Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Mnataka hizo data ili iweje?
La msingi siyo Waziri kufahamu idadi KAMILI, bali tunategemea angefahamu na kutoa ANGALAU rough estimate au approximation kwa mfano, "ninakisia idadi ya magereza nchi nzima ni zaidi ya elfu moja na mia tano" mfano. Kwa kushindwa kutoa ANGALAU makisio ya juu juu ni dalili kwamba hayuko serious and he's basically incompetent.
Wewe si ni mzee wa preciseness wewe? Mimi siridhiki na hiyo "I don't have this info off the top of my head". Hiki siyo kitu kinachobadilika badilika kama idadi ya wahamiaji haramu kutoka Mexico. Hatujengi magereza mapya kila mwaka. Waziri mhusika anatakiwa kujua idadi yake period.
Mnataka hizo data ili iweje?
Mbona wagumu kutofautisha nini tofauti ya mtu kusema "I don't have this info off the top of my head" na "we don't have this info" ?
Yaani watu walivyomshupalia utadhani kasema Wizara haijui tuna magereza mangapi, kumbe data zipo na zimewekwa mpaka mtandaoni, na link tumetoa hapa.
Hivi mnafikiri hii decision making process inafanywa on the fly, off the top of people's heads?
This is exactly what Clouds FM intended, kuwa distract watu kutoka ku discuss serious issues kibao, waende ku focus kwenye trivialities za namba ya magereza. Na wabongo wamekubali line, hook and sinker.
At the end of the day Masha kafanya interview, kaulizwa softball questions, kashafanya distractions, watu wanaongelea trivia.
Akiulizwa anatamba I am in touch with the people and the press, I just did a live interview with a popular radio station and took some burning questions.
Huku watu hawaongelei strategy wala policy, wana focus kwenye trivia za accounting.
Masha na Hando (wa Clouds) walikuwa wanajadili mambo mbalimbali yanayohusu Wizara ya Mambo ya ndani. Walikuwa wanajadili kitengo kimoja hadi kingine. Walipofika kwenye idara ya magereza Hando ali raise issue ya msongamano wa wafungwa/mahabusu katika magereza na basically kutaka kujua wizara/ waziri anafanya nini katika kutatua hilo tatizo.
Sasa ili kusema/kukubali kuwa kuna msongamano ni lazima ujue idadi ya wafungwa/mahabusu na pia capacity ya magereza. Kwa maoni yangu kama jambo hili waziri angekuwa kweli analishughulikia sioni ni kwa nini ashindwe kusema uwezo wa magereza yaliyopo ni upi na idadi ya wafungwa/mahabusu ni ipi. Kwa bahati nzuri alikuwa anakumbuka idadi ya wafungwa na mahabusu (ingawa alikiri sio actual figure) lakini ilipokuja idadi a magereza alishindwa kusema yapo mangapi au angalau angeweza kusema basi hayo magereza yanaweza kuaccomodate wafungwa/mahabusu wangapi (hata kama info hii ipo kwenye website!). Badala yake aliishia kusema aina za magereza zilizopo (max security, ya kilimo, ya wazi nk), jibu ambalo kimsingi lisingeweza kuonesha uwezo wa magereza yaliyopo.
Mimi nilitegemea baada ya kusema hakumbuki idadi kamili ya magereza angalau angesema yaliyopo yana uwezo wa kuchukua wafungwa/mahabusu wangapi ili kuweza kuonesha upungufu uliopo na then alieleze mikakati waliyonayo (say kupunguza mahabusu kwa kiasi fulani, kujenga/panua magereza yawe na uwezo fulani nk nk). Alisema anatembelea magereza mara kwa mara, sasa kama hilo ni kweli na yupo makini angalau angeweza kuonesha huo msongamano kwa kutolea mfano gereza mojawapo kwamba lina uwezo X lakini linapewa mahabusu/wafungwa Y and hence an overload of Z.
Sasa ukiniambia Masha hajui magereza yako overloaded kwa kiwango gani nitaona kachemka. na usiniambie inabidi ujue idadi ya magereza ili ujue magereza yako overloaded kwa kiasi gani, si kweli.
Katika mjadala huo wa msongamano hakuweza kusema magereza yako overloaded kwa kiasi gani. Hilo swali la idadi ya magrezea kimsingi lilikuwa linalenga kutaka kujua msongamano(overload) ni kiasi gani na wizara imejipanga vipi.
Nimecheka sana ninapo-imagine Waziri wa wizara ya mambo ya ndani hana makadirio ya askari police, idadi ya magereza, vituo vya police kichwani mwake.... anategemea computer. Hii ni sawa na mtu kutojua (visualize) urefu wa mita kumi ukoje. Mpaka uletewe mita upime. Kiranga watu hatutaki exact figure.... tunataka angalau makadirio ya karibu + or - something. Vinginevyo inaonyesha asivyowajibika na kazi yake...
Sarungi alikuwa anafanya kazi hata majina ya wasaidizi wake ilikuwa inabidi akumbushwe kila siku, lakini alikuwa mtendaji mzuri tu.
Si lazima kuweka kila kitu kwenye kichwa wakati unaweza kukipata kirahisi.
Now kama Masha angekuwa nuclear physicist aliyegundua nuclear formulaes ambazo hazitakiwi kuandikwa popote, halafu anazisahau sahau, hapo ningeona kuna issue.
Hii thread ilivyokuwa framed kwamba Masha hajui idadi ya magereza iko totally misleading. It actually trivialize the issue of prison overload.
Hii sasa ni ugonjwa... na sitakubali lihalalishe hii issue ya Masha...
Alisema anatembelea magereza mara kwa mara, sasa kama hilo ni kweli na yupo makini angalau angeweza kuonesha huo msongamano kwa kutolea mfano gereza mojawapo kwamba lina uwezo X lakini linapewa mahabusu/wafungwa Y and hence an overload of Z.
Hii sasa ni ugonjwa... na sitakubali lihalalishe hii issue ya Masha...
Hii sasa ni ugonjwa... na sitakubali lihalalishe hii issue ya Masha...
Masha katika hili yuko precise, hakuevade swali, amesema sijui jibu off the top of my head.That is precise to me. Ungeweza kusema hayuko precise kama angetoa a rough estimate, lakini hakutoa.
Wizara iko precise, imekupa breakdown ya magereza by wilaya.
Preciseness gani unayoitaka hapa?
Nyie mnaopiga kelele Masha akumbuke details zote si ajabu hata anniversaries za ndoa/ uchumba/ birthdays hamkumbuki, halafu mnataka damu za wenzenu.
In any case, a more important issue than the mere number of prisons has been identified.I would rather focus on this than the trivia of number of prisons like we are on some TV prize show for useless knowledge.
"just below/above xxx", "not more than xx", "less than xxxx" ni bora maradufu kuliko NO NOTHING. Bila makadirio/makisio yoyote mtu huwezi kuwa na angalau idea ya idadi halisi - who knows, magereza yanaweza kuwa 10 au hata zaidi ya 100,000.
Usikute jamaa alikuwa na early stages za Alzheimer's lol....
Kwa kifupi mimi huyu Masha sijaridhishwa na utendaje wake. Kwanza utendaji mzima wa serikali siridhishwi nao.