Mhadhiri Bakari Muhammed amng'ang'ania Kikwete - Sehemu ya 2

Andiko langu litatofautiana kidogo na wengi. Kwanza nampa pongezi Bakari kwa kurekebisha hesabu zake za kwanza. Ila angekuwa muungwana kwa kukana hesabu zake katika toleo la kwanza. Angalau sasa tunaweza kujadili facts.
Hio figure zako ni stagnant. Kuna vitu vingi hujaviaacount. Naomba nikukumbushe baadhi ya mambo muhim ambayo umeyaacha. Mosi; Wafanyakazi hupanda vyeo. Mf wewe katika sekta uliopo ukiwa unaweza kuwa mhadhiri kamili baadae. Sasa kila sekta watu hupanda vyeo. Pili umesahau kwamba serikali kwa sasa hivi inaajiri saana sekta ya kilimo, afya na elimu. Sijui hesabu za hao watu umeziaccount vipi. Tukiachana na hesabu in real world serikali ikilipa mshahara huo based on yr hesabu ninakuhakikishia ni lazima ifilisike. Kwahiyo ishu iwe ni ukweli kwa kusimamia taaluma na ni vyema pia ukaanisha na madhara kwa uchumi wetu kama mishahara hiyo italipwa.

............hebu tuainishie na wewe basi uhalali wa mahesabu ya JK ili tukusome.....................
 
Kikwete amezidi sana Utapeli.. Ikiwa Takwimu zake mwenyewe zinasema serikali ililipa mishahara ya mwaka 2009/10 Trillioni 1.77 ambayo ni asilimia 5.7 tu ya GDP ile hesabu ya makusanyo ya serikali ya Trillion 5. 7 kwa mwaka yalitoka wapi?.. au Mheshimiwa alichanganya asilimia na makusanyo?
 
Hiyo 5 trillion ndiyo makusanyo ya serikali. Sasa hoja yako 5.7 ya GDP, unataka kusema nini? remember si 5.7 ya budget ni GDP!
 
Astrolojia sio sayansi, ni upuuzi uliopanguliwa zamani sana! Kwa hiyo napata shida kumtake huyu mtu serious.
 
Astrolojia sio sayansi, ni upuuzi uliopanguliwa zamani sana! Kwa hiyo napata shida kumtake huyu mtu serious.

I can challenge you if una uhakika na unachosema na pia kama una facts to back it up.
Tunaweza kujadili hili tukawekana sawa, coz watanzania na waafrika kwa ujumla tunapotoshwa sana,asrtology si uchawi,sasa tujadili ni kivipi siyo science....Ama kwako wewe science ni nini?
 
NB: Baadhi yetu tuliofurahishwa na sehemu ya kwanza ya ushambulizi wa kihoja na kiakili wa hotuba ya vitisho kwa wafanyakazi ya Rais Kikwete tumempa moyo Mhadhiri Bakari Mohammed wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na kupendekeza kwake kwamba japo sehemu ya kwanza ilikuwa imegusa kwa kiasi matatizo ya kifalsafa na kimantiki ya hotuba ya Kikwete Bw. Mohammed angeweza kwenda mbele zaidi. Nashukuru kwamba Bw. Bakari ameenda mbele zaidi katika sehemu hii ya pili ya majibu yake kwa hotuba ya Rais Kikwete. Kinachofurahisha zaidi ni uwezo uliokubuhu wa kuweza kuunganisha hoja zake na sehemu ya historia yetu. Kwa tulio mashabiki wa fikra za Nyerere tumefurahishwa na utetezi wa hoja zake kwa kutumia mojawapo ya hazina kubwa za kifikra yaani hoja za Mwalimu hasa kutoka kijitabu maarufu (ambacho Watanzania wengi nina uhakika hawajawahi kukisoma licha ya kukisikia, yaani "TUJISAHIHISHE". Sehemu hii ya pili ina lengo la kugusa dhamira ya Kikwete na kuamsha dhamira za wananchi kuelewa kuwa mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuwa endelevu (the unsustainability of a corrupt political system). Soma kwa furaha!

HOTUBA YA RAIS KIKWETE (2)
UPEMBUZI WA KITAKWIMU NA KIASTROLOJIA

§ Takwimu za bajeti zabainisha “alivyopotoshwa”
§ Vitisho, jazba, na kebehi nini ishara yake?
§ Ilikuwaje “Siku ya Jumatatu”?
§ Ushauri “elekezi”

Watanzania, wa hali zote za maisha (masikini, matajiri, wakulima, wafanyakazi, wakwezi, wasomi na wanazuoni) bado tungali wanaitafakari hotuba ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa siku ya Jumatatu tarehe 3, Mei 2010. Pamoja na jitihada za mtu mmoja mmoja, vikundi vvya watu hata wazee wastaafu (kama Rais wa Awamu ya Pili – Mzee Ruksa) wanaitafakari hotuba “ile” na hatma ya Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 na miaka mitano ijayo! Kwa kuwa (1) takwimu, (2) vitisho, jazba, na kebehi, na (3) Siku ya Jumatatu vilitumika; kwa hivyo basi, makala haya yanajaribu kupembua: (1) vielelezo vya takwimu za bajeti ili kuona uhalali wa shilingi trilioni 6.85293; (2) ishara ya hamaki aliyoionesha Rais wa Nchi; na (3) Upembuzi wa Sayari ya Jumatatu.

Ukiisoma Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2009/2010 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mheshimiwa Mustafa Haidi Mkullo (MB) aliyoisomwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) tarehe 11 Juni, 2009 na inayopatikana kwenye www.mof.go.tz/mofdocs/budget na kwenye wavuti wa Bunge la JMT ina mengi ya kelezea juu ya mwelekeo wa gharama za mishahara ya watumishi wa Serikali. Pamoja na mambo mengine na kwa kurahisisha haja ya upembuzi tufanye udondozi, upekuzi na uchambuzi wa taarifa za takwimu juu ya malipo ya mishahara peke yake. Jedwali lifuatalo limenyofolewa (detached) kutoka kwenye Jedwali 2a na Jedwali 2b ya Hotuba ya Bajeti 2009/2010.

Download:

Load of crap! Pamoja na ile aliyoandika awali.
 
I can challenge you if una uhakika na unachosema na pia kama una facts to back it up.
Tunaweza kujadili hili tukawekana sawa, coz watanzania na waafrika kwa ujumla tunapotoshwa sana,asrtology si uchawi,sasa tujadili ni kivipi siyo science....Ama kwako wewe science ni nini?

Science ="Science (from the Latin scientia, meaning "knowledge") is, in its broadest sense, any systematic knowledge-base or prescriptive practice that is capable of resulting in a prediction or predictable type of outcome".

Yes nina uhakika, Astrology sio science, Astronomy ndio science.
Uchawi nao ni imani za kipuuzi kama Astrology, sio sawa lakini kundi lile lile.
Sio science kwa sababu relationship wanazozidai ukiziangalia statisticly hazina ukweli wowote.
 
Kimsingi Rais Kikwete yuko shallow ktk ku-analyse mambo. Mimi huwa sipendi hata kuangalia na kusikiliza hotuba zake kwani anakera sana.
 
Mjeshi kalikoroga akidhani sisi watanzania tuna nidhamu ya kijeshi. hajui anaongoza raia.
sasa wacha wataalam wa ukweli wanamzodoa kila ahsubuhi.
Amelikoroga, mwache alinywe
 
Kimsingi Rais Kikwete yuko shallow ktk ku-analyse mambo. Mimi huwa sipendi hata kuangalia na kusikiliza hotuba zake kwani anakera sana.
Sikubaliani nawe kwenye hoja yako hii. Hotuba za JK ni nzuri pengine ni zile za Mwalimu tu ndizo zinazizidi kati ya Marais tuliowahi kuwa nao. Tatizo zinakosa nguvu ya hoja. Ushahidi ni idadi ya thread zilizoanzishwa humu baada hotuba ile. Tumejikita mno kumjadili yeye kama Kikwete na mapungufu yake tunahama nayo kwenda kila thread itakayomgusa. Tulinganishe tu hoja za Mhadhiri Bakari na hotuba ile ya JK.
 
hotuba za kikwete nthuri..bwa bwa bwa bwa bwa bwaaaa ha!!!.......

si bora kumsikiliza bambo au mzee jangala.....!!

hotuba pekee ya kikwete nzuri ni ile aliyoitoa ya kwanza baada ya kuapishwa bungeni...itafuteni!! kweli tukajuwa nyerere kazaliwa...baada ya hapo ni sarakasi mtindo mmoja!!
 
Tumekwisha mchukia basi. Sasa kila atakalolisema litabamizwa ukutani tu. Hotuba ya juzi ilikuwa nzuri ukiondoa "uswahili" mchache alookuwa akiuingiza hapa na pale. Ndio maana bado tunaijadili na wengine wanamjadili yeye badala ya ile hotuba.
 
"Love is blind"!! Hapa watu wanajadili hoja za Mhadhiri Bakari dhidi ya Hotuba aliyoitoa JK na jinsi hotuba ile ilivyokuwa bomu in the real sense of the word. Wewe uliyepofushwa macho kwa 'mahaba' unatuambia hotuba ilikuwa nzuri! Hotuba ilikuwa nzuri; nzuri kwa nani - kwa wafanyakazi ambao ndio waliokuwa walengwa? Labda hotuba ilikuwa 'nzuri' kwa wa wale wanaoneemeka ambao hawaoni mateso wanayopata wananchi wenzao wenye kipato duni.

WildCard tukupe mshahara wa 104,000 kwa mwezi ambao hauna rupurupu la aina yoyote na unatumia siku yako nzima kazini bila kuwa na muda wowote wa kufanya shughuli nyingine itakayoweza kukuongezea kipato; utaweza kuishi? Je, hutanung'unika pale unapoona wapo Watanzania wenzio wakiwemo viongozi wanaopata mara 300 na zaidi ya unachopata wewe kwa sababu ya mgawanyo mbovu wa pato la Taifa usio na uwiano unaostahili.

Acheni utetezi usio na macho ya kuona dhiki na taabu wanazopata Watanzania wenzenu.
 
Kwa kweli Kikwete ana kazi, alidhani watu waoga tusubiri labda atatujibu tunaokosoa hotuba yake!
 
Hiyo 5 trillion ndiyo makusanyo ya serikali. Sasa hoja yako 5.7 ya GDP, unataka kusema nini? remember si 5.7 ya budget ni GDP!
Mkuu sivyo kabisa, ila imenishangaza tu hizi namba zinavyofanana kwani najua fika kwamba asilimia ya Uzalishaji wa ndani sii sawa na makusanyo ya kodi za serikali. Kisha basi, hakuna mtu anayepinga mfumo mzima wa serikali ktk ukusanyaji wa kodi zake kama mimi kwa sababu najua fika wanaoumia ni wajasiliamali na wafanyakazi kuliko matajiri na viongozi wanaoweza kutumia nguvu ya fedha na vyeo vyao kutolipa kodi stahiki.
Niliwahi kusema kwamba Tanzania tunaibiwa sana na hata siku moja tusitegemee kukua kwa GDP kunaweza leta mabadiliko ndani ikiwa mali yetu inachukuliwa na sii kwamba tunafanya biashara na nchi za nje. Mfano mkubwa ni pato la Taifa toka mashirika kama Barricks, mashirika ya Utalii yanayokusanya fedha huko nje, viongozi kupangisha nyumba zao kwa dola pasipo kulipa kodi za mapato (formally NHC na Msajili), wengine wamekodisha nyumba za NHC kwa dollar, hali wao wakilipa Tsh kwa asilimia chini ya 10. Wana misamaha mikubwa ya uagizaji wa mali ktk miradi yao na kadhalika..Hivyo JK anafanya zaidi Usanii wa kucheza na namba vichwani mwa watu badala ya kupinga hoja kiuchumi na kama kiongozi wa nchi..

Kiongozi unapokabiriwa na shaka kama hili ni muhimu kuonyesha athari za kukata matumizi ya serikali, hatari ya kupunguza kodi na mafao ya wafanyakazi hayawezi rekebishika badala ya kutumia Ujumla wa namba kurahisisha mazungumzo. Mkuu nijuavyo bajeti ya serikali haipangwi kama JK alivyosema.

Mara ngapi tumekwenda deficit ya bajeti ktk matumizi ya serikali kwa mabillioni? sii mara moja na nchi kama zetu haiwezekani kabisa serikali kushindwa kutafuta njia mbadala zinazoweza ku deal na mpasuko wa bei badala yake kuwaadhibu wananchi na kusema liwalo na liwe. Ni hao hao wafanyakazi toka kima cha chini wanaofanya mzunguko wa fedha, kwamishahara yao ndio wanunuzi (retailer) wanaoweza kurudisha hali bora ya uchumi wa nchi yetu. Ndio wanunuzi wa mazao ya Wakulima, ndio wao wanunuzi na watumiaji wa mali zote za matajiri na wawekezaji nchini, ndio wanaoendesha nchi uchumi wa ndani na kuboresha pato la serikali sii Wanasiasa. Maisha ya mfanyakazi yanaposhuka chini ndivyo kwa urahisi uchumi wa nchi unadondoka.
Mkuu wangu hotuba ya JK ilikuwa finyu sana kiutaalam na hata kisiasa, ilikuwa majungu na uswahili zaidi ktk hizo hadithi za mbayuwayu zisizohusiana kabisa na uchumi wala hoja husika.
 
Andiko langu litatofautiana kidogo na wengi. Kwanza nampa pongezi Bakari kwa kurekebisha hesabu zake za kwanza. Ila angekuwa muungwana kwa kukana hesabu zake katika toleo la kwanza. Angalau sasa tunaweza kujadili facts.
Hizo figure zako ni stagnant? Kuna vitu vingi hujaviaacount. Naomba nikukumbushe baadhi ya mambo muhim ambayo umeyaacha. Mosi; Wafanyakazi hupanda vyeo. Mf wewe katika sekta uliopo unaweza kuwa mhadhiri kamili baadae. Sasa kila sekta watu hupanda vyeo. Pili umesahau kwamba serikali kwa sasa hivi inaajiri saana sekta ya kilimo, afya na elimu. Sijui hesabu za hao watu umeziaccount vipi. Tukiachana na hesabu hizo, in real world serikali ikilipa mshahara huo based on yr hesabu ninakuhakikishia ni lazima ifilisike. Kwahiyo ishu iwe ni ukweli kwa kusimamia taaluma na ni vyema pia ukaanisha na madhara kwa uchumi wetu kama mishahara hiyo italipwa. Pia hoja zako zinasahau kuainisha matumizi mengine muhim ya serikali km miundo mbinu nk.

Support your claims with facts. Mambo ya "ninakuhakikishia" yamepitwa na wakati. Mhadhiri ameweka mahesabu sasa ni zamu yako na wewe weka zako ili utuhakikishie kuwa serikali itafilisika ikilipa mishahara kama TUCTA wanavyopendekeza
 
Sawa mkuu maligwa tumekupata ila kumbukaubeti wa mzee shaaban robert.. Mwaka ukizinga dira, hupandi huna pandiyo wenzio watakubera,na hali kazi unayotazameni masikhara, ya kutumwa na wenzio tunafanya ndivyo sivyo,tukatizane njiyani
 
Kila asi wa kanuni, ni mjinga wa kulalawa kulala duniyani, mahala penye madhilapenye hasara na dhani, na mauti ya ghafula jibu limefutu swali, mtu kutii kanuni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom