Mh: Rais Waziri akijiuzulu kwa UFISADI aachie na UBUNGE

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Viongozi wote waliohusika ama kutajwa tajwa wakihusishwa na mambo ya UFISADI au hata kama hawajatajwa rasmi lakini wako katika orodha za namna hiyo pindi ikigundulika SISI WATANZANIA TUNAWAOMBA WAJIUZULU MARA MOJA KWA MANUFAA YA TAIFA. MSISUBIRI KUFICHULIWA NDIPO:-
1. Mchanganyikiwe na kushindwa kujibu maswali ya waandishi wa habari
2. Mkihojiwa na waandishi wa habari mnatumia lugha zenu za asili "Vijisenti"
3. Baada ya kuandamwa sana na vyombo vya habari ambavyo ndiyo SAUTI YA WANANCHI mnaomba radhi kwa kuzungumza lugha zenu "vijisenti"
4. Kibano kikizidi unaiaga familia ukiwa waziri kamili unaenda ofisini unakuta BARUA TOKA IKULU ikikutaka utolee maelezo juu ya tuhuma zinazokukabili.
5. Unaaga nyumbani kwako ukiwa jasiri ukiwa waziri kisha unafikia kuandika barua ya kukubali kwamba umekwenda kimyume na msahafu mtakatifu (Biblia au Qran) na katiba ya nchi.
6. Kuachia ngazi uliyopewa kwa kuaminiwa na Rais wako.

MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE​
Ninaomba sana kutoa mawazo yangu japo utayaona kama ni ya kijinga sana, lakini kama kweli umedhamiria sana katika kuhakikisha unarudisha nidhamu ya uwajibikaji na uadilifu basi chukua mawazo yangu.

> Kwa kuwa Mbunge ni Kiongozi ambaye huchaguliwa aidha na wananchi, kuteuliwa na vyama kama mbunge viti maalumu ama kuteuliwa na wewe Mh. Rais, na kisha kuwa Waziri.
> Na kwa kuwa Mbunge yeyote hageuki tabia kabla na baada ya kuwa Waziri.

Je huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuweka utaratibu wa kumwajibisha WAZIRI aliyetuhumiwa kwa UFISADI kutimuliwa na UBUNGE, ili kuweka dhana kwamba Cheo kilichomuweka amekiuka maadili.
Hii ni kwa sababu ifuatayo:
Ikiwa Mbunge huyu amekiuka taratibu na maadili kwa kazi aliyopangiwa na Rais, atashindwa vipi kuwa mbadhirifu wa kazi aliyotumwa na Wananchi wake???
Pili ili kuwakumbusha mawaziri hawa kuwa akitema uwaziri kwa ufisadi huo asitegemee kutumikia wananchi tena.
Hii itasaidia kurejesha uadilifu serikalini.

Chenge.jpg
 
Back
Top Bottom