omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Wanabodi,
Baada ya Samson Mwigamba na Absolom Kibanda kuburuzwa mahakamani kwa uchochezi, leo ni zamu ya Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications, Mzee Theophil Makunga, kuburuzwa mahakamani hapo, kuunganishwa na kesi hiyo.
Habari hizi ni kwa mujibu wa Mzee Theophil Makunga mwenyewe.
"Wahariri Wenzagu, baada ya Kibanda Mimi leo nilihojiwa na polisi kwa takriban saa kadhaa kuanzia saa 4.30 hadi saa saba na nusu kama acting MD wa Mwananchi ambao ni wachapaji (printer) wa magazeti ya Free Media Ltd. Baada ya kuandika maelezo yangu niliambiwa nirudi polisi kesho asubuhi saa tatu na kisha nitapelekwa mahakamani Kisutu kuunganishwa na akina Kibanda. Mimi nitashitakiwa kama mimi si kama Mwananchi Communications Ltd.
Makunga"
My Take.
Kwanza, Mzee Theophil Makunga, pole sana, sambamba na Kibanda na Mwigamba, tuko pamoja sana!
Wanabodi, nawaombeni concetration sasa iwe kwa chanzo cha haya yote na sio matokeo.
Kufikishwa mahakamani ni matokeo tuu, tena tusiwalaumu polisi, wao wanapokea maelekezo tuu, na watoaji maelekezo wanapo pa kuegemea.
Mzizi wa fitna yote hii ni Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976. Hii ni moja ya sheria 40 za ukandamizaji, zilizotajwa na Tume ya Nyalali. Kesi hizi ndio opportunity pekee ya kushinikiza hii sheria iwe scrapped of from the books of laws kabla ya katiba mpya Julai, 2014!
Nime attach hapa hiyo sheria ili tuu kuwajulisha, sheria ipo ila ilikuwa haitumiki, japo sasa matumizi yake ni kwa double standards. Ingetumika ipasavyo, magazeti kama Tanzania Daima, Mwananchi, Mwanahalisi na Raia Mwema, yangeshafungwa zamani!.
Swali dogo la kujiuliza, ni kuwa kama sheria hii siku zote ipo, na imekuwepo ila imekuwa haitumiki, why now?.
Jibu ni very simple, Serikali ya Tanzania inaogopa kilichotokea Misri, Libya na kwingineko, ambako vyombo vya dola, vimeitikia nguvu ya umma, hivyo kama ni kweli, askari wetu, wakiiukubali ushauri wa Mwigamba, na Wantanzania ambao tuna sifa ya utii wa Kikondoo, tukibadilika na kuvaa ujasiri kama wa wenzetu wa Misri, then inajua kitachofuatia!.
Ikulu Tamu Jamani msifanye masikhara!.
Angalizo:
Nawaombeni sana tunapochangia thead hii, tutangulize uzalendo kwa taifa letu Tanzania na viongozi wetu, tuchangie kwa heshima, adabu na nidhamu ya hali ya juu, ili tusiliponze jukwaa letu hili kuonekana na sisi ni 'wachochezi' tusije mponza bure
ndugu yetu, mwenzetu na kamanda wetu Max!.
Natanguliza Shukrani.
Pasco (wa jf).
Background
Kaka shukurani kwa taarifa hii....Wakati nikiungana nawe kuwatakia pole Kaka zangu Absalom Kibanda na Theophil Makunga kwa kuwa naamini kuwa mashtaka yao wameangukia katika wadhifa wao katika vyombo vyao kuliko uhusika wao wa moja kwa moja katika tuhuma za uchochezi kuna mambo yananiumiza kichwa na labda unaweza kunisaidia..
1. Hivi ukipitia ile makala ya Bwana Mwigamba unadhani kuwa alikuwa sawa na ni haki yake kabisa kuandika makala ile? Je nini mtazamo wako wa dhana ya uchochezi kuhusiana na makala ile, unadhani kuwa anaonewa ama dola linahaki na wajibu wa kumshitaki?
2. Kuhusiana na sheria hii ya Uchochezi unadhani kuwa haina umuhimu wake kwa dola na jamii kwa ujumla? Nini mtazamo wako wa kijumla na nini ushauri wako hasa ukitilia maanani muktadha wa uandishi wa makala kama hii husika na sakata hili?
3. Hivi ni kweli unadhani kuwa kesii hii dhidi ya makala hii ambayo imeandikwa na Samsom Mwigamba, ikahaririwa (kwa mujibu wa taratibu) na Absalom Kibanda na kuchapishwa (pia kwa mujibu wa taratibu) na Theophil Makunga ni kutokana tu na shinikizo la watu ama nyadhifa fulani nje ya mfumo wa kidola yaani Polisi na Mahakama ambao ni wajibu wao kushughulikia suala kama hili? Nini sababu zinazokupelekea kuamini kuwa ni shinikizo na sio mwamko - spirit ya utekelezaji wa makujukumu ndio sababu kuu ya mashitaka haya?
4. Ukitilia maanani kuwa Mwandishi wa makala hii inayoshutumiwa kwa uchochezi ni mwandishi wa habari lakini pia ni Kiongozi wa Chama cga Kisiasa (CHADEMA) chenye malengo na maslahi yake hasa wakati huo wa kuandikwa na kuchapishwa makala ambapo kwa upande wa dola kulikuwa na bado kunaweza kuwa na tafsriri ya kuwa nia ya kutumia njia zisizotambulika kikatiba kuondoa madarakani utawala unaotambulika kikatiba, hudhani kuwa ndugu yetu Mwigamba kwa kiasi alishindwa kutekeleza wajibu wake kama Mwandishi na alikosea kuandika na kusambaza makala ile?
NB: Najua kuwa kutokana na style ya ufanyaji kazi wa Kibanda yawezekana kabisa kuwa hakupata wasaa wa kuiona na kuihariri makala ile kwani kuna ushahidi wa wazi wa jitihada zake kubwa za kuzuia makala nyingi za aina hiyo kuchapishwa hapo kabla na hata wakati mwengine kumuweka katika hali ngumu na wenzake ambao wana mitazamo ya kihafidhina kama Mwigamba na Ngurumo, lakini ukweli unabaki kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukilalama kuwa tuna dola shaghalabaghala chini ya utawala legelege na hata kufikia kupigia debe UDIKTETA wa aina fulani tunayoamini kuwa utakuwa suluhu kwa changamoto,matatizo na madhila tunayokumbana nayo....tumekataa kusikia na wala kutambua buzara inayosema UDIKTETA HAUJUI KUCHAGUA MUHANGA....tujitahidi kukomaa na kuilinda demkorasia hii kiduchu lakini inayokuwa.....