Mh. Tundu lissu anena kabla ya hukumu asubuhi hii

Status
Not open for further replies.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
KESI inayomkabili mbunge wa Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, iliyofunguliwa mjini Singida
kupinga ushindi uliomweka madarakani, itatolewa leo ijumaa (Aprili 27, mwaka huu).

Hukumu itatolewa na Jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.

Kesi hiyo imekuwa kivutio sana kwa wananchi wengi wa mkoa Singida na nchini kwa ujumla, kutokana na umaarufu wa mbunge huyo machachari. Jaji anayesikilia shauri hilo mjini Singida, anatoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro.

Walalamikaji wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Ddoma, wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kjtoka mkoani Dodoma, na Lissu amejisimamia mwenyewe. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa CCM, kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na dosari nyingi.

Katika mahojiano na Lissu, amesema vyovyote mahakama itakavyo hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa mbunge wa kwanza kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati. Amesema, kanda hiyo ilijulikana sana kuwa ngome ya CCM, lakini amefanikiwa kuchaguliwa na wananchi ili awatumikie.
 
Kumbuka pia kuwa Kanda ya Kati Tanzania ndio eneo lenye nyumba nyingi za TEMBE na NYASI kuliko ukanda wowote ule duniani. Mungu amewapa Lissu ili awakomboe kwa hiyo sina shaka hata wakimvua ubunge atarudi tena. Kwa kuwa Jaji anaonekana sio MHAYA unafiki unaweza usiwepo...
 
Tuko nyuma yako TL, NA tunauthamin mchango wako kwenye jimbo lako na nje ya jimbo lako. Sasa tunajua kinachoendelea
 
Kanda za kati na kuzini yenye mikoa ya SINGIDA, DODOMA, MTWARA, LINDI,na RUVUMA, ndiyo ngome za ccm lakini ndiyo mikoa iliyo na maendeleo duni kuliko sehemu yoyote hapa nchini. W
 
Kumbuka pia kuwa Kanda ya Kati Tanzania ndio eneo lenye nyumba nyingi za TEMBE na NYASI kuliko ukanda wowote ule duniani. Mungu amewapa Lissu ili awakomboe kwa hiyo sina shaka hata wakimvua ubunge atarudi tena. Kwa kuwa Jaji anaonekana sio MHAYA unafiki unaweza usiwepo...

umeongea fact mkuu,kanda ya kati ndo makazi duni kwa kuishabikia ccm
 
Hawata thubutu kumvua mtu yeyote ubunge kwa sasa, hawawezi gharama za kushndwa ktk chaguzi ndogo.
Wamemvua Lema wameona kazi yake Mwanza, Geita na kwingineko alipoenda kushitaki kwa wananchi
 
Huyo jaji atende haki wala asiingiliwe katika maamuzi ili kumfurahisha mkubwa fulani kwani wanaweza kufikiri wanamkomoa kumbe wanamkomaza kisiasa na kumuongezea sifa pasi na sababu yoyote ya msingi.
 
Hii ya Lisu anaweza kushinda. Jamaa wanaweza kumwambia Jaji amwachie tu huyo! Jimbo la Arusha wanalitaka kwa nguvu ndo maana wanataka kumpiga chini Lema.
 
Roho inaniuma sana:A S-cry:

Bukanga,

Ni kweli kaka.Jipe moyo kamanda.Roho inauma kwa kuwa chombo kinachotakiwa kusimamia haki hakina confidence ya umma.Chombo kinachotakiwa kutoa haki kina historia ya kunyonga haki.Kwangu mimi vyovyote itakavyokuwa Tundu Lissu anabaki kuwa role model katika kusimamia kile anachoamini na pia ni alama ya kupigana na impunity.Ni catalyst katika mabadiliko tuyatakayo.Naomba wale wabakaji wa demokrasia warudie tena kosa ili kuimarisha M4C.Waache watuongezee makamanda wa
kuharakisha mabadiliko ikiwezekana kabla ya 2015
 
kila wanachodani CCM kuwa wakifanya kitawaokoa ni njia ya kujipeleka kaburini wao wenyewe, kupinga ubunge wa wabunge wa CHADEMA ambao mpaka sasa wamwshakubalika kwa asilimia 100 kwa watanzania ni kujipotezea wakati bureee..hata wakimvua ubunge LISU bado CHADEMA ktashinda majimbo yote wanayohisi ni yao CCM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom