Lema sio tuu ni jembe, anaweza kuwa ni zaidi ya jembe, bali ni shoka kabisa au sime ya makali kuwili, asipodhibitiwa ndani ya chama chake, anaweza kuhamashisha maandamano ya wananchi wote, kuelekea Ikulu, kumng'oa rais halali, hivyo anaweza kutenda jinai ya uhaini kwa jina la siasa.
Sio siri, Lema ni hatari, hamungunyi maneno!.
We Pasco acha kutia aibu. Raisi halali gani ambaye hasimamii HAKI? Wewe huoni usambamba kati ya udhalimu wa CCM na ule wa Misri na Libya - ambapo hata kwa mfano serikali za Marekani na Uingereza zimekana kuwatambua Gaddafi na serikali yake, pale umma unapoamua? Hivyo serikali chini ya CCM imepoteza uhalali wa kutawala.