Mh. Sitta kuendelea kukaa kwenye nyumba ya Spika Masaki ni halali?

Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu aliulizwa ni lini Mh Sitta ataondoka kwenye nyumba ya Spika huko Masaki maana sio Spika tena. Kwa maelezo ya mbunge aliyeuliza swali ni kwamba serikali inatumia Tsh million 12 kila mwezi kwa nyumba ya huyu Spika. Lakini kama kawaida Mama Makinda alikurupuka na kujibu swali la serikali akisema kuwa hiyo ni stahiki ya Mh Sitta kama Spika mstaafu.

Wana-JF, Sasa nitawahoji, ni sahihi kwa Mh Sitta kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Spika hata kama sio Spika? Na kwa mantiki hiyo Marais wastaafu wanatakiwa waendelee kuishi IKULU maana wanastahili? Sera ya kuangalia maslahi ya viongozi wakuu wastaafu inasemaje?

Nafikri swala la msingi hapa ni kujua kama anishi kwenye nyumba hiyo kama Spika au kama Waziri? Maana nimeona post ya Mh. Zitto anasema hakuna nyumba ya Spika. Je! Alikuwa anamaanisha kwamba Serikali haijatenga nyumba maalum kwa ajili ya Spika? Kama ndo hivyo basi Bi. Mkora alichemsha kujibu kuwa hizo ni stahili za Mh. Sitta! Haiwezekani mtu bado yuko kwenye utumishi wa umma halafu aendelee kufaidi matunda ya kazi alizoaacha (hata kama zitakuwa zilikuwa na maslahi zaidi ya kazi anayoifanya sasa hivi!). Yaani hili li-nchi unaweza wehuka bure! Mtu ni Waziri halafu anaendelea kupata maslahi hata upande wa pili hii ni nini wazee?

Mimi huwa nashindwa kuwamaliza wasomi wetu (Viongozi), hivi ina maana hata kama umepata Uwaziri utaendelea kukamata posho ya Ubunge, hala unakamata na posho ya Uwaziri? Haki ya nani hii nchi inaporwa bila sisi wenyewe kuchukua hatua. Takukuru inasemaje hili la Mh. Sitta kuendelea kupata mafao ya Spika na Uwaziri? Hii ni "double payment" tukubali tusikubali! Tunaomba wadau walioko kwenye vyombo vya maamuzi hili walifanyie kazi (Hasa walio upinzani maana tunajua magamba hawataweza kutusaidia). Mtumishi wa chini akiwa fisadi utaona wanavyong'aka utafikiri wenyewe wako safi!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ili kuondoa kovu hili la ulafi wa 'vyeo na maisha dezo' kwa mtaji wa kodi za watanzania, muda umefika sasa kwa bunge kuangalia maslahi stahiki ya viongozi wakiwa madarakani na wanapoondoka. Na kama kiongozi amestaafu (including ccm -defination ya kustaafu) lakini akaamua kurukia cheo kingine, basi wakati akiwa kwenye utumishi atapata maslahi ya hicho cheo ya utumishi hadi hapo atakapostaafu.

Kwa mfano: Mh Sitta anaelezwa kuwa yeye ni Spika mstaafu. Lakini Sitta ni Waziri kamili kwenye current cabinet. Hivyo anatakiwa apate malipo kama mawaziri wengin na si vingenevyo. Mara atapostaafu, basi anaweza kuchagua kulipwa mafao na maposho mengine kama (a) Spika mstaafu au (b) kama waziri mstaafu. anatakiwa achaguwe moja. Lakini kwa sasa sioni logic ya kumpa maslahi huyu kama Spika mstaafu. Daylight robbery in my view.


Halafu niulize, kwa Dar es Salaam nyumba ya $7,000 nadhani ni skendo. Hii tabia ya 'kujazia' kodi kati ya mpangaji na mwenye nyumba ilianza taratibu kwa watafutaji nyumba za ma-expats. Unakuta officer anayeangalia housing issue anaongea na mwenye nyumba kodi inakuwa juu then difference wanagawana. Kwa sasa naona huu wizi umeenda na kama serikali haikuwa legelege wangekuwa wamechunguza huu ufisadi.

Inashangaza Spika wa zamani kama Sitta ambaye ki-msingi alikuwa na uwezo wa ku-force serikali ichunguze 'practices kwenye housing market' na hata kusimamia kutunga sheria lakini anaonekana kufuruahia huu ufisadi.
 
Kkuitafuna
Kwani P. Msekwa anakaa kwenye nyumba gani?
Msekwa alikuwa anakaa nyumba ya serikali baada ya kuinunua imekuwa ya kwake. Issue ya Sitta ni tofauti, bado ni mtumishi wa umma na wizara yake inawajibika kwa makazi yake. Kwanini kachagua kuitafuna Bunge? kwa sababu anafaidika na hiyo nyumba aliyojipangishia, wanagawana pasu pasu na mwenye nyumba kutokana na pango la kifisadi!
 
Hata mie niingekuwa makinda ningembembeleza Sitta asihame, ili nyumba yangu binafsi itengenezwe kwa pesa yenu wajinga, nikiacha kazi nibaki nayo
 
Ndio hivyo wanavyoachiana nyumba imeanza toka zamani sababu walikuwa wanabadilishana Madaraka; Kwanza kabla ya Sitta; Lau Masha kwanini asihame nyumba ya waziri ya mambo ya ndani? ili kuifadhili nchi kulipia hoteli kwa Waziri Mpya wa Ndani?
 
Hakuna nyumba ya Spika!

Nadhani kuna haja ya kabisa (it is in the public interest) kujuwa nani anagharamia matengenezo ya nyumba ya Mama Makinda Kijitonyama. Kama ni serikali je kwa sababu zipi, na kepengele gani katika sheria zetu kinaruhusu kufanya hivyo?

Kuna nyumba mpya ya spika inajengwa Dodoma, eneo la Uzunguni; kupitia kwenye barabara iliyopo baa ya Waswano. Nyumba hiyo ipo karibu na nyumba ya Kawawa. Ni bonge la jumba na kibao cha ujenzi kinaonyesha inajengwa nyumba ya spika.
 
Spika mstaafu ???? hivi uspika nao una ustaafu.

Hivi kwa nini wansia wanaenda kujikweza. Sdhani katika siasa kuna ustaafu. Waseme kamaliza muda wake.

Six mwenyewe abila zengwe la CCM leo angekuwa bado ni spika sasa iweje aitwe mstaaafu.

Mtu kagombea uspika kashindwa au hakukubaliwa na chama chake wanamuita spika mstaafu !!!!!
 
Danson Kaijage, Dodoma


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hataondolewa katika nyumba anayoishi kwa kuwa ni Spika mstaafu.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema hayo Bungeni jana wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu na kuweka wazi kwamba Maspika wote wastaafu wanapewa huduna mbalimbali na Bunge ikiwemo matibabu.

"Waheshimiwa, wakati mwingine huwa mnasema kuwa naingilia mambo kinyume na utaratibu, lakini vitu vingine mnavyouliza si sahihi kwani Samuel Sitta ni Spika mstaafu kama ilivyo kwa Pius Msekwa ambao wanahudumiwa mambo mengi na ofisi ya Bunge ikiwemo matibabu hivyo unapouliza hivyo si sahihi unatakiwa kufahamu kuwa huyu ni Spika mstaafu," alisema Spika Makinda hivyo kumfanya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutotoa majibu zaidi kuhusu swali hilo.

"Mheshimiwa Sitta hataondolewa katika nyumbe ile aliyopewa akiwa Spika kwa sababu ni Spika mstaafu na hilo ni moja ya sharti," alisema Makinda. Maelezo ya Spika Makinda, yametokana na swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), aliyehoji ni lini Sitta ataondolewa katika nyumba hiyo aliyopangishiwa iliyoko Masaki ambayo hulipiwa sh milioni 12 kwa mwezi.

Aidha, alisema hivi karibuni Sitta alikwenda nchini India akiwa na mkewe na msaidizi wake kwa kutumia hati ya daraja la kwanza akiwa si Spika, hivyo kuiomba serikali imwamuru kuondoka na kwenda kuishi katika nyumba za mawaziri zilizoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.


 
sasa kwa nini waliuza? unakata tawi ambalo umelikalia wewe mwenyewe? matokeo ndo hayo
 
hata kama anstahili. ni sahihi sitta mpiganaji wa kutetea maskini kuishi nyumba ya kulipia 12 milioni kwa mwezi.

hawa wazee wanajisahau sana.
 
Kwa hiyo Mama spika anatuambia kuwa sitta ataendelea kulipiwa millioni kumi na mbili kila mwezi, mpaka mungu wake atakapomuita!! ni hela hizi hizi wanazotuchangisha walipa kodi au!!!
 
Huu ni ubadhirifu wa hali ya juu. Kwani hana nyumba yake ahamie huko au ya wizara anayoingoza na hiyo akaachiwa mmoja wa "waheshimiwa" ambao bado wanaishi mahotelini ikiwemo mama magamba!?
 

My Take:
Baada ya Sitta kununuliwa na mafisadi kutoka kwa wananchi na CCJ sasa analipwa kwa hizo hizo pesa za wananchi. Tunakumbuka huyu Sitta alikuwa mmoja ya wanaharakati kujionesha kwa unafiki kwamba anajali sana wananchi lakini leo amepewa ok na serikali ya kikwete kuendelea kukaa kwenye hii nyumba ya ofisi ya spika kwa sababu eti yeye ni mstaafu, is this not costly for a poor country? maybe good decision for Sitta. Mimi sishangai Sitta ahami kwenye hii nyumba kwani ilijengwa kwa yeye na familia yake kuishi hapo mpaka akifa na serikali itajenga nyumba nyingine kumpa makinda (shil milioni 200) na 2015 makinda akifukuzwa atapewa nyumba hiyo moja kwa moja. Hii serikali ya kikwete na hawa wahuni wa ccm kweli wamekufuru mpaka wanaona wananchi sio kitu tena na hakuna hata chombo chochote kile kinaweza kuwapeleka mahakani wala jela, hii ndio maendeleo yanayotokana na fikra za ccm. This is increadable kwani hata walioondoka madarakani miaka hiyo ya nyuma leo bado wamechukua hizo nyumba na kujiuzia, what a shame for a republic. Who gave them these rights? Hili shirika la ccm 'national house' kazi yao inaonekana mpaka leo ni kuandikisha viongozi wanaotaka kuchukua nyumba za serikali sioni kazi nyingine. Soma hii article of shame...

'Ni hongo na corruption tupu hakuna lolote hapa. Asante ya ccm kwa watumishi na wateteaji wa fikra zao'

Bunge: Sitta hataondolewa kwenye nyumba


na Danson Kaijage, Dodoma
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hataondolewa katika nyumba anayoishi kwa kuwa ni Spika mstaafu.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema hayo Bungeni jana wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu na kuweka wazi kwamba Maspika wote wastaafu wanapewa huduna mbalimbali na Bunge ikiwemo matibabu.
“Waheshimiwa, wakati mwingine huwa mnasema kuwa naingilia mambo kinyume na utaratibu, lakini vitu vingine mnavyouliza si sahihi kwani Samuel Sitta ni Spika mstaafu kama ilivyo kwa Pius Msekwa ambao wanahudumiwa mambo mengi na ofisi ya Bunge ikiwemo matibabu hivyo unapouliza hivyo si sahihi unatakiwa kufahamu kuwa huyu ni Spika mstaafu,” alisema Spika Makinda hivyo kumfanya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutotoa majibu zaidi kuhusu swali hilo.
“Mheshimiwa Sitta hataondolewa katika nyumbe ile aliyopewa akiwa Spika kwa sababu ni Spika mstaafu na hilo ni moja ya sharti,” alisema Makinda.
Maelezo ya Spika Makinda, yametokana na swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), aliyehoji ni lini Sitta ataondolewa katika nyumba hiyo aliyopangishiwa iliyoko Masaki ambayo hulipiwa sh milioni 12 kwa mwezi.
Aidha, alisema hivi karibuni Sitta alikwenda nchini India akiwa na mkewe na msaidizi wake kwa kutumia hati ya daraja la kwanza akiwa si Spika, hivyo kuiomba serikali imwamuru kuondoka na kwenda kuishi katika nyumba za mawaziri zilizoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Bunge: Sitta hataondolewa kwenye nyumba

Badala ya nchi kuwa na retirement programs kwa kila mwananchi inaonekana pensio za msekwa na Sitta ndio hizi hapo juu. What a shame for the country!

Tatizo linarudi pale pale ni katiba ya kihuni hii.



 
Back
Top Bottom