Mh................!!!

Mjukuu wangu Hao majambazi wa nini tena?
Ngoja nitafakari kidogo!

Hahahahahhhh Babu penzi halina macho lol, popote lachanua LOL

Mi namjua mbaba mmoja hivi alimuoa baamedi aliyekuwa anagawa kama pipi. Huwezi amini alivyobadilika. Hii ishu bana huwezi kupata jibu la moja kwa moja manake inategemea n'tu na n'tu...Ila kuwa safe zaidi.........Usiijaribu sumu kwa kuionja.

BTW ndo kusema nijiandae kukamata mahari ya Jambazi?
Chunga tamaa mbaya.
Okay babu nimekuelewa hapa lol................hapana Mbu wangu si jambazi wala kibaka. Shaka ondoa

Inategemea, hizo tabia mbaya anazifanya kwa kulazimika au kwa kuchagua?
  • Kama anafanya kwa kukosa machaguo, akipata machaguo, anaweza kuchagua kuacha!
  • Kama amechagua hayo maisha, uwezekano wa kuacha ni next to impossible

Aksante kaunga.......lakini kama amechagua kuyafanya si anauwezo wa kuchagua kuyaacha au?
 
kama uamuzi wa kubadilika ulikuwa wa kwake binafsi uwezekano ni mkubwa akaendelea kuwa na tabia njema, ukiongezea na support anayopata kutoka kwa wanaompenda (u inclusive). lakini asiseme anataka kubadilika kwa ajili yako ww! muhimu ni kutambua kuwa kamwe huwezi kumbadilisha mtu tabia,inabidi ajutie na kutaka kubadilika yeye mwenyewe. manipulation haisaidii hata kidogo, lakini toa support yako inapobidi (kwa kumtia moyo na kumuombea pia). Mungu ameweka njia mbili mbele ya kila mwanadamu, huwezi kum'buruzia kwenda njia nzuri
Aksante King'asti nimekupata vilivyo. Ubarikiwe

Uwezekano wa kuziacha kabisa upo au wa kutoziacha,maana inategemea kwanini alikuwa anafanya hivyo,maana kama uchangu,wizi watu wengine wanafanya kwa ajili ya ugumu wa maisha,na wengine wanafanya hivyo kwa hulka na raha zao,thus inategemea na sababu kwanini huyo mtu alijiingiza huko.
Aksante Daffi......je unawezakubet ukajikomiti?? Au ndo hatuwezi kupredict?
MJ1 Nyani N kasema vizuri labda na mimi nifafanue zaidi

1.Wanasema chizi haponi ila huwa anapata nafuu tu,siku akiona jalala anatamani arudi kuchakuachakua.Hivyo kuna uwezekano huyo mtu
akarudia asili yake

2.Lakini kisheria pia mhalifu akipelekwa mahakamani kosa au makosa aliyofanya nyuma hayawezi kutumika kama ushahidi wa kuthibitisha uhalifu
wake alioufanya sasa.Mfano kama mtu anakosa la utapelii akakamatwa na kufunguliwa kesi kisha akatoka kwa dhamana naakiwa chini ya dhamana akatapeli mtu mwingine,mtu huyu akipelekwa mahakamani hiyo ni kesi mpya wala haitakuwa nauhusiano na ile ya mwanzo.

Kwahiyo yote yanawezekana ila isim judge mtu kwa past yake,wapo watu nawafahamu walikuwa na maisha machafu lakini sasa wana ndoa zao stable kuliko za wale walioonekana wana maadili.

Kila raheli,usisahau kutupa mshindo nyuma wa huu mchakato

Charger nashukuru kwa ufafanuzi huu umenisaidia kuclear some issues ambazo nilishaanza kuzijengea hoja.

Hahahaha Mshindo nyuma mtapata tu usikonde!
 
Aksante kaunga.......lakini kama amechagua kuyafanya si anauwezo wa kuchagua kuyaacha au?[/QUOTE]
Swali zuri sana hili
 
Anaweza kuziacha kbs au aziache kwa muda thn arudie tena. Ila sasa ukimkuta aliyeziacha, huwa anaziacha KABISA! anakuwa ni tofauti mpk ukiambiwa mambo aliyokuwa anafanya zamani huwezi kuamini!

Hili nalo neno MaVa....anawezaakaacha kabisa au kwa muda...Mh interesting
Mf. Jambazi, maisha yakiwawia magumu anauwezo wa kurudia? au huwa kuna check mechanisms!
 
My dear,

It is too risks!
It might happen again.
Why should you take a risk?
Does it worth it?
If yes, then go ahaead.
 
Na umri wangu huu nimeona wengi na mengi sana...Ila hata siku moja usiende sokoni kununua matatizo. Hata hivyo, siyo kweli kwamba kama asubuhi ilikuwa na mawingu mazito ya mvua basi jua haliwezi kutoka jioni..tena tamu na la nguvu!!

Mwaya..jitahidi kuchezea kwenye viwanja vyenye majani mafupi mafupi na visafi hata kama huna hakika kama ni natural au artificial!!
 
Huo ni mtihani MJ kwasababu jaribu vitu vingine na sio Maisha ya ndoa hasa kwa sisi ambao Talaka ni Mwiko.....

Duh nimekuelewa Mkirua ....hasa hapo kwenye Talaka Mwiko duh.........sasa napata picha kuwa ule usemi wa Mapenzi ni maua, popote huchanua na ule wa Love doesnt ask why itakuwa na maana nyingine kabisa ambayo mimi siielewi. Kwa mtindo huu, tunatakiwa kudirect hisia zetu za mapenzi kwa kutumia akili ni kama kuendesha gari, unalielekeza liende kule na lisiende huku. Mwe!
 
mkuu kunaa vitu viwili hapo,sababu iliyo mfanyaa mtu[kike]kuwaa changudoa,inawezekanaa ni maisha magumu yaliyo mpelekeaa yeye kuwaa hivyo ilaa moyoni mwake hapendi kabisaa hiyo biashara,so anapopataa mtu wa kumuowaa akabadilikaa kabisaa,na kuna mwingine ni hulka yake huyu ningumu kubalilikaaa,na ukibahatikaa kumpataa changu alie amuaa kutuliaa utafurahi kwani wanakuwaa si wa kuangaikaa ovyoo
 
Je kuna uwezekano wa kurudia tabia zake za zamani au huwa tunabadilika kabisa?

Jibu ni kwamba mtu anaweza kubadilika BUT Binadamu when cornered tends kufanya vitu ambavyo tumezoea and what appears natural to us;

Therefore swali ni kujiuliza je alikuwa na hizo tabia sababu ya mapenzi au kuna kitu kilichopelekea awe hivyo, mfano uchangudoa je ilikuwa njia ya kujipatia pesa au ilikuwa hobby, na kama ilikuwa njia ya kujipatia pesa je pesa zikiisha atarudi kufanya alichofanya...?

Mfano mwengine mtu alcoholic au drug abuser hata kama akiacha hii tabia vitu vikimwendea kombo huwa ana-seek refuge kwenye addiction yake ili kukimbia reality...

Therefore jibu kwa swali lako mtu anaweza kubadilika so long as situation iliyomfanya hadi ajikute ameingia kwenye hiyo tabia isijirudie.. hata kama asiporudi kwenye tabia yake it will take him more will power kuliko mtu ambae hajawahi kuwa na hiyo tabia (unless kwenye hiyo tabia yake alikumbwa na jambo ambalo lilimfanya achukie tabia yake; As you Know Once Bitten Twice Shy)

A Zebra can Never Change its Stripes????; Well Sometimes they can if they are breed with a horse...!!!! :)
 
Aksante Laaziz ...............nadhani ni sahihi kujievaluate na sisi wenyewe............lakini je ukijigundua kuwa wewe uko tayari ku'yaacha' yote utaijenga imani hiyo hiyo kwa mwenzi wako mtarajiwa??
Aksante kwa hiyo link

duhhhhhh!....ama kweli "....na aliye msafi aanze kutupa jiwe!"

Nimesoma michango mbali mbali ya kwenye topik hii, nime conclude kumbe wengi wetu tu wepesi kutupa mawe.
Hivi tunapoanza mapenzi tunatakiwa tuanzie wapi?

Siku tuliyokutana, au ndio inabidi tufungue CV nzima ya maisha ya mtu tangu alipozaliwa?
Je, ni halali kum judge mtu kwa matukio yaliyopita? unajuaje maisha yalimlazimisha kuyatenda yote hayo,
baada ya kuungama na kujitambua, akaamua kubadilika?

Naamini kila mwanadamu anastahili 2nd chance ya kuaminiwa jamani ama?
Hata mfungwa hutumikia kifungo chake, na akishamaliza adhabu anakuwa huru japo tayari keshakuwa branded mkosaji.
Anyway, Mwj1....kwa upande wangu inategemea kosa na kosa kwenye hizo tabia mbaya.

Kama mke/mume ana tabia 'unayoamini' haitabadilishika, then haina hata haja ya kujiingiza kwenye mahusiano hayo.
Haina haja kujiingiza kwenye mahusiano mguu mmoja,...uta trigger alarms tu ambazo mwenzako atakubaini na ata react
vile anavyodhania ni aheri kwake.
 
Aksante mydia kwa kunielewesha hapa. Nadhani ni kweli wengi wetu huwa tunapenda kujiwekea kinga hata mahali ambapo hatunauwezo wa kucontrol...............Ni sawa na vema kuaminiana na kujenga trust kwa mwenzako lakini Mbu kila kukicha huwa tunakutana na maneno haya...kunguru hafugiki..........n.k ndio maana nadhani tunayasumbukia haya makinga yaso na uhakika!!

Thanx darling! (I hope Babu hatokucharge mahari kubwa kwa hii sentensi)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Na umri wangu huu nimeona wengi na mengi sana...Ila hata siku moja usiende sokoni kununua matatizo. Hata hivyo, siyo kweli kwamba kama asubuhi ilikuwa na mawingu mazito ya mvua basi jua haliwezi kutoka jioni..tena tamu na la nguvu!!

Mwaya..jitahidi kuchezea kwenye viwanja vyenye majani mafupi mafupi na visafi hata kama huna hakika kama ni natural au artificial!!

kwenye viwanja vyenye majani marefu yanaweza kukatwa uwanja ukafaa tena kuchezewa...........je hayo majani mafupi hayaweze kukua? b.topic
kuna mazingira yanapelekea mtu kuwa na tabia hiyo.......kubadilika kwa tabia ya mtu inategemea yeye mwenyewe.........unaweza kutana na mtu aliyekuwa na tabia nzuri sana huko mwanzo ghafla bin vuuu anakuwa malaya/jambazi..........mabadiliko yapo
 
Aksante mydia kwa kunielewesha hapa. Nadhani ni kweli wengi wetu huwa tunapenda kujiwekea kinga hata mahali ambapo hatunauwezo wa kucontrol...............Ni sawa na vema kuaminiana na kujenga trust kwa mwenzako lakini Mbu kila kukicha huwa tunakutana na maneno haya...kunguru hafugiki..........n.k ndio maana nadhani tunayasumbukia haya makinga yaso na uhakika!!

Thanx darling! (I hope Babu hatokucharge mahari kubwa kwa hii sentensi)

LOL...mwache huyo, yeye anajipa moyo tshirt yenye jasho lake imesafiri!...
Wengine tuliambiwa...."naku miss hapa nimelala nimevaa chupi yako, !"...kumbe tulikuwa tunasaidiwa vile vile.

Mwj1...
if-it-aint-broke-dont-fix-it-150x150.png
"...if it aint broke, dont fix it!..."
Ni kweli nilikuwa na kunguru asiyefugika, lakini si kila ndege ni kunguru!...

Am an Opportunist,....nategemea sana huko mbele ya safari kuwa na mwenza ambaye
hata niki invest 99.9% ya mapenzi yangu kwake na bado aka ni disappoint kwa tabia zake
sita mjudge "wanawake wote ndio walivyo!" au CV yake ni mbaya tangia utotoni...
Akiamua kufanya ujinga wake kwenye mahusiano yangu, nitaanzia kumjudge hapo...sio ya awali.

Nilipojikubalisha nae, nilijua kuna vigezo atavyokuwa navyo, na kuna vigezo atakuwa na upungufu nao.
Mwenyewe na maskendeli na maskeleton kibao kabatini...hata nikichungulia mwenye hunitisha saa nyingine,...
lakini haina maana hilo halinizuii kujisemea yaliyopita yamepita, Umri umekwenda na busara inahitajika
kwenye maamuzi.

Kwa mgonjwa wa pombe (Alcoholic) hatua ya kwanza ya uponyaji ni kujitambua yeye ni mlevi na anahitaji msaada
...mteja wa unga, mzinifu, nk...wote wanaangukia kwenye kundi hilo...

Kinyume na hapo, nitadata nikimsubiria aliye mweupe kama karatasi. Kwa maisha ya sasa hayupo.
Sote tuna mapungufu kibao, ndio maana tumefungua darasa Jamiiforums.
 
sasa ambadilishe nani.. wewe... au yeye mwenyewe aamue jibadilisha,,,!!!!!
 
LOL...mwache huyo, yeye anajipa moyo tshirt yenye jasho lake imesafiri!...
Wengine tuliambiwa...."
naku miss hapa nimelala nimevaa chupi yako, !"...kumbe tulikuwa tunasaidiwa vile vile.

Toba Yaillah!! Mbu tartibu bwana ndo nini bwana? hapo kwenye angalizo mwe!! Inawezekana ni kweli anaivaa kila anapokukumbuka (akiwa hana hao wengine LOL)............yote maisha lakini ndio tumeumbiwa bana bila hizi experiences nyingine hatutokomaa!!

duh ama kweli mapenzi yanahitaji shule aksante kwa elimu hii.

Mwj1...
if-it-aint-broke-dont-fix-it-150x150.png
"...if it aint broke, dont fix it!..."
Ni kweli nilikuwa na kunguru asiyefugika, lakini si kila ndege ni kunguru!...

Am an Opportunist,....nategemea sana huko mbele ya safari kuwa na mwenza ambaye
hata niki invest 99.9% ya mapenzi yangu kwake na bado aka ni disappoint kwa tabia zake
sita mjudge "wanawake wote ndio walivyo!" au CV yake ni mbaya tangia utotoni...
Akiamua kufanya ujinga wake kwenye mahusiano yangu, nitaanzia kumjudge hapo...sio ya awali.

Nilipojikubalisha nae, nilijua kuna vigezo atavyokuwa navyo, na kuna vigezo atakuwa na upungufu nao.
Mwenyewe na maskendeli na maskeleton kibao kabatini...hata nikichungulia mwenye hunitisha saa nyingine,...
lakini haina maana hilo halinizuii kujisemea yaliyopita yamepita, Umri umekwenda na busara inahitajika
kwenye maamuzi.

Kwa mgonjwa wa pombe (Alcoholic) hatua ya kwanza ya uponyaji ni kujitambua yeye ni mlevi na anahitaji msaada
...mteja wa unga, mzinifu, nk...wote wanaangukia kwenye kundi hilo...

Kinyume na hapo, nitadata nikimsubiria aliye mweupe kama karatasi. Kwa maisha ya sasa hayupo.
Sote tuna mapungufu kibao, ndio maana tumefungua darasa Jamiiforums.

Na kweli mwaya ya nini kujipa presha ama sivyo itakuwa kila relationship unakondeana kwa dhana!! Umenikumbusha taarab flani ya zamaaani (in 1980s) sikumbuki iliimbwa na nani wala kikundi gani. Ilikuwa na aneno yasemayo......
Dhana usinidhanie, hofu moyoni kuweka
Mwengine sifikirie, Wewe sitokuepuka
Ridhika na Utulie, Uache kunung'unika X2

Chorus: Dhana usinidhanie, shaka moyoni kuweka
Daima mimi na wewe, mwenginewe hatozuka.

  • Thanks
Reactions: Mbu
Namjua mama mmoja ambae mwanae wa ndoa tunalingana tulikuwa majirani tangu utoto. Mama alikuwa muuza bar na aliolewa akiwa amezaa mtoto mmoja na mbaba ambae namjua na si aliyemuoa. Ila yule mama alikuwa na tabia nzuri kuliko wamama wengi niliowajua utotoni na ana mvuto kweli kweli. Tatizo ni mumewe bwana. Unajua wanaume wanaopenda wanawake walio na kazi zisizo na heshima kama kujiuza na kuuza bar most cases wanakuwa na wao hawajatulia. Kwa hiyo mama aliamua kutulia kabisa tena alikuwa mama wa kanisa; mumewe ambae alikuwa na kazi nzuri sana aliendelea kutembea na wauza bar wengine. Na alishafariki na kilichomuua bado ni utata. But they were married for more than 30 years before he died. Mkewe alikuwa ni mvumilivu hajabu na mtafutaji na ni wale mama ambao huwezi fikiri kama anagombana na mumewe (maana mumewe alikuwa mapepe kweli) kwa vile alimtoa mbali nadhani.

Ila mimi kama mimi siwezi kupenda mtu hopping nitambadilisha. What if hatabadilika??? Hapo ni kucheza karata. Kuna wadada nawajua waliolewa na wanaume wa maana lakini kwa kuwa walikuwa wanajiuza waliachika na tetesi ni kuwa waliendelea na biashara zao. Kuna wanaume nawajua walikuwa maplayer wameoa na wanaendeleza libeneke kama kawa na wake zao wanakuwa wadogo kwani walikuwa wanajua fika tabia za waume zao kabla hawajaolewa. Kwa hiyo ukiamua kuoa mtu mwenye tabia mbaya wewe jiwekee tu kuwa umekubali yote kuna kubadilika au kutokubadilika.
 
Tatizo ni kuwa ataendelea kusumbuliwa na wateja wake na wewe kama una wivu waweza kuishi maisha magumu sana. Afu kingine ni social stigmatization. Yani nduguzo wajue umeoa changu nambie mziki wake.

mkuu kunaa vitu viwili hapo,sababu iliyo mfanyaa mtu[kike]kuwaa changudoa,inawezekanaa ni maisha magumu yaliyo mpelekeaa yeye kuwaa hivyo ilaa moyoni mwake hapendi kabisaa hiyo biashara,so anapopataa mtu wa kumuowaa akabadilikaa kabisaa,na kuna mwingine ni hulka yake huyu ningumu kubalilikaaa,na ukibahatikaa kumpataa changu alie amuaa kutuliaa utafurahi kwani wanakuwaa si wa kuangaikaa ovyoo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom