Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Lakini hiyo mikakati yenu ndiyo suluhisho la matatizo yanayolikabili taifa? Kwamba mkishaianika CDM gharama za maisha zitashuka, elimu itakuwa bora, ubadhirifu utaisha, malighafi za nchi zitalindwa, ajira zitapatikana?
Haya ndiyo mambo yaliyopo kwenye fikra za watu na si mashindano ya kuchafuana vyama kisiasa.

dah!kaka umetisha sana,maana huyu jamaa rejao mimi simuelewagi kabisa.eti tunapanga kuichafua chadema,hivi huyu jamaa anathink kweli?katika kipindi kigumu kama hiki ambacho nchi inapitia kama kuongezeka kwa deni la taifa,tatizo la ajira,mfumuko wa bei na mengineyo mengi bwana rejao wewe huoni hilo kua ni tatizo kwako tatizo ni chadema?we wa ovyo kabisa!SHAME ON YOU REJAO
 
Kikwete+na+Nimrod+Mkono+30+machi+2008+Butiama.jpg
 
mzee mzoefu kama huyu kufikia hatua hiyo! looo amejitahidi. yetu macho na masikio hapo kesho wa ukweli tumeawaona na wanafiki wa piga kelele kwa maonesho tumeshawaona. sasa tuone la kesho! dunia ina mambo watu wakikuchoka bwana kubali matokeo.
 
Mkono is nothing than a very smart guy. Kwa kutiani saini anajua kuwa jina lake litasafishika. lakini on the other hand anajua kuwa Magamba hawataafiki kupiga kura ya no confidence kwa Mtoto Fake wa Mkulima kwa maana wote ni Wachumia tumbo and they dont know what will be the next course of action.

As you can see, mmeshaanza kumuona Mkono shujaa while in fact ni one of Top Fisadiz. The guy knows mathematics.

Kilichopo hapa ni Kugangamaa na hoja na kama Bi Kiroboto akiizima, the next stage iwe ni Mkakati wa Kumwondoa yeye Bi. Kiroboto kwa kutumia Kanuni.

Nadhani unapoanza vita unakuwa na adui mmoja ili ushinde na Zitto analifahamu hilo. Kwa sasa mission yake ni kukusanya saini hata Pinda akitaka kusaini atampa asaini. Kumbuka hoja ikipita utahitaji kura zao wote ili kumtoa, ukianza kuwabagua sasa hivi utashindwa. Ukisha shinda ndio unaanza kufuatilia na maovu ya nyuma ya wale wale waliokusaidia kushinda.
 
Kazi ipo kweli kweli nadhani wengi sasa wameona namna mambo yanavyokwenda halijojo ndani ya serikali yetu
 
Mimi kwa kumbukumbu zangu finyu, Mkono ni mmoja wa watu waliofanya ufisaidi mkubwa nchini, hivyo kusaini ni kujikosha tu. yeye ni mmoja wao.
Let me ask you guys hivi ukishatenda kosa huwezi tena kutenda mema throughout your life?
 
lazima tutafakari mara kadhaa! tunachotaka hapa sasa si nani anafanya nini! ila uwingi wa kura una umuhimu mkubwa katika hili. hakuna anaye mkubali mkono hapa, ila kwa kitendo chake hicho, twaweza kumpa credit fulani.
 
Lakini huyu jamaa si naye yuko kwenye kundi la mafisadi wanaoinyonya nchi hii kupitia kampuni yake ya uwakili?
 
Na hivi ndiyo tuseme raisi wetu yeye anafanya kazi yake vizuri tu na hivyo bado tuna imani naye?

Or is the president beyond reproach?
 
Mjumbe wa NEC CCM na mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Nimrodi Mkono muda huu amesaini waraka ambao utapelekwa Bungeni kesho kuhusu kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu.

Huyu amekuwa Mbunge mwingine miongoni mwa wabunge wa CCM ambao wameamua kuusaini waraka huo kabla ya kuwasilishwa Bungeni kesho siku ya jumatatu.

Huyu ni mjumbe wa NEC ya CCM , tafsiri ya jambo hili nini maana yake .....

UPDATE:

Amesema kuwa yeye ni mbunge wa NEC (ya CCM) wa kuchaguliwa na wabunge na wabunge ndio wanalalamika hivyo hawezi kukaa kimya nchi ikiwa inapotea!
Haha ajab lakini kweli...hivi amesahau kampuni yake ilivokua inakomba pesa kutokana na kesi za serikali fees kwa mabiloni? kweli wajaabu sana sisi
ametajirika kutokana na nini? ameuza ngombe? ana shares bank m. maxinsure na marafiki zake ni wale EPA...KHAAA NAONA KINYAA
 
All of a sudden Mkono kageuka kuwa shujaa.
Kila mtu kasahau kama yuko kwenye "list of shame".

Lakini kwakua ana umuhimu wake kwa sasa,ngoja atumike tu.
Nitauliza siku za mbeleni kama kwenye list bado yupo au
katoka.

Sipati picha Lowasa na Chenge wakitia sign this night
wataitwaje.

Hata hao wakitia sign bado watakuwa kwenye kundi linalotaka uwajibikaji wa hii serikali, lakini tukirudi kwenye list bado wako.Hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Unajua mapaka sasa watu hawajaifahamu zaidi CDM. Wanaikurupukia tu. Tuna mikakati ya kuanika all about CDM. Stay tunned!
Mimi nilifikiri mna mikakati ya kujenga hospitali nyingi kumbe ni mikakati ya kuanika umbea. Kama hizo ndizo strategy za CCM basi kamwambie bosi wako Nape hiyo nayo ni sababu mojawapo kwa nini CCM inakimbiwa na wanachama wake.
 
Watanzania ni watu wa matukio sana baada ya hapo uwa wanayasahau yote.

Katika orodha ya Slaa aliyoitaja pale Mwembe Yanga Temeke Nimrod Mkono alikuwemo.

Leo baada ya kusaini amekuwa shujaa na kwenye kundi la ufisadi hayumo tena.

Hii ni ishu nyingine wala haihusiani.
 
hongera mzee kwa kusoma nyakati naomba mumweleewe watu wa ccm alisaini sio nkono ni wananchi wa MUSOMA VIJIJINI
 
Back
Top Bottom