denoo49
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 6,113
- 6,937
Kama watu watakumbuka vizuri kama kweli wana JF ni watu waliosoma vitabu huwezi msahau Yusph Halimoja, ni mwandishi mahili na wa siku nyingi na ndo mwandishi wa makala hii tunayojadili.
Kwenye makala hii sioni tatizo, mwenzetu kaleta mada ya kujadili ikiwa na observation zake, hebu kama watu huku ndani ni wasomi wenye uelewa wa mambo hebu jadili kipengele kimoja kimoja ukipinga au kuunga mkono hoja.
Ukisoma post nyingi hapa zilizokwisha za kupinga hapa zinakosa mashiko kwa sababu hatuna data za kutufanya tupinge hoja hii, mana wanasema ''kama huna data huna haki ya kuongea''
Tusipende kutumia insictinct kwenye hoja ambazo zinahitaji tuwe na majibu sahihi yaliyofanyiwa tafiti, majibu yanayokuja hapa ni dhahiri mwandishi yuko sahihi mana mifano tunaiona hapa, badala ya kujibu hoja wengine wanatukana, tena matusi mabaya, kwa nini tusiamini haya yanayozumzwa na mwandishi.
Wana jf tujifunze kujenga hoja na siyo kutumia matusi katika hoja
heri we uliyemsupporrt kihoja japo upofu wako wa kung'amua ndo'umepelekea hivyo.
Sasa tujiulize mi na wewe, kaanza na kushtumu CDM kuwa inaendeshwa kidikteta kua wasemacho dk.slaa na mh. Mbowe ndicho hicho hicho. Hivi inakuingia akilini. Inamaana viongozi na baadhi ya makada waliomo ktk ngazi za uongozi hawana ufahamu wa kutosha kama wako mpaka wamekubali hali hiyo? Na je hawa wenye kauli mbiu ya "ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI" unahisi hapa hamna udikteta, mpaka ujeuandike udikteta wa cdma? maana kauli mbiu tu yatoshakujulisha kilichopo ndani, kua afikiriacho na kunena mwenyekiti kibaki hivyo hivyo na kudumu.
2. Kadai kifo cha Marehemu Mwangosi chanzo ni CDM, hii hoja hata kisheria we mleta mada utaonekana Zuzu kama sio "kilaza". Inamaana CDM ndo'ilimpiga bomu/guruneti marehemu mpaka kupeleka kifo chake? Na je kama ni CDM, cdm ni nani? Na kwa nini husiwashauri polisi kutokana na ufahamu wako, wawafikishe mahakamani cdm wote na wamwanchie yule askari alipelekwa mahakamani?
3. Kadai marehemu alikua ni mwandishi wa cdm ndo'maana anahisi polisi walichukua fursa ya kutimiza wajibu wao. Hivi ni sheria ipi Tanzania\duniani inayoruhusu polisi kuzuia na ikiwezekana kuua mwandishi wa habari anapokua katika utendaji kazi yake, isipokua kama si mwandishi wa chadema?
Mwisho Mwenyezi Mungu katujalia vichwa kuhifadhia ubongo wenye akili na ufahamu na si vinginevyo.