MH Sitta ni kiongozi aliyefanikiwa kupita kwenye nyazifa mbalimbali ndani ya serikali ikiwemo uspika pamoja na uwazir,ni kiongozi ambaye amekuwa akitoa kauli nyingi ambazo binafsi hazitoi taswira ya moja kwa moja kwamba kasimamia wapi,ni mtu ambaye amekuwa akiikosoa serikali ambayo yeye ni kiongozi,pengine anafanya hivyo kwa kuwa anajua serikali inayotuongoza kwa sasa ni dhaifu lkn siamini kama ingekua ni serikali ya mkapa angethubutu kuropoka hovyo kama anavyofanya,kama mh sitta ni kiongozi shupavu atoke ndani ya CCM ili atuaminishe watz kuwa ni mwanharakati wa kweli ambaye ana uchungu na nchi yake,aachie nyumba ya uspika ambayo ina gharimu serikali gharama kubwa,authibitishie umma pia hakuwahi kuwa mwanzalishi wa CCJ,kwa kuwa ameonyesha dhahiri kutofautiana na serikali ambayo na yeye ni sehemu ya serikali basi hana sababu ya kuendelea kuwa ndani ya CCM tofauti na hapo ni mnafiki ambaye anapaswa kupingwa kwa kila jambo aache kuwaongopea watz,ni huyuhuyu Sitta alisimama bungeni na kusema posho za wabunge ziongezwe huku akijua kuwa wabunge wamekuwa ndo wanaonufaika kwa sasa na kusahau kuwa wafanyakazi ambao ndo nguvu kazi ya nchi yetu wanalipwa ujira mdogo,pengine alifanya hivi ikiwa ni namna ya kujipigia kampeni ya kurudi kwenye nafasi ya uspika ingawa pia CCM ilimtosa,kwa mtizamo awe jasiri ahamie upinzani au CCJ ili watz tuamini haya anayoyasema na pia ili awe huru zaidi kuzungumza.....
Naomba kutoa hoja
Aondoke CCM aende wapi? Tanzania kuna chama kimoja tu na ni CCM, wengine wote ni chamgamsha bunge.