Mhariri wa Mwanahalisi akatwa mapanga

Nawewe umezidi kuwa desperate kwa watu kutembelea website yako,break news hapa hapa kama unazo acha gimicks za kuvutia trafic kwenye kitovuti chako

Sidhani kama umelazimishwa kwenda huko KLH News.
Wengi wetu tumekwenda huko na tumepata hiyo breaking news na wewe unaweza tu kuendelea kutazama TVT na kusikiliza radio Tanzania maana ndio uhuru wa habari huo.

Asante
 
duh ,Je ingekuwa vipi kama Mzee Mwanakijiji angekuwa naye anishi bongo,Je EL angemuacha?
 
Hii Kali kweli, Mtu wa Pwani!! unamtanguliza mwenzako kwenye hukumu ya mwenyezi Mungu kirahisi hivyo? ama unataka kutuambia unafahamu ama ulishiriki kuchapa mapanga na unauhakika hata pona? pole pole mkuu

Hii taarifa inayoenezwa kwa njia ya SMS kuwa Bwana Kubenea alimwagiwa Tindikali '' ACID'' Usoni na Bw. Ndimara alikatwa mapanga wakiwa ofisini wakiandika habari za Ufisadi uliyokuwa ukimhusisha ROSTAM na Kampuni ya KAGODA, je wanaJF mnaweza kujua lolote juu ya habari hizi?

MwanaHalisi ni gazeti la aina yake Tangu nchi hii ipate uhuru. Hakika hakuna gazeti lililokuwa na habari nzito na zilizochambuliwa kwa umakini. Wahariri wa gazeti hili walikuwa wanafanya kazi kwa niaba ya watanzania huku wakituletea habari zilizochunguzwa. Hivyo naamini kabisa kuwa kilichofanywa ni dhamira ya kuwanyamazisha waandishi hawa na baadhi ya watu ambao wamejikuta maslai yao yakianikwa hadharani na gazeti hili.
Licha ya kuwepo ktk hali ya maumizi. WanaJF tuungane pamoja kuendeleza kazi nzuri iliyokwisha kuanzishwa na mwanahalisi. Mungu awasaidie wapate kupona haraka japo sijui ni kwa kiasi ghani tindikali imemuathiri Mr. Kubenea Machoni maana kwa picha iliyoonekana akiwa Muhimbili ni kuwa alikuwa amefumba macho huku akiongea kwa shida. TUSIMAME IMARA DHIDI YA GENGE LA UWARIFU LILILO IKAMATA NCHI
 
Hivi kama huyu mwandishi aliiba mke wa mtu! je bado jamii inastahili kulaani hiki kitendo kwa uzito huo?
Au jamii ilaaani kitendo hicho kama vitendo vingine vya ujambazi na uhalifu kwa watu wengine wote?
Maana naona matamko mazito kabla hata ya uchunguzi wa polisi.!
Tukiendelea kikasuku hivi uandishi itakuwa kichaka cha waovu kwenye jamii maana watakuwa miungu watu! maana wao wanapakusemea kuliko vyombo vyote vingine vyote.
Nafikiria tu upande mwingine wa shillingi maana ripoti ya uchunguzi bado.
 
Kilitime, unataka kuingia kwenye mtego wa kina Raila ambapo laana dhidi ya vitendo viovu inategemea motive na kisa nyuma yake na siyo uovu wenyewe.

leo hii kuna habari kule Vingunguti ya Bibi wa watu anayetuhumiwa uchawi kuokolewa na Polisi baada ya mob ya watu kushambulia nyumba yake hasa baada ya mwili wa wa Bingi Halima aliyetoweka tarere 29 disemba kukutwa pembezoni mwa mto wa Msimbazi.

wananchi wenye hasira wakata kumfanyizia bibi huyo kwa madai ni "mchawi" na uongozi wa mtaa wakaingia hadi nyumba ya mama huyo na kuangalia kama "kuna wototo wengine".

Mwandishi wa channel 10 alikuwa anazungumza kana kwamba kweli mama huyo anahusika hasa baada ya mwili kukutwa ukiwa "hauna viungo nyeti" (hakuna anayeelezea kama mwili umekuwepo hapo kwa muda wote huo kwaninin viungo nyeti viwepo!)

Sasa badala ya watu kulaani kitendo cha binti huyo kuuawa (kama kuna alama za mchezo mbaya au ajali) na badala ya watu kulaani kitendo cha Bibi wa watu kuvunjiwa nyumba yake watu wanajaribu kutafuta uhalali wa kufanya hivyo.

Ninachosema ni kuwa regardless kama Kubenea alishambuliwa kwa sababu ya kuomba "chumvi" au kwa sababu za kisiasa, kitendo hicho lazima kilaaniwe na kitajwe kwa vile kilivyo yaani ni cha kinyama. Uzito wa ubaya wa kitendo hicho hautokani na motive za kitendo hicho. There are some certain actions that are intrisically evil and devoid of any morality in them. This is one of them.

Ndiyo maana watu wengine wanaona kuuawa kwa Wakikuyu ni sahihi kwa sababu "mkikuyu" mmoja amewaibia kura!
 
Baraza la Vijana wa Chadema wametoa tamko hili:

IJANA WA CHADEMA TUNALAANI SHAMBULIO KWA WAANDISHI
• Vijana wa Tanzania wasikubali kutumika na mafisadi
kufanya uhalifu
• Vyombo vya dola vichunguze wahusika wakuu na kusudio
la shambulizi
• Ni uvamizi dhidi ya haki ya kikatiba ya kupata na
kutoa habari
• “Kalamu za Wanahabari zina nguvu kuliko upanga wa
mafisadi”

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA),
vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda haki na ukweli
kote nchini kutoa pole kwa wanahabari Saed Kubenea na
Ndimara Tegambwage kwa kushambuliwa kwa mapanga na
tindikali. Mwenyezi Mungu awawezeshe kupona haraka
waweze kurejea katika majukumu yao ya kulijenga na
taifa na kwa namna ya pekee tunaziombea familia zako
utulivu katika kipindi hiki.

Aidha tunalaani vikali uvamizi na shambulizi hili
dhidi ya wahabari hawa na ofisi yao wakiwa katikati
ya jukumu la kuandaa toleo la gazeti kwani ni
shambulizi dhidi ya binadamu na juu ya haki ya
kikatiba ya kupata na kutoa habari.

Kutokana na mtiririko wa matukio na ushahidi wa
kimazingira, tungependa tukio hili lisichukuliwe kama
vitendo vya kawaida vya ujambazi bali lichunguzwe kama
kitendo cha kigaidi na uharamia dhidi ya waandishi wa
habari, uandishi wa habari na chombo cha habari. Si
wajibu wa wananchi kuhukumu, na ni mapema mno
kuhusisha moja kwa moja tukio hili na ‘mtu’ au ‘watu
fulani’. Hata hivyo, kwa mtiririko wa matukio na
ushahidi wa kimazingira ni rahisi kutuhumu kuwa upo
uwezekano mkubwa wa uvamimizi na shambulizi hili kuwa
limefanywa na baadhi ya mafisadi wakiwatumia vijana
kufanya tendo hili la kifisadi.

Wanahabari hawa na chombo chao wamekuwa mstari wa
mbele kwa uwazi bila woga katika mapambano dhidi ya
ufisadi na kutetea rasilimali za taifa, na kuwa sehemu
ya mashujaa wa habari nchini. Mwanahalisi ni moja ya
magazeti ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika
kuandika tuhuma za ufisadi na/au matumizi mabaya ya
madaraka zinazowakabili viongozi kadhaa wa serikali,
makampuni na taasisi mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa, mwishoni mwa mwaka jana vyombo
mbalimbali vya habari viliandika kuhusu vitisho
vinavyotolewa kwa chombo hicho cha habari na vyombo
vyake. "Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari na Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Saed
Kubenea, ilieleza kuwa kuna mienendo ya chinichini ya
kusambaza vitisho kwa vyombo vya habari hususan
MwanaHalisi, wachapishaji wake, wahariri, waandishi na
wachangiaji wa makala na taarifa mbalimbali.(Rejea
Tanzania Daima-28/9/2007). Hilo lilikuja baada ya
gazeti hilo kuandika habari na kuweka hadharani majina
ya waliotajwa kwenye ‘orodha ya mafisadi’.

Pamoja na kuwa jeshi la polisi limetangaza kuwatafuta
watuhumiwa vijana watatu waliohusika na uvamizi huu;
tungependa kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba
jitihada za uchunguzi zielekezwe katika kuwaibaini
pia waliowatuma vijana hawa kufanya uhalifu huo.
Katika mazingira ya wahalifu vijana wa kawaida, ni
vigumu kuhusisha jitihada za kulenga mwanahabari na
kummwagia tindikali machoni, hali ambayo inaashiria
shambulizi hili ni la kutumwa na ‘mtu’ ama ‘mtandao
Fulani wa watu’. Kadhalika, pamoja na kuwatafuta
wahusika, vyombo vya dola vichunguze kusudio hasa ya
shambulio hilo- kama nia ilikuwa ni kuwadhuru
waandishi hawa siku hiyo ili habari Fulani isitoke au
ni kisasi kutokana na habari Fulani ambayo chombo
hicho kimekuwa kikiandika. Uchunguzi kamilifu kama huu
na hatua zitakazochukuliwa kutokana na uchunguzi huo
ni muhimu katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari na
kulinda maisha ya wanahabari hapa nchini.

Kama kweli shambulio hili limefanywa na watuhumiwa hao
kwa kutumwa na ‘fisadi’ ama ‘mtandao Fulani wa
mafisadi’ wanaotapatapa, basi tunasikitishwa na pia na
jinsi ambavyo ‘habari’ na ‘mwanahabari’
wanavyochukuliwa. Tunakumbusha kuwa mwanahabari ni
mjumbe tu wakufikisha ujumbe katika jamii; ambaye
anapaswa kulindwa na kuheshimiwa. Tabia inayoanza
kuchipua ya kumshambulia mjumbe au chombo
kilichofikisha ujumbe tena kwa njia ambazo ni kinyume
cha sheria na ustaarabu wa binadamu badala ya
kuushughulikia ujumbe wenyewe; ikiachwa ikashamiri
inaweza ikatishia ufanisi wa sekta ya habari ambayo
inapaswa kudumishwa kama mhimili wa nne wa dola.

Serikali ni vyema ikalichukulia suala hili kwa uzito
wake, kwani vitendo kama hivi vya wanahabari
kushambuliwa vikiendelea vinaweza kuhamia kwa watetezi
wengine wa haki; na hali hii ikiachwa itazalisha chuki
miongoni mwa jamii na hatimaye jamii itaanza kutoa
hukumu ya umma(mob justice) kwa wanaotuhumiwa kufanya
vitendo kama hivi vya kifisadi.

Aidha tunachukua fursa hii kutoa mwito kwa vijana kote
nchini kutokubali kutumika kufanya vitendo vya
uhalifu, na tunatoa rai kwa jamii kuwataja
wanaowatumia vijana kufanya vitendo hivyo vya kinyama.
Fisadi yoyote aliyetayari kuyaweka rehani maisha ya
watanzania waliowengi kwa ufisadi wake hawezi
kushindwa kuweka hatarini maisha ya mtanzania mmoja
ambaye anachimbua ufisadi wake na kumweka katika
mstari kuhukumiwa; hivyo vijana wasikubali kuingia
katika mtego huu wa kufanya kazi za mafisadi. Mwisho,
tunawaomba vijana wote nchini wakiwemo vijana
wanahabari kuendeleza harakati za kutetea haki na
ukweli kwa kutumia uandishi wenye kuchochea fikra
mbadala zenye kuleta demokrasia na maendeleo nchini.
Vitisho visirudishe nyuma uandishi wa habari wenye
kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa
kwani “kalamu za wanahabari zina nguvu kuliko upanga
wa mafisadi”

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553

Tunasubiri mabaraza ya vijana wa vyama vingine nao kutoa matamshi yoyote yale.
 
wakuu heshima mbele,
ukiangalia maelezo ya bwana kubenea ya kwamba alisharipoti polisi kuhusiana na meseji alizokuwa anatumiwa,kwa kuwa polisi hawakuchukua hatua zozote mpaka maangamizi yamemkuta,naomba kuunda tume huru kuchunguza suala hili
na ripoti iletwe hapa JF kabla ya ijumaa..Naomba kupendekeza majina ya watakao unda tume.Tume itakuwa chini ya HALISI na wajumbe watakuwa Mwanakijiji,Lunyungu,Kana Kasung,masatu,Admin,zitto,Kitila na MZEE E
 
Mkombozi, polisi watasema "hatujashindwa uchunguzi wetu" na zaidi ya yote tayari kimeundwa kikosi maalum (task force) ya Polisi ambapo hadi hivi sasa watu wawili wametiwa mbaroni..
 
Mwanakijij,
walikuwa wapi kuunda task force walipoletewa habari kuwa watu wanamtishia nguli kubenea?
as far as i kno task force huwa zinatumia pesa nyingi kama posho..je hawa mapolisi wetv wanategemea posho ili wafanye kazi?
ila Muungwana Muungwana tu,mzee wa kutake advantage.,utasikia kesho serikali kugharimikia matibabu ya kubenea!
wajumbe naomba mnikubalie na nitawapa ushirikiano wa masuala ya kisheria wa kutosha kabisa mkihitaji,
 
...duh jk opportunistic kweli...alafu anaposema kuwa ""waandishi mnapoandika habari za watu mchukue tahadhari kwa kuwa kuna watu hawataki habari zao ziandikwe" hapo ana maana gani? kama amiri jeshi mkuu anasema hivyo tukimbilie wapi??....alijaribu pia kulainisha kwa kusema kuwa vitendo vya kumwagiana tindikali hutokea mara kwa mara ..citing tukio la kumwagiwa tindikali kwa yule kipa mkali wa NYOTA NYEKUNDU ..enzi hizo [alimsahau]...lakini anaitwa SHEIKH ABDALAH..walimpofua masikini...na siku hiyo kesho yake ilikuwa wacheze NYOTA NYEKUNDU na YANGA....
 
...tunapomuangalia kubenea na kumuombea ..pia tumkumbuke marehemu STASLAUS KATABALO..ambaye Alijitoa sana muhanga enzi zake kuibua na kuandika hadi mauti kuhusu kashfa ya LOLIONDO....
 
Yeah mwenyewe JK anasema ni "work hazards"... halafu akazimulia kwa kusema "siyo kwamba nawatishia, fanyeni kazi zenu"...
 
KAMA ALIKUWA HANA LA KUSEMA ..SIJUI KWA NINI AKAENDA PALE..rais anategemewa kila jambo analofanya liwe ni statement ya maelekezo..sio maneno shallow tu ya juu juu yasiyoweka muongozo..

kama hakuwa na ujumbe aliopanga kuufikisha kwa ziara ile[as certain gesture] rather angeabakia ikulu acheze karata kwenye laptop yake ..au kutuma mails kwa marafiki....akisubiria kuonana na watu wa ODM
 
Ndio maana I love this forum, yaani Mkuu Theory, hebu weka vitu mwanangu, tuchambue mchele na pumba!

Kwa kifupi unachosema GT ni kwamba huyu mwandishi amefanya kosa la kuelewana na mafisadi kwa kukubali fedha zao lakini akaendelea kuwaumbua gazetini. Am I right? And by the same token unaelekea kutoshtushwa na yaliyompata. Am I right again?

Mkuu GT,heshima mbele,
nimesoma post yako unadai kuwa ndugu Kubenea alikuwa "anavuta hela" kutoka kwa hao mafisadi ili asiwaumbue,na kuwa kumwagiwa kwake acid ni mafarakano baina yake na hao jamaa,sasa kuna FMES alikuwa anadai ushahidi kutoka kwa baadhi yetu waliousisha tukio la kumwagiwa acid kwa Kubenea na CCM an mafisadi,na akawataka watoe ushaidi,sasa mi pia nakuuliza swali moja,hilo swala la Kubenea kuwamo katika payroll ya mafisadi unao ushahidi wake?Ikiwa hoja yako itakuwa sahihi kuwa alifarakana na mafisadi ambao humlipa (kama unavyodai wewe kulingana na ushahidi utakaoutoa hapa) basi wewe na kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this.

Quote:-

"kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this."

Mkuu sio mfisadi wote ni wana-CCM, na CCM has nothing to do na mafisadi, halafu ninaomba nikuambie wazi kuwa so far toka hii topic ianze GT ndiye peke yake ametoa hard evidence ya anachokisema, ninaweza kumpa some support kwa sababu wengine wote mmeshindwa kutoa angalau a hint kuhusiana na madai yenu kuwa serikali ya CCM au mafisadi ndio wanaohusika na huu uharamia,

Ninarudia tena so far ni GT peke yake ndiye anaye make a sense kwa kutoa angalau "Evidence" ku-back up theory yake, hebu na nyinyi toeni japo dataz kidogo, badala ya kuanza analysis over analysis, bila dataz, siamini 100% anayosema GT, lakini kama mjadala ukifungwa sasa theory yake inasimama tena kwa nguvu sana, kwamba Mwandishi alikuwa aki-play double stadard against the rules za uandishi, Mkuu Kithuku, lete facts tuacheni na analysis bila facts!

Please tunahitaji facts na sio itikadi na hisia, pia tunawaombea walioathirika kupona haraka warudi kutuamusha wananchi. Lakini ukisoma hapa chini GT makes a lot of sense na pia ana back-up theory yake na some "Evidence" ingawa siamini lakini angalau mnyonge mnyongeni lakini ninaichukulia hii chini as a fact unless mwingine aje naz tofauti, please enough of analysis tunahitaji facts!!

Kinachokufanya useme GT katoa "hard evidence" ni nini? So far yeye kaja na theory nyingine tu ya possible reasons za ndugu yetu kupigwa mapanga na kumwagiwa tindikali. Nasema hivyo kwasababu hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa alikuwa anapokea pesa toka kwa hao mafisadi unless mzee unajua zaidi ya haya yanayosemwa hapa.

FMES: Evidence aliyetoa GT kuhusu huyu bwana kuwa kwenye payroll ni ipi? Can you please show us pengine itasaidia nasi kubadili mawazo yetu.

Kubenea ambaye amepata athari katika macho yake, ameondoka muda si mrefu kuelekea India kwa matibabu zaidi ili kumuepusha na upofu.

Baraza la Vijana wa Chadema wametoa tamko hili:

IJANA WA CHADEMA TUNALAANI SHAMBULIO KWA WAANDISHI
• Vijana wa Tanzania wasikubali kutumika na mafisadi
kufanya uhalifu
• Vyombo vya dola vichunguze wahusika wakuu na kusudio
la shambulizi
• Ni uvamizi dhidi ya haki ya kikatiba ya kupata na
kutoa habari
• “Kalamu za Wanahabari zina nguvu kuliko upanga wa
mafisadi”

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA),
vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda haki na ukweli
kote nchini kutoa pole kwa wanahabari Saed Kubenea na
Ndimara Tegambwage kwa kushambuliwa kwa mapanga na
tindikali. Mwenyezi Mungu awawezeshe kupona haraka
waweze kurejea katika majukumu yao ya kulijenga na
taifa na kwa namna ya pekee tunaziombea familia zako
utulivu katika kipindi hiki.

Aidha tunalaani vikali uvamizi na shambulizi hili
dhidi ya wahabari hawa na ofisi yao wakiwa katikati
ya jukumu la kuandaa toleo la gazeti kwani ni
shambulizi dhidi ya binadamu na juu ya haki ya
kikatiba ya kupata na kutoa habari.

Kutokana na mtiririko wa matukio na ushahidi wa
kimazingira, tungependa tukio hili lisichukuliwe kama
vitendo vya kawaida vya ujambazi bali lichunguzwe kama
kitendo cha kigaidi na uharamia dhidi ya waandishi wa
habari, uandishi wa habari na chombo cha habari. Si
wajibu wa wananchi kuhukumu, na ni mapema mno
kuhusisha moja kwa moja tukio hili na ‘mtu’ au ‘watu
fulani’. Hata hivyo, kwa mtiririko wa matukio na
ushahidi wa kimazingira ni rahisi kutuhumu kuwa upo
uwezekano mkubwa wa uvamimizi na shambulizi hili kuwa
limefanywa na baadhi ya mafisadi wakiwatumia vijana
kufanya tendo hili la kifisadi.

Wanahabari hawa na chombo chao wamekuwa mstari wa
mbele kwa uwazi bila woga katika mapambano dhidi ya
ufisadi na kutetea rasilimali za taifa, na kuwa sehemu
ya mashujaa wa habari nchini. Mwanahalisi ni moja ya
magazeti ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika
kuandika tuhuma za ufisadi na/au matumizi mabaya ya
madaraka zinazowakabili viongozi kadhaa wa serikali,
makampuni na taasisi mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa, mwishoni mwa mwaka jana vyombo
mbalimbali vya habari viliandika kuhusu vitisho
vinavyotolewa kwa chombo hicho cha habari na vyombo
vyake. "Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari na Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Saed
Kubenea, ilieleza kuwa kuna mienendo ya chinichini ya
kusambaza vitisho kwa vyombo vya habari hususan
MwanaHalisi, wachapishaji wake, wahariri, waandishi na
wachangiaji wa makala na taarifa mbalimbali.(Rejea
Tanzania Daima-28/9/2007). Hilo lilikuja baada ya
gazeti hilo kuandika habari na kuweka hadharani majina
ya waliotajwa kwenye ‘orodha ya mafisadi’.

Pamoja na kuwa jeshi la polisi limetangaza kuwatafuta
watuhumiwa vijana watatu waliohusika na uvamizi huu;
tungependa kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba
jitihada za uchunguzi zielekezwe katika kuwaibaini
pia waliowatuma vijana hawa kufanya uhalifu huo.
Katika mazingira ya wahalifu vijana wa kawaida, ni
vigumu kuhusisha jitihada za kulenga mwanahabari na
kummwagia tindikali machoni, hali ambayo inaashiria
shambulizi hili ni la kutumwa na ‘mtu’ ama ‘mtandao
Fulani wa watu’. Kadhalika, pamoja na kuwatafuta
wahusika, vyombo vya dola vichunguze kusudio hasa ya
shambulio hilo- kama nia ilikuwa ni kuwadhuru
waandishi hawa siku hiyo ili habari Fulani isitoke au
ni kisasi kutokana na habari Fulani ambayo chombo
hicho kimekuwa kikiandika. Uchunguzi kamilifu kama huu
na hatua zitakazochukuliwa kutokana na uchunguzi huo
ni muhimu katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari na
kulinda maisha ya wanahabari hapa nchini.

Kama kweli shambulio hili limefanywa na watuhumiwa hao
kwa kutumwa na ‘fisadi’ ama ‘mtandao Fulani wa
mafisadi’ wanaotapatapa, basi tunasikitishwa na pia na
jinsi ambavyo ‘habari’ na ‘mwanahabari’
wanavyochukuliwa. Tunakumbusha kuwa mwanahabari ni
mjumbe tu wakufikisha ujumbe katika jamii; ambaye
anapaswa kulindwa na kuheshimiwa. Tabia inayoanza
kuchipua ya kumshambulia mjumbe au chombo
kilichofikisha ujumbe tena kwa njia ambazo ni kinyume
cha sheria na ustaarabu wa binadamu badala ya
kuushughulikia ujumbe wenyewe; ikiachwa ikashamiri
inaweza ikatishia ufanisi wa sekta ya habari ambayo
inapaswa kudumishwa kama mhimili wa nne wa dola.

Serikali ni vyema ikalichukulia suala hili kwa uzito
wake, kwani vitendo kama hivi vya wanahabari
kushambuliwa vikiendelea vinaweza kuhamia kwa watetezi
wengine wa haki; na hali hii ikiachwa itazalisha chuki
miongoni mwa jamii na hatimaye jamii itaanza kutoa
hukumu ya umma(mob justice) kwa wanaotuhumiwa kufanya
vitendo kama hivi vya kifisadi.

Aidha tunachukua fursa hii kutoa mwito kwa vijana kote
nchini kutokubali kutumika kufanya vitendo vya
uhalifu, na tunatoa rai kwa jamii kuwataja
wanaowatumia vijana kufanya vitendo hivyo vya kinyama.
Fisadi yoyote aliyetayari kuyaweka rehani maisha ya
watanzania waliowengi kwa ufisadi wake hawezi
kushindwa kuweka hatarini maisha ya mtanzania mmoja
ambaye anachimbua ufisadi wake na kumweka katika
mstari kuhukumiwa; hivyo vijana wasikubali kuingia
katika mtego huu wa kufanya kazi za mafisadi. Mwisho,
tunawaomba vijana wote nchini wakiwemo vijana
wanahabari kuendeleza harakati za kutetea haki na
ukweli kwa kutumia uandishi wenye kuchochea fikra
mbadala zenye kuleta demokrasia na maendeleo nchini.
Vitisho visirudishe nyuma uandishi wa habari wenye
kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa
kwani “kalamu za wanahabari zina nguvu kuliko upanga
wa mafisadi”

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553

Tunasubiri mabaraza ya vijana wa vyama vingine nao kutoa matamshi yoyote yale.

KAMA ALIKUWA HANA LA KUSEMA ..SIJUI KWA NINI AKAENDA PALE..rais anategemewa kila jambo analofanya liwe ni statement ya maelekezo..sio maneno shallow tu ya juu juu yasiyoweka muongozo..

kama hakuwa na ujumbe aliopanga kuufikisha kwa ziara ile[as certain gesture] rather angeabakia ikulu acheze karata kwenye laptop yake ..au kutuma mails kwa marafiki....akisubiria kuonana na watu wa ODM

Jamani eeeh..ndio kwanza nimeingia na naona kuna hija nyingi tuu mmezieleza ila ningependa kupanya ufafanuzi zaidi

Pamoja na kuwa watu wanataka kuamini kuwa MEDIA tanzania iko kwa ajili ya mtanzania lakini ukweli ni kuwa MEDIA zetu zote zoko kwa ajili ya masalahi yao ambayo ni kuuza magazeti na matangazo

Sasa katika kesi ya MWANAHALISI na huyu SAIDI naweza kuconfirm kuwa alipewa onyo na wahusika kutokana na mwenendo wake wa kutoipa serikali nafasi ya kupumua na aliiitwa mpaka kwenye mkutano lakini defese yake ilikuwa:

1) Yeye ana NJAA

2) HAPEWI MATANGAZO kama magazeti mengine

3) Slution kwake ni kwenda na hizo SENSATIONAL STORIES

Katika ule mkutano waliokuewpo wakakubali hoja zake na ikaamuliwa yafuatayo:

1)HAITOWEZEKANA kumpa matangazo as soon as that hivyo waliomba muda

2) ALIPEWA KIASI KIKUBWA TU CHA PESA ili kumkeep going for a while wakati azimio la kwanza linafanyiwa ufumbuzi

3)SAISI KUBENEA likubali zile pesa na kwa muda alisizi yale mashambulizi

sasa wakati wahusika walipokuwa wako tayari na mpango mzima wa kuuupatia ufumbuzi wa muda mrefu wa MWANHALISI bwana saidi aliamua ku go all out on attack sasa jamaa waliamua kushelve plan nzima...sasa options zilizokuwepo mezani zilikuwa

a) Awe NEUTRALIZED

b) Gazeti na mchpishaji wapewe mtego ambao watachapisha habari ya uwongo kisha wakafilisiwe mahakamani

" Mheshimiwa " alikataa hoja zote zilizopelekwa mbeleyake na zaidi aliikataa ile option A sasa jamaa waliamua kwenda rogue na kumpa message kupitia GARILAKE ambalo lilivunjwa/chomwa moto

baada ya hapo Akarudi kulalama kuwa anafuatwa kwa kuomba mkutano wa pili ambao jamaa walimtolea nje na yeye kujibu mashambulizi aliamua kuligeuza MWANAHALISI kama vile NEWYORK POST if not THE SUN!...ambayo ilikuwa fuelled zaidi na NJAA au watoto wamjini wanaita NZARA iliyo mjaa bwana saidi

lakini kwa kuonyesha kuwa SAIDI KUBENEA na SERIKALI wanajuana, mtu wao JK alienda kumtembelea hosptalini

sasa maswali ya kujiuliza ni:

1-NANI ANAMLIPIGIA GHARAMA ZA KUTIBIWA INDIA?

2-MBONA WALE WAANDISHI WALIOPIGWA NA WANAJESHI HAWAKUPELEKWA INDIA?

3-MBONA WAANDISHI WA IPPMEDIA WALIPOPIGWA NA CUF HAWAKUPELEKWA KUTIBIWA INDIA?

-Kubenea INDIA, MUDHIHIR ujerumani...jamani huyu ni mtu wao sema ndio kichwa chake ni kigumu tuuu na nivizuri mkalijua hilo

MSG to MNYIKA

Ebwana wewe shule unarudi nlini au ndio basi tena? mzee umri huyo unhitajika shule na jamaa kwa uliyowafanyia wainsist wakulipie shule walau hata LINCOLN if not UEL
 
Nadhani Mwanahalisi was one of the best selling papers in Dar.If that's the case,sidhani kama Bw Kubenea na ndugu zake (ambao hatujui uwezo wao wa kifedha) wanashindwa kumudu gharama za maibabu India.Nasisitiza,NADHANI....
 
Gharama za matibabu zimechangiwa na "wadau mbalimbali wa habari" na serikali si mmojawapo waliochangia.. as far as I know.. na kwenda India wengi wanapelekwa India hata watoto wenye matatizo ya moyo..
 
Taarifa ya uhakika ni kwamba serikali ndiyo inagharimia safari na matibabu; kama ambavyo hufanya kwa vingunge na watu wengine muhimu wanapopelekwa nje kwa matibabu. Hayo ni maagizo ya JK alipomtembelea mgonjwa.
 
Back
Top Bottom