Mh.Rais naomba nyumba ya kuishi

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Mheshimiwa,
Tunaweza kukubaliana kwamba katika jiji letu la Dar es Salaam na majiji mengine makubwa,kero ya usafiri na nyumba za kupanga ni nambari moja.

Katika pitapita ya maeneo ya Ikulu na Ofisi ya Waziri mkuu kwa sababu majengo haya yameambatana,nimegundua kuwa na nyumba takribani nne ambazo hazina mtu wa kuishi,nyumba hizi kwa kuziangalia ni rahisi kuona uzuri wake wa asili ingawa kiukweli ni kama makazi ya ndege wasiofugwa.

Ninaloomba kwako mheshimiwa Rais,naweza kupata walau chumba kimoja tu kama siyo nyumba nzima? Nyumba ninayoishi kodi yake imeisha,mvua zilizonyesha mwezi April zimeharibu kila kilicho changu isipokuwa roho yangu ndo nimebaki nayo.Mwenye nyumba anataka nichangie gharama ya ukarabati ambayo inazidi hata pesa ya pango ninayolipa kwa mwezi.

Nakuahidi kwa kunipa chumba hata kama siyo nyumba nzima,nitakuwa mlinzi dhidi ya wavuta bangi waliozoea kuzunguka ukuta wa Ikulu yako "tukufu".Nitajitahidi kuwaelimisha wakaanga samaki na waendesha dalladala kuwa ustaarabu ni kitu cha bure,wasipige kelele hovyo na hiyo mimoshi ya samaki wasielekeze kwako.

Najua Salva Rweyemamu unaweza kuwa na wasiwasi kuwa ntachukua nafasi yako ya Mkurugenzi wa habari,nataka nikuhakikishie kuwa mimi nitakubali kupangiwa kazi hata kama itakuwa ni kuwasimamia wafanya usafi maana kwa kuangalia tu hata ukataji wa bustani za Ikulu si linganifu,mbaya zaidi mvua inyeshapo ninaona maeneo ya ikulu hujaa maji ambayo hutuama.Nadhani ili kuepuka mazalia ya mbu waenezao malaria ni bora niyafukie nitakuwa nimesaidia kueneza kaulimbiu yako ya MALARIA HAIKUBALIKI.

Sina kodi ya kukulipa mie,nisamehe bure!
 
nina uhakika ujumbe wako umemfikia kwan hata yeye ana browse haa JF japo sio member ni guest
 
zipo kibao nyumba za hivyo,umenichekesha we ntuuu,lakn ukiangalia kodi zetu zimepotea buuure
 
Wewee! Unataka nyumba kutoka kwa mzee wa kaya? Basi kama una dada ako mzuri amejaa sawa sawa hakika utapata nyumba alafu awe mweupe kidogo kama v....k, nawakilisha.
 
Ubutu na uomba omba, fanya kazi kwa bidii kama alivyofanya yeye akafika Ikulu.
 
Hakuna kaa zako huko huko mwananyamala kwa binti kopa. Kwanza wewe kura za urasi ulimpa Slaa halafu nyumba ya kuishi upewe na JK?
 
Back
Top Bottom