Mheshimiwa JOHN MNYIKA atoa ufumbuzi wa tatizo la MAJI eneo la KIMARA hadi UBUNGO

Wakuu kwa swala la maji jimbo la ubungo huyu dogo mnamuonea. Anapambana kweli kweli ukizingatia na ukiritimba wa idara za maji na zile za serikali. juzi nilimuona kwenye baragumu ya channel ten na alizunguumzia swala hili la baadhi ya watu ku collude na watumishi wa DAWASA na kujiunganishia maji ili wauze kwenye malori na wananchi wengine wasipate maji ya bomba. Kwa kuwa hii biashara ni syndicate ya watu wengi, hutegemei suluhisho lipatikane kwa siku moja. kwa ufupi huu mchakato ni mrefu ila nilimsikia na jamaa wa wizara alipopigiwa simu alikiri tatizo hilo na akasema now wanashughulikia mawazo ya Mnyika na EWURA wameanza process ya kuwadhibiti hawa wauza maji kwa bei za kujipangia.
Tuache unafiki, Mnyika is realy serious na maji ya jimbo la ubungo.
 
Jk alitoa ahadi zaidi ya 50 katika uchaguzi uliopita but hilo wana nchi tumelisahau lakin kumkomalia Mnyika kama yeye ni BOT,hela zinatoka hazina sio kwa mbunge kama tunavyo jua yeye ni msimamizi tu sio mtoaji wa fund,hata nyie mnao pinga humu mkipewa huo wadhifa hamuwezi fanya aliyo fanya Mnyika,me naamin huyu ni kiongozi imara na anaye weza kongoza tatizo la maji sio kimara tu ni nchi nzima msiutumie upinzani wa Mnyika kama defending pointi yenu.
 
Huyu Mnyika amezidi uchochezi, ndio maana DAWASA wakamlakamikia. Haiwezekani ukawa mbunge halafu kwenye wiki ya maadhimisho ya maji badala ya kuungana na viongozi wa serikali yeye anafanya uchochezi: JOHN MNYIKA: WIKI YA MADAI YA MAJI

Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao mlipata mamilioni ya fedha ka nia za posho katika kuadhimisha wiki ya maji. Kama watendaji katika sekta ya maji mlitakiwa katima madhimisho ya aina hii kila mwaka mantoa takwimu za watanzania wapya waliounganishwa katika mtandao wa maji safi. Kwa kuwa hilo halifanyiki ni dhahri kuwaManyia kama mwakilishi wa watu yuko sahihi kuwataka wananchi kudhimisha wiki hiyo kwa kutekeleza mikakati mbali mbali ya kudai haki ya msingi ya kupata maji safi.

Sehemu ya 2 ya Ibara ya 4 Sheria ya Maji namba 12 ya 2009 kinatamka bayana kuwa ni haki ya kila mtanzania kupata maji safi aidha kifungu hicho kinataka kila mtu mwenye mamalka ya kutekeleza sheria hii kuzingatia maudhui ya sera ya maji ya 2002 ambayo katika sehemu ya 3 HUDUMA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA MIJINI IBARA 3 (i) Maji safi na usafi wa mazingira ni muhimu kwa maendeleo na hivyo ni haki ya kila mwananchi kupatiwa huduma ya majisafi na uondoaji majitaka (vi) Wakazi wenye kipato kidogomijini watafikiriwa wakati wa kuweka mtandao wa kusambaza maji na kupanga bei za maji.

Ni kwa msingi huo wakati wenye mamalak ya kutekeleza sheria na sera za maji wakilipana posho kuadhimisha wiki ya maji wakati ambapo wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sera na sheria walizopitisha wenyewe ndio maana Mhe Mnyika anawataka wananchi nao kuadhimisha wiki hiyo kwa kudai haki zao za msingi kama ya kupata maji safi kwa mujibu wa sera na sheria zilizopo
 
Mnyika usiwe mwoga wanaofanya biashara ya maji unawajua TENA ni wanachama wa CDM; leo unawasingizia DAWASCO kuwa wanashirikiana nao!!! Huo ni uzushi; kuwa mkweli na UTHUBUTU wa kuwakanya akina Mangi kuvuruga miundo mbinu ya maji ili wauze maji
Kwa hiyo kama kuna waizi na ni wanachama wa CDM aitoe taarifa polisi......chadema siyo kama CCM kuwa kuna kulindana kwingi....wenye jukumu la kudhibiti ni DAWASCO siyo Mnyika wana wana CDM...
 
Huyu Mnyika amezidi uchochezi, ndio maana DAWASA wakamlakamikia. Haiwezekani ukawa mbunge halafu kwenye wiki ya maadhimisho ya maji badala ya kuungana na viongozi wa serikali yeye anafanya uchochezi: JOHN MNYIKA: WIKI YA MADAI YA MAJI

Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao mlipata mamilioni ya fedha ka nia za posho katika kuadhimisha wiki ya maji. Kama watendaji katika sekta ya maji mlitakiwa katima madhimisho ya aina hii kila mwaka mantoa takwimu za watanzania wapya waliounganishwa katika mtandao wa maji safi. Kwa kuwa hilo halifanyiki ni dhahri kuwaManyia kama mwakilishi wa watu yuko sahihi kuwataka wananchi kudhimisha wiki hiyo kwa kutekeleza mikakati mbali mbali ya kudai haki ya msingi ya kupata maji safi.

Sehemu ya 2 ya Ibara ya 4 Sheria ya Maji namba 12 ya 2009 kinatamka bayana kuwa ni haki ya kila mtanzania kupata maji safi aidha kifungu hicho kinataka kila mtu mwenye mamalka ya kutekeleza sheria hii kuzingatia maudhui ya sera ya maji ya 2002 ambayo katika sehemu ya 3 HUDUMA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA MIJINI IBARA 3 (i) Maji safi na usafi wa mazingira ni muhimu kwa maendeleo na hivyo ni haki ya kila mwananchi kupatiwa huduma ya majisafi na uondoaji majitaka (vi) Wakazi wenye kipato kidogomijini watafikiriwa wakati wa kuweka mtandao wa kusambaza maji na kupanga bei za maji.

Ni kwa msingi huo wakati wenye mamalak ya kutekeleza sheria na sera za maji wakilipana posho kuadhimisha wiki ya maji wakati ambapo wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sera na sheria walizopitisha wenyewe ndio maana Mhe Mnyika anawataka wananchi nao kuadhimisha wiki hiyo kwa kudai haki zao za msingi kama ya kupata maji safi kwa mujibu wa sera na sheria zilizopo
 
sisi tunaokaa huku ubungo maeneo ya mbezi luis tunaona jitihada za mbunge wetu, ingawa watendaji wachache wa ccm wanamwangusha lakini anajitahidi swala hilila maji. ukitaka kujua nenda kule nenda njia ya mpigi magoe, makabe mpka goba uwaulize, tumsaidie bilakumalumu
 
:nono: Mhe Mnyika aoneshwe mradi wa maji almaarufu kama maji ya Wachina amabo umegharimu fedha nyingi lakini maji hayakutoka. Utafiti ufanywe haraka na ufumbuzi upatikane.
 
usikate tamaa mnyika,tungeweka gamba hata lisingesema chochote,jipange tupiganie wananchi wako bwana.
 
usikate tamaa mnyika,tungeweka gamba hata lisingesema chochote,jipange tupiganie wananchi wako bwana.

viongozi wa serikali na chama tawala wengi wao mafisadi.Mashirika ya umma yanahujumiwa na watendaji waliowekwa na dola ya kifisadi.
 
kilichoelezwa na Mh. Mnyika ni kweli kabisa, huku kimara B kuna watu amboa laini zao ni za zamani sio za mchina wao maji yanatoka lakini hawa jamaa wanauza maji hayo na kupeleka hesabu kwa mabosi DAWASCO. Hivyo anachotakiwa ni kufumua huo mtandao wote.
 
pambana Mh! Mnyika tuko pamoja najua yoyote anayejaribu kupinga juhudi zako ni yule ama ni mmja wa magamba au amebahatika kutoa mawazo JF lakini uwezo wake wa kufikiria ni mdogo kwa huyu tutamwelimisha lakini kwa Gamba endelea siku inakuja!
 
Ndugu zangu, tuwe makini kujadili hoja! Hiki ni kibaraza cha Great Thinkers wanaoibua hoja ili ziwe stormed na kupatiwa majibu hapahapa na walengwa iwapo wameguswa nazo, mfano wa hoja hii inayomhusu mbunge wangu Mnyika.
Mbunge wangu Mnyika kitachokukwamisha usipate kura za kutosha uchaguzi ujao ni suala la MAJI na miundo mbinu(madaraja ya Golani na Bonyokwa).
Wiki iliyopita ulituhutubia wananchi pale Kimara mwisho, mimi nlikuwepo na nlikusikiliza vzr sana. Ulijieleza na kutoa ufanunuzi ambao ulikuwa ni wa kisiasa sana, baada ya kumaliza kikao muongoza mkutano wako alikusihi uende ukanywe kahawa na wakeretwa wa CDM kijiweni Kimara, baada ya kunywa kumaliza kunywa kahawa yako kama unakumbuka nlikufuata na kukueleza tatizo la maji kwa baadhi ya maeneo ambayo hayapati kabsa hata hayo maji ya mgawo kwa miezi minne mpaka sasa.
Nilikueleza kuwa eneo la SHULE YA MSINGI MAVURUNZA lilipo kimara matingini halipati maji kwa miezi minne sasa, nikiwa na maana hata maji ya mgawo wa wiki hakuna kabsa
Nikakueleza pia eneo lote lililo kaaribu na SHULE YA MSINGI SARANGA halina maji miaka yote
Ukanieleza nimuone diwani kwa tatizo la maji maeneo a karibu na shule ya msingi kimara, nikakujibu wananchi wa eneo hilo wamemuona diwani hakuna kilichofanyika
Ulinijibu kuwa tatizo hili lingekuwa limetatuliwa baada ya siku mbili, unfortunately wakazi wa eneo hili bado wana-suffer!
SARANGA ndo kabsa, hawajui na wala hawaoni support yako kuhusu maji,
Mnyika uelewe kuwa ulichaguliwa ili tusaidiane kumaliza matizo hayo na si kwa kwa sababu ya chama chako!
Nasikitika ahadi zako hazitelezwi kwa mfano hoja nliyoileta mbele yako na tukaongea ana kwa ana, hii inanipa shida kukuamini mbunge wangu kwa kuwa ni ahadi nyingi sana uliahidi kabla ya uchaguzi mfano suala la uchimbaji wa visima kata yetu ya kimara, hili ulisema lingekuwa kipau mbele cha kwanza, sasa ni mwaka wa tatu oolaa!
Nataka nikuambie hivi watu kimara wanachotaka ni MAJI sio SIASA, tunaiheshimu CDM na sera zake,
plz Mnyika tekeleza ahadi zako!
Wanajamvi wote na wadau wote mliokaribu naye huyu mbunge nawaombeni mshirikisheni Mnyika ujumbe huu, cna access na cmu yake, mlio na cmu yake mwambieni achungulie humu JF mana hiki ni kibaraza cha mgongano wa mawazo unaojenga kama huu.
Plz Myika tutakutosa ikiwa utaendelea na siasa za majukwaani zisizotelezeka! since huwa unachungulia humu ndani ni mategemeo yangu utatekeleza
 
Ufumbuzi gani sasa katoa? MNYIKA hakubaliki tena, na uchaguzi wa vijibweni umedhihirisha hilo ambapo yeye alikuwa kamanda. Sisi matatizo ya maji tunayajua na hatutaki story. Wananchi wanataka maji yatoke kwenye pipe zao sio POROJO.
 
Kwa mpango huu, jamaa yangu Mnyika inabidi ukaze buti maana lile jimbo ni kubwa na linamiundombinu hafifu. Nadhani wabunge waliopita wamelihujumu sana kiasi ya kwamba hata kuliweka sawa inachukua muda mrefu. Cha muhimu kama kiongozi inabidi uweke pilot areas zinazohitaji immediate action. Wewe ni msomi mzuri, waweza kuandaa harambee kwa ajili ya mradi utakaousimamia wewe. Usitegemee DAWASCO kumaliza hili tatizo, wapiga kura wako wanategemea ulete mabadiliko japo kidogo maana ni kweli jimbo lina changamoto nyingi sana. All the best brother in your leadership.
 
Michango iliyotolewa ni mizuri, ila sina uhakika kama Mhe Mnyika anafuatilia michango hii. kama ndiyo, ni vema akafanya majumuisho na kueleza hatua atakazochukua.
 
Jamani hili siyo swala la kisiasa, Maji ni uhai. wiki ya maji wakati maji hakuna, mimi nisingetengemea Mh. Mnyika akasupport hilo. Nani isiyejua ukubwa wa tatizo la maji siyo kwa Ubungo, siyo kwa Dar es Salaam tu bali nchi nzima. Kama kiongozi uliyemchangua hatashughulikia kero zako, unamtengemea afanyenini, asubiri kwenda kusinzia bungeni. Hiyo siyo sawa!!!
Kwenye maswala ya msingi yanayowahusu wananchi na maisha yao ya kilasiku ni lazima tushirikiane kuyatatua. Kama tunawapata viongozi walio na uthubutu wa kuyavalia njunga basi tuwaunge mkono, wala haifai kuwabeza, wala haifai kuwaonea wivu kwa kuwa watakuwa maarufu.
Keep it up Mh. Mnyika.:smile-big:
 
Back
Top Bottom