Mhemiwa Zambi on Maghembe's neck

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Kasema Maghembe kajiundia bodi ya kahawa ya nchi nzima yenye wanakilimanjao tupu, kaenda Mbeya wananchi wakagomea kanuni za manunuzi ya kahawa mbichi still akaja Dar fasta na kusaini kanuni zitumike. Kwa kifupi kasema ni ujeuri tu Maghembe hivyo kawaomba wabunge wazalendo wasipitishe bajeti ya waziri mkuu mpaka waziri mkuu atengue hizo kitu.

My take, kwa mwendo huu CCM itafika kweli 2015 maana moto wa Mpina bado jivu halijatoweka, huku Filikunjombe naye anataka change ya rada ipewe jina lake stahiki yaani CHANGE YA RUSHWA YA RADA au CHANGE ILIYOTOKANA NA RUSHWA YA RADA!
 
Hongera sana Mh Zambi. Soko la kahawa limesheheni sana SIASA ambayo si hasa. Watu wa kaskazini wameitawala TCB miaka nenda miaka rudi kama vile wao ni wakulima stadi wa kahawa pekee. ndo maana wana Kagera wanaona heri kuuza kahawa yao Uganda pamoja na kupata kipato zaidi Uganda.

Kahawa ni zao dada na Pamba katika kuingiza hela za kigeni nchi hii - Pinda aache porojo zake alishughulikie suala hili bila kupepesa macho.

Viva Zambi.
 
Hadi sasa sijaelewa ni kwanini rais Kikwete aliona Proj Maghembe anafaa kuendelea kuwa kwenye baraza la mawaziri? Huyu Prof aliharibu sana kilimo na sasa yuko wizara ya maji. Hana jipya hata kidogo.

Bodi ya kahawa kuna mambo hayako sawa. Mwenyekiti wa bodi ni Dr Hawa Sinare, huyu anatoka Rex Attorney ambao ni walikuwa wanatoa ushauri kwa Dowans! Balozi wa Tanzania Washington Mama Majaar ambae pia na undugu na huyu Dr Hawa nae alikuwa Rex Attorney! Inawezekana wawili hawa wana uwezo wa kufanya kazi lakini kunapokuwa na utata kwenye mambo wanayosimamia basi inazua maswali.

Lakini kwangu mimi swali muhimu ni hili, wajumbe wa hizi bodi wanapatikanaje? Wakubwa wanaangalia nini hasa?
 
ZITTO alipo pitisha karatasi ya kuto kuwa na imani PM akiwa na maana ya cabinet nzima, hakuunga mkono leo anajifanya anauchungu sana eti siungi mkono hoja hadi majibu yapatikane hiki ni kiini macho
 
Zambi anajaribu kujisafisha. Anafikiri watanzania hawajui alipofumaniwa na Kafulila akipokea rushwa.
 
Mnyonge, Mnyongeni; HAKI yake mpeni. The MP spoke his heart out! Na kasema anafanya vile kuisaidia serikali "SIKIVU" ya chama chake ili ijirekebishe!

Kwa wasiojua tu - Serikali SIKIVU ni dongo lililorushwa na Mh. Mbunge Viti Maalum CUF wakati akizungumzia madhila ya wananchi wa Rufiji.
 
mambo ya kusadikika ya rushwa yasituyumbishe tukatoka kwenye issue nzima ya wakulima wadogo dogo kuuza kahawa mbichi badala ya ile processed - CPUs zifanye kazi gani sasa baada ya kutumbukiza hela zote hizo.
 
Hongera sana Mh Zambi. Soko la kahawa limesheheni sana SIASA ambayo si hasa. Watu wa kaskazini wameitawala TCB miaka nenda miaka rudi kama vile wao ni wakulima stadi wa kahawa pekee. ndo maana wana Kagera wanaona heri kuuza kahawa yao Uganda pamoja na kupata kipato zaidi Uganda.

Kahawa ni zao dada na Pamba katika kuingiza hela za kigeni nchi hii - Pinda aache porojo zake alishughulikie suala hili bila kupepesa macho.

Viva Zambi.


Makah kwa haraka haraka ningependa kukushauri ufuatilie historia ndipo utoe maoni badala ya kushabikia kitu usichokijua au pia yawezekana unakijua.Kama ulisoma makala aliyoiandika Bw King cobra kama sijakosea kwenye jukwaa la habari mchanganyiko ameelezea vizuri tu swala hili la Cherry kule Mbozi na watu na masilahi yao.

Kwanza napenda kukueleza kuwa anachopigania Bw Zambi ni masilahi yake kibiashara na sio kitu kingine na pia uelewe sio yeye Zambi anaeongelea hili peke yake ni anamwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Bw Adolph Kumburu amabye ana masilahi yake pia binafsi kwenye zao hili.

Kwa kifupi ni kwamba hawa bwana Zambi na rafiki yake Kumburu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa wakishirikiana na wazungu wao hawapo tayari kuwekeza kwenye biashara hii kama kufunga Mashine za kumenya kahawa mbichi ila wanachokitaka ni kukuta mkulima kesha umia wao wabebe kahawa ambayo mkulima kaumia nayo kwa bei poa tu na sio kitu kingine mkuu
Na pia wanachokiona ni kuwa wale waliofunga mashine za kumenya kahawa kwa sasa ndio wanaopata kahawa toka kwa wakulima kutokana na mashine walizofunga za kumenya kahawa hivyo ifikapo mwezi wa saba wale ambao hawana hizo mashine watakosa kahawa na huku wameshajicomit kwa wazungu wao.Pia fuatilia mijadala iliyopita utaelewa vizuri sana.
Unavyosema watu wa kasikazini wameitawala bodi sio kweli kwanza naomba ujue kuwa nchi hii haina ukabila na pili ukifuatilia bodi 2 zilizopita huko nyuma watu wa Magharibi ndio waliokuwa wanaitala bodi na sio watu wa kasikazini mkuu
Nakushauri uache ushabiki kwa kitu usichokijua.Kuanzia Balozi Mulokozi na hatimaye Ngeze omba list ya hizo bodi ndipo utakapoelewa unachokiongelea kama ni sahihi au la!
watu na masilahi yao aliyewekeza na kumsaidia mkulima kupata bei nzuri kutokana na kahawa kuwa nzuri ndio wanaopigwa vita waondoke turudi kwenye ujima stone age mkuu washauri wawekeze ili kumpa mkulima ushindani na sio kuwafukuza wale waliowekeza kwa kutumia vyeo vyao walivyo navyo mpaka kufikia kumpa Waziri Mkuu amri jiulize mara mbili mbili .
 
Ninachopinga ni siasa katika zao hili muhimu. Mpeni Waziri mkuu na vyombo vyake wabaini ukweli uko wapi. hii ya kila mtu kumuweka mkulima mdogo dogo kama ngao katika vita hii inayoelekea kwenye siasa si sahihi. Bunge bado linaendelea na mjadala basi ajitokeze mwingine amkanushe Mh zambi kama kasema uongo.

Wakulima wadogo dogo kuuza kahawa mbichi kunaonyesha dhiki waliyonayo - tuanzie hapa kuwasaidia wauze kahawa ambayo ni processed na hivyo imeongezwa value kama kweli tuna uchungu nao.
 
FJM.Nafikiri Mkuu wa nchi na washauri wake wanajua wanalolifanya.Hata ingekuwa ni wewe una uwezo wa kufanya kazi na wakakuona ungepewa kazi kutokana na uwezo wako.Ila sijui kama niko sawa hapo yawzekana ni mmoja wao pia.
Hapa inaonekana huyu Mwenyekiti Dr Hawa Sinare alipoingia kwenye hii bodi kakuta kuna matatizo mengi sasa anapojaribu kufanya kazi aliyotumwa na Mh Raisi ya kurekebisha matatizo mahali inakuwa tatizo
Tukumbuke kuwa huko miaka ya nyuma hizi bodi zilikuwa zinawekwa wanasiasa wastaafu na wale wazee ambao walisha staafu na walikuwa kwenye ngazi za juu serikalini kwa sasa mabadiliko yanakuja na kuweka wafanya kazi wa kweli kweli ndio kelele zinaanza ilikuwa Mkurugenzi wa bodi yoyote anakuwa na nguvu sana hivyo akimwambia Mwenyekiti lolote yule mzee wa watu hana ubishi nae hivyo ulaji unaendelea tu.
Kwa ushauri wangu wa bure kabisa mshauri Bw Kumburu akubali matokeo na akapiganie ni kwa nini Bodi yake imefungiwa na Bodi ya PPRA soma gazeti la Mwananchi la Jumamosi uk wa 3 Bodi ya kahawa ni moja kati ya makampuni 36 yaliyofungiwa sasa anaacha kuhangaikia hilo lenye hatari kwake anahangaika na cherry kwa kumtumia Zambi Mp na pia ni sawa unavyosema kuna matatizo ni kweli kabisa na kwa sasa nimechunguza huyu Bw Kumburu yupo Dodoma kwa kampeni hizo
Mbona Mh Zambi hamuulizi Bw Kumburu anapeleka wapi fedha za wakulima anapowabadilishia kutoka kwenye dola kuwa shilingi hiyo tofauti anapeleka wapi ??? anampa mkulima au wanakula wao pale bodi na menejiment yake?.!
Kwa Mwenye kiti wa bodi kutoka Rex nafikiri hiyo sio issue hata angetoka sehemu nyingine na akawa strong katika kufuata KANUNI NA SHERIA angeonekana mbaya tu hapa issue ni anatakiwa mtu wa kupindisha sheria ndio hawa jamaa watamuona ana maana sana na waziri mkuu aliongelea vizuri tu alhamisi iliyopita katika kumjibu Mh Zambi lakini bado hakuelewa na analazima PM aende kinyume na sheria haiwezekani kamwe.

SWALI LA KUJIULIZA NI KWA NINI HAWATAKI KUSUBIRI KAMA WALIVYOAMBIWA NA PM KUWA SWALA HILO LINAFANYIWA KAZI NA WANASHERIA HIYO WASUBIRI ?? KUNA KITU HAPA TUFUNGUE MACHO ZAIDI TUONE MBELE
 
Ina maana Anachokifanya Mh Zambi ni mtoto/kijana wa kazi katumwa dukani halafu anaomba rist ya manunuzi ili akaonyeshe baba/tajiri yake kuhalalisha alichopewa ? kama ndivyo basi hehehehehehehehehehehehehehehe !
 
ukiona hawa jamaa wa ccm wakikomalia jambo ujue wana masilahi nalo. refer mkono na kiwira .
 
Mheshimiwa Zambi anaendelea kulazimisha jambo ambalo ameishajibiwa na Waziri Mkuu kuwa linafanyiwa kazi. Analazimisha kwa vile aliyemtuma Bw. Kumburu(Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Kahawa) anaona mwisho wake unakaribia. Hivyo kwa maslahi ya Kumburu yuko tayari amlazimishe Waziri Mkuu avunje katiba ya nchi kwa kutoa amri ya kusimamisha utekelezaji wa sheria. Mh. Zambi anatakiwa kujua kuwa kuna utaratibu wa kufuata kufikia maamuzi ya kutengua kanuni na kwamba hatutegemei ataishinikiza serikali ivunje hizo taratibu.

Wote tunajua kuwa kupambana kote huko kwa mh. Zambi ni kumlinda Kumburu kwa vile kwa mdomo wake tarehe 24.05.2012 mjini Morogoro katika Mkutano Mkuu wa Wadau alimuhakikishia Kumburu kuwa asiogope atamlinda. Anataka kumlinda muhalifu ambaye amethibitika kutenda makosa. Serikali imekuwa inashindwa kumchukulia hatua kwa vile alikuwa amenunua Bodi ya Wakurugenzi iliyopita chini ya Bw. Pius Ngeze. Bw. Ngeze alikuwa amemwakikishia ya kuwa asihofu chochote kwa vile kiutaratibu Wizara ya Kilimo hata ikimkuta ana makosa hawana ubavu wa kumwajibisha bila ya kuandikiwa kwanza barua na Bodi yake. Maneno haya Bw. Ngeze aliyasema katika kikao cha Wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Kahawa Moshi. Hii pengine ndiyo iliyopelekea serikali kuweka Bodi mpya kwa kutumia vigezo vya kuteua wajumbe wasiokuwa na njaa na au kuendekeza njaa ili wasijenunuliwa na Kumburu.

Hatua za kwanza zilizoanza kuchukuliwa na Bodi hii mpya zinatia matumaini kama, kuamuru wafanyakazi ambao Kumburu alitaka kuwafukuza bila ya kufuata taratibu warudishwe kazini. Pia kumtaka aite kikao cha wafanyakazi wote ili kuondoa migongano na kujenga timu itakayoleta ufanisi kazini. Kitendo cha kuamuamuru Kumburu awarudishe kazini wafanyakazi ambao wanatofautiana naye kimtazamo kuhusu uendeshaji wa shirika la umma kukidhi maslahi yake binafs hakukubaliani nacho. Hivyo ili kutotaka kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi, kwanza akatumia visingizio mbali mbali asiite kikao cha wafanyakazi, alipobanwa akaendelea kumtumia mh. Zambi alete vurugu ili serikali ifute Bodi ya Wakurugenzi. Matumaini yake ni kuwa Bodi ya Wakurugenzi ikishafutwa hata maamuzi yaliyotolewa na Bodi hiyo yawe batili aendelee kuliendesha shirika la umma bila ya kufuata misingi ya sheria.

Hivyo vurugu anazofanya mh. Zambi zinadhaminiwa na Kumburu mwenyewe na pengine zinafadhiliwa na maboss wanaomtumia Kumburu mathalani ecom,café Africa,Technoserve, armajaro,Hanns neumannn na Solidaridad ambao wameunda mtandao wa kudaka kahawa ya Tanzania chini ya mpango utakao sajili kahawa ya Tanzania kama utz kwa kutumia pesa za Bill & Melinda Gates Foundation. Mtandao huu unataka kutumia vikundi vya wakulima. Hii ndiyo maana Kumburu akajiingiza kwenye kikundi cha Songea Network Center ili mgao wake upitie huko. Ushahidi ni kwamba Kumburu mwenyewe alishapelekwa kutembelea makampuni hayo au baadhi ya makampuni hayo na Café Africa miaka kama miwili iliyopita. Hata miezi kama miwili iliyopita alienda ujerumani kwa kisingizio cha kufuatilia maonyesho lakini nia kubwa ilikuwa ni kukutana na Padre kiongozi wa Kikundi chake cha Songea Network Center na maboss wa ecom kukamilisha mikataba.

Ili mtandao huu ufanikiwe wanapigana kuua masoko mengine ili wakulima walazimike kuwauzia kahawa wao kwa wale wasiokuwa wanachama na wana shida ya kuuza kahawa kutatua shida za dharura. Hii inatokana na uzoefu walioupata Technoserve katika kuendesha miradi yao Kaskazini. Miradi hiyo ilishindwa ushindani ikabidi Technoserve iisimamishe huko kaskazini, wakazanie Kusini huku wakimtumia Kumburu aondoe ushindani Kusini. Wakishinda kuondoa ushindani kusini ndipo warudie huko kwingine.
Kutokana na hali hii ni wazi suala la wajumbe wengi kutoka kaskazini siyo hasa linalomsukuma mh. Zambi kupambana Bodi ya Wakurugenzi ivunjwe. Nia hasa ni kutaka kumlinda Kumburu ambaye anaona dhahiri hawezi tena kutumia nafasi yake kwa maslahi binafsi.

Mimi naishangaa serikali kwa kushindwa kumwajibisha Kumburu kwa kutenda makosa yenye ushahidi wa wazi kama kuendesha Bodi kwa kutumia mfumo ambao haujaidhinishwa na serikali, kukihuka sheria ya manunuzi hadi Bodi ya kahawa ikaadhibiwa na PPRA, upotevu wa pesa za kuchapia makaratasi ya usajili wa wakulima, kunyanyasa wafanyakazi n.k. Nimeambatanisha dossier inayoonyesha makosa ambayo Kumburu amekuwa akiyatenda tangia amekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa. Watu wanajiuliza hivi serikali inamwogopa nini kumwajibisha mara moja huku yeye anaendelea kuwachafua viongozi wake.
Hivi serikali ilipompa kazi haikum- vet. Kama alikuwa veted hawakupata historia ya tabia yake ya mapambano jinsi alivyovuruga Mbinga Coffee Curing akipambana na aliyekuwa Meneja wake Bw. Kasongo. Baada ya kuacha amewavuruga ndipo alikimbilia Technoserve. Wito ni kuwa safari hii asiachiwe akimbilie sehemu nyingine kwenda kufanya uharibifu, tunahitaka serikali imfikishe TAKUKURU na kisha mahakamani ili awajibike kwa yote aliyoyatenda.

Mwisho niseme, Waziri kulingana na sheria ya kahawa anamamlaka ya kuteua wajumbe wa Bodi peke yake. Mwenyekiti uteuliwa na Mh. Rais. Kati ya wajumbe 8 walioteuliwa na waziri, wajumbe wanne ndio wanatoka mkoa wa Kilimanjaro na hata hao wajumbe imetokea tu wakatoka Kilimanjaro kwa vile waliteuliwa kuwakilisha taasisi ikatokea wakawa wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, mathalani prof. James Terri anatoka Tacri(Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania), Bw. Ngimaryo antoka TCA(Tanzania Coffee Association) na biashara yake iko based Mbeya, Bw. Swai anatoka KNCU (Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro), Bw. Msuya anatoka serikalini ila anauzoefu wa kuongoza Bodi za Serikali. Na hii siyo mara ya kwanza kujikuta wajumbe wakatoka sehemu moja. Bodi zilizopita zilizonyingi wajumbe wake wengi walikuwa wanatoka mkoa wa Kagera. Mbona hatujawahi kusikia mh. Zambi akilalamika kuwa Mbinga yenye kahawa nyingi huko nyuma haikuwa na mwakilishi kwenye Bodi na sasa ina wawakilishi wawili.

Mh. Zambi kila mtu anaona wazi kuwa unazuia serikali isimwajibishe Kumburu.
 

Attachments

  • WARAKA+WA+WAFANYAKAZI+WA+BODI+YA+KAHAWA+TANZANIA%5B3%5D..doc
    110.5 KB · Views: 375
Nakubaliana na mtazamo kwamba kelele zote za mhe zambi ni kumlinda mhalifu kumburu kwani dg huyu yuko tcb kulinda maslahi yake binafsi na kambpuni za washirika wale technoserve na kilicafe;mwaka 2008 niliingia ktk biashara ya kahawa kwa stle ya kuaz kutumia kikundi,tokana na mtikisiko wa uchumi duniani kipindi kile na hatari iliyokuwepo ya kuporomoka kwa bei za zao la kahawa nilifunga safari tokia mbinga mpaka moshi tcb kuomba msaada kwa bwana kumburu ili aokoe kikundi cheti kwa kutupa mwogozo wa namna tutaweza kuuza kahawa bila kupata hasara atuahirisho mauzo mpaka msimu mwingine;nitaeleza kwa kirefu nini kilijiri kati yangu na bwana kumburu na anguko la kikudii cheti na kiini maccho cha vikundi anavyovitetea kwa maslahi yake bila kumsahau bwana zambi kwani nayeye alishiriki kusaidia uanzishwaji wa kikundi chetu.
Mkwara tu,hawezi zuia bajeti ya PMO kupita wakati ijumaa iliyopita aliunga mkono Bajeti ya Serikali!
 
Kasema Maghembe kajiundia bodi ya kahawa ya nchi nzima yenye wanakilimanjao tupu, kaenda Mbeya wananchi wakagomea kanuni za manunuzi ya kahawa mbichi still akaja Dar fasta na kusaini kanuni zitumike. Kwa kifupi kasema ni ujeuri tu Maghembe hivyo kawaomba wabunge wazalendo wasipitishe bajeti ya waziri mkuu mpaka waziri mkuu atengue hizo kitu.

My take, kwa mwendo huu CCM itafika kweli 2015 maana moto wa Mpina bado jivu halijatoweka, huku Filikunjombe naye anataka change ya rada ipewe jina lake stahiki yaani CHANGE YA RUSHWA YA RADA au CHANGE ILIYOTOKANA NA RUSHWA YA RADA!

Haaaahaaa! Hawa vijana siku hizi wameamua kupiga za usoni wazee wao!!
 
ZITTO alipo pitisha karatasi ya kuto kuwa na imani PM akiwa na maana ya cabinet nzima, hakuunga mkono leo anajifanya anauchungu sana eti siungi mkono hoja hadi majibu yapatikane hiki ni kiini macho

kila kukicha katika mjadliano ya bajeti za mwaka huu kunaibuka mapya, lakini , haohao wa MAGAMBA, walipitisha kwa kishindo na kusema ni bajeti nzuriInasikitisha sana kuona mambo ya kitaalam yanafanywa kwa hisia za kisiasa, huku wakijineemesha kimasilahi.Na pia wakifumbiwa macho na wakubwa.
 
Zambi ni jembe ila ile kashfa aliyoisema Kafulila ilimtia doa!


Zambi sio jembe wala koleo ni msanii tu mchumia tumbo ; kama angekuwa mzalendo angesaini karatasi ya Zitto kama wanaume wenzie walivyofanya!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom