangu December, tuliambiwa tatizo ni mvua, mvua iliponyesha na tatizo kuendelea tukaletewa suala lingine.
Hapa ukweli kuhusu chanzo cha tatizo ni wao wanaoujua, na sababu tunazopewa inaonekana si sahihi, hivyo kila tunavyojaribu kushauri kulingana na tulivyodanganywa kuhusu tatizo husika, tunakuwa tunajichoresha tu...(inatia hasira kuchoreshwa!).
Mpaka tutakapoujua ukweli na wao kuonyesha kweli kuhitaji ushari ndipo tunaweza kushari, kwasababu ushari wa wataalamu wa Tanesco kuna kumbukumbu zinaonyeshwa unapuuzwa na kutosikilizwa, halafu wanaigiza kuja mitaani kutaka ushari unadhani hapo tuna cha kushauri kweli? Kwa sasa tule tu kila mtu kwa urefu wa kamaba yake.
 
Mtumania cha ndugu hufa masikini. Tunaweka matumaini yetu yote kwa wanasiasa, hatuwezi kufika hata siku moja, kwa sababu tunabweteka na kusema Waziri Kivuli yupo atoe solution. Toa wewe mwananchi solution kisha mlazimishe Waziri kivuli na serikali waitekeleze.
Si umeona hapo juu pendekezo langu Gaijin.., alafu nikianza kulipigia debe hili suala nani ataendelea kulima haya majaruba ya mpunga (unajua tena classification and division of labor) (wapo watu ambao hii ndio kazi yao na posho wanakula)

Ndio maana nikasema mimi nipo tayari kutoa mchango wa hali na mali na kuwaomba wananchi wenzangu tujaribu hata kuonyesha kwamba inawezekena..., unajua tena sisi wananchi tumeshatoa mchango wetu sana wa kodi zetu ingawa tunaowapa kodi hawawezi kazi hivyo basi inabidi tuwaonyeshe na jinsi ya kufanya kazi yao
 
Kwa maoni yangu naona kuna hasara kubwa sana kwenye ukodishaji huu wa mitambo ya kufua umeme. Kama capacity charge inalipwa kwa siku bila kujali kama mtambo umewashwa au la; na kama jukumu la kununua mafuta ni la kwetu kwa maana ya kulipia in "advance" ili mtambo uzalishe tutaishia kulipa capacity charges bila kupata umeme.

Mimi nilitegemea kabisa badala ya Tanesco kukodisha hii mitambo, wangeingia kwenye mkataba wa "Hire Purchase" ambapo benk kama Stanbic wana hiyo product; hii ingefanya baada ya muda fulani mitambo iwe ya Tanesco badala ya Symbion na Aggreko.

Naamini kabisa Hire purchase payments + interest ingekuwa ndogo kuliko Capacity charges payments + purchase of electricity.
 
Back
Top Bottom