Mhadhiri Bakari Mohammed wa Mzumbe University amjibu JK kisayansi!

Sikubaliani na Kokotozi gharama la huyu mhadhiri wetu. Hivi kweli msomi kama wewe tena kwenye faculty heshimika katika masuala haya unaweza kutoa maoni kama haya na takwimu hizo? Yaani wafanyakazi wote wa nchi hii wapewe kima cha chini cha mshahara!!!!! kweli kweli kweli!!!!!!! umenisikitisha sana, umenifadhaisha sana na umenidhalilisha sana katika hili naomba kumwandikia mkuu wa chuo namrudishia degree yangu niliyoipata kutoka faculty hiyo. Unapotoa ufafanuzi kama huo jiridhishe kwanza wewe kabla ya kuutoa katika jamii maana unajidhalilisha wewe, chuo chako pamoja na wahitimu tuliotoka hapo. Pole mheshimiwa rahisi kumbe unawajua wafanyakazi wako ndiyo maana unawafanya ma - toy
Mkuu hata kama ulikimbia hesabu unashindwa kusoma hata kilichoandikwa waziwazi na Mhadhiri. Sasa Mhadhiri huyu Dr. Bakari akikuita kwa mfano kuwa wewe ni kiazi atakuwa amekosea. Mhadhiri ametoa mahesabu ya kima cha chini kwa sababu ndizo hesabu alizotumia Kikwete kutoa hesabu ya trilioni 6.9 kwa wafanyakazi wote wa Serikali. Yeye kasema hapana hesabu hiyo ni uwongo siyo Trilioni 6.9 bali ni Trilioni 1.5. Soma hapa sehemu ya maandishi yake Mhadhiri alipokuwa ananukuu hotuba ya rais. Wewe maandishi haya hukuyaona?.

''Rais Kikwete, alitoa mfano kwamba Serikali ikitoa kiwango cha shilingi 315,000 (laki tatu na kumi tano elfu) za ki-Tanzania kwa kila mtumishi (mfanyakazi) itabidi iwalipe watumishi (wafanyakazi) zaidi ya 300,000 (laki tatu) wa sekta ya umma shilingi 6.9 trilioni (Mwananchi), shilingi 6.85 trilioni (Uhuru), na shilingi 6,852.93 bilioni (HabariLeo)''.
 
Sikubaliani na Kokotozi gharama la huyu mhadhiri wetu. Hivi kweli msomi kama wewe tena kwenye faculty heshimika katika masuala haya unaweza kutoa maoni kama haya na takwimu hizo? Yaani wafanyakazi wote wa nchi hii wapewe kima cha chini cha mshahara!!!!! kweli kweli kweli!!!!!!! umenisikitisha sana, umenifadhaisha sana na umenidhalilisha sana katika hili naomba kumwandikia mkuu wa chuo namrudishia degree yangu niliyoipata kutoka faculty hiyo. Unapotoa ufafanuzi kama huo jiridhishe kwanza wewe kabla ya kuutoa katika jamii maana unajidhalilisha wewe, chuo chako pamoja na wahitimu tuliotoka hapo. Pole mheshimiwa rahisi kumbe unawajua wafanyakazi wako ndiyo maana unawafanya ma - toy
Toa za kwako sasa sio unakimbilia kukosoa bila mbadala.

Raisi alikua anaongelea kima cha chini na kama takwimu alizotoa ni sahihi basi ina maana zaidi ya 5 trilion wanachukua hao wakubwa na kwa maana hiyo wana uwezo wa kupunguza hizo za wakubwa na kuwatimizia mbayuwayu madai yao.
 
Usimshambulie msomi wa watu mwenye uchungu na matatizo ya wananchi wenziwe na si wewe unayejali tumbo lako na kuwa na jeuri ya usomi! Maneno yako mweleze Rais aliyedanganywa na wasaidiai wake hadi akatoa figures hizo kwa jazba bila concentration inayostahili na bila ufafanuzi. Katika uongozi jazba haitakiwa kinachotakiwa zaidi ni busara na kujali subjects unaowatumikia.

Na hilo la Rais kuambiwa viongozi wa TUCTA walitakiwa mkutanoni saa nne wakafika saa nane wakati barua inaonyesha vinginevyo hilo nalo unalielezeaje wewe unayejidai msomi? Acheni usanii wenu na makidai katika mambo yanayohusu maisha ya wananchi wanaoteseka. Mtalaaniwa!

Rais unayemtetea amechemka vilivyo maana kadhihirisha jinsi asivyokuwa na uchungu hata tone wa matatizo ya wananchi hususan wafanyakazi wa nchi hii. Hivi kweli yeye anaweza kuishi comfortably kwa fedha za kodi wanazokata wafanyakazi halafu wanapodai nao waangaliwe maslahi yao anakuwa mkali na kuwafokea?

Nyie vibaraka acheni zenu msizidi kututia hasira!
Bora maisha achana na hoyo MJM, kwa sababu Mhadhiri akisoma bandiko lake anaweza kumwita kiazi. MJM hajasoma kilichoandikwa amekurupuka tu. Dr. Bakari ametoa mahesabu ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa umma kwa sababu ndiyo mahesabu ambayo Kikwete alitumia kutolea mfano wake. Bahati mbaya hayo mahesabu ya mfano wake Kikwete yakiwa ya uwongo. Ndio Mhadhiri akatoa mahasabu sahihi kwa kufuata mfano aliotoa Kikwete. Nimemjibu huyu MJM angalia hapo juu.
 
Ndio tatizo la shule za msondo ngoma, ila nasikia jk alikua mtaalam wa hesabu pale lugoba mwaka 1965 ,japo kuwa kuna na wafanyakazi wa kati na juu basi tufanye wastani wa watumishi 500,000 na uwalipe tshs. 500,000.00 x 12 haifiki 6,000,000,000,000/= ni 3,000,000,000,000/= .

Aliepika huo ugali wa 6,000,000,000,000/= sasa yeye ndie ana lake jambo, na jk akili za kuandikiwa changanya na kuhakikisha mwenyewe
 
Kuongeza kima cha chini si lazima uwaongeze kwa uwiano sawa sawa wale wa kima cha kati na cha juu (wale walio juu ya Tsh. 315,000). Rais ameshindwa kuelewa kwamba angeweza kuongeza kima cha chini mpaka Tsh. 315,000 bila hata kuathiri bajeti ya OC (other charges). Inawezekana watumishi wanaopata kipato chini ya Tsh. 315,000 hawazidi hata 250,000 which means roughly ukiwaongeza mishahara wale wote walio chini ya Tsh. 315,000, ongezeko linaweza lisizidi hata Shs. bilioni 600 kwa mwaka ambayo ni robo ya matumizi ya chai katika ofisi za serikali.

Naamini mh. Rais aliamua ku compliketisha mahesabu ili watu waamini kama hili jambo haliwezekani!!
 
Tukubali kuwa Rais ana makosa makubwa, Je, hana macho? Hana akili timamu? Si mdadisi? Mimi ninahisi watanzania walipoteza mwelekeo wao mwaka 2005 walipomchagua huyu jamaa.
Ninaogopa kitu kimoja: Ukiona kiongiozi yeyote na matendo yoyote anayoyafanya, mchunguze utajua tabia na ukomo wa uelewa wa watu waliomchagua: Kama alichaguliwa kihalali na yupo madarakani kwa uhalali kufuatia kura za wananch wa nchi husika.
Shime watanzania, asipewe tena kura huyu, hata kama atashinda ashinde kwa asilimia 30 na si zaidi ya hapo.
Hakuna kitu kinauma sana kama dharau, lakini ukidharauliwa kwakuwa unaonekana mjinga na muoga basi dharau hiyo inauma zaidi. Huyu JK amewadharau watanzania! Ameona akitaja tu takwimu yoyote, watanzania wataipokea kama mazuzu na kupiga makofi kama wale wazee waliokuwa wamepewa usafiri wa bure kuja na kuondoka pale Diamond Jubilee. Si bado anaamini kale ka-msemo: "...ukitaka kumficha kitu mtanzania kiweke katika maandishi...." na tena anadhani kwa vile 'Hisabati' ni somo linaloongoza kwa kufelisha wanafunzi Tanzania basi acha ajitamkie tu viji-takwimu vyake!
Ndugu zangu, Mhadhiri msaidizi pale Mzumbe na wengineo, watanzania hawajakuwa bado na uelewa wa haya mambo. Tuhimizane tuwafumbue macho wenzetu ili tuwa na nguvu ya wengi tunaoujua ukweli. Maana wasipo ujua ukweli watashangilia kama wale wazee juzi pindi huyu JK atakapoanza kupita kuomba idhini ya kurudi magogoni! Mfano mrahisi tu ni jinsi watu wengi walivyoona takwimu zilizotolewa na Jk kuwa za kweli ilhali wangefanya uchunguzi na uchambuzi wa kina japo kidogo tu kama ndugu yetu Muhadhiri hapa, wangekunja sura tangu mapema.
Wasomi, wanaharakati, wafanyakazi tuungane pamoja kuwaelimisha wananchi wengi wasioujua ukweli waujue na ndipo tuwaombe kuungana pamoja nasi dhidi ya huyu jamaa na kundi lake ambao hawana hata aibu wala uchungu kutembele V8s hapa mjini Dar es Salaam ilhali maisha ya wananchi ni duni na mahitaji yao yanapuuzwa.
 
hi wajameni

Tuwache Jazba, tuangalie uhalisia wa Mambo . MIMI binafsi nampongeza sana Mhadhiri kwa Makala yake nzuri.

LAKINI:

Nimesikitishwa sana na uchambuzi wake, kama alivyotudanganya Mheshimiwa JK, nathubutu kusema kuwa na yeye pia anataka kulidanganya TAIFA . na pengine kutufanya SISI wote humu kwenye JF ni watu wasiojua hesabu kama yeye.

Mimi nahisi sio miongoni mwa hao WASIOJUA hesabu humu kwenye JF. Tunaposema hii ni kwa great Thinker basi na tuwe hivyo.

SIKUBALIANI kabisa na takwimu za muhadhiri kuwa wafanyakazi wote 400000 wanalipwa MSHAHARA sawa hizi ni hesabu za wapi, ama ni kigezo gani kimetumika.

NI lazima Atuambie ametumia Scheme of Service ya WAPI? , ama labda MZUMBE kila mfanyakazi analipwa equal amount na mwengine.

KIUFUPI ALIEANDIKA HII MAKALA NDIE ANATAKIWA ASHANGALIWE ZAIDI KULIKO HATA HUYO RAISI.

PHD holder wa Mzumbe university. PUMBA TUPU. nadhani ndio maana hata yule mama wa UTUMISHI na yeye ni wastaili hiyo hiyo.
 
Kikwete alipewa kazi asiyositahili kabisa. Juzijuzi tu alisaini sheria ya uchaguzi iliyopachikwa vitu ambavyo havikujadiliwa na Bunge, hakusoma kabla ya kusaini. Muda mfupi tu ametoa mahesabu ya uwongo kwa watanzania. Sasa mtu asiyetaka kusoma kwa nini alipewa urais na kwa nini aligombea? Jamani hatuna rais.
 
MW, nadhani kuna point umeiacha mahali fulani. Kuzidisha hicho kima cha chini mara idadi ya wafanyakazi sio sahihi. Kumbuka, tunaposema kima cha chini ni 315,000/= maana yake kuna wengine wanaolipwa kima cha kati na wengine kima cha juu. Sasa fikiria huyu wa 104,000/= akiongezewa ili mshahara wake ufikie 315,000/= Je yule wa kima cha juu, ambaye kwa mfano mshahara wake wa sasa ni 4M atafikia wapi. Kwa vyovyote vile ongezeko la kima cha chini lazima litaathiri na wale wa kima cha kati, na cha juu labda. Ukishapata mishahara hiyo yote mipya kulingana na kima cha kila mmoja, ndipo ujumlishe hiyo mishahara yote. Labda ndiyo hesabu alizotumia. Hata hivyo ujue kuwa mpaka sasa kuna wafanyakazi wengi tu ambao wamevuka kima cha chini, kwa hiyo sio rahisi kupata hilo jawabu kwa kuzidisha hivyo tu. Japo kwasababu hatujuai hiyo mishahara mingine bado hatuwezi kuridhika na maelezo ya JK maana hatuwezi kuthibitisha.

Mwadilifu, umenena vyema. Hata hivyo ukikisia ili kuziba pengo la mshahara wa kiwango cha juu kabisa, ukaassume kuwa kima cha chini kiwa laki sita na serikali inawatumishi laki sita. yaani 600,000 X 600,000 X 12 = 4,320,000,000,000 haifiki hiyo trilioni sita ya Mkuu.

Hiyo ni hesabu ya wapi au kiwango cha juu cha mshahara mtumishi wa serikali ni milioni mia moja?
 
Mnatakiwa kuelewa yafuatayo:-

1. Kuweka mshahara 315,000/= kuandana na kuongeza social security contribution na benefit zote ambazo zinategemea basic salary kwenye computation.

2. Ukiongeza mshahara wa chini kutoka 315,000/= kwanza lazima uongeze significantly wale wote ambao wako kati ya 104,000/- hadi 315,000/= na pia lazima uguse mishahara yote.

3. Compensation system ni kigezo kimojawapo kwenye performance management... na lazima kuwe na tofauti kati aliyekimbia umande huyo anayetaka 315,000/= na jamaa lililojipinda pale Mhimbili au FOE.

4. Watanzania tunaweza kujilipa mshahara wowote provided tuzalishe kwa wingi, whatever tulichonacho sasa ni kidogo sana.

5. Suluhisho la mishahara ambayo sitegemei kima cha chini kuwa 315,000/- kwa namna tunavyo-weka kipaumbele chetu kwenye kupanga matumizi badala ya kutafuta fweza. linaletwa na kupunguza matumizi yasio ya maana... na kuwalipa vizuri pia walioko juu wasihemee safari.
 
Toa za kwako sasa sio unakimbilia kukosoa bila mbadala. Raisi alikua anaongelea kima cha chini na kama takwimu alizotoa ni sahihi basi ina maana zaidi ya 5 trilion wanachukua hao wakubwa na kwa maana hiyo wana uwezo wa kupunguza hizo za wakubwa na kuwatimizia mbayuwayu madai yao.

Tayari nilikwishaeleza katika mada zilizotangulia kwa hiyo sina haja ya kurudi huko. Sijawahi kumtetea rais katika jambo lolote ambalo naona hana haki ya kutetewa kama hili. Wala siko agaist maslahi ya wafanyakazi tunayodai (me inclusive). Tatizo ni kwamba watu wanapanick na kusoma katikati ya mistari. Suala hapa kama msomi alitakiwa aje na mshahara unaolipwa sasa na aongeze impact ya ongezeko la mshahara full stop siyo kupiga 350,000 X 315,000 X 12. Ndiyo maana nauliza wafanyakazi wote wanalipwa kima cha chini cha mshahara? Simple logic! No research no right to speak. Tunapochallenge data za rais tuje na za kwetu ambazo ni sahihi na si potoshi kama hizo. Nilitegemea watu kama hawa ndiyo wawe wanatuelewesha mambo haya ili tujue tunadai nini tusipoteze mwelekeo. Ulitaka rais atoe majedwari yote ya utumishi, hizo information zipo utumishi na hata TUCTA nahisi wanazo na zitakuwa zikitumiwa katika mijadala yao. Can TUCTA wanaweza kutusaidia katika hili?.
 
Nchi za wenzetuwalioendelea lazima watu mchague raisi "mwenye akili" lakini sisi tulizoa tu pumba tukaifanya presidaa....ni aibu ya mwaka raisi wa nchi anazidiwa upeo na wananchi wengi kiasi hiki,
Haya majibu DK Bakari yatafutiwe nafasi kwenye gazeti lolote ili mkuu aonekane laivu akiwa hana nguo......na watu wengi.
 
Ndio tatizo la shule za msondo ngoma, ila nasikia jk alikua mtaalam wa hesabu pale lugoba mwaka 1965 ,japo kuwa kuna na wafanyakazi wa kati na juu basi tufanye wastani wa watumishi 500,000 na uwalipe tshs. 500,000.00 x 12 haifiki 6,000,000,000,000/= ni 3,000,000,000,000/= .

Aliepika huo ugali wa 6,000,000,000,000/= sasa yeye ndie ana lake jambo, na jk akili za kuandikiwa changanya na kuhakikisha mwenyewe

Angalia hapa alivyochanganya na za kwake..... Lakini jana TUCTA katika mkitano uliofanyika katika Ofisi za Shirika la Kazi Duniani (ILO) Dar es Salaam walionyesha barua ya mwaliko inayotaja muda waliopaswa kufika kuwa ni saa nane na si saa nne kama alivyokuwa amesema Rais Kikwete juzi katika hotuba yake.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba TYC/B/280/69 ya Aprili 22, 2010, ikiwa imeandikwa kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi, ikiwa saini Shogholo Msangi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, inawaalika TUCTA kuhudhuria kikao hicho Aprili 23, 2010.

Hivi wapi figures sahihi za malipo ya wafanyakazi zinapatikana watu wafanye hesabu za mizania
 
hi wajameni

Tuwache Jazba, tuangalie uhalisia wa Mambo . MIMI binafsi nampongeza sana Mhadhiri kwa Makala yake nzuri.

LAKINI:

Nimesikitishwa sana na uchambuzi wake, kama alivyotudanganya Mheshimiwa JK, nathubutu kusema kuwa na yeye pia anataka kulidanganya TAIFA . na pengine kutufanya SISI wote humu kwenye JF ni watu wasiojua hesabu kama yeye.

Mimi nahisi sio miongoni mwa hao WASIOJUA hesabu humu kwenye JF. Tunaposema hii ni kwa great Thinker basi na tuwe hivyo.

SIKUBALIANI kabisa na takwimu za muhadhiri kuwa wafanyakazi wote 400000 wanalipwa MSHAHARA sawa hizi ni hesabu za wapi, ama ni kigezo gani kimetumika.

NI lazima Atuambie ametumia Scheme of Service ya WAPI? , ama labda MZUMBE kila mfanyakazi analipwa equal amount na mwengine.

KIUFUPI ALIEANDIKA HII MAKALA NDIE ANATAKIWA ASHANGALIWE ZAIDI KULIKO HATA HUYO RAISI.

PHD holder wa Mzumbe university. PUMBA TUPU. nadhani ndio maana hata yule mama wa UTUMISHI na yeye ni wastaili hiyo hiyo.
Wewe nawe Mhadhiri akisoma post yako atakuita Kiazi sana. Soma post Na. 94 na 95 utapata majibu. Mhadhiri alichofanya ni kusahihisha mahesabu ya uwongo ya Rais. Kikwete alitoa mfano kuwa wafanyakazi wote wa umma wakilipwa kima cha chini kwa wafanyakazi wote cha 315,000 watalipwa shilingi Trioni 1.5 siyo Trioni 6.9 kama alivyosema yeye. Nyerere alisema kama unampenda mtu kwa sura yake kanywe naye chai siyo kumpa urais. Inaonekana wewe unampenda Kikwete kwa sura hata maandishi unaogopa kuyasoma, nenda kanywe naye chai lakini ameshindwa kazi ya urais. Kasaini kwa mbwembwe sheria feki, hakusoma. Tena anatoa hesabu feki, hakusoma. Ataongozaje nchi mtu asiyependa kusoma?
 
Mhadhiri Bakari Mohammed wa Mzumbe University amjibu JK kisayansi!
HOTUBA YA RAIS KIKWETE INA UPUNGUFU WA KISAYANSI
  • Alitumia jazba, vitisho na kebehi
  • Takwimu alizopewa ni "ghushi"
  • Hakujibu madai mengine ya TUCTA
Kwa kuwa mantiki ni mtiririko wa hoja zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika; na kwa kuwa sayansi ni elimu inayotokana na uchunguzi, majaribio, vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo; kwa hiyo basi, hotuba nzuri ni ile inayozingatia kanuni za kisayansi kwa utumizi wa uchunguzi na mantiki. Sayansi lazima itumike kwa kuwa ndiyo inayoweza kuonesha ukweli na kuutenga na uwongo – uwe wa kimaslahi au vinginevyo – hotuba, kwa hivyo lazima isheheni ukweli na uhakika.

Makala haya nayaandika baada ya kuiskiliza hotuba ya Mhashimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa mbele ya wale waliyoitwa kuwa ni "Wazee wa Dar es Salaam" siku ya Jumanne tarehe 3 Mei, 2010 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kwa ujumla, ilikuwa hotuba nzuri ya kisanii – kwa jinsi ilivyotumia lugha rasmi, mifano (mbayuwayu na kigong'ona) na vionjo vya lugha ya kwetu.

Mantiki ya jumla ya hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa kuijibu TUCTA japokuwa alitumia nafasi hiyo kuzungumzia Mkutano wa Uchumi wa Dunia (World Economic Forum). Pamoja na mambo mengine ya utangulizi, sehemu muhimu na yenye kuhitaji upembuzi makini na wa kisayansi (uchunguzi + majaribio + vipimo + ithibati + mantiki) ni juu ya matumizi makubwa ya jazba, vitisho, kebehi na hisabati ghushi za takwimu zilizotumika katika kujibu hoja moja (kati ya tatu muhimu) zilizotolewa na TUCTA.

Rais Kikwete alitumia mfano wa "Mauwaji ya Wakata-miwa wa Kilombero" yaliyotokea miaka ya 1980 baada ya FFU (Kikosi cha Kutuliza Ghasia, maarufu kama fanya fujo uone) kutumia risasi za moto na kuuwa! Rais aliendelea kusherehesha juu ya madhila yanayoweza kutokea pale wafanyakazi watakapopambana na POLISI. Sidhani kama ni sahihi kudhani kuwa siku zote migomo huandamana na vurugu na/au ghasia zinazoweza kuzaa utumizi wa nguvu za ki-POLISI na hata mauwaji! Ulikuwa mfano mbaya kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi, aliyesheheni "nguvu" za mamlaka ya kutumia vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Ushahidi wa hili unajionesha wazi hata pale penye hadhara yenyewe (Diamond Jubilee): ulikuwapo uongozi wa (1) POLISI; (2) MAGEREZA; (3) Usalama wa Taifa; (4) JWTZ; na (5) Askari wa Siri (Secret Police). Kwa ujumla, mkutano ule ulipambwa na kila aina ya vitisho!

Japokuwa Rais ni Kiongozi wa Nchi na ana mamlaka ya kuamuru majeshi (Ibara ya 33(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 [2005]) bado sayansi ya utawala haikubali kwa kiongozi muadilifu anayefuata haki na insafu kwa watu wake kutumia madaraka hayo dhidi ya utashi halali wa umma! Matumizi ya nguvu za ki-POLISI na/au kijeshi yamewahi kuziingiza nchi kadhaa kwenye sintofahamu na/au songombingo za kisiasa, kijamii na kiuchumi – kama tulivyoshuhudia Kyrgyzstan na tunavyoshuhudia sasa Thailand. Nguvu za ki-POLISI na/au kijeshi zitumike kwa hekima na si vitisho kwa raia (hususan wafanyakazi walalahoi – kama wakata-miwa).

Kwa upande wa utumizi wa lugha yenye murua – kiongozi yeyote awaye na mwenye mamlaka ya juu kiutendaji ana wajibu wa kuchagua maneno yenye hekima; kwa kuwa "hekima ni uhuru"! Rais Kikwete ametamka waziwazi kwamba, "…wafanyakazi wanaotaka kugoma waache kazi…kwa kuwa kuna watu wengi wanaohitaji kazi…." Ni ukweli usiyopingika kwamba "soko la ajira" Tanzania limefurika watu wanaotafuta kazi; lakini si kweli kwamba watu wote wanaotafuta kazi wana sifa stahiki kwa kila kazi.

Haitoshi, si kada zote za kazi (ziwe za kitaaluma na/au kimenejimenti) zina wazalendo wa kutosha kujaza nafasi zitakazoachwa wazi kutokana na: (1) wafanyakazi watakaouwawa (kama nguvu za ki-POLISI zitatumika); (2) watakaofutwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma; na (3) watakaoacha na kukimbilia ughaibuni [brain drain]. Nadhani hekima ilibidi itumike hapa ili wafanyakazi wasijione wanyonge mbele ya "Mwajiri Mkuu." Naomba nichukue fursa hii kunukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere aliyoyatoa Dar es Salaam kwenye Sherehe za Mei Mosi mwaka 1974:

Tulipoanzisha vyama vya wafanyakazi, na halafu baada ya Uhuru kwa uamuzi wa Serikali ya TANU, wafanyakazi wa Tanzania wamelindwa wasinyonywe na matajiri wao, watu binafsi, na hata mashirika ya umma. Na ulinzi huo umezidishwa siku hata siku. Kima cha chini cha mishahara kimewekwa na kimekuwa kikiongezwa mara kwa mara. Sasa ni vigumu sana kumfukuza mfanyakazi, na kila mfanyakazi apate heshima yake kama binadamu (Julius K. Nyerere (1974): UHURU NI KAZI, National Printing Company Ltd, Dar es Salaam, ukurasa 15).

Nukuu hii inatufundisha msimamo wa Mwalimu Nyerere juu ya kuwahakikishia wafanyakazi: (1) ulinzi wa ajira zao dhidi ya unyonyaji unaofanywa na matajiri, watu binafsi, na mashirika ya umma (kama PPF); (2) kuweka kima cha chini cha mshahara na kukibadilishabadilisha kila mara kuendana na utashi wa mwendo wa kiuchumi; (3) kuondoa vitisho vya wafanyakazi kufukuzwa na waajiri; na (4) kuwapa wafanyakazi heshima yao kama binadamu [Ibara ya 12(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)].

Hotuba ya Rais Kikwete imeonesha wazi kuwa leo wafanyakazi wa Tanzania si kama "Enzi za Mwalimu." Soko la ajira la leo limewapa nafasi matajiri, watu binafsi, mashirika ya umma na Serikali (yenyewe) kunyonya jasho la wafanyakzai, kuendesha vitisho, kulipa mishahara isiyokidhi maisha (na mafao duni ya uzeeni na/au kiinua mgongo), vitisho vya kufukuzwa kazi, na ukosefu wa heshima kwa wafanyakazi! Inawezekana haya ni matunda ya kuliuwa Azimio la Arusha na mahala pake kuliweka "Azimio la Zanzibar!"

Ukiachilia mbali jazba, vitisho, na kebehi vilivyotumika kwenye hotuba hiyo kuna suala la utumizi wa takwimu ghushi (au ghashi). Kwa mujibu wa hotuba yenyewe (ambayo niliisikiliza mwanzo-mwisho), kutangazwa moja kwa moja (mubashara) na vituo vya runinga vya TBC1 na Star TV na kunukuliwa na magazeti kadhaa yakiwamo: Uhuru (ISSN 0876-3896, Namba 20553 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010); HabariLeo (ISSN 1821-570X, Namba 01230 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010); na Mwananchi (ISSN 0856-7573, Namba 03608 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010). Kwa pamoja, japo numerali (nambari) zilizotumika kwenye habari iliyonukuliwa ni tafauti, bado ukweli unabaki palepale juu ya takwimu zilizotumiwa na Mheshimiwa Rais kuwa ni ghushi.

Rais Kikwete, alitoa mfano kwamba Serikali ikitoa kiwango cha shilingi 315,000 (laki tatu na kumi tano elfu) za ki-Tanzania kwa kila mtumishi (mfanyakazi) itabidi iwalipe watumishi (wafanyakazi) zaidi ya 300,000 (laki tatu) wa sekta ya umma shilingi 6.9 trilioni (Mwananchi), shilingi 6.85 trilioni (Uhuru), na shilingi 6,852.93 bilioni (HabariLeo). Kwa ujumla, takwimu zote zilizonukuliwa zinaonesha kuwa gharama ya kuwalipa watumishi (wafanyakazi) wa Serikali wapatao 350,000 (laki tatu na hamsini elfu) hivi ni shilingi za ki-Tanzania trilioni 6.85293 (kwa mujibu wa gazeti la Serikali, HabariLeo). Takwimu hizo za gharama ya mishahara zilitumiwa na Rais Kikwete kulinganisha na makadirio ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2010/2011 yanayokadiriwa kufikia trillion 5.7573 (kwa mujibu wa gazeti la Serikali, HabariLeo) na hivyo kuonesha nakisi ya bajeti ambapo Serikali itawajibika kukopa!

Ilinichukuwa muda kukaa na kutafakari juu ya "ukweli" huu wa ki-hisabati. Japokuwa hisabati ni tatizo la taifa, namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nilipata bahati ya kusoma hisabati tangu nilipoanza kufundishwa hesabu za vidole hadi chuo kikuu! Ziwe hisabati za kikwetu (Traditional Mathematics), hisabati za Entebbe (Entebbe Mathematics), hisabati za msingi (Basic Mathematics), hisabati za ziada (Additional Mathematics), hisabati za juu (Advance Mathematics) hata hisabati halisi (Pure Mathematics) haziwezi kukubaliana na udondozi wa ki-takwimu uliyotumiwa kurahisha hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Rais! Na tutumie mifano ili kuelezea hoja ya ki-hisabati kwa utumizi wa sayansi ya nambari (observation + logic).

Achilia mbali wafanyakazi 350,000 (laki tatu na hamsini elfu), tuchukue Serikali ina watumishi (wafanyakazi) 400,000 (laki nne). Angalia jedwali lifuatalo jinsi ya udondozi na/au ukokotozi wa kihisabati:

KIKOKOTOZI GHARAMA

IDADI YA WATUMISHI (iliyokadiriwa)

MSHAHARA KWA MWEZI + Bima + Akiba

IDADI YA MIEZI KWA MWAKA

GHARAMA

Mshahara
400,000
315,000.00

12

1,512,000,000,000.00

Akiba (Mifuko ya Hifadhi ya Jamii)
400,000
315,000.00 (15%)

12

226,800,000,000.00

Bima ya Afya
400,000
315,000.00 (3%)

12

45,360,000,000.00

JUMLA
400,000
371,70.00

12

1,783,160,000,000.00

Kama tukichukuwa mshahara kama "kikokotozi cha gharama" pasipokuwapo na 15% ya akiba (kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – PPF, PSPF, LAPF na NSSF) na 3% ya bima ya afya (NHIF) serikali itatumia shilingi 1.512 trilioni! Huu ni ukweli wa kihisabati kama wafanyakazi 400,000 (laki nne) watalipwa kima cha chini cha mshahara wa shilingi 315,000 (laki tatu na kumi na tano elfu) Serikali itagharamia shilingi trilioni 1.512 na si shilingi trillion 6.85293! Na hata kama tutachukuwa akiba (15%) na bima (3%) ya afya kwa pamoja (na gharama za huduma nyingine – OC) bado gharama haiwezi kuzidi trilioni 2! Huu ni ukweli wa ki-hisabati na si vinginevyo. Kosa kubwa la kihisabati lililofanywa hapa ni kama asilimia 74 (74%) kutoka kwenye ukweli – hili ni kosa kubwa ki-hisabati – ni mara tatu hivi kutoka kwenye gharama halisi!

Inawezekana Mheshimiwa Rais alipewa takwimu ghushi ili kuonesha kuwa watumishi (wafanyakazi) wa Serikali hawana uzalendo kwa kudai mishahara "mikubwa" kuliko uwezo wa Serikali kugharamia mishahara hiyo! Kama ni kweli alipewa takwimu ghushi, basi aliyempa (na/au waliyempa) wanastahili "adhabu" stahiki kwa vile takwimu hizo ndizo zilizomfanya Mheshimiwa Rais kuhamaki na kupandwa na jazba na hata kutoa vitisho na lugha ya kebehi kwa wafanyakazi. Watu wote waliyomdanganya Mheshimiwa Rais hawana budi kushughulikiwa ipasavyo – na kama ni wasomi wa vyuo vyetu vya ndani basi vyuo vilivyowatunuku stashahada na/au shahada hizo havina budi kuwanyang'anya – kwa vile wamempotosha Rais wa Nchi!

Jambo la mwisho kabla sijahitimisha makala haya nimalizie na nukta kwamba Mheshimiwa Rais hakujibu madai mengine "nyeti" na muhimu yaliyotolewa na TUCTA. Ni yale ya kodi kubwa ya mapato (inayotokana na mishahara) na mafao duni ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii (hususan PPF). Si jambo jema kuukwepa ukweli japokuwa unasemwa na mtu anayeonekana "duni" na "dhalili." Ukweli utabaki kuwa ni silaha ya jasiri na uwongo ni silaha ya mwoga! Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kuandika hivi:

Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa…. Ukweli haupendi kupuuzwa-puuzwa... Wakati mwngine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za ki(bi)nafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano siyo sita…. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazozitumia kuwashawishi watu wakatae mawazo yetu huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 3).

Nadhani ni wakati muafaka sasa tuukubali ukweli – hali za wafanyakazi wa Tanzania kwenye sekta ya umma na sekta ya binafsi zinahitaji marekebesho yenye dhamira nzuri – na si vitisho na/au utumizi wa takwimu zisizo na ukweli ili kuogopa kisasi cha ukweli. Mwalimu Nyerere aliliona hili na ndiyo maana aliamua kutuachia urithi wa kitabu hiki chenye umri wa miaka takriban sawa na Uhuru wa Tanganyika! Tujaribu kuyaangalia maneno haya ya Mwalimu Nyerere kwa kuyanukuu kama yalivyo:

Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiyotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la u(bi)nafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 5).

Haitakuwa vema na wala si haki tukiacha kusimamia ukweli. Ili kuogopa ukweli usijilipize kisasi (Nyerere, 1962) hatuna budi kama raia wa Tanzania kusimamia ukweli ili haki itendeke. Asiachwe mkubwa atende makosa huku wananchi wakimshangilia kwa nyimbo za "sema usiogope" na vigelegele vya tangazo la kuwafuta kazi watumishi watakaogoma! Tanzania ni ya Watanzania na itajengwa na Watanzania kama uongozi utazingatia haki, usawa na uadilifu katika matumizi bora ya rasilimali watu na vitu. Maendeleo ya watu hayaji isipokuwa kwa sera na siasa safi isiyokinzana na utashi wa ki-maumbile.

Sidhani kama kuna watumishi wa Serikali wenye kuona "gere" au kuwa na "hiyana" na CCM hata kutengeza "zengwe" lililoitwa agenda binafsi ya uchaguzi 2010! Wafanyakazi waliitumia Mei Mosi 2010 kutoa wito wao wa "Uchaguzi Mkuu 2010 uwe Suluhisho la Kero za Wafanyakazi." Nadhani huu ni ukweli wafanyakazi wana kero zao pamoja na (1) mishahara isiyokidhi haja, (2) kodi kubwa ya mapato yatokanayo na mishahara, na (3) mafao duni ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii (hususan PPF) – huu sio upinzani wa kisiasa na wala hauwezi kutumika kama "agenda ya siri" dhidi ya CCM. Tukumbuke Mwalimu Nyerere (1962) aliwahi kuandika hivi:

Pengine kundi "letu" ni sisi Wana TANU, na "lao" ni la wale wasiokuwa Wana TANU. Kwa mfano, baadhi ya Wana TANU husahau kabisa kuwa baadhi ya watumishi wa serikali ni wananchi safi kabisa kama sisi, na pengine kuwazidi wengine wetu. Lakini kwa sababu hawana kadi za TANU, basi, hufanywa kuwa si kitu. Pengine huongezeka kosa lile lile la kuwafanya wao kuwa ni watumishi tu ambao hawastahili heshima yoyote ya utu. Pengine, kwa sababu baadhi yao wanayo elimu nzuri, huongezeka kosa lile la kuwatilia mashaka wenye elimu. Sisemi kwamba huwa hawana budi wahukumiwe kwa makosa yao ya kweli, si kwa kubwagwa tu katika kundi la walaumiwa bila makosa yao wenyewe (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 13).

Nukuu hii ni muhimu kwa wakati huu. Isitokezee Serikali ya CCM ikadhani kuwa watumishi safi ni wanaCCM pekee – hiyo itakuwa kuwahukumu watumishi wengine wasiyokuwa wanaCCM pasipo na haki. Hakuna haja ya kuwatilia mashaka wenye elimu kwa kuwa uzalendo haupimwi kwa kuwa na kadi ya "chama tawala" isipokuwa utumishi uliyotukuka! Mwisho tukumbuke kuwa, "kila raia anastahili fursa na haki sawa, kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi [Ibara 22(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)].

Na asibaguliwe mtu kutokana na itikadi yake ya kidini, kisiasa, kiuchumi au kijamii. Na Mamlaka ya Nchi ihakikishe kuwa, "kila mtu anayefanya kazi (ya halali) kwenye sekta binafsi au ya umma anastahili kupata malipo ya haki [tazama Ibara 23(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)]. Mwenyezi Mungu Mtukufu azikunjue nafsi zetu na Atupe hekima ili tuwe huru na mawazo ya chuki dhidi wa watu wasiyo na hatia – na tunapohukumu basi tuhukumu kwa haki kwa kuzingatia usawa, insafu na uadilifu.

"TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA KUPUUZWA. SASA TUNATAKA MAPINDUZI, MAPINDUZI YATAKAYOTUFANYA TUSIONEWE, TUSINYONYWE NA TUSIPUUZWE TENA," (AZIMIO LA ARUSHA, 1967).

MUNGU IBARIKI TANZANIA WABARIKI NA WATANZANIA

Makala haya yameandikwa na:

Bakari M Mohamed
Mhadhiri Msaidizi
Kitivo cha Biashara,
Chuo Kikuu Mzumbe,
S.L.P 6,
Mzumbe – Tanzania.
Simu ya kiganjani: +255 713 593347
Barua pepe: maligwa1968@yahoo.com , bakari.mohamed@mzumbe.ac.tz

Bora maisha achana na hoyo MJM, kwa sababu Mhadhiri akisoma bandiko lake anaweza kumwita kiazi. MJM hajasoma kilichoandikwa amekurupuka tu. Dr. Bakari ametoa mahesabu ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa umma kwa sababu ndiyo mahesabu ambayo Kikwete alitumia kutolea mfano wake. Bahati mbaya hayo mahesabu ya mfano wake Kikwete yakiwa ya uwongo. Ndio Mhadhiri akatoa mahasabu sahihi kwa kufuata mfano aliotoa Kikwete. Nimemjibu huyu MJM angalia hapo juu.

Watanzania, asante. Inatia hasira! Watu wanadai uwepo mgawanyo unaostahili wa 'keki' ya taifa na si watu wachache waishi kama wako peponi kwa migongo ya maskini ambao wanalipa kodi na wale ambao mishahara yao midogo wanakatwa bila huruma. Eti zitatoka wapi fedha za huduma zingine za jamii endapo watumishi wa kima cha chini watalipwa 315,000. Huduma zipi hasa za jamii zinazowafikia watu wa kima cha chini ama maskini wengine vijijini? Leo hii mwenye mshahara mdogo akiugua ama kuuguliwa na mwanawe hata kama atakuwa na hiyo bima ya afya kuna hospitali zingine hazikubali kabisa kupokea bima hizo kwa kudai kwamba hawapati malipo yao kwa wakati. Hiyo dawa ya malaria ya Sh. 600 waliyoitangaza, mwananchi ambaye hana kazi ama mwanakijiji ambaye anategemea kupata laki 3 kwa mwaka akiuza mazao yake; ama hata huyo mfanyakazi wa kima cha chini ambaye mshahara wake hautoshi hata wiki mbili atatoa wapi hiyo Sh. 600 akanunue dawa ya Malaria? Shule za watoto wa maskini hazina madawati wala waalimu. Miundombinu gani ambayo mvua zikinyesha barabara za vijijini na mijini hazipitiki isipokuwa zile za lami wanazozitumia wateule wenye fedha zao na viongozi wenye magari ya kifahari waliyoyapata kutokana na jasho la wananchi? Na kila ikifika kipindi cha uchaguzi ndio wanafanya "danganya toto" kwa kukwangua na kumwaga vifusi kwenye barabara mitaani vinavyosababisha tope tu wakati wa mvua na ndio unakuwa wakati wa viongozi kupunguza safari zao na kuanza kuzungukia majimbo ama Rais na mkewe kupunguza safari za nje na kuzunguka nchini waonekane kwamba wanajali. Unafiki mtupu!

Rais na watu wake wangelikuwa wanajali hayo wangelielewa kwamba wao ni wanyonyaji wakubwa wanaostahili kuzomewa na kufokewa na wafanyakazi wanyonge wa nchi hii pamoja na wananchi wavuja jasho mashambani ambao kila mwaka huzalisha chakula ili wanyonyaji hao na familia zao wapate kula yao ya kila siku!

Ni aibu sana hasa kwa Serikali na Chama ambacho kimetokana na misingi thabiti ya kujali utu wa kila Mtanzania bila ubaguzi.
 
Tayari nilikwishaeleza katika mada zilizotangulia kwa hiyo sina haja ya kurudi huko. Sijawahi kumtetea rais katika jambo lolote ambalo naona hana haki ya kutetewa kama hili. Wala siko agaist maslahi ya wafanyakazi tunayodai (me inclusive). Tatizo ni kwamba watu wanapanick na kusoma katikati ya mistari. Suala hapa kama msomi alitakiwa aje na mshahara unaolipwa sasa na aongeze impact ya ongezeko la mshahara full stop siyo kupiga 350,000 X 315,000 X 12. Ndiyo maana nauliza wafanyakazi wote wanalipwa kima cha chini cha mshahara? Simple logic! No research no right to speak. Tunapochallenge data za rais tuje na za kwetu ambazo ni sahihi na si potoshi kama hizo. Nilitegemea watu kama hawa ndiyo wawe wanatuelewesha mambo haya ili tujue tunadai nini tusipoteze mwelekeo. Ulitaka rais atoe majedwari yote ya utumishi, hizo information zipo utumishi na hata TUCTA nahisi wanazo na zitakuwa zikitumiwa katika mijadala yao. Can TUCTA wanaweza kutusaidia katika hili?.

Je Kikwete hakutoa mfano wa mshahara wa kima cha chini kwa wafanyakazi wote wa umma kama mfano? kufundisha mtu mgumu kuelewa shida kweli. Kwa kukusaidia soma post 94 na 95. Kama hutaelewa nenda Muhimbili wachunguze kichwa chako.
 
vyovyote vile Rais alishindwa kutoa vitu dhahiri vinavyo-support hoja zake
1. amekosea hesabu (huu ni umbumbumbu)
2. hakutoa mikakati yeyote ya Serikali yake ya namna kuongeza pato la Taifa
3. hakutoa mikakati yeyote ya Serikali yake ya kuthibiti matumizi mabaya ya fedha (kubana matumizi yasiyo muhimu.
4. alishindwa kutoa hoja za kueleweka za kuwafanya wafanyakazi wawe na moyo wa kufanya kazi.

poor presentation, poor hoja, poor president.
 
Tayari nilikwishaeleza katika mada zilizotangulia kwa hiyo sina haja ya kurudi huko. Sijawahi kumtetea rais katika jambo lolote ambalo naona hana haki ya kutetewa kama hili. Wala siko agaist maslahi ya wafanyakazi tunayodai (me inclusive). Tatizo ni kwamba watu wanapanick na kusoma katikati ya mistari. Suala hapa kama msomi alitakiwa aje na mshahara unaolipwa sasa na aongeze impact ya ongezeko la mshahara full stop siyo kupiga 350,000 X 315,000 X 12. Ndiyo maana nauliza wafanyakazi wote wanalipwa kima cha chini cha mshahara? Simple logic! No research no right to speak. Tunapochallenge data za rais tuje na za kwetu ambazo ni sahihi na si potoshi kama hizo. Nilitegemea watu kama hawa ndiyo wawe wanatuelewesha mambo haya ili tujue tunadai nini tusipoteze mwelekeo. Ulitaka rais atoe majedwari yote ya utumishi, hizo information zipo utumishi na hata TUCTA nahisi wanazo na zitakuwa zikitumiwa katika mijadala yao. Can TUCTA wanaweza kutusaidia katika hili?.

Fanya wewe kazi hiyo maana wewe ndio umekuja hapa na kuchallenge data za Dr. Bakari! Rais anao wasaidizi wake wao ndio walipaswa kupekua majendwali ya utumishi na kumpa Rais hesabu sahihi na zinazoweza kueleweka kwa wananchi. Lakini hawakufanya hivyo wakampa Rais figures tata na za uongo na wakati Rais anachemka jukwaani wao walikuwa wanakenua na kuona anafanya jambo la maana. Kapuya na timu yake angelikuwa wa kwanza kutimuliwa kwa hili. Hata huyo mwandika hotuba naye hakufanya homework yake ipasavyo.

Hata hivyo nadhani Rais alipandwa na midadi akawa anaogelea tu aliposikia wazee wale wanampigia makofi. Which is very wrong for a leader katika suala nyeti linalohusu maslahi na maisha ya wananchi wake!
 
Back
Top Bottom