Elections 2010 Mh. Vuai Nahodha nini nafasi yake baada ya Uchaguzi?

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Kama CCM ikichukua Zanzibar, Mh. Nahodha hawezi kuwa Waziri Kiongozi. Je ni nafasi gani atapewa?

1. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje?

2. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano?

3. Waziri ndani ya SMZ?

4. Katibu Mkuu CCM?

5. Katibu Mwenezi CCM

6. ????
 
Utamaduni wa kupenda madaraka sijui utakwisha lini TZ, hivi akitulia kijijini kwake akafanya miradi yake na kufaidi pension yake kuna ubaya gani?
Mimi ningependa apumzike awaache wengine nao watengeneze CV
 
Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka(ya kisiasa),utakuta mtu alikuwa hajulikaniki,lakini baada ya kupata tu hayo madaraka kuacia inakuwa nongwa,angalia wabunge kelele kila siku za kutaka wabakie kuwa wabunge,akina Makweta,Ngombale,Mungai,Malechera.
Kama kuacha madaraka angeacha Dr Shein na Bilali lakini wapi ,wanataka wasikike wao na watoto wao,anagalia watoto wao akina Hussein Mwinyi,Ridhiwani,Vita Kawawa,Januari Makamba.
Zamani nilikuwa nawacheka Wakenya ambao watoto wao walikuwa wanarithi ubunge kutoka kwa baba zao utafikiri watoto wa kichifu lakini

sasa ndio tunayaona Tanzania.Wengi wao hawana uwezo mbali ya kuwatumia wazazi wao walio kwenye madaraka.
AHERI YA ULEVI WA GONGO KULIKO ULEVI WA MADARAKA
 
Utamaduni wa kupenda madaraka sijui utakwisha lini TZ, hivi akitulia kijijini kwake akafanya miradi yake na kufaidi pension yake kuna ubaya gani?
Mimi ningependa apumzike awaache wengine nao watengeneze CV
Kwanini tusitumie ujuzi na uzoefu wake kuendeleza mbele maendeleo yetu? Vijana wapya wa dot com hawana uzoefu na wana tamaa sana, harakaharaka anataka gari, nyumba, shamba katika miaka miwili tu ya kazi. Acha tufaidi busara za wazoefu. Alifanya vizuri sana kipindi chake zenj.
 
Kwakuwaameshafikiakuwawazirikiongozihawezi kupewamadaraka yoyote yale ndani ya Zenji zaidi a kuwa Rais wa visiwa hivyo au kupewa uwaziri mkuu bara au zaidi ya hapo.

Na kama atakosa vote atabaki kama mwakilishi wa kawaida kama alivyo Mzee Malecela au Lowassa.

Safari hii ameinamua kugombea mjini katika jimbo la mwanakwelekwe
 
Utamaduni wa kupenda madaraka sijui utakwisha lini TZ, hivi akitulia kijijini kwake akafanya miradi yake na kufaidi pension yake kuna ubaya gani?
Mimi ningependa apumzike awaache wengine nao watengeneze CV

Akirudi kijijini atachaka kama mangula.
 
Kwanini tusitumie ujuzi na uzoefu wake kuendeleza mbele maendeleo yetu? Vijana wapya wa dot com hawana uzoefu na wana tamaa sana, harakaharaka anataka gari, nyumba, shamba katika miaka miwili tu ya kazi. Acha tufaidi busara za wazoefu. Alifanya vizuri sana kipindi chake zenj.

Kwani EPA, Richmond, Meremeta nk. zilifaywa na vijana? Uzoefu ndiyo kitu gani, Masha alikuwa na uzoeu gani wa uongozi kumzidi Kagasheki?Msiwaonee vijana pia wanadeserve kuishi maisha mazuri iwapo tu mifumo inaruhusu kupata vitu hivyo. Mimi sijawahi kukwapua hela ya mtu baada ya kuhitimu lakini nimejitahidi nimepata hivyo wengine pia watatamani wafike hapo. Lakini siyo wabanwe kwenye ushenzi wa TGS D wazee wakwapue mseme vijana wana tamaa. Kwani mshahara wa professionals kwa nchi zetu za kiafrika wakilipwa watz watashindwa kupata hayo mpaka mtu aende Botswana au South ndiyo tuone anaweza kuwa na vitu hivyo.

Vuai kaingia madarakani katika umri mdogo sana. Kustaafu sasa hivi ni matumizi mabaya ya nguvukazi. Kweli hii ni Changamoto inayotokana na kuanzia juu "He is a victim of his own success"
 
kwa sasa hakuna kazi inayomfaa nahodha,iwe bara au visiwani.maana pinda lazima aendelee kuwa waziri mkuu,na nahodha hawezi kupewa aendelee tena na uwaziri kiongozi maana atakuwa kikwazo kwa dr shain..na hawezikushuhwa madaraka kwa kupewa uwaziri wowote ule zaidi ya uwaziri kiongozi..du kazi ipo hapo.ila sitashangaa akiendelea na uwaziri kiongozi
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom