Mhasibu adaiwa kutoroka na Sh 370 milioni

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MHASIBU wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka jijini Mwanza (Mwauwasa) Moses Ndaki ameripotiwa kutoroka kazini na kutokea upotevu wa Sh 370 milioni.

Habari za ndani kutoka katika mamlaka hiyo, zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Boti ya Mwauwasa, Padri Dk Charles Kitima na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba.

Awali ilielezwa kwamba mhasibu huyo, alitoroka baada ya kuhamishiwa kitengo kingine na kutakiwa kukabidhi kwa mhasibu mpya nyaraka na fedha za makusanyo ya malipo ya Ankara za wateja.

Ilielezwa kuwa kutokana na Mamlaka hiyo kusuasua katika makusanyo, menejimenti na uongozi wa Bodi ya Mwauwasa, iliamua kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika idara ya fedha na wahasibu wanaopokea malipo waliondolewa na kuwekwa wapya.

“Kulikuwa na taarifa za kichinichini kutoka kwa baadhi ya wahasibu kuwa fedha za Ankara za malipo ya wateja zimekuwa hazipelekwi benki kwa muda mrefu na kusababisha utendaji wa mamlaka hiyo, kushindwa kutimiza majukumu yake.

Kutokana na hali hiyo, kikao cha bodi kilichoketi Januari 8, mwaka huu kiliagiza kufanyika kwa mabadiliko ya idara ya uhasibu,” alisema mmoja wa watumishi wa mamlaka hiyo.

Ilielezwa kuwa baada ya mabadiliko hayo, wizi wa kutisha ulibainika kutokana na nyaraka mbalimbali za malipo ndani ya Kompyuta kuonyesha kulikuwa na kiasi kikubwa cha fedha ambazo zilikusanywa, lakini hazikuwa zimeingizwa katika akaunti ya mamlaka hiyo.

Pia nyaraka za benki zilionyesha fedha zilizokuwa zikiingiwa katika akaunti zilikuwa ni za malipo ya hundi pekee.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka hiyo, Padri Dk Charles Kitima alisema kutokana na maadhimio ya kikao cha bodi cha Januri 8, mwaka huu, mhasibu huyo, alipotakiwa kukabidhi nyaraka mbalimbali za mahesabu, aliondoka kazini na mapaka leo.

“Cashier mmoja hakuweza kukabidhi nyaraka mbalimbali za mahesabu yake, lakini pia tangu siku hiyo hajatokea kazini, sasa hatujui kama anaumwa au kaacha kazi, lakini tumeagiza uongozi kulishughulikia suala hilo kwa kutumia vyombo vya dola, na wakaguzi wa masuala ya fedha,” alisema Dk Kitima.

Alisema kutokana na tukio hilo, baadhi ya watumishi kadhaa wamehojiwa na jeshi la polisi.

“Mpaka sasa mimi siwezi kujua ni kiasi gani cha fedha kimepotea mpaka uchunguzi utakapokuwa umekamilika," alisema Dk Kitima.

Polisi na uongozi wa mamlaka hiyo ulilazikika kuvunja kasiki la fedha (Safe), lakini hawakukuta nyaraka wala fedha zozote.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Nonosius Komba alisema polisi wanafanya uchunguzi kuhusiana na upotevu wa fedha hizo na kwamba mpaka sasa watumishi watatu wa idara ya fedha wanashikiliwa na polisi.

“Wwapo watumishi ambao tunawachunguza, lakini mmoja ametoweka kazini tunamsaka kwa ajili ya kutaka kujua kwa kina baadhi ya mambo, lakini sasa siwezi kutoa taarifa zaidi mpaka hapo baadaye,” alisema Kamanda Komba.
 
siku hizi ndo ujanja mtaani utasikia watu wanamsifia jamaa KATOKA TAYARI. hapa JOB nilipo watu wanapiga m250 100 wanasepa kimya kimyaaaaa kweli bongo zaidi ya uijuavyo
 
Sidhani kama huyo atakuwa mhasibu. Unawezamwita karani, maana mhasibu ni mhitimu mwenye shahada ya juu ya uhasibu yaani CPA na ameandikisha na Bodi ya Taifa ya Uhasibu baada ya kutimiza kigezo cha uzoefu wa miaka mitatu tangu alipotunikiwa CPA
 
Shida iko wapi vijisenti vidogo tu ndo wampigie kelele? Mbona wameiba mabilioni na bado wako madarakani. Mbaya zaidi pesa zenyewe za kitz?
 
Shida iko wapi vijisenti vidogo tu ndo wampigie kelele? Mbona wameiba mabilioni na bado wako madarakani. Mbaya zaidi pesa zenyewe za kitz?
Vijisenti vidogo kwako ila kwa maskini ni pesa nyingi man!
 
Sidhani kama huyo atakuwa mhasibu. Unawezamwita karani, maana mhasibu ni mhitimu mwenye shahada ya juu ya uhasibu yaani CPA na ameandikisha na Bodi ya Taifa ya Uhasibu baada ya kutimiza kigezo cha uzoefu wa miaka mitatu tangu alipotunikiwa CPA

Proved: kuwa na elimu(CV) nzuri haimaanishi huyo mtu ana maadili mema pia, angalia mafisadi wana elimu nzuri tu lakini cheki matendo yao ni tapu tupu.
 
Proved: kuwa na elimu(CV) nzuri haimaanishi huyo mtu ana maadili mema pia, angalia mafisadi wana elimu nzuri tu lakini cheki matendo yao ni tapu tupu.

Awali ilielezwa kwamba mhasibu huyo, alitoroka baada ya kuhamishiwa kitengo kingine na kutakiwa kukabidhi kwa mhasibu mpya nyaraka na fedha za makusanyo ya malipo ya Ankara za wateja.

Huyu hakuwa mkuu wa kitengo, si rahisi Mamlaka ya maji kuwa na Wahasibu kamili wawili yaani mkuu wa idara na huyu aliyeiba
 
Back
Top Bottom