Mh. Rais zile ahadi zetu vipi? Muda unakwenda sana

Mh Rais Muda umezidi kukimbia sana bila matumaini yoyote ya maisha bora kwa kila mtanzania, au Mheshimiwa utagombea tena kwa kipindi cha tatu ili utekeleze hata japo ahadi chache ulizotuahidi wananchi wako?

Kwani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika.

Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.

Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.
Umesahau zingine aliahidi pia kujenga machinja complex kila mkoa hilo vipi?au ndo atasingizia majengo yanayojengwa na NSSF kwani hayo tumejaribu kuulizia bei inaonekana sio kwa sisi wamachinga ni kwa ajili ya mafisadi wenye hela zao
 
Mh Rais Muda umezidi kukimbia sana bila matumaini yoyote ya maisha bora kwa kila mtanzania, au Mheshimiwa utagombea tena kwa kipindi cha tatu ili utekeleze hata japo ahadi chache ulizotuahidi wananchi wako?

Kwani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika.

Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.

Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.
hivi hii bajati ya itajibu maswali ya mleta mada.....
 
Back
Top Bottom