Mh.Sitta kuondolewa Uspika ni njia kwa Lowassa kuwania Urais 2015?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Naomba maoni yenu wana JF kwa hili kwani ilikuwa tetesi kuwa Sitta hatakuwa spika na imekuwa.Je haiwezi kuwa Lowassa anataka Urais na akawa?Ebu angalieni njia aliyoitumia Chenge kumshambulia inaonyesha dhahiri kuwa lengo lake lilikuwa kuchafua hali ya hewa.
 
mhh Labda rais wa Monduli....
Tayari tunaandaa vitabu vya historia yake hata nikidondoka niwaachie Vijana wasije wakadanganywa na mvi wakamchagua
siunajua wengi tulifikiri Mvi nyingi ni Busara kumbe Nehyiiiiiiiiiiiii
 
It is true. Kwa Kikwete everthing is posible. Sisi tunaoelewa ubaya wa hawa watu, tusipofanya bidii ya kuwaelemisha ndugu zetu walioko vijijini ubaya huo, itakuwa vigumu kung'oa chama fisadi madarakani. Tuanze sasa kuhamasisha, ili 2015 Serikali itakayoundwa na CHADEMA iongoze nchi. Kwa pamoja tutafanikiwa.
 
Kwa mfumo tulio nao inawezekana kabisa Lowasa kuwa rais, kwani hata nguruwe akisimamishwa na CCM kugombea urai s atakuwa rais, hili halina ubishi kwani hata JK hakuchaguliwa na Watanzania kuwa rais lakini NEC imemtangaza kuwa Rais kinyume na matakwa ya Watanzania.
 
Inasemekana anne ni swahiba wa el na kweli amewekwa pale kuhakikisha hilo
 
yangu macho lakini mwenye hela mpishe, ila kama ameshindwa kuchakachua Arusha hivi vihela vyao vinaweza liwa bure alafu akapata asilimi 30%
 
Back
Top Bottom