VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,355
Heshima Mbele Mkuu na Hongera kwa Kazi Nzuri....
Ni kweli kwamba nyie sio wakusanya Kodi lakini tulipofika tunahitaji msaada sababu kinachofanyika sasa hakifanyi kazi….
Plan A: Serikali, Waziri Ngereja na watu wake wameshindwa kazi kinachoendelea sasa ni usanii na watu hatupewi majibu yanayoeleweka
Plan B: Kuandamana mpaka kieleweke lakini sidhani kama hii itasaidia na je isiposaidia ni nini kitafuata…. what is Plan C:
Sababu watu waliotakiwa kufanya kazi yao wameshindwa tunaomba wewe Waziri kivuli tushauliane ni nini cha kufanya, na tuone kama sisi wananchi tunaweza kujinasua wenyewe katika hii laana ya kujitakia ambayo imepelekea uchumi kusimama...
Ni ukweli usiopingika kwamba sasa hali ni mbaya sana sehemu kama Mbeya, Arusha na Mwanza watu hawana umeme kwa takriban wiki sasa. Yaani umeme haurudi hata dakika moja watu wamebadilisha fridge kuwa kabati na kuvaa nguo ambayo haijanyoshwa imekuwa fashion.
Mwanza huwa wanapata mgao wa 42MW kutoka grid wakati sasa wanapewa 4MW… Sasa Je tatizo ni nini je ni mitambo au mafuta ndio hayapo na kama ni mafuta kwanini tunakodi mitambo ambayo itakuja kutumia mafuta hayo hayo na kama ni mvua iweje baada ya bajeti kupita ndio maji kuisha kabisa (yaani ule umeme tuliopata wakati bajeti haijapita ulitoka wapi..)
Pendekezo
Sababu Serikali imeshindwa Je sisi wananchi tunaweza kuchangia nini..?, Kama tatizo ni mafuta ni vema tukajua hayo mafuta gharama ni kiasi gani ili wananchi na wadau tuweze kujitolea (sababu ni more expensive kutumia generator ndogo ndogo kuliko generator kubwa za Tanesco ambazo ni more efficient). Mfano Nyakato Mwanza huwa kuna Generator sasa kama hizi hazijawashwa nina uhakika wafanya biashara wote watakuwa tayari kuona kwamba hizi zinawashwa hata kwa kuchangia gharama...
Kwa niaba ya wananchi wengine tunakuomba tuchangie mawazo ni kipi tunaweza kufanya ili kuondokana na huu usumbufu.., hata kwa kuonyesha mfano kwa kuondoa huu usumbufu hata kwa kusaidia mtaa mmoja au kuhakikisha inapita harambee ya kuchangia mafuta… (kama tatizo ni mafuta..) (nina uhakika hii italipa dividends come 2015)
Ninaomba mawazo yako mkuu wewe kama Waziri Kivuli na Mwana-Jamvi mwenzetu sababu hii emergency solution kama itafanikiwa December ambapo mvua zitaanza sioni kwanini ziitwe emergency kwangu mimi zinaonekana kama long term solution

Voiceofreason,
Nashukuru kwa maoni yako na ya wachangiaji wengine. Suala hili nitalitolea tamko rasmi. Hoja yako ilikuwa mwezi Agosti, wakati mpango wa dharura ndio ulikuwa kwenye hatua za awali za utekelezaji. Serikali ilihodhi usimamizi wa utekelezaji wa mpango husika na kiwango kikubwa iliachiwa Wizara ya Nishati na Madini. Nilitahadharisha kwamba kwa mfumo huo malengo yaliyotajwa bungeni hayatatimia kwa wakati. Sasa tuko mwezi Oktoba na malengo ya mwezi Septemba ya mpango wa dharura sehemu kubwa hayajafikiwa; tunapoelekea sio kuzuri kama hatutakuwa na Plan C kuanzia mwezi wa Oktoba/Novemba. Tuendelee kujadili na kuchukua hatua za haraka
JJ