Nyahende Thomas
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 211
- 104
Nakubaliana na wewe mia kwa mia kujua wajue then nchi iendelee, hivi unadhani dunia haijui kama Maalim Seif na safari hii kaibiwa? wanajua ila amewaonea imani wananchi wa Zanzibar angekataa wangeteseka na ugumu wa maisha ilhali yeye anaponda raha na kubadilisha mboga. Tafakarini jamani maana hawa wanasiasa sometimes wanataka kututmia kama ngazi.
My take.
Slaa kubali kwa grounds kuwa NEC ni yao na ndio maana ameshinda INFACT Slaa atakuwa wa ajabu sana akiamini kuwa kwa tume iliyokuwepo ingemtangaza yeye mshindi na hapo ndio ninapo pata wasiwasi uelewa wa viongozi wetu sijui ni kweli wana nia ya dhati kututumika au laa.
sasa hapo umeongea nini? kama hata wewe unajua kwamba nec haikutenda haki halafu unakuja kumhamasisha Dr. Slaa asitafute haki yake, unataka tukueleweje? halafu ni wapi Dr. Slaa ametangaza kuingia msituni ama kuleta machafuko? unajua wakati mwingine hizi propaganda mnazotangaza kila kukicha zinawatisha sana wananchi na hata kushindwa kutafakari vizuri mapungufu ya nec yako wapi na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kila mara mnalialia tuuu, Dr. Slaa, Dr. Slaa, yani mnamuwekea maneno mdomoni. Tumsubiri, ameshasema kwamba kesho atatoa tamko sasa tusianze kuwa ma-sheikh yahya hapa JF.