Mhariri wa Mwanahalisi akatwa mapanga

Pole sana Kichwamaji unataka kubishana na jiwe ? Haya endelea watu wako kazini .Wanataka Ushahidi kama ule Mkapa alitaka katika mkutano wa hadhara Singida juu ya mwekezaji wa barabara hahaha . Ushahidi , ushahidi, source nk ujinga mtupu .

Ukitaka la Zitto na Mbatia kifo chake utapewa a clear picture na bado utaomba ushahidi . Ndiyo mlengwa alikuwa Zitto kuna hata recorded voices Zitto anaulizwa na Waziri mmoja yuko maeneo gani kitu ambacho hakipo maana hawana mawasiliano ya akaribu ila alijua kwamba Zitto anaenda Songea .In like 3 minutes ajali ikatoea huyo waziri hakuwa na la kumuuliz Zitto zaidi ya kusema uko wapi .Akapewa jibu la uongo niko Njombe mjini.

Huu by itself ni ushahidi tosha bora watawale hao CCM mpaka tutakapo kuwa tayari. Kama ndio "kuthink faster" kwenyewe ndio huku, Im more than happy to remain "slow thinker" or not a "thinker at all"
 
Seems Kubenea has lost sight(or some greater part of it). Kwa kweli inasikitisha.

JK amesema amepokea kwa mshituko habari hizo.
 
na nimemwambia ES hapo juu kwamba sitarajie kuona ushahidi wa kushikika hapa...yeye bado anataka ushahidi....staili ya mkapa ya kukwepa hoja ya rushwa.

Mkuu "Kichwamaji"

Kwanza ninaomba nikukaribishe tena, baada ya kunikwepa kwa muda sasa, naona umepata nguvu mpya ya kupambana na mimi karibu sana mkuu, Katika hii forum kuna ishus zinahitaji dataz na kuna zisizo hitaji, this one inahitaji ili kulinda heshima ya hii forum, angalau dataz tuzichambue wenyewe, ni vipi serikali au CCM inahusika na huu uvamizi?

Ushahidi wa ubadhirifu wa Mkapa, upo n umeshtolewa mara nyingi kinachosubiriwa time tu kuwa right, then Mkapa atatinga mahakamani, hilo halina ubishi!

2.
Tusi-conclude...we jipe muda tu, utajua haya usiyoyajua...

Tusi-conclude wakati wewe tayari umesha-conclude kuwa ni serikali na CCM ndio wanaohusika na uvamizi, kama ni kujipa muda wa kusubiri then ina maana wote hatuna facts ila tusubiri zitakapotoka kama ninakuelewa sawa sawa, unless kun something nina miss!

Otherwise, hata yawe maneno ya kejeli namna gani, bila facts hoja haiwezi kupita hapa bila ya kuulizwa, hatusifiki hapa kwa hiy tabia ya kukubali bila kuuliza!
 
1.
hata mimi si mjinga kutoa ushhidi kwa watu nisiowajua...

Now look at this, wewe ni mwerevu kwa kutoa maneno kuwa serikali na CCM inahusika na uvamizi huu wa waandishi wa habari kwa watu usiowajua, lakini at the same token pia huwezi kuwa mjinga kutoa ushaidi ku-back up maneno yako mwenyewe kwa watu usiowajua?

2.
Lakini kumbuka yapo mengi yanayotendeka na ushahidi haupatikani, na bado yapo yanaonekana na yanatuathiri. Unataka kusema tuyakane hadi ushahidi utakapopatikana? Basi, JF imekuwa court of law!

Kwa kuuliza ukweli kuhusu hiii habari kwamba serikali na CCM inahusika na uvamizi huu wa waandishi wa habari basi JF inakuwa Court Of Law?
 
Jamani ameshaomba Msamaha asamehewe Mtu wa Pwani. Ila na wewe uwe unaangalia maada inasemaje ndio uropoke. Duu ila huu majadala sasa naona umeshakuwa wakisiasa jamani watu waliofanya hivi hawajajulikana tusiwe mahakimu suala la amsngi tuombe Mungu wapatikane na kumuombea Bw Kubena apone haraka arudi kwenye majukumu yake na azidi kuongeza changamoto ambazo nahisi wengi zinawagusa. Get well Soon Kubena.
 
huyu naye alikuwa hasikii alishapelekewa taarifa zamani lakini wapiiii yuko ka Benazir Bhutto vilee

Kwahiyo kwa busara zako ulimtaka abadili mwelekeo wa uandishi wa habari zake ulingane na Uhuru,Mzalendo,DailY/Sunday News+Habari Leo,Habari Corporation?The guy risked his life for you and me na walalahoi wengine,contrary to Benaziri who went back to Pakistan to serve the interests of her masters (US and UK).Alichofanya Kubenea hakina tofauti na ulichofanya wewe kutunong'oneza kwamba kuna mzungu ana access ya "siri za serikali ktk ubalozi wetu huko Holland"

Na kwa nyie waungwana mnao-doubt mafisadi kuhusishwa na tukuio hili mnapaswa kutambua kwamba wananyooshewa kidole kwa kuzingatia ushahidi wa kimazingira,na hilo si geni kwani hata "kwa hawa wenzetu wanaodai kuendesha mambo yao transparently" (nchi za Magharibi) matukio ya namna flani huhusishwa na watu flani kwa kuzingatia ushahidi wa kimazingira (mfano ni kifo cha Princess Diana).

Kwanini Mafisadi?Jibu jepesi ni kwamba gazeti la Mwanahalisi ndilo pekee lililotaja majina yao kama yalivyoorodheshwa na akina Slaa,ilhali magazeti mengine yooote yalikwepa kutaja majina hayo.Ni kwa sababu hiyo ndio maana mafisadi walitishia kulipeleka mahakamani kwa kashfa,kumbe mahakama yenyewe ni hii ya kifisadi na kinyama!!!Sishangai kwani kama wako tayari kuyaweka rehani maisha ya mamilioni ya Watanzania watashindwaje kutamani roho ya mwandishi mmoja wa habari.Wanachosahau ni kwamba ipo siku (hata kama itachukua karne ngapi) watapambana na hukumu yao,inshallah.

Naamini wanaotutaka tusiwahusishe mafisadi na tukio hili wanafanya hivyo aidha kwa uzembe wao wa kuunganisha dots,uchovu wa wikiendi au kuongeza idadi ya posts tu lakini mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kushindwa kusoma maandishi yaliyo ukutani kuhusiana na tukio hili
 
Kwahiyo kwa busara zako ulimtaka abadili mwelekeo wa uandishi wa habari zake ulingane na Uhuru,Mzalendo,DailY/Sunday News+Habari Leo,Habari Corporation?The guy risked his life for you and me na walalahoi wengine,contrary to Benaziri who went back to Pakistan to serve the interests of her masters (US and UK).

Mlalahoi::: I THINK YOU HAVE A SRTONG POINT THERE!!!.."The guy risked his life for you and me na walalahoi wengine"", Au kuna mtu haoni hivyo??. Mungu awe nao wapone mapema.
 
Kubenea, tnakuombea upate nafuu hara upate kuendelea na kazi yako nzuri.

Hivi siku hizi majambazi wanatembea na acid na kuwamwagia watu usoni? Nionavyo mimi hawa sio majambazi bali ni watu ambao walitaka asiweze kufanya kazi yake ya uandishi tena maishani.
 
Kubenea, tnakuombea upate nafuu hara upate kuendelea na kazi yako nzuri.

Hivi siku hizi majambazi wanatembea na acid na kuwamwagia watu usoni? Nionavyo mimi hawa sio majambazi bali ni watu ambao walitaka asiweze kufanya kazi yake ya uandishi tena maishani.

Yes, Shaka
Kwa akili ya kawaida jambazi habebi acid, afu mbona hatujasikia wameiba computer.. na mali kadhaa?? This is out of ujambazi!
 
Naamini wanaotutaka tusiwahusishe mafisadi na tukio hili wanafanya hivyo aidha kwa uzembe wao wa kuunganisha dots,uchovu wa wikiendi au kuongeza idadi ya posts tu lakini mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kushindwa kusoma maandishi yaliyo ukutani kuhusiana na tukio hili

Mkuu Mlalahoi,

Heshima mbele mkuu, unajua siku zote ninazipa heshima sana posts zako humu, isipokuwa sijawahi kuona ukitumia mabavu kupitisha hoja, Yaaaani matusi mazito kama kuwaita wananchi wazembe, wachovu wa weekend, na wanaotaka kuongeza idadi za posts hapa,
kwa sababu tu ya kuuliza kistaarabu iwapo kuna ukweli kwamba serikali n CCM inahusika na huuu uvamizi?

Maandishi yaliyo ukutani mnayoyaona some of you ambayo sis wengine hatuyaoni yako wapi hayo mkuu? Ndimara ninamfahamu sana amekuwa mbunge wa upinzani kwamuda hakumwagiwa acid, Slaa mwenyewe hajamwagiwa acid, Zitto hajamwagiwa acid, sasa iweje leo imwagiwe kwa waandishi tu?

Mimi kama ni fisadi, ninammwagia acid Zitto/Slaa wenye evidence, au waandishi wa habari ambao wanasubiri habari toka kwa Zitto na Slaa? I mean kama ni acid unaimwaga kwa chanzo cha evidence na sio messengers kina Ndimara, hii ishu ni nzito sana mkuu ni lazima tuichukulie serious sana kabla ya kuhukumu bila ushahidi maana in the end mambo kama haya yanaweza kuwa na influence kubwa sana kwa maamuzi ya kesi hiyo ya mafisadi, maana tukumbuke kuwa bado kuna muda mkubwa na wa kutosha kulingana na sheria zetu kwa mafisadi kwenda mahakamani, sasa maneno yasikyokuwa na uhakika kama haya yanaweza kuwapa nguvu hawa, maana kama ni acid unaimwaga kwa chanzo cha evidence na sio kwa muandishi tu wa habari, maana pia tujue kuwa kuna hili gazeti kuharibu biashara za magazeti mengine kwa kutoa habari nzito sana na hivyo kuuza kwa wingi kuliko magazeti ya establishment, kama kuna fats zaidi ziwekwe hapa jamani sio mabavu!

Mlalahoi, you are too big for this mkuu!
 
Mimi sina ushahidi wa kuhusika kwa serikali ya CCM. Lakini kuna mifano mingi tu huko nyuma inayonipa sababu za kuwa na wasiwasi. Kuna mwanasheria mmoja aliuawa kijambazi na inasemekana huyu ndiye aliyekuwa mwanasheria wa rais mstaaafu. Mpaka leo wauaji wake hawajajulikana. Kuna ripoti zilizowahi kuandikwa magazetini juu ya urafiki wa waziri mkuu na wakuu wa majambazi Arusha---mmojawao ambaye alitolewa jela karibuni, inasemekana baada ya waziri mkuu kukutana na Jaji mkuu aliyeteuliwa katika mahakama ya rufaa. Sasa ukiongezea hii ya mwandishi habari, na hapa hatujasahau yaliyompata marehemu Amina Chifupa na bila kumtaja gavana wetu wa benki kuu, inaniwia vigumu kuwa na imani na serikali yetu ya CCM.
 
Nadhani kuharakisha na kusema CCM inahusika ni kutokuwajibika kwani standard ya ushahidi ni kubwa zaidi. Hata hivyo pia kusema kuwa waliotajwa kwenye ufisadi pia ni kuharakisha zaidi kwani unless kuna ushahidi wa aina fulani ni madai tu yasiyo na msingi.

Hata hivyo, kupuuzia kuwa kuvamiwa kwa Bw. Kubenea ni kitendo cha nasibu na ujambazi tu ni kuwa naive na kutokuelewa maji aliyokuwa amejaribu kuyaogolea. Kwa wale ambao tunafuatilia kazi za Kubenea tunatambua kuwa hii si mara ya kwanza kwa yeye kupatwa na ajali za ajabu kama hizi.

Tarehe 13/6/2007 (hii ilikuwa kabla ya orodha ya Ufisadi) alitumiwa ujumbe wa simu ambao uliweka wazi kuwa kuna watu hawafurahishwi na kazi yake ya "kutaja hata majina" kwenye habari za gazeti lake. Kumbukeni kuwa magazeti mengi yamekuwa yakitaja watu kwa mafumbo tu bila kuwataja wahusika wenyewe kwa hofu ya kufikishwa mahakamani. Gazeti la Mwanahalisi halikopeshi kijiko kinaitwa kijiko na sepetu inaitwa sepetu!

Huko nyuma utaona mahali ambapo Mtot wa Mkulima ameandika kidogo kuhusu Kubenea na Tegambwage na kuonesha matatizo anayoyaona katika maandishi ya watu hawa wawili na sitoshangaa baadhi ya watu wanahisia kama hizo pia. Soma Hapa mawazo ya Mtot wa Mkulima

Hata hivyo hilo halitoshi, Septemba 28, 2007 Gazeti la Tanzania Daima liliandika makala yenye kichwa cha habari "Mwanahalisi:"Tunatishwa" na ndani yake walisema hivi kuhusu vitisho dhidi ya gazeti hilo:
"Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Saed Kubenea, ilieleza kuwa kuna mienendo ya chinichini ya kusambaza vitisho kwa vyombo vya habari hususan MwanaHalisi, wachapishaji wake, wahariri, waandishi na wachangiaji wa makala na taarifa mbalimbali.

Hilo lilikuja baada ya gazeti hilo kuandika habari na kuweka hadharani majina ya waliotajwa kwenye ile orodha ya aibu ya ufisadi. Waweza kusoma makala nzima HAPA

Katika toleo la 63 la gazeti lake Said aliandika makala yenye kichwa cha habari "Watafuna nchi hawa hapa" na hapo wakayataja majina tena ya wale waliotajwa kwenye orodha ya ufisadi.

Lakini anayefikiria kuwa yawezekana kushambuliwa kwake ni sababu za kisiasa atakuwa amekosea. Said amewahi kuwavaa Waislamu katika makala yake ya "Waislamu wamelogwa na nani?" Katika makala hiyo ambapo alikuwa anajadili mahusiano ya Bakwata na Waislamu. Katika makala hiyo bila ya shaka Said amejijengea maadui wengine; wale ambao hawataki kuoneshwa makosa na mapungufu yao!

Hata hivyo huko nyuma mwaka 2003 Bw. Kubenea alijikuta kwenye makali ya watu wa Rai pale ilipodaiwa kuwa aliandika habari ya mahojiano yake na kiongozi mmoja wa CCM ambapo gazeti la Rai liliandika kuwa Kubenea alikutana na mwanasiasa huyo (Bw. Ngeze). Rai wakaamua kuandika habari ya kuomba msamaha kwa ngeze na wakaandika kuwa watamfikisha Kubenea kwenye baraza la Habari kwa ajili ya usuluhishi na yeye Kubenea pia aliamua kulifikisha Rai kwenye baraza hilo hasa baada ya kuona hakutendewa haki.

Naweza kuendelea kwa kirefu, lakini ninachoweza kusema ni kuwa kushambuliwa kwa Bw. Kubenea siyo kwa bahati mbaya na itakuwa ni naivette of the first class kufikiri hivyo. Kimoja ambacho ni dhahiri ni kuwa kumetokana na kazi yake ya uandishi.

Wahusika ni kina nani? Kwa vile nilivyoonesha hapo juu basi kukurupuka na kusema "fulani amehusika" ni kutojua kina cha tatizo na kutomtendea haki yeye KUbenea na wanaotajwa. Kama waliofanya hivyo ni watu wa serikali na serikali ni ya CCM basi kama vile watu walivyosema kuwa ATC ni serikali na chochote ATC inafanya basi serikali inawajibika basi siyo dhambi kuona CCM inahusika; Kama waliofanya hivyo ni watu binafsi kwa sababu zao binafsi ambazo hatuzijui basi wao wanahusika; kama waliofanya hivyo ni kikundi cha waislamu ambao hawakufurahishwa na Kubenea basi kikundi hicho kinahusika na kama ni baadhi ya vyombo vya habari au waandishi ambao hawafurahishwa na Kubenea basi wao nao wanahusishwa.

Vyovyote vile, kitendo cha Bw. Saed Kubenea kushambuliwa kina lengo malengo mawili makubwa. Moja ni kuinyamazisha sauti hii ya mabadiliko na kulitia hofu gazeti la Mwanahalisi na Mseto ili wafikiri mara mbili huko mbeleni na pili kuwapiga mkwara waandishi wowote wale ambao watakuwa na uthubutu wa kusema na kufanya kama anavyofanya Kubenea. Kama vile Ikulu ilivyosema leo kuwa kama kitendo hiki kilimlenga Bw. KUbenea kwa sababu ya kazi yake basi "kimerudisha nyuma" mafanikio ya vyombo huru vya habari.

Ni kwa sababu hiyo kama ilivyosema Ikulu leo, vyombo vya dola vitumie uwezo wake wote kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kinyama wanasakwa, wanatiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake. Kinyume cha hapo, ni kuendelea kuchora mstari ambao Bw. Kubenea anautambua kuwa yote ni matokeo ya "Mgongano wa mawazo". Ni yale ninayosema "mapambano ya kifikra"

Aluta Continua!
 
Quote:-

Naweza kuendelea kwa kirefu, lakini ninachoweza kusema ni kuwa kushambuliwa kwa Bw. Kubenea siyo kwa bahati mbaya na itakuwa ni naivette of the first class kufikiri hivyo. Kimoja ambacho ni dhahiri ni kuwa kumetokana na kazi yake ya uandishi. Wahusika ni kina nani? Kwa vile nilivyoonesha hapo juu basi kukurupuka na kusema "fulani amehusika" ni kutojua kina cha tatizo na kutomtendea haki yeye KUbenea na wanaotajwa.

Fair enough, tunamuombea mkuu Kubenea na wenziwe wapone haraka ili warudie kazi yao ya kutuaamusha wananchi!
 
IS HE STILL ALIVE?kama mzima basi arudi salama...
Mwanakjj article yake na waislam usichanganye ni Hii habari..kama hivyo ndivyo waislam wanaHaki zaid ya kumfanyia Mabaya MREMA kuliko Kubenena.MREMA kama makubwa ambayo hayatasahaulika dhidi ya waislam. lkn waislam hawakumfanyia baya zaid ya kumshitakia M/Mungu ampoke Mamlaka aliyompa...
MAFISADI wanaMTANDAO wao...pia kwa system za nchi zilivyokaa watu wana HALI mbaya za kiuchumu..ADUI anaweza organize group ya vijana walochoka wakakupiga mapanga na alie Engineer/plot hio asijulikane...
 
Yengele mtindo mmoja kama kawa, mie nipo interested na hali ya kiafya ya bwana mwandishi! tafadhali, mwenye nazo atufanyie uungwana.
 
Kwahiyo kwa busara zako ulimtaka abadili mwelekeo wa uandishi wa habari zake ulingane na Uhuru,Mzalendo,DailY/Sunday News+Habari Leo,Habari Corporation?The guy risked his life for you and me na walalahoi wengine,contrary to Benaziri who went back to Pakistan to serve the interests of her masters (US and UK).Alichofanya Kubenea hakina tofauti na ulichofanya wewe kutunong'oneza kwamba kuna mzungu ana access ya "siri za serikali ktk ubalozi wetu huko Holland"

Na kwa nyie waungwana mnao-doubt mafisadi kuhusishwa na tukuio hili mnapaswa kutambua kwamba wananyooshewa kidole kwa kuzingatia ushahidi wa kimazingira,na hilo si geni kwani hata "kwa hawa wenzetu wanaodai kuendesha mambo yao transparently" (nchi za Magharibi) matukio ya namna flani huhusishwa na watu flani kwa kuzingatia ushahidi wa kimazingira (mfano ni kifo cha Princess Diana).

Kwanini Mafisadi?Jibu jepesi ni kwamba gazeti la Mwanahalisi ndilo pekee lililotaja majina yao kama yalivyoorodheshwa na akina Slaa,ilhali magazeti mengine yooote yalikwepa kutaja majina hayo.Ni kwa sababu hiyo ndio maana mafisadi walitishia kulipeleka mahakamani kwa kashfa,kumbe mahakama yenyewe ni hii ya kifisadi na kinyama!!!Sishangai kwani kama wako tayari kuyaweka rehani maisha ya mamilioni ya Watanzania watashindwaje kutamani roho ya mwandishi mmoja wa habari.Wanachosahau ni kwamba ipo siku (hata kama itachukua karne ngapi) watapambana na hukumu yao,inshallah.

Naamini wanaotutaka tusiwahusishe mafisadi na tukio hili wanafanya hivyo aidha kwa uzembe wao wa kuunganisha dots,uchovu wa wikiendi au kuongeza idadi ya posts tu lakini mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kushindwa kusoma maandishi yaliyo ukutani kuhusiana na tukio hili


SAIDI KEBENEA tatizo lake siyo ku expose UBADHIRIFU bali tatizo lake ni njaa

Alienda kwa hao ambao kila kukicha anawaandika kwenye magazeti wakampa pesa za kumpooza mbona hakutoa kwenye gazeti kuwa alipewa RUSHWA?

Huyu mtu all of a sudden watu wanamwonea huruma lakini cha ajabu hakuna anyesema kuwa naye yuko kwenye payroll sema tatizo lake ni pale alipoambiwa apunguze eyey akaamua kuwa ataongeza kwa kisingizio hapati matangazo

walimtumia MSG kupitia gari lake hivyo yeye alishajua kuwa hana muda mrefu na zaidi angweka wazi kuwa hao wanaopinga CHANGES wanajaribu kumnyamazisha...akakaa kimya huku akiendelea kuvuta pesa sasa juzi kafarakana nao tena ndio yamemkuta haya na kusema ukweli jamaa hawataki kumwondoa kwani its not in anyone's interest kufanya hivyo

Nilimfananisha na Bhutto ambaye alijua nani wabaya wake lakini still akaamua kujiachia mpaka wakamwondoa kwa kesi ya SAIDI ni kuwa hawajataka kumwondoa lakini still ni nuisance kwa jamaa
 
Game,

Aaaahaaa, basi yawezekana jamaa anataka ku-commit suicide. Bhutto yake ilikuwa "suicide by suicide bomber," ya huyu jamaa itaitwa "suicide by mafisadi"......seriously, jamaa anaendeleaje kiafia huko 'spitalini??
 
Kwa kifupi unachosema GT ni kwamba huyu mwandishi amefanya kosa la kuelewana na mafisadi kwa kukubali fedha zao lakini akaendelea kuwaumbua gazetini. Am I right? And by the same token unaelekea kutoshtushwa na yaliyompata. Am I right again?
 
nilianza kuamini uandishi wa habari umevamiwa. lakini sasa napata mashaka kuhusu credibility ya huyu ndugu. Je kama kuna ukweli wa hilo Ndimara na yeye alikuwa anavuta hela? kwa nini na yeye kabamizwa sasa. habari inatisha hii kwa kweli. Mzee mkjj usijaribu kuvuta kidogodogo ndugu yangu, watakumwagia acid, ohhooo!
 
Back
Top Bottom