Mhe. Mkapa Umejidhalilisha!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Ukiwa kama rais mstaafu na amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama unatakiwa kuwa mshauri mkuu na mlezi wa viongozi wa kisiasa wa vyama vyote bila ubaguzi. Unatakiwa kuwa encyclopedia kwa mambo yote muhimu ya kitaifa.

Kuendelea kushiriki kwako katika harakati za kisiasa kunakuondolea sifa ya kuwa kiongozi mstaafu! Kuendelea kutoa matusi na kejeli kwa vyama vya upinzani kama ulivyofanya Igunga na Arumeru Mashariki kumekuondelea heshima kwa jamii! Kuendelea kuwashambulia kwa kejeli wanasiasa binafsi kunaonyesha jinsi usivyo na busara! Kuendelea kujisifu na kujigamba namna ulivyotumia vibaya ikulu kujinufaisha na kuwaita watanzania wote kuwa ni wavivu wa kufikiri ni utovu wa fadhili na heshima uliyopewa na watanzania.

Nakushauri kaa chini na ujirudi kwa kuwaomba radhi Watanzania! Watanzania wana mioyo ya imani watakusamehe!
 
Huo ni ukweli kabisa ....before nilikuwa namheshimU BWM lakini kwa sasa heshima yangu kwa sasa nimeitoa kabisa
 
Ukiwa kama rais mstaafu na amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama unatakiwa kuwa mshauri mkuu na mlezi wa viongozi wa kisiasa wa vyama vyote bila ubaguzi. Unatakiwa kuwa encyclopedia kwa mambo yote muhimu ya kitaifa.

Kuendelea kushiriki kwako katika harakati za kisiasa kunakuondolea sifa ya kuwa kiongozi mstaafu! Kuendelea kutoa matusi na kejeli kwa vyama vya upinzani kama ulivyofanya Igunga na Arumeru Mashariki kumekuondelea heshima kwa jamii! Kuendelea kuwashambulia kwa kejeli wanasiasa binafsi kunaonyesha jinsi usivyo na busara! Kuendelea kujisifu na kujigamba namna ulivyotumia vibaya ikulu kujinufaisha na kuwaita watanzania wote kuwa ni wavivu wa kufikiri ni utovu wa fadhili na heshima uliyopewa na watanzania.

Nakushauri kaa chini na ujirudi kwa kuwaomba radhi Watanzania! Watanzania wana mioyo ya imani watakusamehe!

hana hadhi ya kuitwa Mheshimiwa.
 
Aibu ukubwani haifai!
Mtu mwenyewe tumbo kubwa vile, anajitafutia kashfa ya nini badala ya kuccheza wa wajukuu kwake?

Kama ni fadhila anazowapa CCM kwa kutomfungulia mashtaka kwa kutumia madaraka yake vibaya akiwa Ikulu, basi ajue kuwa mashtaka yapo palepale na yatafunguliwa baada ya CCM kuporomoka kutoka madarakani 2015!
 
Nasiki yu hoi toka jana usiku eti plesha inapanda plesha inashuka. Kisa boy wa mzungu kawa mbunge. k4c
 
Vita ya panzi karamu ya kunguru! wanapopoana wenyewe, nasi tuliokuwa underdogs tunaendelea kukomboa nchi
 
Binafsi namkubali sana huyu mzee kwa mambo mengi hasa uchumi na mipango ya maendeleo lkn zile kauli kweli ameni disappoint sana. Kwa heshima yake cdhani kama ilikuwa busara kudeal na personalities jukwaani badala ya kujikita kwenye sera na labda ku substantiate weakness za oponenents. Too low for him. Labda ndo mapungufu ya kibinaadam au alishauriwa vibaya na wachora ramani ya ushindi kuwa hiyo ndo approach sahihi kutokana na nature ya audience!. Tena huyu walitakiwa kumficha kama silaha yao ya mwisho 2015.
 
Kweli kajiharibia vibaya, asipojiangalia ataamsha hasira za watanzania wanaopenda afikishwe mahakamani kwa kufanya biashara akitumia vibaya nafasi ya kukaa ikulu.vinginevyo ajitathimini upya,atulie aendelee kula pension yake taratibu.mambo ya siasa za kuchafuana na kutukanana awachie akina lusinde ambao wanaichimbia ccm kabuli bila kujua.
 
aah huyu mzee kajishusha sana...

akome na mbio zake za sakafuni:bounce:
 
Wamelewa madaraka wanadhani Tanzania ni yao sasa watakiona cha moto, Mwenyezi Mungu ameamua kuingilia kati.
 
Hajakaa kimya, anacheka kimoyomoyo, yeye ndiye aliyemchomekea.
Kisa? BWM alimcheka JK alivyonangwa na EL kuhusu Richmond kwenye kikao kule Dodoma.

SS umesema kweli Jk kamfanya mbaya sana BWM. Kamam ulikuwa kichwani mwangu. Maana Mkapa ndiye aliyekuwa role model na hivyo watu walikuwa wakimnanga JK kuwa kwa nini usiwe kama Mkapa? Sasa hivi kamfanya aonekane wa hovyooooooooooooooooo kuliko hata Livingstone...........Lusindo!!!!! Kwa kiswahili tunasema "amemchomesha" jamaaa kamuuzia issue.
 
Misdhani kuwa BWM anapenda kufanya kampeni,issue ni kuwa analazimika since anapigwa bit kuwa usipoenda wapinzani watakapo chukua nchi ile issue yako ya kumiliki Kiwila watakusweka Lupango.
So whether apende au asipende lazima ajumuike na wana CCM wenzake ata kama ni kwa shingo upande
 
Ukiwa kama rais mstaafu na amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama unatakiwa kuwa mshauri mkuu na mlezi wa viongozi wa kisiasa wa vyama vyote bila ubaguzi. Unatakiwa kuwa encyclopedia kwa mambo yote muhimu ya kitaifa.

Kuendelea kushiriki kwako katika harakati za kisiasa kunakuondolea sifa ya kuwa kiongozi mstaafu! Kuendelea kutoa matusi na kejeli kwa vyama vya upinzani kama ulivyofanya Igunga na Arumeru Mashariki kumekuondelea heshima kwa jamii! Kuendelea kuwashambulia kwa kejeli wanasiasa binafsi kunaonyesha jinsi usivyo na busara! Kuendelea kujisifu na kujigamba namna ulivyotumia vibaya ikulu kujinufaisha na kuwaita watanzania wote kuwa ni wavivu wa kufikiri ni utovu wa fadhili na heshima uliyopewa na watanzania.

Nakushauri kaa chini na ujirudi kwa kuwaomba radhi Watanzania! Watanzania wana mioyo ya imani watakusamehe!

Kwa kiwango alichofikia Mzee Mkapa, hastahili kusamehewa wala kuheshimiwa.
  • Ana ubabe wa kifisadi
  • Ni mjeuri asiyekiri makosa
  • Mdhalimu na mbadhirifu
  • Ni nembo ya utawala mbaya na ndiye aliyewahi kufanya dhambi kuu ya ufisadi; kujimilikisha mgodi wa Kiwira
  • Hana moyo wa toba na ndio maana pamoja na madhambi yake yote na makosa (kumbuka dhambi na makosa ni vitu viwili tofauti) hajutii na anatukejeli
    • Makosa ni yale unayotenda kwa kukosea kwa bahati mbaya. Hukuwa na nia ya kuharibu, imetokea
    • Dhambi ni kujua jambo ni kosa na ukafanya kwa makusudi
Mkapa hafai kusamehewa maana hajaonyesha kutambua makosa yake na hataki kujutia dhambi zake
 
Back
Top Bottom