Mh. Zitto respect...

ukazkazini uko wapi hapo?kusema kweli ndo ukazkazini?zitto anafaa kusifiwa ila pia ni mtu wa kuogopwa

Ukweli upi umesemwa hapo? Halafu kama wewe ni mtu makini just try to read between lines you will sense a smell of Ukaskazini kwenye post ya huyo nduguyo. Halafu kama siyo unafiki wa kutupwa, kwa nini umsifie mtu halafu umuogope? Huo ni uvuguvugu ambao ni hatari kwa kijana. Kamanda Lissu alishawahi kusema "Ukiwa mnafiki ujanani, uzeeni lazima uwe mchawi/mwanga" take care kijana.
 
Yaani mtu akiangalia ulichokiorodhesha hapo atagundua moja kati ya mawili yafuatayo.
1. Umeathirika na mfumo kaskazini ndani ya CDM
2. Unapenda sana story/ umbea wa kwenye vijiwe vya kahawa na kwa jinsi una akili ndogo unauamini bila hata kutafiti.
Ntakusaidia kwa machache yanayozungumzika lakini kwenye mambo ya umbea peleka hukohuko kwenye vijiwe vya kahawa.
Zitto alisema hapa jukwaani kwamba hajamjibisha yule mzee wenu kwenye gazeti tajwa ingawa hakubaliani na mawazo yake ya kibaguzi. Hata mimi binafsi sikubaliani na mtu mwenye mawazo ya "kijinga" kama ya kale kazee.
Kuhusu kutaka nadaraka kwani ni dhambi kusema malengo yako ya baadaye ndani ya CDM? Huu ni upuuzi.
Halafu sidhani kama mnamfamyia haki Zitto kumchagulia hadi marafiki ama watu wa kuinteract nao. Mbona hamuulizi uhusiano kati ya Mbowe na William Malecela? Acheni wivu wa kijinga. Maana ya upinzani sio uadui, zinapingana hoja na itikadi zetu lakini in normal life sote ni Watanzania.
Hayo mengine uliyosema yamejaa umbea na hayajibiki na mtu makini.

kaka uko alright sna jamaa anataka siasa nayo iwe km simba na yanga wanavyovyomwagiana chupa za mkojo uwanja wa taifa
 
Hizi ndio zilezile nyuzi ambazo magamba wakiweka huwa wanalipwa na wakina NApe. Wana CDM!!! Ccm wanataka kutumia jina la zitto kusambaratisha Chama Chetu jamani tuzipuuze hizi thread za kijinga tusi comment tuangalie watafanyaje! Kwani huyo zitto yupo ccm ? Tunawaburuza tuu kwanini wasimpe big up lusinde Pambaf !!!
 
Kwanza nitoe pongezi kwa mh.zitto kwa jinsi alivyoliongoza taifa la walalahoi(wananchi walio wengi) kutetea au kuzungumzia masuala na pointi muhimmu leo bungeni..bigup kaka.
mh.mnyika sijakusahau..

ila namzungumzia zitto kwa sababu kuna vidudu mtu vina roho za unafiki,umbea na kuchafuana za kumsemea vibaya mh.huyu..
eti mara ni gamba,mara anatumwa,mara....etc
Hivi kweli Tz hii na CDM kwa ujumla mnaweza kuipuuza michango na nondo anazozitoa zitto,
au ndio wale wale anao sema MR.BEN MKAPA kua ni wavivu wa kufikiri.

Mbona wewe husimami tukakuona michango yako katika taifa hili,kazi kufyata tu na kuwachafua wenye akili zao.
Alitoa mtazamo wake kuhusu uprezida,na hakusema anagombea,ila akadai anasifa stahiki za kufanya hivyo ila ni kwa ridhaa ya chama chake na wananchi kwa ujumla ndio wenye uwezo wa kumpa nafasi hiyo..na kweli sifa anazo kama hutaki meza wembe.

Kati ya mawaziri wako hapa TZ,nani anamgusa,ukitaka kujua moto wake muulize mkulo na enzi zile KALAMAGI.watakusimlia A-Z.

USHAURI:
simama kwa miguu yako,angalia unakokwenda,pia kumbuka ulikotoka ili ikusaidie kuongeza mwendo ufike haraka uendako.(usisahau kuangalia chini usijikwe)
majungu,fitina,umbea na roho mbaya hivina msaada kwako.watie nguvu na imani wale waliokwisha simama kuonyesha njia na matumaini kwa WA-TZ wengi,
sio kuendekeza chuki zisizo na msaada kwako na taifa kwa ujumla..

BIGUP MH.ZITTO...tupo pamoja

RETHINK

fanya kila jambo mahala pake, kwa wakati wake, vinginevyo inakuwa ni fujo. Wakati watu wanakula chakula, utakapoanzisha wimbo na kuwaambia wanaokula waitikie na kucheza, unakuwa umefanya ndivyo sivyo. Kampeni kichama ziko arumeru, wewe unasimama jukwaani na kutamka mimi URAIS ninautaka! How fool are you! Acha hizo wewe.
 
Chadema sio jambo la kuficha kama hujatoka huku kwetu kask tunakuangalia kwa macho mawili mawili ndo tukupe uongozi tena kama hueleweki ndo kabisaa sahau.Tunaogopa chama kisije kikafa tukiwepo zitto ni kijana mzuri lakini mhh
 
Mh kaongea, Sugu kaongea, mnyika kaongea, na kipengele kubadilishwa CDM wameongea, nadhani wawe inpirations kwa vijana wa CCM km akina January.Nadhani chadema wawe km bacelona wapende sifa za pamoja,ccm pia, na mwishowe wote wapeane pongezi linapokuja suala la kitaifa.
 
Mwana CDM yeyote akianza kusifiwa na CCM au akiwa anawasifia CCM anakosa sifa ya kuwa kiongozi ndani ya CDM na ana amua kwenda CCM au kubaki kama mwanachama wa kawaida...

Mpende Msipende, Maana CDM itakuwa ni sasa na CCM endapo mtu huyo akiwa kiongozi mkuu wa Chama au Nchi..

Huhitaji kuwa na Degree kuiona hilo bali Common sense tu.
 
Kwanza nitoe pongezi kwa mh.zitto kwa jinsi alivyoliongoza taifa la walalahoi(wananchi walio wengi) kutetea au kuzungumzia masuala na pointi muhimmu leo bungeni..bigup kaka.
mh.mnyika sijakusahau..

ila namzungumzia zitto kwa sababu kuna vidudu mtu vina roho za unafiki,umbea na kuchafuana za kumsemea vibaya mh.huyu..
eti mara ni gamba,mara anatumwa,mara....etc
Hivi kweli Tz hii na CDM kwa ujumla mnaweza kuipuuza michango na nondo anazozitoa zitto,
au ndio wale wale anao sema MR.BEN MKAPA kua ni wavivu wa kufikiri.

Mbona wewe husimami tukakuona michango yako katika taifa hili,kazi kufyata tu na kuwachafua wenye akili zao.
Alitoa mtazamo wake kuhusu uprezida,na hakusema anagombea,ila akadai anasifa stahiki za kufanya hivyo ila ni kwa ridhaa ya chama chake na wananchi kwa ujumla ndio wenye uwezo wa kumpa nafasi hiyo..na kweli sifa anazo kama hutaki meza wembe.

Kati ya mawaziri wako hapa TZ,nani anamgusa,ukitaka kujua moto wake muulize mkulo na enzi zile KALAMAGI.watakusimlia A-Z.

USHAURI:
simama kwa miguu yako,angalia unakokwenda,pia kumbuka ulikotoka ili ikusaidie kuongeza mwendo ufike haraka uendako.(usisahau kuangalia chini usijikwe)
majungu,fitina,umbea na roho mbaya hivina msaada kwako.watie nguvu na imani wale waliokwisha simama kuonyesha njia na matumaini kwa WA-TZ wengi,
sio kuendekeza chuki zisizo na msaada kwako na taifa kwa ujumla..

BIGUP MH.ZITTO...tupo pamoja

RETHINK

Umetumwa? Hatuhitaji mropokaji wa kwenye majukwaa. For now mwambie he has to strugle very much for WISDOM and TEAM WORK. aache kulewa misifa. ( THE GUY IS SO CONTRAVERSIAL).
 
ukomavu gani wa kisiasa am ao unauzungumzia ww? Huu wa kumtukana founder wa chama chako tena hadharani kwenye magazeti ya jambo leo, au ule wa kutaka madaraka kwa udi na uvumba? Au ule wa kumshawishi Halima mdee wasitoke nje ya bunge eti kisa JK ni muislamu mwenzake? Au ule wa kumpigia kampeni Jakaya badili ya mgombea urais wa chama chake(slaa) 2010? Au ule wa kushirikiana na usalama wa taifa kuchakachua kura za slaa 2010? Au ule wa kuwatetea wakina nape kwenye vyombo vya habari kuliko hata wenzake wakina mnyika? Au ule wa kumtumia kafulila kuivuruga Nccr? Au ule wa kuitetea dowans ilipwe? Au ile ya kutangaza nia ya urais kipindi wenzake walikuwa vitani arumeru? Au ule wa kupewa vyeo kibao na ccm ili kuziba mdomo kwenye mambo yatakayogusa maslahi ya ccm? Au ule wa kumsingizia marehemu Regia mtema ndio alotowa wazo la kuonana na rais badala ya kamati kuu ya chama? Au ule wa kuandaa genge la vijana maradical wahuni kuvuruga uchaguzi wa bavicha 2010? Au ule wa kuwa na urafiki wa kushibana na akina Rostam? Au ule wa kuhongwa mabati na barick ili usiwakemee tena mjengoni?
BASI NIPE JIBU JE KATI YA BAADHI YA UCHAFU HAPO JUU KWELI NDIO UKOMAVU WA KISIASA AU NI UMAITI WA KISIASA?
Tanx u a lot. LONG LIVE ZITTO AND BIGUP PEZDAA"

What do you mean? WEWE NDO MIONGONI MWA HAO ZITTO'S ENEMIES,LAKINI USIJALI KWANI HAYO NDO YATAMFANYA AWE MWANASIASA NA MTAWALA BORA,MH ZITTO ANASOMA KUPITIA WALIMU WENGI,WEWE UKIWA MMOJA WAO,NA IPO SIKU MTAKUWA NJIA MOJA.
 
ukazkazini uko wapi hapo?kusema kweli ndo ukazkazini?zitto anafaa kusifiwa ila pia ni mtu wa kuogopwa

Sure, zitto ni wakumuogopa kama ukimwi kwani ni mtu ambaye hatabiriki, yaani ana unafiki fulani, kwa mtazamo wangu hafai kuongoza nchi kwa nafasi ya urais. Atakuwa kama kikwete jinsi jamii ilivyo mwamini kumbe alikuwa na moyo wenye hila, sasa mambo yanaenda mzobemzobe
 
Hakuna mtu mnafiki na ndumilakuwili katika siasa za tz kama zitto kabwe!mimi natokea mwanza huyu habaguliwi na cdm ni ndumilakuwili wa hatari!anajifanya yuko juu ya cdm.akae akijua hamna mtu yuko juu ya chama!cdm walipotoka bungeni 2010 alisema wametoka kisa jk ni muislamu!leo hii anamshambulia mtei kwa maoni yake.mimi ni kijana wa 25 yrs msukuma mwana cdm ntaanzisha movement ya kuwaelimisha vijana wote wa tz kuhusu huyu ndumilakuwili.leo anaidhoofisha cdm kesho anajifanya kushambulia serikali wajanja tumeshamjua!tatizo la aliyeleta hii thread amedandia siasa.shame on you na zitto kamwe hatapata urais kupitia cdm labda aende ccm.kwa nini awe yeye tu???mbona lissu,lema,mnyika pia wako juu mbona hawapo kama huyu ndumilakuwila!!!!!!!!!!!!!
Mfatilieni kila siku ni mtu wa chokochoko za kuibomoa cdm!hatafanikiwa
 
hakuna mada hapa ila kuna malumbano na vijembe visivyo na tija. ngoja niendelee kuandika kitabu changu sina cha kuchangia hapa.
 
japokuwa na umahili wote huo zitto but bado hujazidi sifa za kiushujaa kama za jembe langu lema.

neno la hekima..........

kwenye team moja, kwa mfano ya soka, wachezaji wote hawafanani kiuchezaji lakini kila mmoja ana mchango wake mkubwa katika timu.

mathalani barcelona wana messi (tuseme huyu ni zitto), halafu kuna xavi (mnyika), lakini pia kuna puyol(labda huyu ni sawa na lema). usipomtumia mmoja kati ya hawa, lazima timu haitakuwa katika kiwango chake.
 
Vijana wa CDM wanafanya kazi wote na si Zito peke yake. Tunakubali kazi yake Zito lakini tusisahau utata wake pia. Hivyo tunamuomba apime kila jambo kabla ya kutoa hewani.
 
Yaani mtu akiangalia ulichokiorodhesha hapo atagundua moja kati ya mawili yafuatayo.
1. Umeathirika na mfumo kaskazini ndani ya CDM
2. Unapenda sana story/ umbea wa kwenye vijiwe vya kahawa na kwa jinsi una akili ndogo unauamini bila hata kutafiti.
Ntakusaidia kwa machache yanayozungumzika lakini kwenye mambo ya umbea peleka hukohuko kwenye vijiwe vya kahawa.
Zitto alisema hapa jukwaani kwamba hajamjibisha yule mzee wenu kwenye gazeti tajwa ingawa hakubaliani na mawazo yake ya kibaguzi. Hata mimi binafsi sikubaliani na mtu mwenye mawazo ya "kijinga" kama ya kale kazee.
Kuhusu kutaka nadaraka kwani ni dhambi kusema malengo yako ya baadaye ndani ya CDM? Huu ni upuuzi.
Halafu sidhani kama mnamfamyia haki Zitto kumchagulia hadi marafiki ama watu wa kuinteract nao. Mbona hamuulizi uhusiano kati ya Mbowe na William Malecela? Acheni wivu wa kijinga. Maana ya upinzani sio uadui, zinapingana hoja na itikadi zetu lakini in normal life sote ni Watanzania.
Hayo mengine uliyosema yamejaa umbea na hayajibiki na mtu makini.

Ningekuona unabusara kama usingekua mbaguzi! Ukaskazini? Kajipange upya weye!
 
Back
Top Bottom