Mhadhara Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi: Mwakyembe, Sitta, Shivji et al ndani!

hehehehehe.... Swali la kizushi hapa.. hivi ikitokea Shivji anahitaji Urais mtampa KULA ZENU!? :biggrin1::biggrin1:

Nadhani Shivji alipenda kazi yake ya kufundisha,enzi za nyerere inasemekana alishawahi kupewa nafasi ya ukuu wa wilaya,akamwambia nyerere haiwezi baada ya kuripoti eneo la kazi na kukutana na changamoto gani sijui,na alitoa sababu zenye mantiki,akarudi mlimani kuendelea kufundisha,nadhani hata leo bado ana msimamo ule ule,ni mtu anayependa kuuishim ukweli!
 
Msikilizeni Pro Shivji peke yake. Hawa wengine ndo wale wale. Wataeleza nini wakati serikali iliyoko madarakani ni ya kwao. Nani kati ya hao anaweze sema ukweli kuhusu umaskini wa waTz.

Kumbuka ni juzi tu wametoka kwenye semina elekezi ambako wameambiwa hakuna kutofautiana kati ya waziri na waziri mwenzake katika kutetea mazuri ya serikali - kama yapo. Labda kama Six na Mwakyembe wameuchoka uwaziri wao, kitu ambacho ni muujiza. Tutasikia ngonjera zile zile tu, na watu wanatia ndani per diem.

Ni bahati mbaya Prof Shivji hakutokea! Flight cancellations. Ni mtu mmoja tu alinikuna wengine hawakuwa na jipya!
 
Napomsoma Shivji mara nyingi naamini mawazo yake mengi ni ya Kisocialist, hivyo Kibongo Bongo huyu anaweza kuchukua Urais lakini ktk hali ya Ukabila na Udini uloingia sidhani kama atapita hata uchakachuaji wa kwanza..
 
Mh. Samwel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe, Prof. Issa Shivji, Prof. Suleiman Chambo na Mr. Mangasini ndio watoa mada wakuu katika kongamano hili hapa chuo cha ushirika na biashara Moshi.
Leo tunataka tujue sababu ya huu umaskini wetu baada ya miaka 50 ya uhuru, kama kuna mchawi tumjue.
Wanajamii forums naomba mtoe mawazo yenu wakati mi nawaletea yale yanayo jadiliwa hapa chuoni .

Shivji Prof hakutokea nduugu!
 
watapiga porojo tu hapo hao akina 6 na mwakyembe kama wanataka kweli kuondoa umaskini uliopo basi watoke kwenye chama cha magamba au wasiwe ndani ya serikali ijnayoundwa na chama hicho.

Shivj ameshaongea sana kwenye majukwaa mpaka anabore
 
Anasema yeye hawezi kurubuniwa na cheo cha uwaziri kwani uwaziri huo alikuwa nao toka 1970 na kwamba yeye hawezi kuhama ccm
Ni mojawapo ya maswali niliyotaka kumuuliza. Sijui mtamwita moderator ama vipi ila kiu ya maswali haikukatwa hata baada ya Sitta kutoa go ahead ya kuulizwa maswali toka nyanja yoyote.

Nilitaka Mh Sitta atwambie aliposema kuwa hawezi kuhama chama kwa sababu ana mtaji mkubwa sana CCM, je akitokea mwanachama ama kikundi cha wanachama wakamtaka yeye Sitta atoke kwenye chama chao kama ambavyo Paul Makonda aliwahi kumwambia Lowasa atoke bado atang'ang'ania?
Je haoni kuwa tangu walipohongwa vyeo vya uwaziri hawaoni kuwa mapambano yao na mafisadi yamepungua? Yeye mwenyewe amekiri kuwa uwaziri ni cheo kikubwa! Makonda kama unapita humu mfikishie ujumbe, maana hata wewe umekiri kuwa unataka mitandao yote wapate taarifa ikiwemo JF.
 
Mbona ni kama wamefanya usanii usanii tu?
Baada ya kujua chanzo cha umasikini, Have they discussed out any way forward?

Mkuu ungekuwa na bahati ya kumsikiliza Mangasini ungejua kuna watu wanajua kubomoa. Kwachambua sawasawa. Yaani katika watu walioweza angalao kujibu hii mada ni huyu jamaa Mangasani.
Anasema hajui fomula wnayotumia kupata kipato cha mtanzania. Yeye anahisi kuwa wanachukua za magamba wanachanganya na zetu then wanapata huo wastani wa dola 590 kwa mwaka.
 
Wengine tulisema na tutaendelea kusema,

  • Huwezi kujifunika ndani ya blanketi na mtu mwenye chawa wewe ukasalimika usipate chawa.
  • Huwezi kukauka wakati bado uko mtoni ulikopiga mbizi katika kuogelea hadi utoke majini.
  • Huwezi kuishi kwenye nyumba chafu na hapo hapo ukadai wewe ni mtu anayechukia uchafu.
  • Huwezi kuoga kwenye tope shati lako jeupe likabaki na rangi yake na lisipate doa.
  • Huwezi kudai unapiga vita ufisadi wakati unavaa ufisadi, unakula ufisadi na unalala na mafisadi.
Asanteni Chuo cha Ushirika Moshi, mmetufungua macho tuliokuwa MaTomaso, Sita na Mwakyembe ni wanafiki na walafi wa kutupwa. Eti Sita hawezi kuhongwa Uwaziri kwani amekuwa Waziri toka 1970, anasahau kuwa tupo tunaomfahamu toka hata kabla ya miaka hiyo.

CCM ni kimbilio na hifadhi ya wote wale wanaojaribu ku"launder their past" kwani nje ya CCM watabaki uchi. Salama yao ni kubaki huko huko ingawa ukweli hauwezi kuzikwa na kusahauliwa, kuna siku "it is bound to raise its ugly head" na ole wao watu kama Sita na Mwakyembe.
 
Inaelekea hawa jamaa hawakuelewa mada [ Sitta]ndio maana wakaanza kuelezea historia ya maisha yao na wasia waliopewa na Mwalimu! Tamzania ni maskini kwasababu hatujui kuzitumia rasilimali zetu kwa faida ya wananchi wake na hii inatokana na kutokuwa na viongozi bora ambao wana upeo wa kuongoza na pia wazalendo. Mwakyembe anaposema hatuna wataalam; hao waliojazana huko Afrika ya Kusini na kwingineko duniani sio wataalam? Tatizo letu ni viongozi ambao wanamaneno mengi lakini vitendo hakuna 'They don't walk the talk'. Hata hao wanaokwenda kuwaambia warudi nyumbani"Diaspora'" wengi wamejaribu kurudi nyumbani lakini wakifika wanaamua kurudi ughaibuni kwani the environment is not receiptive due to poor organizational leadership.!!
 
Baada ya mtiririko wa habari toka kwa wanajamvi huko Muccobs....
Tunashuru ukweli unaendelea kuwa wazi zaidi juu ya hao wanafiki wawili (Sitta na Mwakyembe) kuwa dhahiri zaidi.
Kweli SWAGGA za kiharakati zinataka watu wanaoweza kujitoa muhanga...................
I like CDM swaggaz!
 
kwa kifupi saana!
1.Bajeti yetu ni trilioni 8
2.total exports ni trilioni
-GOLD = 1.365bn$
-Tourism =1.23bn$
-kilimo na viwanda =1.1bn$
Kwa ujumla tanzania in 2010 tuliexport 5.1bn$.

3.total imports
-Oil = 2bn$
-Others =3.83bn$
Kwa ujumla ni 5.83bn$
Ni asilimia 4% ya ardhi ya Tanzania ndiyo inafaa kwa kilimo,hatuna mafuta,dhahabu ilyopo itaisha in 20yrs,gesi tuliyonayo inatumika kuzalisha umeme ambao hata hautoshi na itaisha si zaidi ya miaka 15 ijayo,ingawa ya mnazi bay ndiyo inaweza kutusaidia baadae.Nchi nzima ina madaktari 1200 tu.
swali:Tufanye nini ili tuwe medium income state?
 
kuna jamaa anaitwa mangasini ndiye aliyetema cheche za ukweli.wengine mbwembwe tu.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, amesema anapitia nyakati ngumu za kisiasa kutokana na uamuzi wake wa kusimamia misingi ya haki, usawa na uadilifu iliyoachiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lakini akaapa kupambana na mafisadi hadi nchi itoke mikononi mwao.

Kauli hiyo ya Sitta inakuja kipindi ambacho joto la siasa nchini limekuwa likipanda siku hadi siku huku chama chake cha CCM kikiwa katika kipindi kigumu cha mpito kutekeleza mpango mkakati ujulikanao kama kujivua gamba.

Akizungumza katika kongamano la miaka 50 ya Uhuru na maisha ya Watanzania lililofanyika katika Chuo Kikuu kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara Moshi (MUCCOBS) na kuwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya kanda ya kaskazini, Sitta alisema kamwe hawezi kubadilika na atabaki kwenye viwango.

“Nawahakikishia nitapigana vikali kuhakikisha CCM inakua safi na nitapambana na waliokiharibu chama hadi kupoteza mwelekeo,” alisema Sitta.

Waziri Sitta alirejea tambo zake akisema yeye ni mwanasiasa mwenye viwango na ndiyo maana, wengi wanamgombania, lakini akawataka watambue kuwa hawezi kuhama chama chake kwa sasa baada ya miaka 50.

Alisema kitendo cha kuhama chama kwa sasa hakipo na anachokifanya ni kupambana na maovu yote yaliyopo ndani ya CCM na kuhakikisha kinarejesha heshima aliyoiacha Mwalimu Nyerere.

Chanzo. Gazeti la Mwananchi,Jumatatu
 
Jamani kuna mtu yeyote mwenye kumbukumbu ya mazungumzo ya moshi atutilie hapa ukumbini?. Nina hamu sana kusikia changamoto za wasomi juu ya watawala.
 
Samyy Sitta aende kujipumzisha. Nchi haiwataki watu waliochoka akili tunataka akili yenye fikra mpya. Ya Wazanzibari hayajamtosha bado?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom