Mh. Rais zile ahadi zetu vipi? Muda unakwenda sana

Ndugu yangu Nape naomba leo uwaambie watanzania kama rais wa Tanzania mheshimwa JK anakumbuka ahadi alizotoa toka ameingia madarakani na ngapi ametekeleza na ngapi ambazo bado na kwa nini bado. Na je kama CCM inajua kuwa mwanadamu anahitaji maji na kama anahitaji mbona maji hakuna?

Kama anahitaji huduma bora za afya mbona hapa TZ ni mbovu hadi nyinyi wakubwa mkiugua mankimbilia India kwa kuwa mnajua za hapa ni mbovu. Na kama CCM inajua elimu ni muhimu mbona leo wanafunzi wanahitumu shule ya msingi huku wakiwa wameshinda kwenda sekondari huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika wakati nyinyi watoto wenu wanasoma ulaya kwa sababu elimu ya TZ mnaitambua kuwa haina kiwango.

Je bado CCM inaamini kuwa foleni barabarani ni maendeleo hii ni nukuu ya mwenyekiti wa CCM taifa. Na je umeme ni muhimu kwa maendeleo ya nchi mbona haupo au bado mko kwenye mchakato na wazee wa megawat.

Naomba kujuzwa ili nitulie nisulizie tena mambo ya maji,afya,umeme,elimu barabara kwa kuwa CCM imeisha timiza ahadi zake au mko kwenye mchakato. Na vile viwanja vya ndege vya kimataifa kila mkoa na mameli makubwa je.

Nape tiririka.
 
Sidhani kama Nape anaelewa kitu hapo, kwanza wakati wa kampeni alikuwa na hangover ya kubwagwa na Hawa Ng'umbi na kukataliwa kujiunga na CDM huku ccj ikibwagwa na Tendwa. Kifupi 2010 haukuwa mwaka mzuri kwa huyu jamaa hata zile ahadi 80 sidhani kama anazijua.
 
Sidhani kama Nape anaelewa kitu hapo, kwanza wakati wa kampeni alikuwa na hangover ya kubwagwa na Hawa Ng'umbi na kukataliwa kujiunga na CDM huku ccj ikibwagwa na Tendwa. Kifupi 2010 haukuwa mwaka mzuri kwa huyu jamaa hata zile ahadi 80 sidhani kama anazijua.

Hapana Mkuu anakumbuka moja ambayo haikutajwa ambayo Ya safari za Mwenyekiti wao
 
Mlimnukuu vibaya, wala hakuwahi kuhaidi hayo mambo. Yeye alihaidi Mahakama ya khadhi pamoja na kuigeuza Zenji kuwa Dubai ndogo.
 
muulize ritz naona anamshambuli Nassari ambaye ana miezi miwili huku kikeete baba yake akiwa na miaka kibao ikulu huku nchi ikitokomea gizani
 
Last edited by a moderator:
mchakato ushaanza, wataalam wako site, na wafadhili wameshakubali, serikali yenu ni sikivu na tuko makini
kilichobaki ni final drafting ile utekelezaji uanze mara moja kama ilivyoainishwa katika ILANI YA CCM hatutachelea kuchukua hatua zozote za dharura kwa jambo lolote linalohusu maslahi ya wananchi serikali yenu imefanya,imethubutu, na itaendelea kufanya...CCM OYEEE...wancchi
 
Nikivaa gwanda naweza kutolewa baruti labda nape anipe tu majibu ili moyo wangu utulie

Bwana mdogo pengine wewe ni kati vijana wadogo msiojua asili ya khaki dress iliyoletwa na waisraeli.
Hili lilikuwa linatumiwa na JKT miaka ya 60 na 70, na ni vazi zuri tu usiwe na woga nalo.
 
Lakini kwani hizo ahadi si ni kwa kipindi cha miaka 5. Mda bado wa kuuliza utekelezaji wa ahadi zote kwani zinatekelezwa hatua kwa hatua
 
Pia aliahidi atawasamehe wale wezi wote wa EPA warudishe tu sababu ni masela wake.
 
Mh Rais Muda umezidi kukimbia sana bila matumaini yoyote ya maisha bora kwa kila mtanzania, au Mheshimiwa utagombea tena kwa kipindi cha tatu ili utekeleze hata japo ahadi chache ulizotuahidi wananchi wako?

Kwani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika.


Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.

Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.

Mkuu, umeongea ukweli. Hebu tuwekee hapa zile ahadi zote za 2005 na 2010 ili tumtathmini huyu jamaa. Maana watanzania ni wazuri wa kusahau. au nitumie kwa email hii: quality.chality0@gmail.com
 
wani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

Mwinjilisti mmoja akihubiri akawambia washirika wake kwa nini mnadanganywa na wahubiri wa uongo wakati Biblia mnayo kwanini msijisomee wenyewe ili kuona ukweli uliomo ndani ya Biblia? hapo mimi naona ni uvivu wa kusoma. Mimi sijafika Dubai lakini kwa simulizi za rafiki yangu aliyefika huko aliniambia Dubai ni mji mzuri sana kwamba Dar es salaam ni kama kijiji kwa Dubai if that is the case maana yake Kigoma itakuja iwe mji mkubwa kuliko Dar es salaam?

yale yalikuwa ni maeno ya kudanganyia watz wavivu wa kusoma
 
Mh Rais Muda umezidi kukimbia sana bila matumaini yoyote ya maisha bora kwa kila mtanzania, au Mheshimiwa utagombea tena kwa kipindi cha tatu ili utekeleze hata japo ahadi chache ulizotuahidi wananchi wako?

Kwani huwezi kwamuda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka juzi.

Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika.


Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.

Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.

ahadi ya dubai jaman......hii ahad ntaendelea kuishangaaa,inanchekesha sana,,,,,
 
Hapana mheshimiwa ataweka rekodi ya kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru raisi J. Kikwete aliweza kukabidhi vizuri madaraka kwa Dr. Wilborad mwaka 2015. Hivyo basi hizi ni mbinu za mheshiwa raisi kukabidhi bila kumwaga damu. Kwani akitekeleza ilani ya uchaguzi inaweza ikawa vigumu kwa CDM kuingia madarakani. Kwa taharifa huu ni mpango madhubuti ambao kikwete anao akilini ili tuweze kumkubuka kwa kutuacha mikononi mwa CDM ambako ndiko kutakuwa na tulizo na matumaini kwa watanzania.

Asante Mh. Kikwete kweli una dira na unastahiki kutunukiwa tuzo ya NOBEL kama utafahulu kukamilisha mpango wako.
 
Back
Top Bottom