Mhe. Rais: Vunja Baraza na Bunge!

Anaweza kuvunja Baraza sio BUNGE. Kuvunja BUNGE kuna taratibu zake ( Katiba ya Jamhuri 90(1) na (2a-e) toleo la 1977.
 
Safi sana ndugu yangu. Sina katiba hapa ila naomba uangalie kipengele kinachohusu nini kinaweza kutokea endapo Bunge litakataa kupitisha hoja ya serikali kama vile bajeti. Na labda kama kuna kipengele kinachogusia nini kifanyike endapo Rais atatofautiana na Bunge katika maamuzi mengine yaliyofanywa na Bunge!

Okay...nimekupata mh. Kifungu chenyewe hichi hapa:

90.-(1) Baada ya Uchaguzi Mkuu Rais ataitisha Mkutano wa
Bunge Jipya ufanyike kabla ya kupita siku saba tangu kutangazwa
matokeo ya huo Uchaguzi Mkuu katika majimbo ya uchaguzi yote
isipokuwa katika majimbo yale ambako uchaguzi umefutwa na
kufanywa upya.
(2) Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati
wowote, isipokuwa tu-

(a) kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake kwa
mujibu wa ibara ya 65 ya Katiba hii; au wakati wowote
katika miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai wa
Bunge, isipokuwa tu kama Spika amepokea taarifa
rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalum
ya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumuondoa Rais
madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba hii;
(b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti
iliyopendekezwa na Serikali;

(c) kama Bunge limekataa kupitisha Muswada wa sheria
kwa mujibu wa idara ya 97(4) ya Katiba hii;
(d) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya
msingi katika sera za Serikali, na Rais anaona
kwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteua
Waziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu;
(e) endapo, kutokana na uwiano wa uwakilishi wa Vyama
vya Siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba hakuna
uhalali kwa Serikali iliyopo kuendelea kuwapo, na wala
haiwezekani kuunda Serikali mpya.

(3) Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwa
kuwa limevunjwa; isipokuwa kwamba muda huo ukisha wakati
wowote ambapo Jamhuri ya Muungano iko katika vita Bunge
laweza mara kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibara
ya 65 ya Katiba hii kwa muda usiozidi miezi kumi na miwili mara
kwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi kuongezwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara ndogo kwa muda unaozidi miaka
mitano.
(4) Kukitokea hali ya hatari au kama kuna hali ya hatari
ambayo Rais anaona inasababisha kuitisha Mkutano wa Bunge na
iwapo wakati huo Bunge limevunjwa na matokeo ya kura zilizo
nyingi za Uchaguzi Mkuu hayajatangazwa basi Rais aweza kutoa
Taarifa Maalum ya kuitisha Mkutano wa Bunge na kuangiza
kwamba Spika na watu wote waliokuwa Wabunge mara tu kabla
Bunge halijavunjwa wahudhurie Mkutano huo wa Bunge na watu
hao pamoja na huyo Spika, watahesabiwa kuwa ndio Wajumbe
wa Bunge kwa madhumuni ya Mkutano huo na watahesabiwa
hivyo mpaka usiku wa manane wa siku yatakapotangazwa
matokeo ya kura zilizo nyingi za Uchaguzi Mkuu.


Ibara ya 97(4):
(4) Iwapo Muswada umerudishwa kwa Bunge na Rais, halafu
ukaungwa mkono kwenye Bunge na Wabunge ambao idadi yao
haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kama ilivyoelezwa
katika ibara ndogo ya (3) na kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya
kupata kibali chake kwa mara ya pili kabla haujamalizika muda wa
miezi sita tangu uliporudishwa, basi Rais atatakiwa kuukubali
Muswada huo kabla ya kumalizika muda wa siku ishirini na moja
tangu Muswada huo ulipowasilishwa kwake la sivyo basi itabidi
alivunje Bunge.


Hivyo kwa rais kuvunja Bunge sio kitu cha kuamka asubuhi na kufanya. Lazima kuwe kumetokea hitilafu kubwa ya kikatiba.

Lakini wazalendo si utani rais ana nguvu...itabidi na mimi nije kuwa rais. Ndo maana anakuwa fisadi na kutojali wananchi
. Kwa hiyo rais akitoka Chama A, na bunge likawa na majority ya Chama B, basi Rais anaweza kuvunja Bunge kwa madai kuwa hawezi kuunda serikali. Huo uchaguzi unaofuata ni utakuwa wa Wabunge pekee au hadi rais?

Opps...jibu nadhani ni hili, alafu hiyo itakuwa imekula kwa rais pia...hahahaha:
41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais.
 
Labda avunje baraza la mawaziri lakini bunge aache ili awe na nguvu kikatiba kuliunda upya. Lakini huo ubavu anao? Akishaanza kucheka cheka na kung'ata kucha kama ..m, thubutu!! avunje?
 
Mr. Mtoto,

Kwa ibala ulizo zitoa hapo juu na kwa maelezo yako yafuatayo

"Lakini wazalendo si utani rais ana nguvu...itabidi na mimi nije kuwa rais. Ndo maana anakuwa fisadi na kutojali wananchi. Kwa hiyo rais akitoka Chama A, na bunge likawa na majority ya Chama B, basi Rais anaweza kuvunja Bunge kwa madai kuwa hawezi kuunda serikali. Huo uchaguzi unaofuata ni utakuwa wa Wabunge pekee au hadi rais?"


Na ndio maana wengi hudai katiba ifanyiwe marekebisho maana ina walinda sana viongozi wengi walioko madarakani kwa kuipindisha katiba kwa maamuzi yao binafsi na manufaaa yao wao wenywe wayatakavyo.


 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.
Wabaya wa Muheshimiwa ni akina nani hao? Chochote kitakachofanyika kwa sasa katika vitu hivyo viwili ni kuwaongezea mzigo mwingine mzito walipa kodi wa tz.

kauchaguzi kanakuja mwakani; kwasasa ngoja tuvumilie hii shida! kama kweli yu makini, asituletee tena makapi kwenye uchaguzi ujao na baraza lijalo. na sisi wananganyika ndio waamuzi.
 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.
Mkuu wa shamba.
unamshauri Muungwana avunje baraza la mawaziri na Bunge??
kuvunja kabinet anaweza kwani kikatiba anaruhusiwa. ila mpaka alivunje bunge ni kasheshe kwani kikatiba bunge huvunjwa linapoigomea serikali kupitisha muswada wa bajeti.

Lakini hujakosea, nadhani ungesema BUNGE ligonge kura ya kukosa imani na muungwana ili livunjwe hatimaye tukajipange foleni kuchagua mafisadi wapya.

Ila amini nakuambia muungwana huyu atakusoma atacheka kisha huyoooo atawahi eapoti katika safari zake za kusaka rais mwenye mvuto
 
MM heshima mbele,

Wanajamiiforums.......hivi ni lazima kuendeleza mjadala wa thread isiyoeleweka? aua kwa vile kaleta mzee.

Chonde chonde mzee, kama kuna jipya la kutukerehesha lilete tu. Tumesazoea kushushwa sukari.
 
Mkuu MMKJ,

Heshima mbele, naomba leta huo muchere uliopata!! Otherwise your post does not make sense!! The fact is HAWEZI VUNJA BARAZA KWA SASA!!!!!:confused:
 
Mtoto,
Mkuu wangu wala sii kazi kubwa kabisa.. rais anaweza tumia kifungu cha E kama anavyojieleza yeye na ikakubalika kisheria. Sii lazima unachokiona wewe ndicho halali ya kuwezesha kifungu cha D au E..
Siku zote marais wanapovunja bunge huwa hawana sababu nje ya kile wanachokiona wao, vifungu hivi vinaweza kabisa kukubaliana na mtazamo waoa mabo sii lazima uwe sawa na hali halisi.
 
Sikujua kama Raisi anaweza kuvunja bunge,kama ni kweli hatuna demokrasi!
 
Akifanya hivi kwa hiari yake atakuwa anaongoza mkondo wa maji ya mafuriko; akisubiri mafuriko mengine ya Lowassa atalazimikawkuitafuta safina ya Nuhu
 
Akifanya hivi kwa hiari yake atakuwa anaongoza mkondo wa maji ya mafuriko; akisubiri mafuriko mengine ya Lowassa atalazimikawkuitafuta safina ya Nuhu

Mkuu unaweza ukatupa whats cooking?... Najua there must be some critical info behind this statement.
 
Mkuu unaweza ukatupa whats cooking?... Najua there must be some critical info behind this statement.

Pole sana ndugu yangu, naona jamaa ameamua kutoa dose yake taratibu. May be atatoa, tumpe muda!
 
Mr. Mtoto,

Kwa ibala ulizo zitoa hapo juu na kwa maelezo yako yafuatayo

"Lakini wazalendo si utani rais ana nguvu...itabidi na mimi nije kuwa rais. Ndo maana anakuwa fisadi na kutojali wananchi. Kwa hiyo rais akitoka Chama A, na bunge likawa na majority ya Chama B, basi Rais anaweza kuvunja Bunge kwa madai kuwa hawezi kuunda serikali. Huo uchaguzi unaofuata ni utakuwa wa Wabunge pekee au hadi rais?"


Na ndio maana wengi hudai katiba ifanyiwe marekebisho maana ina walinda sana viongozi wengi walioko madarakani kwa kuipindisha katiba kwa maamuzi yao binafsi na manufaaa yao wao wenywe wayatakavyo.



Mtoto,
Mkuu wangu wala sii kazi kubwa kabisa.. rais anaweza tumia kifungu cha E kama anavyojieleza yeye na ikakubalika kisheria. Sii lazima unachokiona wewe ndicho halali ya kuwezesha kifungu cha D au E..
Siku zote marais wanapovunja bunge huwa hawana sababu nje ya kile wanachokiona wao, vifungu hivi vinaweza kabisa kukubaliana na mtazamo waoa mabo sii lazima uwe sawa na hali halisi.

Waheshimiwa,

Unajua uzuri wa sheria ni mahakama zina nguvu ya ku-interpret maana ya maneno au vifungu vizima. Na hii inaipa sheria uhai, nikiwa na maana sheria inaweza kubadilika kuendana na nyakati. Hivyo, naamani kabisa, kama mahakama zitafanya kazi yake kifasihi, nguvu za rais katika Katiba zinaweza kuwa limited kutoka interpretation ya hiyo misamiati iliyotumika na sio lazima kukaa chini na kuandika mpya. Hata ikiandikwa mpya, kumbuka kuwa mahakama ndo msemaji wa mwisho. Na wao wataweza kuipa maana tofauti kabisa na jinsi mlivyotegemea. Kuna mifano mingi sana katika nchi zinazofuata mfumo wa Parliamentary Supremacy ambapo mahakama zimepindisha the obvious meaning ya kifungu kwa kusudi la kulinda Haki au ku-limit nguvu za watu. Hivyo kwa kusudi la kutambua hasa nguvu ya rais itabidi kwanza ishu iende mahakamani, tuone hawa Learned Brothers wanasemaje. Sina uhakika kama kuna kesi zozote juu ya vifungi hivi. Tungezipata ingekuwa fresh.
 
Mtoto,
Pengine mimi ndio sikuelewa kifungu cha sheria ulichoweka lakini inaposema hivi:- Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu- blaaa blaa blaaa!

Nimeelewa kwamba kama moja ya kifungu hicho ipo basi rais anaweza fanya hivyo WAKATI WOWOTE. Hili neno wakati wowote linabeba uzito mkubwa zaidi kuonyesha kwamba hakuna sababu wala kusubiri maamuzi ya mahakama. Sijaona kifungu kinachomtaka raios apeleke mashtaka au malalamiko yake kwanza mahakamani inapotokea au anapoona ulazima wa kuvunja bunge kutokana na vifungu hivyo.
Ndivyo nilivyoelewa mimi, na pengine ndivyo marais wengi huvunja bunge pasipo kusubiri mahakama..Ikiwa nimeelewa vibaya naomba somo mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom