Mhariri wa Rai, Danny Mwakiteleko Afariki Dunia

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Mhariri wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, Danny Mwakiteleko, amefariki dunia.

Habari ambazo blogu ya Beda Msimbe, "Lukwangule Ent." alizozipata alfajiri ya leo na kuthibitishwa na watu wa karibu zinasema kwamba Mwakiteleko amefariki leo alfajiri katika hoispitali ya Muhimbili.

Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahututi Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.

Katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku. Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku.

Mwakiteleko alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa uangalizi hadi saa 12 asubuhi, ambapo madaktari waliamua apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Baada ya uchunguzi Muhimbili, madaktari walisema majeruhi alikuwa ameumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi (semi-conscious) hivyo ikabidi apelekwe katika chumba cha upasuaji ambako madaktari walimhangaikia kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana.

Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda kumwona na kuelezwa kwamba hali yake inaendelea vyema.












Source: wavuti
 
poleni ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
 
RIP Danny
Poleni familia, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na marafiki wote
Mungu awape faraja wakati huu wa majonzi mazito
 
Aaah my good friend now YOU are gone, we are behind you! Rest in peace brother danny,we will miss you dearly!
 
Poleni familia,ndugu,jamaa na marafiki.
Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom