Mhariri Mtanzania: Kwa siasa za shari, CHADEMA kinajifuta; marehemu alikuwa akiifanyia kazi CHADEMA

Kuna maandishi ya bwana/bibi mmoja anaitwa 'ukwelimkweli' katika gazeti la raia mwema. Kuna kufanana sana kimaandishi kati yake na huyu kanjanja mzoefu, halimoja.
 
Mhariri huyu angekuwa hana uhusiano na Serikali, gazeti hili lingefungiwa kwa uchochezi. Kumbe MTZ akiwa chama cha upinzani ni halali kuchinjwa kama kuku? Hivi haki ya kuishi ni kwa Wana CCM tu?

Mhariri akumbuke kwamba upinzani umesaidia sana kufuchua ufisadi na rushwa iliyotamalaiki. Huyu mhariri anatakiwa awe shahidi Na. 1 katika kesi ya mauji ya Mwangosi. hata hivyo nina wasi wasi kama Muuaji anaweza kumleta kama shahidi.
Nina uahakika atakapouwa mke wake, kama anaye, ndipo atakapopata akili.
 
Tume huru zaidi ya hapo mazingaombwe.

Kuna tume iliyotajwa kwenye hii post uliyoijibu?

quote_icon.png
By zomba

Haki ya kufanyika mikutano ya "wapiganaji" wakachangishana halafu viongozi wakakopa kujengea majumba? hiyo ndio haki ya kuweza mtu kujiuwa? au siyo?
 
Kabla sijachangia hapa,ningependa kujuwa kama hili gazeti lina wasomaji wa kutosha bongo,kama linao,nitachangia kuhusu mada iliyoko kwenye bandiko hili.

Kama sivyo,sitoweza kufanya hivyo,sababu ni kwamba hata mimi kuna magazeti nilikuwa siyasomi kwasababu ya mwelekeo wa kifisadi.Wenye kufahama tafadhali tujulishane.Natanguliza shukran.

Kwa kweli hili ni gazeti lisilo na wateja kama lile la uhuru.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
..Atawalaye kwa upanga, hakika atakufa kwa upanga.
Napata shaka na udadafuzi wako mkuu, hivi umeelewa alichokuwa anakieleza mkuu uliyemjibu hoja yake au umekurupuka tu just because you have to write on this topic? muwe mnasoma na kuelewa jamani ebo, mkuu kasema wapenzi wa CHADEMA humu JF kama ilivyo ada kwao wanaamini matusi, fujo, kejeli na dharau katika kujenga hoja zao ambazo kimsingi ni hoja za nguvu na za kibabe, badala yake wanaacha kutumia nguvu ya hoja katika mijadala kama hii ambayo ndio tamaduni yetu wanamapinduzi wa kweli.

Rai yangu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wa chadema, mnapoona hoja imewekwa mezani basi mtoe michango yenye tija kuliko kutuandikia vitu ambavyo vimeshazoeleka ili at least tuone kama chadema inawanachama hai maana hizo fujo na matusi mnazotumia hamna tofauti na mateja.
 
Haki ya kufanyika mikutano ya "wapiganaji" wakachangishana halafu viongozi wakakopakujengea ndhaki ya kuweza mtu kujiuwa? au siyo?

CCM ndio tabia viongozi wenu. CDM wananchi wanajua wanafanya kazi ndio maana wanachangia shughuli zao za kisiasa. Wameaminiwa na wanaendelea. Hata mkilia machozi ya mamba hakuns
tena wa kusikiliza .
 
JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:05 NA YUSUF HALIMOJA, DAR ES SALAAM

HAPANA shaka wasomaji wa gazeti la Mtanzania Jumapili watakumbuka kwamba Jumapili iliyopita niliandika makala iliyosomeka “CHADEMA na ndoto ya nchi isiyotawalika.”

Baada ya hapo waandishi wawili wa kampuni inayochapisha gazeti hili walipokea simu kutoka kwa vijana wanaoaminiwa kuwa ni wanachama wa Chadema. Katika simu yao vijana hao walidai kuwa kama wangejua napatikana wapi wangenifuata wanipige kofi! Sababu? Naichafua Chadema!

Hakuna asiyejua kuwa Chadema ni chama kinachotaka kipewe sifa nzuri wakati wote hata inapofanya vibaya. Nichukue nafasi hii kuwahakikishia vijana wa Chadema kwamba hawawezi kunitisha kwa sababu hata viongozi wao, Mbowe na Slaa, hawakufanikiwa kunitisha.

Ni kweli walijitahidi kunitia mfukoni kama walivyowatia mfukoni watumishi wengine wa Chadema, kwangu walikwama. Maana huwezi kufanya kazi Chadema kwa furaha kama hukubali kutiwa mfukoni na viongozi wa chama hicho.

Kwa hiyo nawataka vijana wa Chadema na mashabiki wa chama hicho wafahamu kuwa naiandama Chadema kwa sababu naijua vizuri kuliko wanavyojua wao. Chadema si chama cha kushabikia.

Niwaarifu tu vijana wa Chadema kwamba nilikuwa mtumishi wa Chadema miezi sita Makao Makuu ya Chadema. Sikuwahi kuomba kazi yoyote ya Chadema lakini ni viongozi wenyewe wa Chadema walionitafuta. Moja kwa moja nikaajiriwa kuwa mkufunzi wa mafunzo ya siasa.

Binafsi wakati wote sikukubaliana na uongozi wa kidikteta wa Mbowe na Slaa. Kwa mfano, watumishi wote wa chama Makao Makuu tulitarajiwa tusishirikiane na Chacha Wangwe. Lakini nilishirikiana na Chacha Wangwe kwa wazi.

Na watumishi wote wa Makao Makuu ya Chadema wanajua kuwa nilichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa Chacha Wangwe katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti. Mbowe na Slaa hawakumtaka Chacha Wangwe. Lakini mimi nilimtaka. Nikawashinda. Wakati wangu demokrasia ilishinda udikteta.

Kama ninachosema ni uzushi basi wanachama na mashabiki wa Chadema nchini kote wasubiri kuona kuwa Mbowe na Slaa watakanusha nilichosema. Chadema nilikuwa kiboko cha Mbowe na Slaa. Nilipambana na udikteta wao bila kuchoka. Wenyewe ni mashahidi.

Chadema kinaendeshwa kwa matakwa ya Mbowe na Slaa na wala si kwa matakwa ya Kamati Kuu ya Chadema au Baraza Kuu. Wanachoamua Mbowe na Slaa lazima kitakuwa. Chadema ni watu wawili: Mbowe na Slaa. Hii ni kusema kwamba watu hawa wawili wakipewa nchi wataiendesha kwa matakwa yao. Si kwa matakwa ya wananchi. Mashabiki wa Chadema wajue hivyo na Watanzania wajue hivyo.

Kwa vyovyote mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei, alitaka chama kiendeshwe kidemokrasia. Kinyume chake kinaendeshwa kidikteta. Matakwa ya Mbowe na Slaa yamegeuzwa kuwa matakwa ya chama.

Binafsi siamini kwamba wanachama wa Chadema – wenye akili timamu wanataka chama chao kiendeshwe kwa shari. Ukombozi wa Watanzania unaodaiwa kushughulikiwa na Chadema hautaletwa na siasa za shari.

Viongozi wa Chadema hawawezi kutuaminisha kuwa utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni mbaya zaidi kuliko ulivyokuwa utawala wa Mwingereza hata wapambane na CCM na serikali yake kwa shari.

Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere aliona mbali. Akajua kuwa TANU isingeweza kukomboa Tanganyika kwa siasa za shari. Kwa hiyo Nyerere alihubiri kutafuta ukombozi kwa kutumia silaha ya umoja na amani. Mbowe na Slaa wanahubiri kutafuta ukombozi wa Tanzania kwa kutumia silaha ya umoja na shari.

Kwa hiyo watu wenye akili timamu wanajiweka kando. Wanajua kuwa Mbowe na Slaa wanaipeleka nchi pabaya. Yote hayo ni matokeo ya tamaa ya kuingia Ikulu. Basi wakati TANU haikumwaga damu katika ukombozi wa Tanganyika Chadema inamwaga damu katika ‘ukombozi wa Tanzania’.

Katika makala yangu ya Jumapili iliyopita niliandika kwamba Chadema isifanye mambo kama vile tayari ni serikali. Isikae hapa kuwaamuru viongozi wa polisi na wa serikali kwa jumla watimize matakwa ya Chadema. Eti bila hivyo nchi itashika moto!

Chadema siyo serikali ya pili ya Tanzania Chadema ni chama tu cha siasa ambacho tunakishuhudia kikijifuta chenyewe kutokana na siasa zake za shari.

Wasichojua viongozi wa Chadema ni kwamba Watanzania ni wapenda amani. Ndiyo maana nchi yao ikaitwa “Kisiwa cha amani”.

Lakini kwa sababu wanafundisha vijana wao wachangamkie siasa za shari na wanachangamkia basi viongozi wa Chadema wanaona kwamba siasa za shari ndizo zinazotakiwa na Watanzania. Si kweli. Watanzania wanataka siasa za amani.

Hakuna anayekataa madai kwamba polisi wamehusika na mauaji katika maandamano ya Chadema sehemu mbalimbali za nchi hii. Lakini lazima tuseme kweli bila kumwogopa mtu yeyote wa Chadema. Hayo yote yamekuwa matokeo ya siasa za shari zinazoendeshwa na Chadema.

Ni kweli maandamano ni haki mojawapo ya raia wa Tanzania. Lakini maandamano yasiendeshwe kwa shari kwa sababu tu kila mtu ana haki ya kufanya maandamano. Polisi wakiwa na sababu ya msingi ya kukataza maandamano basi busara itumike. Mbowe na Slaa wasing’ang’anie maandamano kwa lengo tu la kutimiza siasa zao za shari. Hakuna Rais wa Tanzania aliyekwenda Ikulu kwa shari.

Kwa jumla wapenda amani wa Tanzania wameshangazwa kusikia kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, anabanwa eti kwa kutamka kwamba anaweza kuifuta Chadema ikiendelea kuendesha siasa za shari. Nani anataka siasa za shari? Chadema kiendelee na siasa za shari lakini kisifutwe? Kivumiliwe tu! Eti hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Ni demokrasia iliyochimbuka nchi gani?

Ni ukweli usiopingika kwamba karibu mauaji yote yaliyotokea katika maandamano ya Chadema yametokana na ukaidi na uchochezi wa viongozi wa Chadema.

Cha ajabu na tunachoshuhudia sasa ni kulaumiwa Jeshi la Polisi tu kuhusu mauaji hyo huku watu wa Chadema wakishiriki katika kulaumu bila kuona aibu.

Hii ni bahati mbaya kwamba watu wanashughulika na matokeo badala ya kushughulika na chanzo. Msajili wa Vyama vya Siasa ni miongoni ma watu wachache wanaoshughulika na chanzo. Chanzo cha vurugu zote na mauaji katika Tanzania yetu ya leo ni tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

Mbele ya Chadema uvunjaji wa sheria ndiyo demokrasia. Chukua, kwa mfano, mauaji yaliyotokea Arusha baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Baada ya uchaguzi ule Chadema walilazimisha kufanya maandamano kupitia kwenye njia ambazo Jeshi la Polisi liliwazuia kuzitumia. Wao wakazitumia. Na walipotakiwa kuacha maandamano hayo waliendelea na kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu. Wakafa watu watatu. Waliosababisha vifo hivyo si polisi waliolinda sheria bali ni viongozi wa Chadema walioleta ukaidi. Tuwe wakweli.

Kule Morogoro siku ya pili tu ya sensa Chadema iliitisha maandamano kinyume cha maagizo ya polisi. Katika vurugu zilizotokea wakati polisi walipoingilia kati maandamano hayo aliuawa Ally Singano. Hayo, tena, yalikuwa matokeo ya Chadema kuleta ukaidi mbele ya Jeshi la Polisi.

Hata kule Iringa ni Chadema iliyosababisha kifo cha Daudi Mwangosi. Siyo polisi. Ni matokeo mengine ya tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

Kwa bahati mbaya katika vurugu zinazosababishwa na Chadema viongozi wa Chadema hawakamatwi. Sasa wananchi wamefika mahali ambako wanaulizana kuna maelewano gani kati ya uongozi wa juu wa polisi na uongozi wa juu wa Chadema? Mbona polisi wanapambana na wanaoshiriki vurugu huku wakiwaacha bila kuwagusa wanaochochea au wanaoongoza vurugu hizo?

Kinachoonekana hapa ni ukweli kwamba vurugu za Chadema ni kukaidi kwa chama hicho amri ya polisi kunatokana na jeshi hilo kuidekeza Chadema. Hali hiyo ndiyo imefikisha Tanzania mahali pabaya.

Viongozi wa Chadema ni wanasiasa uchwara. Hawajui siasa. Siasa haiendeshwi kwa mabavu wala kwa shari.

Tazama! Kule Iringa Slaa alimpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi akisema, “IGP nasubiri simu yako, wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha na mabomu ya kutosha.”

Huo ulikuwa ujumbe wa Slaa kwa Mkuu wa Polisi nchini katika kuihakikishia polisi kwamba haina ubavu wa kuizuia Chadema kufanya inachotaka. Kwa siasa hizi za shari kwa nini Chadema kisifutwe?

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza tishio la kuitisha maandamano nchi nzima ya kupinga mauaji ya Mwangosi na wananchi wasio na hatia wakati wapenda amani wanajua kuwa mauaji hayo yanasababishwa na Chadema kukaidi amri ya polisi.

Kwa hivyo maandamano kama hayo yalipaswa yaitishwe na CCM nchi nzima kupinga uvunjifu wa amani unaotokana na ukaidi wa Chadema. Kwa nini CCM isifanye hivyo?

Mbele ya viongozi wa Chadema kila mtu ni mbaya isipokuwa wao!

Wanataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ajiuzulu. Na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Na Mkuu wa Operesheni ya Mafunzo. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa. Na wananchi waisusie TBC kwa madai kuwa inapendelea CCM! Ipendelee Chadema.

Halafu imedaiwa Rais Kikwete akishindwa kuwawajibisha viongozi hao basi nchi nzima itaandamana kwa ghafla – maandamano ambayo Mbowe anadai polisi itashindwa kuyazima. Halafu kifuate nini? Uvunjifu wa amani nchi nzima. Kwa manufaa ya nani? Jibu wanalo wasomaji.

Ukitaka kusema kweli tayari wananchi wa kawaida wamewekwa roho juu. Hawajui kitakachotokea mwaka 2015.

Tazama! Hali hii mbaya inatokea wakati CCM ipo kimya. Chadema inapambana na serikali. Je, mapambano ya Chadema na CCM yatakuwaje mwaka 2015. Na ndoto ya Chadema ya kuingia Ikulu ikipotea itakuwaje?

Chadema wanataka tume huru iundwe kuchunguza mauaji mbalimbali nchini yaliyohusisha shughuli za Chadema. Si kitu kibaya. Lakini ni vema tume kama hiyo ikianza kuchunguza kifo cha utata cha Chacha Wangwe ambacho viongozi wa Chadema hawakusikika wakidai kiundiwe tume.

Mwisho, kwa ndugu zangu wanahabari. Jumapili iliyopita niliandika kwamba ni vema wanahabari wajitazame upya ili mbele ya serikali na umma wasionekane kwamba wao na Chadema ni kitu kimoja au wanaitumika Chadema. Najua wengine hawakunielewa.

Nitatoa mfano hai.

Mkuu wa Operesheni ya Chadema inayodaiwa kuwa ni ya Vuguvugu la Mabadiliko, Benson Kigaila amesema kwamba kabla marehemu Mwangosi hajauawa alimwambia Kigaila kuwa alikuwa na wasiwasi juu ya uhalali wa askari waliokuwa katika operesheni ya kuwadhibiti wafuasi wa Chadema.

“Marehemu mwangosi aliniambia ana shaka na askari waliopo eneo hilo na alikuwa ameniahidi kwamba atanionyesha picha za askari asiowafahamu,” amesema Kigaila.

Baada ya hapo Mwangosi aliwafuata polisi.

Hapa inaleta picha kwamba marehemu alikuwa akiifanyia kazi Chadema. Na askari walimwona. Kwa hiyo askari mmojawao alipojaribu kumwokoa Mwangosi akisema kwamba anamjua kuwa ni mwandishi wa habari haikusaidia kitu.
Polisi wengine walimwona kuwa ni mfuasi wa Chadema chama wanachopambana nacho.

Jukwaa la Wahariri litafakari hayo.

Hakuna kiumbe mwenye haki ya kuchukua uhai wa mtu mwingine,huu ni uchizi na ulevi wa madaraka.
Hakuna mwenye akili timamu anaweza kuungana na wewe,
Chadema haina jeshi wala polisi au polisi ni wanachama wa Chadema?Waandish kama wewe Rwanda walinyongwa baada ya Mauaji ya Kimbali.Kuwa makini unaweza usijue utafia wapi kama viongozi wengi waafrika wa sasa.
Huwezi zuia mabadiliko.
 
JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:05 NA YUSUF HALIMOJA, DAR ES SALAAM

HAPANA shaka wasomaji wa gazeti la Mtanzania Jumapili watakumbuka kwamba Jumapili iliyopita niliandika makala iliyosomeka "CHADEMA na ndoto ya nchi isiyotawalika."

Baada ya hapo waandishi wawili wa kampuni inayochapisha gazeti hili walipokea simu kutoka kwa vijana wanaoaminiwa kuwa ni wanachama wa Chadema. Katika simu yao vijana hao walidai kuwa kama wangejua napatikana wapi wangenifuata wanipige kofi! Sababu? Naichafua Chadema!

Hakuna asiyejua kuwa Chadema ni chama kinachotaka kipewe sifa nzuri wakati wote hata inapofanya vibaya. Nichukue nafasi hii kuwahakikishia vijana wa Chadema kwamba hawawezi kunitisha kwa sababu hata viongozi wao, Mbowe na Slaa, hawakufanikiwa kunitisha.

Ni kweli walijitahidi kunitia mfukoni kama walivyowatia mfukoni watumishi wengine wa Chadema, kwangu walikwama. Maana huwezi kufanya kazi Chadema kwa furaha kama hukubali kutiwa mfukoni na viongozi wa chama hicho.

Kwa hiyo nawataka vijana wa Chadema na mashabiki wa chama hicho wafahamu kuwa naiandama Chadema kwa sababu naijua vizuri kuliko wanavyojua wao. Chadema si chama cha kushabikia.

Niwaarifu tu vijana wa Chadema kwamba nilikuwa mtumishi wa Chadema miezi sita Makao Makuu ya Chadema. Sikuwahi kuomba kazi yoyote ya Chadema lakini ni viongozi wenyewe wa Chadema walionitafuta. Moja kwa moja nikaajiriwa kuwa mkufunzi wa mafunzo ya siasa.

Binafsi wakati wote sikukubaliana na uongozi wa kidikteta wa Mbowe na Slaa. Kwa mfano, watumishi wote wa chama Makao Makuu tulitarajiwa tusishirikiane na Chacha Wangwe. Lakini nilishirikiana na Chacha Wangwe kwa wazi.

Na watumishi wote wa Makao Makuu ya Chadema wanajua kuwa nilichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa Chacha Wangwe katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti. Mbowe na Slaa hawakumtaka Chacha Wangwe. Lakini mimi nilimtaka. Nikawashinda. Wakati wangu demokrasia ilishinda udikteta.

Kama ninachosema ni uzushi basi wanachama na mashabiki wa Chadema nchini kote wasubiri kuona kuwa Mbowe na Slaa watakanusha nilichosema. Chadema nilikuwa kiboko cha Mbowe na Slaa. Nilipambana na udikteta wao bila kuchoka. Wenyewe ni mashahidi.

Chadema kinaendeshwa kwa matakwa ya Mbowe na Slaa na wala si kwa matakwa ya Kamati Kuu ya Chadema au Baraza Kuu. Wanachoamua Mbowe na Slaa lazima kitakuwa. Chadema ni watu wawili: Mbowe na Slaa. Hii ni kusema kwamba watu hawa wawili wakipewa nchi wataiendesha kwa matakwa yao. Si kwa matakwa ya wananchi. Mashabiki wa Chadema wajue hivyo na Watanzania wajue hivyo.

Kwa vyovyote mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei, alitaka chama kiendeshwe kidemokrasia. Kinyume chake kinaendeshwa kidikteta. Matakwa ya Mbowe na Slaa yamegeuzwa kuwa matakwa ya chama.

Binafsi siamini kwamba wanachama wa Chadema – wenye akili timamu wanataka chama chao kiendeshwe kwa shari. Ukombozi wa Watanzania unaodaiwa kushughulikiwa na Chadema hautaletwa na siasa za shari.

Viongozi wa Chadema hawawezi kutuaminisha kuwa utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni mbaya zaidi kuliko ulivyokuwa utawala wa Mwingereza hata wapambane na CCM na serikali yake kwa shari.

Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere aliona mbali. Akajua kuwa TANU isingeweza kukomboa Tanganyika kwa siasa za shari. Kwa hiyo Nyerere alihubiri kutafuta ukombozi kwa kutumia silaha ya umoja na amani. Mbowe na Slaa wanahubiri kutafuta ukombozi wa Tanzania kwa kutumia silaha ya umoja na shari.

Kwa hiyo watu wenye akili timamu wanajiweka kando. Wanajua kuwa Mbowe na Slaa wanaipeleka nchi pabaya. Yote hayo ni matokeo ya tamaa ya kuingia Ikulu. Basi wakati TANU haikumwaga damu katika ukombozi wa Tanganyika Chadema inamwaga damu katika ‘ukombozi wa Tanzania'.

Katika makala yangu ya Jumapili iliyopita niliandika kwamba Chadema isifanye mambo kama vile tayari ni serikali. Isikae hapa kuwaamuru viongozi wa polisi na wa serikali kwa jumla watimize matakwa ya Chadema. Eti bila hivyo nchi itashika moto!

Chadema siyo serikali ya pili ya Tanzania Chadema ni chama tu cha siasa ambacho tunakishuhudia kikijifuta chenyewe kutokana na siasa zake za shari.

Wasichojua viongozi wa Chadema ni kwamba Watanzania ni wapenda amani. Ndiyo maana nchi yao ikaitwa "Kisiwa cha amani".

Lakini kwa sababu wanafundisha vijana wao wachangamkie siasa za shari na wanachangamkia basi viongozi wa Chadema wanaona kwamba siasa za shari ndizo zinazotakiwa na Watanzania. Si kweli. Watanzania wanataka siasa za amani.

Hakuna anayekataa madai kwamba polisi wamehusika na mauaji katika maandamano ya Chadema sehemu mbalimbali za nchi hii. Lakini lazima tuseme kweli bila kumwogopa mtu yeyote wa Chadema. Hayo yote yamekuwa matokeo ya siasa za shari zinazoendeshwa na Chadema.

Ni kweli maandamano ni haki mojawapo ya raia wa Tanzania. Lakini maandamano yasiendeshwe kwa shari kwa sababu tu kila mtu ana haki ya kufanya maandamano. Polisi wakiwa na sababu ya msingi ya kukataza maandamano basi busara itumike. Mbowe na Slaa wasing'ang'anie maandamano kwa lengo tu la kutimiza siasa zao za shari. Hakuna Rais wa Tanzania aliyekwenda Ikulu kwa shari.

Kwa jumla wapenda amani wa Tanzania wameshangazwa kusikia kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, anabanwa eti kwa kutamka kwamba anaweza kuifuta Chadema ikiendelea kuendesha siasa za shari. Nani anataka siasa za shari? Chadema kiendelee na siasa za shari lakini kisifutwe? Kivumiliwe tu! Eti hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Ni demokrasia iliyochimbuka nchi gani?

Ni ukweli usiopingika kwamba karibu mauaji yote yaliyotokea katika maandamano ya Chadema yametokana na ukaidi na uchochezi wa viongozi wa Chadema.

Cha ajabu na tunachoshuhudia sasa ni kulaumiwa Jeshi la Polisi tu kuhusu mauaji hyo huku watu wa Chadema wakishiriki katika kulaumu bila kuona aibu.

Hii ni bahati mbaya kwamba watu wanashughulika na matokeo badala ya kushughulika na chanzo. Msajili wa Vyama vya Siasa ni miongoni ma watu wachache wanaoshughulika na chanzo. Chanzo cha vurugu zote na mauaji katika Tanzania yetu ya leo ni tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

Mbele ya Chadema uvunjaji wa sheria ndiyo demokrasia. Chukua, kwa mfano, mauaji yaliyotokea Arusha baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Baada ya uchaguzi ule Chadema walilazimisha kufanya maandamano kupitia kwenye njia ambazo Jeshi la Polisi liliwazuia kuzitumia. Wao wakazitumia. Na walipotakiwa kuacha maandamano hayo waliendelea na kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu. Wakafa watu watatu. Waliosababisha vifo hivyo si polisi waliolinda sheria bali ni viongozi wa Chadema walioleta ukaidi. Tuwe wakweli.

Kule Morogoro siku ya pili tu ya sensa Chadema iliitisha maandamano kinyume cha maagizo ya polisi. Katika vurugu zilizotokea wakati polisi walipoingilia kati maandamano hayo aliuawa Ally Singano. Hayo, tena, yalikuwa matokeo ya Chadema kuleta ukaidi mbele ya Jeshi la Polisi.

Hata kule Iringa ni Chadema iliyosababisha kifo cha Daudi Mwangosi. Siyo polisi. Ni matokeo mengine ya tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

Kwa bahati mbaya katika vurugu zinazosababishwa na Chadema viongozi wa Chadema hawakamatwi. Sasa wananchi wamefika mahali ambako wanaulizana kuna maelewano gani kati ya uongozi wa juu wa polisi na uongozi wa juu wa Chadema? Mbona polisi wanapambana na wanaoshiriki vurugu huku wakiwaacha bila kuwagusa wanaochochea au wanaoongoza vurugu hizo?

Kinachoonekana hapa ni ukweli kwamba vurugu za Chadema ni kukaidi kwa chama hicho amri ya polisi kunatokana na jeshi hilo kuidekeza Chadema. Hali hiyo ndiyo imefikisha Tanzania mahali pabaya.

Viongozi wa Chadema ni wanasiasa uchwara. Hawajui siasa. Siasa haiendeshwi kwa mabavu wala kwa shari.

Tazama! Kule Iringa Slaa alimpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi akisema, "IGP nasubiri simu yako, wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha na mabomu ya kutosha."

Huo ulikuwa ujumbe wa Slaa kwa Mkuu wa Polisi nchini katika kuihakikishia polisi kwamba haina ubavu wa kuizuia Chadema kufanya inachotaka. Kwa siasa hizi za shari kwa nini Chadema kisifutwe?

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza tishio la kuitisha maandamano nchi nzima ya kupinga mauaji ya Mwangosi na wananchi wasio na hatia wakati wapenda amani wanajua kuwa mauaji hayo yanasababishwa na Chadema kukaidi amri ya polisi.

Kwa hivyo maandamano kama hayo yalipaswa yaitishwe na CCM nchi nzima kupinga uvunjifu wa amani unaotokana na ukaidi wa Chadema. Kwa nini CCM isifanye hivyo?

Mbele ya viongozi wa Chadema kila mtu ni mbaya isipokuwa wao!

Wanataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ajiuzulu. Na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Na Mkuu wa Operesheni ya Mafunzo. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa. Na wananchi waisusie TBC kwa madai kuwa inapendelea CCM! Ipendelee Chadema.

Halafu imedaiwa Rais Kikwete akishindwa kuwawajibisha viongozi hao basi nchi nzima itaandamana kwa ghafla – maandamano ambayo Mbowe anadai polisi itashindwa kuyazima. Halafu kifuate nini? Uvunjifu wa amani nchi nzima. Kwa manufaa ya nani? Jibu wanalo wasomaji.

Ukitaka kusema kweli tayari wananchi wa kawaida wamewekwa roho juu. Hawajui kitakachotokea mwaka 2015.

Tazama! Hali hii mbaya inatokea wakati CCM ipo kimya. Chadema inapambana na serikali. Je, mapambano ya Chadema na CCM yatakuwaje mwaka 2015. Na ndoto ya Chadema ya kuingia Ikulu ikipotea itakuwaje?

Chadema wanataka tume huru iundwe kuchunguza mauaji mbalimbali nchini yaliyohusisha shughuli za Chadema. Si kitu kibaya. Lakini ni vema tume kama hiyo ikianza kuchunguza kifo cha utata cha Chacha Wangwe ambacho viongozi wa Chadema hawakusikika wakidai kiundiwe tume.

Mwisho, kwa ndugu zangu wanahabari. Jumapili iliyopita niliandika kwamba ni vema wanahabari wajitazame upya ili mbele ya serikali na umma wasionekane kwamba wao na Chadema ni kitu kimoja au wanaitumika Chadema. Najua wengine hawakunielewa.

Nitatoa mfano hai.

Mkuu wa Operesheni ya Chadema inayodaiwa kuwa ni ya Vuguvugu la Mabadiliko, Benson Kigaila amesema kwamba kabla marehemu Mwangosi hajauawa alimwambia Kigaila kuwa alikuwa na wasiwasi juu ya uhalali wa askari waliokuwa katika operesheni ya kuwadhibiti wafuasi wa Chadema.

"Marehemu mwangosi aliniambia ana shaka na askari waliopo eneo hilo na alikuwa ameniahidi kwamba atanionyesha picha za askari asiowafahamu," amesema Kigaila.

Baada ya hapo Mwangosi aliwafuata polisi.

Hapa inaleta picha kwamba marehemu alikuwa akiifanyia kazi Chadema. Na askari walimwona. Kwa hiyo askari mmojawao alipojaribu kumwokoa Mwangosi akisema kwamba anamjua kuwa ni mwandishi wa habari haikusaidia kitu. Polisi wengine walimwona kuwa ni mfuasi wa Chadema chama wanachopambana nacho.

Jukwaa la Wahariri litafakari hayo.

Sishangai Yusufu najua huo ndio msimamo wa chama-CCM_B,Lazima tukubaliane pia mauaji ya waandamanaji yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 yalifanywa na CCM_B..........NDIO!Ukiwa mpinzani tu we ndio muuaji.
 
Napata shaka na udadafuzi wako mkuu, hivi umeelewa alichokuwa anakieleza mkuu uliyemjibu hoja yake au umekurupuka tu just because you have to write on this topic? muwe mnasoma na kuelewa jamani ebo, mkuu kasema wapenzi wa CHADEMA humu JF kama ilivyo ada kwao wanaamini matusi, fujo, kejeli na dharau katika kujenga hoja zao ambazo kimsingi ni hoja za nguvu na za kibabe, badala yake wanaacha kutumia nguvu ya hoja katika mijadala kama hii ambayo ndio tamaduni yetu wanamapinduzi wa kweli.

Rai yangu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wa chadema, mnapoona hoja imewekwa mezani basi mtoe michango yenye tija kuliko kutuandikia vitu ambavyo vimeshazoeleka ili at least tuone kama chadema inawanachama hai maana hizo fujo na matusi mnazotumia hamna tofauti na mateja.

Huyo niliyemjibu aliandika yafuatayo...

"By KIBE tatizo moja la chadema kuambiwa ukweli hawataki..wakiambiwa ukweli wanatoa matusi tu....umewekewa hoja mezani jadili hoja jibu hoja mleta hoja katoa na sababu zake wewe kama unapinga njo na sababu za kupinga hoja.... Yani liko wazi chadema bado ni chama cha kukurupuka.... Wanaleta fujo tu huku wakizani ndo njia ya kuingia ikulu..... Pokeeni ushauri acheni jazba na matusi"

Na mimi ndio nikamjibu. Ukiangalia vyema, utaona mwishoni mwa maandishi yake anasema kuwa ... "Yani liko wazi chadema bado ni chama cha kukurupuka.... Wanaleta fujo tu huku wakizani ndo njia ya kuingia ikulu..... Pokeeni ushauri acheni jazba na matusi"

Umesoma hapo ??? Anamaanisha kuwa Chadema ni Chama cha fujo tu. Umesoma hapo ??
Ndio nikamkumbusha kuwa hizo fujo anazosema ni Chadema kufungua matawi kule Iringa!!! Umesoma hapo juu???
Yaani kwa lugha rahisi kabisa, huyo KIBE anaunga mkono polisi kumuua Mwangosi kwa sababu ya 'fujo' za Chadema wakati wanafungua matawi !!! Umeelewa hapo ???

Sasa hata wewe hapo kwenye blue umesema kama KIBE alivyosema kuwa Chadema wana 'fujo'.
Au labda sijawaelewa sawasawa ?? Kwenu ninyi, Chadema kufungua matawi kule Iringa ni 'FUJO' !!!
Ndio maana mkawaagiza polisi kumuuwa Mwangosi ili kuichafua Chadema !!!
 
Kuna tume iliyotajwa kwenye hii post uliyoijibu?

Hujitambui,vifo vilivyotokea pana kukwepa ukweli kwa hiyo kuondoa kunyosheana vidole suluhu yake ni TUME HURU.Ili wale wote walohusika hatua kazi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.Weye yaelekea hujui nini mana ya TUME HURU?Ili kukuweka sawa we jembe bila mpini, ni kwamba penye mashaka kama haya mauaji Rais akiunda tume ujue maamuzi yake yana sheria timilifu.Joto la nn ili hali hujausika na vifo hivyo?
 
Wacha niachane Na Upuuzi ulioandikwa na huyo Mhariri yenye mlengo wa MwangoSi alistAhili kupigwa Bomu.

Kingine its Obvious Mhariri ana Conflict of IntereSt na Viongozi wa Chadema (Slaa+Mbowe).
Kwa sabAbu alikuwa kAmbI ya Upinzani ndani ya Chadema (Wangwe)

So,Kwa mtu anayejua kazi ya Ubongo,Kwa yeyoye AnayetAkA 'Negative news' kuhuSu Chadema na Viongozi wake atamuonA huyO BwAna.

Lakini,tutambue ivi vichache

1. KilA BinadamU AnA Haki ya Kuishi.
2. Kuandamana pasipo Kibali/Ruhusu ni Kinyume cha Sheria na kuna Adhabu zake basi Serikali ikufanye zile Fine zake kuongeza Pato lao kAma kweli inaweza kusimAmia sheria.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kweli kama huyu ni mhariri kazi ipo huyu asiyejua hatakutazama na kuona tofauti.......... hawa ndio wale ambao JK aliwaita makanjanja............
 
gazeti lilinunuliwa kwa sababu ya kupandikiza viongozi wasio na sifa tusishangae kuona likiponda ukweli, ccm iandamane kujipinga huyu si mhariri ni mwehu na mtu ambae atanunua gazeti lake atakuwa na matatizo, vibaraka wapo kila sehemu hii ni aibu kwa tasinia ya habari,
 
duh kwa hyo kama mwakosi alikuwa akfanya kaz na chadema ni haki kuuwawa? Mambo ya chacha wangwe c upeleke ushaidi polc ili wahuska wakamatwe! Shenz kabsa...ur totaly fraud!....
 
duh kwa hyo kama mwakosi alikuwa akfanya kaz na chadema ni haki kuuwawa? Mambo ya chacha wangwe c upeleke ushaidi polc ili wahuska wakamatwe! Shenz kabsa...ur totaly fraud!....we jamaa unachekesha nibora ao wenye shar kuliko awa wauwaj na mafsadi, unataka mbowe na slaa wakujbu ili upate umaarufu?...
 
Back
Top Bottom