Mh Sumaye achaguliwa kuwa mkurugenzi CRDB

Wanahisa wa kampuni huwa na haki ya kuthibisha wakurugenzi wote waliopendekezwa kuwa kwenye bodi ya wakurugenzi. Bodi ya wakurugenzi ina wakurugenzi wa aina mbili. Kundi la kwa kwanza linakuwa na wakurugenzi ambao wanafanya kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza executive directors). kundi la pili linakuwa na wakurugenzi ambao hawafanyi kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza non-executive directors). MAKUNDI YOTE MAWILI YANATHIBITISHWA NA WANAHISA SIKU YA KIKAO CHA MWISHO WA MWAKA WA FEDHA WA KAMPUNI HUSIKA. Kwahiyo basi CRDB itakuwa imepitisha wakurugenzi wa bodi leo ambapo Sumaye naye amedhibitishwa kuwa mkurugenzi. kwakuwa sikuwepo wala sijasikia agenda na wakurugenzi watarajiwa wa kampuni hiyo sijui kama amethibitishwa kuwa mkurugenzi wa kundi la kwanza au la pili. Ila mara nyingi sitegemi waziri mkuu mstafu awe executive director. Nadhani maelezo haya yatakuwa yamesaidia kiasi kwa watu kuelewa taratibu za uongozi kwenye makampuni duniani.

Mkuu uko sahihi. Non-executive directors huchaguliwa, executive directors huomba kazi na kuhojiwa na bodi ya wakurugenzi ama kamati ya bodi hiyo nadhani kisha wanapata baraka za AGM. Hawa executive directors huunda Management Team.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wanahisa wa kampuni huwa na haki ya kuthibisha wakurugenzi wote waliopendekezwa kuwa kwenye bodi ya wakurugenzi. Bodi ya wakurugenzi ina wakurugenzi wa aina mbili. Kundi la kwa kwanza linakuwa na wakurugenzi ambao wanafanya kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza executive directors). kundi la pili linakuwa na wakurugenzi ambao hawafanyi kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza non-executive directors). MAKUNDI YOTE MAWILI YANATHIBITISHWA NA WANAHISA SIKU YA KIKAO CHA MWISHO WA MWAKA WA FEDHA WA KAMPUNI HUSIKA. Kwahiyo basi CRDB itakuwa imepitisha wakurugenzi wa bodi leo ambapo Sumaye naye amedhibitishwa kuwa mkurugenzi. kwakuwa sikuwepo wala sijasikia agenda na wakurugenzi watarajiwa wa kampuni hiyo sijui kama amethibitishwa kuwa mkurugenzi wa kundi la kwanza au la pili. Ila mara nyingi sitegemi waziri mkuu mstafu awe executive director. Nadhani maelezo haya yatakuwa yamesaidia kiasi kwa watu kuelewa taratibu za uongozi kwenye makampuni duniani.

Kwenye maelezo yako kuna sehemu uko sahihi na zingine hauko sahihi. Iko hivi , ni kweli kuna kuna aina mbili za wakurugenzi, ila executive directors hawachaguliwi na mkutano mkuu kwani wao ni waajiriwa na wanalipwa mishahara, wao huchaguliwa na bodi ya wakurugenzi ambayo inaundwa na non executive directors. Na hao non executive directors huchaguliwa na mkutano mkuu wa wanahisa, ambapo wao wanakuwa sio waajiriwa bali wanalipwa directors fees. Sasa Sumaye yeye ni Non executive directors !
 
Benki ya CRDB leo hii ilikuwa inafanya mkutano wake mkuu wa 16 huku Arusha katika ukumbi wa AICC. Katika kikao hicho, Mh. Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye alikuwa anagombea ukurungezi wa benki hiyo, ambapo wanahisa walimchagua kwa kwa asilimia 60%.

Tunakupongeza Sumaye kwa kuchaguliwa kwako, sasa chapa kazi na usiingize siasa katika benki.

Hiyo ndio nafasi nzuri kwa Sumaye kurudi tena kwenye siasa. Huyu bwana bado hajakamilisha ndoto yake ya kuwa mkuu wa nchi hapo anajijenga upya umesahau alikwenda masomoni juzijuzi tu unafikiri ni kwa nini?
 
Sumaye hafai kuwa rais wa nchii hii. mikataba mingi mibovu ilisainiwa akiwa waziri mkuu na mtu dikteta mkubwa huyu hafai hata kidogo!
 
Siamini kama kuna benki makini ikamchagua mkurugenzi kwa staili hiyo. Huyu atakuwa amechakuliwa ama kuwa mwenyekiti wa wanahisa au mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ingawa hili la pili pia sio rahisi kuchaguliwa kwa staili hiyo. Mtoa thread atakuwa hakuwa makini katika kujua ukweli hebu afuatilie tena upya ili ku-edit hiyo thread na kuja na kitu sahihi. Hata Sumaye mwenyewe hawezi leo akawania kuwa kurugenzi wa benki CRDB, ni kujishushia hadhi kwake yeye na si mtaalamu wa maswala ya fedha.

Kwa lugha nyingine wanaitwa non-executive directors. Au wana Board. Sumaye kwa cheo alichowahi kuwa nacho, kamwe hawezi kuwa mtendaji(Executive officer) wa taasisi yoyote zaidi ya PM aand above, vinginevyo uniambie kuwa amekuwa Mangula aliyetaka uenyekiti wa CCM mkoa kutoka ukatibu mkuu.
 
Majibu ya members wengi yaonyesha wengi hawaifahamu sheria ya makampuni, 2002. Kifupi kila kampuni inapaswa kuwa na wakurugenzi (directors) ambao wana jukumu la kuiongoza (manage) kampuni. Wakurugenzi wapo katika makundi mawili executive na non-executive, wanachaguliwa kwa kupigiwa kura katika mkutano mkuu wa wanahisa (Annual General Meeting).

Ni jambo la muhimu kama mwanahisa/mtu unayetaka kuanzisha kampuni ujue haki zako na namna bora ya kuendesha kampuni (good corporate governance). Usome sheria ya makampuni, katiba ya kampuni (memorandum of association na articles of association) na kama kampuni ipo listed Dar es Salaam Stock Exchange soma pia the Capital Markets and Securities Act Guidelines on Corporate Governance Practices, 2002 ujue haki zako kama mwanahisa. Pia utajua namna ya kumuwajibisha mkurugenzi wa kampuni, malipo, duties and liabilities of directors.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwenye maelezo yako kuna sehemu uko sahihi na zingine hauko sahihi. Iko hivi , ni kweli kuna kuna aina mbili za wakurugenzi, ila executive directors hawachaguliwi na mkutano mkuu kwani wao ni waajiriwa na wanalipwa mishahara, wao huchaguliwa na bodi ya wakurugenzi ambayo inaundwa na non executive directors. Na hao non executive directors huchaguliwa na mkutano mkuu wa wanahisa, ambapo wao wanakuwa sio waajiriwa bali wanalipwa directors fees. Sasa Sumaye yeye ni Non executive directors !

Mkuu ni non-executive director kwa kuwa amechaguliwa kwenye AGM.
 
hao shareholders hawastahili heshima kabisaa!!! hao sio kitu wanapokua anga zetu!!.... hata hivyo wao ndo wale wale tunaokwachomelea hizo million wanazokusanya..... lakini himaanishi nafurahia ushenziii huu... wapuuuzi kabisaaa!!! Khaaaa!!! Pumbavuuuu!!!
..kichaa siyo lazima avae chupi kichwani.
 
Tuache matusi. Kama mtu haelewi aombe kuelimishwa. Humu ndani kuna ilimu mbalimbali. Tatizo la watu wengine humu ni kupinga tu na kutukana bila hata kujua mantiki ya post. Kuna watu hawaelewi lakini wanajifanya ni vinara. Hawawezi kutofautisha Executive Director na Non-executive Director. Mtu yeyote ambaye ni shareholder wa CRDB Plc anaweza kuwa Mkurugenzi akichaguliwa na AGM. Hisa za CRDB Plc zinauzwa sokoni na kila mtu ana fursa ya kuzinunua na kupata fursa ya kuwa mkurugenzi. Tatizo hapa ni ukurugenzi wa Sumaye. Tatizo lingine ni kiswahili manake mtu akisia tu mkurugenzi basi inaingia kichwani kwa wakurugenzi watendaji; kiswahili hakitofautishi kati ya executive na non exective director tumezoea kuwaita wakurugenzi.

Kwa taarifa tu hata wale wa mashirika mbalimbali ama wakala wa serikali ambao wenyeviti wao huteuliwa na Rais a wajumbe kuteuliw na mawaziri huwa ni Wakurugenzi!!
 
Tatizo la watu humu ndani wakiisha mchukia mtu basi huwa hata fikra pevu hawana. Nadhani kwa hili ulilo waambia watakuelewa, kwani hata wao wanaweza kupata huo ukurugenzi pia
 
Mkuu sasa ambacho hukitaki hapo ni kipi ? Ninacho kuambia ndicho na mie ni mtu makini hapa JF kwenye thread zangu. Mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa (annual shareholders meeting) huchagua wakurugenzi wa kampuni (non executive directors) kwa njia ya kura ya siri. Kwa maana hiyo basi, Sumaye yeye amechaguliwa kuwa mkurugenzi ambapo atakuwa ni mjumbe wa bodi. Na sheria ya benki kuu inasema bodi ya wakurugenzi inatakiwa kuwa na watu wenye professional mbali mbali, sio lazima watu wenye elimu ya fedha tu. Soma na fuatilia mambo acha kukurupuka
Wewe ni mtu makini? Nani kakwambia mtu makini anajitaja hivyo! Tena povu linakutoka.
 
Kwani ww bank unafuata mtu au huduma ? think critically mkuu

hujui kama taasisi inaongozwa na 0 kuna hatari ya kaumbikiza ujiniaz kwa wafanyakazi? sura ya taasisi tunaanza kuiona kwa kiongozi wake.
nakuomba na ww uthink critically...mtu umetoka kuwa waziri mkuu tena kwa miaka kumi...halafu unaenda kugombea kuongoza benki? huoni kama kwa nafasi aliyopata kuongoza kuingia benki kunaleta mgongano wa kimaslahi?
 
Kwa iyo amechukua nafasi ya mr Martin,yule director of finance ppf au? Alaf sumaye anakuwa board chairman? Mi najua mwenyekiti wa bodi,au ndo iyo mkurugenzi wa board? Mkuu niweke sawa apo!
 
hao shareholders hawastahili heshima kabisaa!!! hao sio kitu wanapokua anga zetu!!.... hata hivyo wao ndo wale wale tunaokwachomelea hizo

million wanazokusanya..... lakini himaanishi nafurahia ushenziii huu... wapuuuzi kabisaaa!!! Khaaaa!!! Pumbavuuuu!!!

Kuna tatizo gani Jamani Romance kwani haifa? na kama hafai ni kwasababu gani? labda itasaidia badala ya kuwatukana!
 
hujui kama taasisi inaongozwa na 0 kuna hatari ya kaumbikiza ujiniaz kwa wafanyakazi? sura ya taasisi tunaanza kuiona kwa kiongozi wake.
nakuomba na ww uthink critically...mtu umetoka kuwa waziri mkuu tena kwa miaka kumi...halafu unaenda kugombea kuongoza benki? huoni kama kwa nafasi aliyopata kuongoza kuingia benki kunaleta mgongano wa kimaslahi?

Mkuu siamini kama hapa kuna mgongano wa kimaslahi. Yeye ni shareholder (kwa lugha nyepesi ni miongoni mwa wamiliki wa CRDB Plc) kwa hiyo ana haki ya kuangalia maslahi yake yaani umiliki wake. Mtu ni mmiliki wa kitu sasa kuna mgongano gani wa kimaslahi ukiwa kiongozi wa mali yako? Au hujui kama Sumaye ni miongoni mwa wamiliki wa CRDB Plc?
 
Back
Top Bottom