Mhe. Opulukwa ashinda kesi dhidi ya pingamizi alokuwa amewekewa

Kwa hiyo wakuu mpaka sasa tumewapiga ngapi? Maana sasa hata hesabu nimeshapoteza ni 7-3 au 8?
 
Kimbunga,
Tunatambua kabisa hila zinazofanyika na chama na serikali yenu kuhakikisha mnapora haki ya wanaubungo kupitia mhimili unaoyumba wa mahakama kwa kuwatumia majaji wa vodafasta, baada ya kushindwa kuchakachua ndani ya sanduku la kura.
Tunatambua ni kwa kiasi gani mnapenda ushindi wa mezani, lakini tumejiandaa vizuri sana kukabiliana nanyi. Tunasubiri hukumu ya Ubungo kwa shauku kubwa sana, kwani tayari maluwe luwe yameshaanza.
Mwita Maranya huwa unanichekesha. Muktadha wa hiyo post ni kwamba CDM wameshangilia leo sijui na jana kwa Silinde hivyo wanapozwa na kuanza kukubali kwamba haki imetendeka. Baada ya muda tena wageuke kwamba haki haikutendeka.

Mkuu katika miongoni mwa wabunge wa CDM Mnyika ni mmoja wa ninaowakubali sana. Ni mbunge wangu na wala sitamani hata kidogo avuliwe ubunge. Mnyika ana hoja ambazo huwa zimetafitiwa kwa umakini mno. Juzi tu kwenye Kikao cha Bunge alitoa pendekezo moja juu kupinga na kurekebisha kauli ya Kamati ya Bunge kutoa uamuzi kwamba TPA ichukue mkopo sijui toka wapi na kazi apewe kampuni ya CCCC nikaona Kijana anazama sana. Aliunganisha mambo mengi toka pande mbalimbali na alitoa pendekezo zuri sana. Kwa sisi tunaojua, kwa pendekezo lile Mnyika aliwakata baadhi ya watu maini.

Namkubali Mnyika.
 
Feedback,
Kadri navyofahamu, kulikuwa na kesi ya kupinga ushindi wa Mh. Opulukwa. Lakini ripota anasema kesi dhidi ya pingamizi alilokuwa amewekewa.
Kwahiyo nilitaka anyooshe maelezo yake, ingawa nilikuwa nafahamu kwamba kwa taarifa hii Opulukwa atakuwa ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake wa kuwa mbunge.

Katika lugha ya kimahakama/kisheria, ukizungumzia kitu kinaitwa pingamizi unakuwa na tafsiri fulani.

anyway, all is well, tuendelee kuvuta subira kusikiliza kitakachotokea Ubungo, maana huko ndiko macho yote yameelekezwa.
Mwita Maranya

Ok umeeleweka ila naomba niweke sawa, tukiachana na content ya thread yenyewe ambayo maneno yake yanaeleweka 'CDM yatoka kidedea' hata heading yake haina utata, 'Mhe. Opulukwa ashinda kesi dhidi ya pingamizi alokuwa amewekewa' , angalia neno dhidi ya...., labda angesema ashinda kesi ya pingamizi... hapo ingeleta utata.
 
Au Mwita...ametekewa?
bdo nadhani uliisikiliza kwa makini hotuba ile ya Mkuu tarehe 30 Dec 2005 pale uwanja wa uhuru (Zamani taifa). Neno la kwanza kutamka kwa Watanzania baada ya kuapishwa alisema "Nimetekewa"
 
Hizi ni habari njema sana, ingawa bado nina maumivu ya hukumu ya kesi ya Jimbo la Segerea.
 
mwendo mdundo
wasiwasi kwa Mnyika magamba hayaaminiki
wakithubutu kumtoa wamekwisha kwani ndio watazidi kujitafutia kifo
but i trust mama msuya namwamini sana mtu wa haki na CV yake ni kubwa
 
sasa mnashangilia nini wakati majaji wanatekeleza agizo la kuhakikisha marudio ya Chaguzi yanapunguzwa kwa kadri iwezekanavyo. Hata Lema atarudishiwa ubunge wake. Uchaguzi utafanyika sumbawanga mjini tu basi
 
Bukutonaga kama sijakusoma vizuri.
Opulukwa ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake wa ubunge ama kesi dhidi ya pingamizi alilokuwa amewekewa, na kama ni pingamizi lipi hilo?na hiyo itamaanisha kwamba kesi haijaisha!?

Kaka utazeeka kabla ya wakati. Hivyo ndivyo viswahili vyetu. Msamehe bure. Opulukwa ameshinda kesi iliyofunguliwa kupinga ushindi wake wa ubunge.
 
cdm ikishinda haki imetendeka, ccm ikishinda judge kahongwa! Naomba msada hapa.:a s confused:

lazima iwe hivyo kwasababu kesi zote hizi ni za katibu mkuu wa zamani wa ccm yusuf makamba aliyetemeshwa wadhifa, na kama bado angekuwa yuko madarakani nadhani angehalibu zaidi, sababu akili yake ilianza kuota vinundu.
 
Haki imetendeka. Taraaatiuuu Ubungo inawekwa kwenye kilengeo.

Ubungo na Arusha hata asimame bubu asiyejua kuongea atawaburuza vibaya magamba....
sorry kama nimewanyanyapaa Mabubu, lakini ki ukweli CCM haina cha kujieleza mbele ya watanzania
 
Mwita Maranya huwa unanichekesha. Muktadha wa hiyo post ni kwamba CDM wameshangilia leo sijui na jana kwa Silinde hivyo wanapozwa na kuanza kukubali kwamba haki imetendeka. Baada ya muda tena wageuke kwamba haki haikutendeka.
Kimbunga

Kwa mahakama zetu zilivyo haki ikitendeka sehemu moja siyo guarantee kuwa lazima itendeke sehemu nyingine.
 
Mwita Maranya huwa unanichekesha. Muktadha wa hiyo post ni kwamba CDM wameshangilia leo sijui na jana kwa Silinde hivyo wanapozwa na kuanza kukubali kwamba haki imetendeka. Baada ya muda tena wageuke kwamba haki haikutendeka.

Mkuu katika miongoni mwa wabunge wa CDM Mnyika ni mmoja wa ninaowakubali sana. Ni mbunge wangu na wala sitamani hata kidogo avuliwe ubunge. Mnyika ana hoja ambazo huwa zimetafitiwa kwa umakini mno. Juzi tu kwenye Kikao cha Bunge alitoa pendekezo moja juu kupinga na kurekebisha kauli ya Kamati ya Bunge kutoa uamuzi kwamba TPA ichukue mkopo sijui toka wapi na kazi apewe kampuni ya CCCC nikaona Kijana anazama sana. Aliunganisha mambo mengi toka pande mbalimbali na alitoa pendekezo zuri sana. Kwa sisi tunaojua, kwa pendekezo lile Mnyika aliwakata baadhi ya watu maini.

Namkubali Mnyika.

Ha ha haa, Kimbunga wacha na mimi nicheke japo kidogo, kwamba huwa nakuchekesha? mimi nimeona comment yako nikajua tayari hukumu unayo mkononi, kama ile ya mahanga ilivyoelezewa kuwa mikononi mwa wanaccm wiki moja kabla haijasomwa mahakamani!!:glasses-nerdy:

Issue hapa sio chadema wameshinda jimbo gani, na ccm wanatakiwa kushinda jimbo lile ili kubalance. Kinachotakiwa hapa na ndicho kinachopiganiwa ni halki kuonekana ikitendeka, mahakama zetu zikiendelea kutumiwa na wanasiasa kiasi hiki ambacho watu wengi wanaupeo mkubwa wa kupambanua mambo itakuwa ni hatari kwa mahakama yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Afadhali huyu mpiganaji ameshinda kesi. Nafikiri alijipanga vizuri sana this time, as I can remember in 2005 alipata mizengwe sana lakini akarudi 2010. Inaonekana ni mpiganaji makini asiyerudi nyuma
 
Safiiiiiii Peoples Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrr leo ni bia kwa kwenda mbele mtu haniambii kitu hadi raha Magamba kwishaaaaaa na kile kizee chao Makamba kilichokuwa katibu Gamba wamepata aibu ya mwaka
 
Du hii imekaaje? Hapa hakuna kweli mkono wa ikulu kushinikiza hii hukumu?au haki ndiyo imetendeka?
 
jaji mdini anapendelea wakristo wenzie wa chadema

Kumbe magamba ni waislamu, mi nilikuwa sijui!!!!! Ukweli wa kitakwimu hakuna chama kinachoweza kujikita katika dini moja kitaweza kushinda katika nchi hii, labda muungano uvunjike na Zanzibar iwe nchi peke yake na vyama viwe vya milengo hiyo, hapo wakristu itakuwa imekula kwao!!!! Lakini kama TZ ni hii hii???!!! Udini hata kwa 'simple majority' tuliyonayo hautampa yeyote tija ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom