Mh. Spika, Nakupa Ushauri: Kabla ya Kuongea kitu Tafakari!

UTAJUA

Member
Apr 4, 2012
68
17
Mh. Spika Hebu angalia unavyoendesha Bunge, kwa kweli Inasikitisha. Sijui Tanzania Tunaelekea wapi.... Maswali ya maana ya Wawakilishi wa Tanzania, Unayakataa yasipewe majibu, Unajibu kwa mkato, Unajibu kwa jinsi unavyojisikia wewe badala ya kwa manufaa ya Tanzania.

Tafadhali JITAFAKARI Mh.
 
Nimeshtuka alipotamka kuwa waandishi wa habari wanaandika habari za 'kipuuzi'. hii ina maana kuwa anayeandika upuuzi ni mpuuzi pia,hivyo hatuna waandishi wa habari
 
hahahahah hasa wale waandishi wa gazeti la uhuru hahah... huyu mama kwa kweli.. Upuuzi na dhaifu lipi tusi jamani....kazi tunayo . kuomba muongozo kwa kujadili watu wanaokufa mikoa mingine isiyokuwa na Lugalo hospital ni kupoteza muda ... na yeye haimuhusu ni suala la serikali... halafu kuna watu wanawaambia ma dr wawe na huruma ... wakati spika aliechaguliwa kuwaongoza wawakilishi wa hao wananchi haimuhusu....
 
Nimeshtuka alipotamka kuwa waandishi wa habari wanaandika habari za 'kipuuzi'. hii ina maana kuwa anayeandika upuuzi ni mpuuzi pia,hivyo hatuna waandishi wa habari
Waandishi wanaNUKUU...hivyo kama wao bungeni wanaongea UPUUZI anategemea waandike nini?
We unazuia maswali kama wewe ndio muulizwa wa swali
unakatiza hoja kwa kisingizio cha muda halafu unaanza kututambulisha wageni binafs
unakeme minor things na unaacha mawaziri kutoa majibu ya hovyohovyo na kutoa shukrani zisio na tija...rejea muda waziri wa faranga alivyotumia nusu saa kutaja wabunge 300 kwa majina na uwakilishi wao eti kutambua michango yao,mbona hukumwambie ageneralize tu tua wabunge kadhaa wamec hangia kwa maneno na kadhaa kwa maandishi ili ule muda unaolipiwa posho na air time za TV utumike vema
mtindo wa kura za ndiyo au hapana ni AIBU.......tumia mifumo ya kisasa na kumbuka kura ni SIRI ya mtu,unatufndisha nini wewe kamakiongozi unapovunja hizo common LAWs?
 
anakiri maswala ambayo yako mahakamani hayatakiwi kujadiliwa wakati ameacha yamejadiliwa anaelekezwa anakuwa mkali.... Spika dhaifu, Raisi Thaifu n a ule mhimili mwingine Rushwa imetawala... sasa nchi itatawalikaje...
 
Hivi hichi kiburi cha kumwita mtu mpuuzi anakitoa wapi? Hivi viongozi wetu ni lini wataanza kuwajibika kwa matendo yao na maneno yao. Mie mpaka sasa natafakari waziri mkuu alimaanisha nini alivyosema liwalo na liwe. Je ni kuwa watawafukuza madaktari na kwa kuwa wao ni wababe basi kitakachowakuta wananchi ndio hivyo tena, liwalo na liwe?
 
anakiri maswala ambayo yako
mahakamani hayatakiwi kujadiliwa wakati ameacha yamejadiliwa
anaelekezwa anakuwa mkali.... Spika dhaifu, Raisi Thaifu n a ule mhimili
mwingine Rushwa imetawala... sasa nchi itatawalikaje...

haya ndo natuunda ya kuchagua rais legelege(dhaifu) automatically utapata baraza la mawaziri dhaifu lenye maamuzi dhaifu,viongozi waandamizi km spika dhaifu,na mwishowe serikali yote itakuwa DHAIFU
 
Aisee leo nimeamini kuwa kiti cha spika kimejaa upumbavu.
Issue za leo zote zilikuwa muhimu sana.

swala la Tandahimba, tatizo ni serikali yenyewe na wala sio wananchi.
Mgomo wa Drs, mahakama ilishatoa maamuzi kuwa mgomo usitishwe na Drs wamesema mgomo lazima uendelee. Sasa hapa ukisema mgomo hautakiwi kujadiliwa bungeni maana yake ni upumbavu tu wa kiti.

Mahakama imeshindwa, serikali imeshindwa na muhimili uliobaki ni bunge, nalo linashindwa. sasa wananchi hawana utawala tena.
Anachomaanisha spika ni kuwa wananchi tutafute suluhisho wenyewe maana mihimili ya Dola imeshindwa.
Raisi Dhaifu, bunge limejaa uzembe.

Nadhani tukusanye ujasiri tuanzishe TAHRIR SQUARE YETU
 
Yatamshinda mbona anafikiri bunge ni family yake anamiliki anavyotaka yy anakosea sana
 
Ukikumbuka mchakato mzima uliopelekea huyu mama kukalia hicho kiti - basi tulijua tu bunge litakuwa la namna gani. cha msingi hata wakizima hoja za maana bado wananchi tunaelewa kinachoendelea.
 
Spika Anne Makinda kama anasoma hapa au kama kuna mtu wake wa karibua basi ningependa kumuambia kuwa hakuna mtu aliyeni-dissapoint kama Anne Makinda. Ameharibu kabisa heshma ya bunge, amegeuza bunge kuwa taasisi ya serikali. Bunge ni mdomo wa watanzania, ndio sehemu ya watanzania kupitia wawakilishi wao wanatunga sheria za nchi na pia kuhoji/kushauri wale wanaopewa dhamna ya kuongoza.

Lakini kwa sababu anazozijua yeye Anne Makinda, ameamua kuziba watanzania midomo (kuziba wabunge maana yake ni kuziba midomo watanzania waliowatuma). Mtindo wake wa kuongoza vikao vya wawakilishi wa watanzania kwa hasira, pupa, matumizi/tafsiri potufu ya kanuni za bunge na kujiona yeye ndiye mtu pekee anayezielewa kanuni za bunge imechangia sana kujenga chuki kati wa raia na serikali na kwa maana hiyo CCM. Bunge limekuwa la mabavu na mipasho. Ni afadhali mara 1000 Jenista Muhagama angekuwa Spika.

Wabunge wa CCM wanaweza kufurahia anachokifanya Makinda, lakini gharama za huu uendeshaji mbovu wa bunge watazilipa kwenye sanduku la kura. Ni nadra sana kumpata mtu anayeona kuwa Makinda anaendesha vikao vya bunge vizuri! Lakini pengine tukumbuke jambo moja, Anne Makinda ni mjumbe wa CC ya CCM. Hiki ndio chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya CCM. Hivyo ni vigumu huyu mama kwenda kinyume na maazimio ya CC. Hatuna bunge and certainly hatuna spika.
 
Spika unatakiwa uelewe hili Bunge si lako.
 
Waandishi wanaNUKUU...hivyo kama wao bungeni wanaongea UPUUZI anategemea waandike nini?
We unazuia maswali kama wewe ndio muulizwa wa swali
unakatiza hoja kwa kisingizio cha muda halafu unaanza kututambulisha wageni binafs
unakeme minor things na unaacha mawaziri kutoa majibu ya hovyohovyo na kutoa shukrani zisio na tija...rejea muda waziri wa faranga alivyotumia nusu saa kutaja wabunge 300 kwa majina na uwakilishi wao eti kutambua michango yao,mbona hukumwambie ageneralize tu tua wabunge kadhaa wamec hangia kwa maneno na kadhaa kwa maandishi ili ule muda unaolipiwa posho na air time za TV utumike vema
mtindo wa kura za ndiyo au hapana ni AIBU.......tumia mifumo ya kisasa na kumbuka kura ni SIRI ya mtu,unatufndisha nini wewe kamakiongozi unapovunja hizo common LAWs?

Nimependa uchambuzi wako
 
hata kuwekwa kimada wa nusu sekunde hajawai unasema kuolewa,ndio maana anajibujibu ovyo nashushua wabunge,anaongea bila kufikiri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom