Mhemiwa Zambi on Maghembe's neck

Hongera sana Mh Zambi. Soko la kahawa limesheheni sana SIASA ambayo si hasa. Watu wa kaskazini wameitawala TCB miaka nenda miaka rudi kama vile wao ni wakulima stadi wa kahawa pekee. ndo maana wana Kagera wanaona heri kuuza kahawa yao Uganda pamoja na kupata kipato zaidi Uganda.

Kahawa ni zao dada na Pamba katika kuingiza hela za kigeni nchi hii - Pinda aache porojo zake alishughulikie suala hili bila kupepesa macho.

Viva Zambi.

waziri mkuu japo mtoto wa mkulima ni nyoka wa kibisa hana jipya , jmabo hili analifahamu kwa kina , je kama halijifahamu uslama wa taifa inafanya kazi gani kuhujumu uchumi wetu?

Pia mwaka jana mtoto wa mkulima alikwenda mwanza akatangaza bei ya juu ya 1,200/= kilo , baadaye magembe akaenda hukohuko na kutangaza kuiteremsha ikaw chini kwa T.shs.300/= ;wala mtoto wa mkulima hakufanya lolote japokuwa kulizusha malalamiko mengi kutoka kwa wakulima.

Pia magembe amekuwa akituhumiwa kuwakigia kifua matendaji wakuu wa bodi ya pamba huku wilifu wakifanya ubadhirifu mbalimbali.xaxa kama mtoto wa mkulima kitengo cha usalama wa taifa kikuu cha kuhusu masuala ya uchumi na viongozi, mbona kipo kwake , maake hajui hata hili?maghembe kuna kitu anakula na wakubwa hawa.
 
Bei za mazao ya biashara zinatawaliwa na soko la dunia, zinaweza kupanda au kushuka. We ulitaka bei zikishuka katika soko la dunia eti kwa vile waziri mkuu ameshatangaza bei, bei ya Tanzania ibaki hapo hapo. Ukiona Waziri Mkuu alikaa kimya uelewe wazi aliridhika na maelezo aliyopewa na washauri wake wakiwemo usalama wa Taifa.
 
Makah kwa haraka haraka ningependa kukushauri ufuatilie historia ndipo utoe maoni badala ya kushabikia kitu usichokijua au pia yawezekana unakijua.Kama ulisoma makala aliyoiandika Bw King cobra kama sijakosea kwenye jukwaa la habari mchanganyiko ameelezea vizuri tu swala hili la Cherry kule Mbozi na watu na masilahi yao.

Kwanza napenda kukueleza kuwa anachopigania Bw Zambi ni masilahi yake kibiashara na sio kitu kingine na pia uelewe sio yeye Zambi anaeongelea hili peke yake ni anamwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Bw Adolph Kumburu amabye ana masilahi yake pia binafsi kwenye zao hili.

Kwa kifupi ni kwamba hawa bwana Zambi na rafiki yake Kumburu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa wakishirikiana na wazungu wao hawapo tayari kuwekeza kwenye biashara hii kama kufunga Mashine za kumenya kahawa mbichi ila wanachokitaka ni kukuta mkulima kesha umia wao wabebe kahawa ambayo mkulima kaumia nayo kwa bei poa tu na sio kitu kingine mkuu
Na pia wanachokiona ni kuwa wale waliofunga mashine za kumenya kahawa kwa sasa ndio wanaopata kahawa toka kwa wakulima kutokana na mashine walizofunga za kumenya kahawa hivyo ifikapo mwezi wa saba wale ambao hawana hizo mashine watakosa kahawa na huku wameshajicomit kwa wazungu wao.Pia fuatilia mijadala iliyopita utaelewa vizuri sana.
Unavyosema watu wa kasikazini wameitawala bodi sio kweli kwanza naomba ujue kuwa nchi hii haina ukabila na pili ukifuatilia bodi 2 zilizopita huko nyuma watu wa Magharibi ndio waliokuwa wanaitala bodi na sio watu wa kasikazini mkuu
Nakushauri uache ushabiki kwa kitu usichokijua.Kuanzia Balozi Mulokozi na hatimaye Ngeze omba list ya hizo bodi ndipo utakapoelewa unachokiongelea kama ni sahihi au la!
watu na masilahi yao aliyewekeza na kumsaidia mkulima kupata bei nzuri kutokana na kahawa kuwa nzuri ndio wanaopigwa vita waondoke turudi kwenye ujima stone age mkuu washauri wawekeze ili kumpa mkulima ushindani na sio kuwafukuza wale waliowekeza kwa kutumia vyeo vyao walivyo navyo mpaka kufikia kumpa Waziri Mkuu amri jiulize mara mbili mbili .

Unamsikia au umemsikia Prof Mwakyusa kuhusu Vibali kichaa maghembe alivyvitoa kwa makampuni kununua kahawa mbichi?????????? Tuwasaidie wakulima wetu wanyonge. mtu anaewekeza kwenye CPU akitegemea atalindwa na Waziri si mwekezaji ambae kafanya homework ya kutosha - assumptions zake zime misfire. Hajaiweka SWOT analysis yake vizuri.

Tuwe na huruma na tuwasaidie wakulima wetu. Soma ripoti lukuki za awali za Coffee Management Unit ya Wizara ya Kilimo na za Coffee and Stabex Management Unit upate sababu kwa nini wabunge Mwakyusa na Zambi wanawatetea wakulima hususan wadogo dogo.
 
kila kukicha katika mjadliano ya bajeti za mwaka huu kunaibuka mapya, lakini , haohao wa MAGAMBA, walipitisha kwa kishindo na kusema ni bajeti nzuriInasikitisha sana kuona mambo ya kitaalam yanafanywa kwa hisia za kisiasa, huku wakijineemesha kimasilahi.Na pia wakifumbiwa macho na wakubwa.
Mkuu tatizo lao wanaogopa hatima itakayo wapata wasipo pitisha bajeti ila wangekuwa serious bajeti za wizara zitakazo kuwa mbaya wasipishe
 
Unamsikia au umemsikia Prof Mwakyusa kuhusu Vibali kichaa maghembe alivyvitoa kwa makampuni kununua kahawa mbichi?????????? Tuwasaidie wakulima wetu wanyonge. mtu anaewekeza kwenye CPU akitegemea atalindwa na Waziri si mwekezaji ambae kafanya homework ya kutosha - assumptions zake zime misfire. Hajaiweka SWOT analysis yake vizuri.

Tuwe na huruma na tuwasaidie wakulima wetu. Soma ripoti lukuki za awali za Coffee Management Unit ya Wizara ya Kilimo na za Coffee and Stabex Management Unit upate sababu kwa nini wabunge Mwakyusa na Zambi wanawatetea wakulima hususan wadogo dogo.

Hata kama aliweka SWOT analysis yake vizuri hakuna ambaye angetarajia kuwa viongozi wa serikali wanaweza kuwa Threat kiasi cha kwenda kinyume na sera ya soko huria. Prof. Mwakyusa atakuwa ameingizwa mkenge na Mh. Zambi mpaka akadai kuwa wamefanya utafiti asilimia 94.4% ya wakulima wa kahawa kwenye jimbo lake hawataki kuuza kahawa mbivu. Kama ni hivyo tatizo liko wapi, si kahawa zao hawatawauzia hao wanunuzi au mh. Zambi amemdanganya kuwa wanunuzi wakishapata leseni wanalazimisha wakulima kuwauzia kahawa.

Kuhusu kuiba kahawa huu ni uhalifu wa kawaida kwani hata kama hakuna wanunuzi rasmi bado wezi hawakosi pa kuziuza, wenye vikundi mara kwa mara ndio wanunuzi.Kinachotakiwa ni vyombo vya dola kuwakamata. Aidha usimamizi wa sheria ya kahawa ni jukumu la Bodi ya Kahawa na katika kufanya hivyo inawatumia wakaguzi wa kahawa ambao kuteuliwa kwao kunashirikisha Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kuwasaidia wakulima sio kuzuia baadhi ya masoko bali ni kuwaelimisha faida za kila soko ili wao ndio wafanye maamuzi ya wapi pa kuuza kulingana hali halisi (to make informed decission). Endapo wakulima wameelimishwa tayari ila asilimia 5.6% bado inataka kuuza Red Cherry kwa nini hii asilimia tuinyime uhuru wa kuchagua mahala pa kuuza.
 
Back
Top Bottom