Mh.Prof Mwandosya: Tanzania inaongoza Africa kupeleka Wananchi wake India Kwa Matibabu

Huyu mleta uzi huu ni msokile wa huko huko anakotoka Mwandosya hivyo sintaona ajabu kama vita vyao vya kisiasa anavileta hapa kwa kutaka kumpakazia mbaya wake; vita piganeni huko huko kwenu msitake kutuingiza na sisi havituhusu!! Nyie wengine ndio mliokuwa mnamzushia kifo alipokuwa huko India na nyie tena ndio hao hao mnaospin taarifa hizi; mshindwe na mlegee!

Pole mkuu kama imekuumiza lakini, sijawai, sitaweza kumuzushia wala kumwombea mtu kifo. Karibu tujadili hoja ambayo source yake ni REDIO one mimi nimewashrikisha tu kama wachambuzi makini jikite kwenye hoja. Ugomvi au urafiki wangu na Prof haufuti hoja hiyo.
Nini maoni yako juu ya kali ya Prof,
 
Kuna mtu kaweka speech na collage ya Mwandosya anatoa hotuba Mbeya, anachemsha kuanzia kujieleza mpaka mantiki.

Anawachochea watu kuchukua rushwa. Anachochea ukabila. Yaani nimefikiri sana, nikasema na huyu ndiye Professor aliyeenda Ivy League, hao wenzangunamie ambao hawana neither exposure nor proper schooling sijui hata cha kutegemea.
 
Redio one wanarudia habari za siku nzima hapo saa nne usiku naomba wote msioamini kama haya ni mameno ya Prof , Sikilizeni taarifa ya marudio.
 
Sisi madaktari wa hapa nchini hatuaminiki,na hapa muhimbili hupitia tu wakiandaa utaratibu wa kwenda India!
 
Sisi madaktari wa hapa nchini hatuaminiki,na hapa muhimbili hupitia tu wakiandaa utaratibu wa kwenda India!

Mungu anisamehe! Kama ni kweli katoa kauli hii ni afadhali asingerudi hai ili kupunguza idadi ya wanaodidimiza sekta ya afya ya nchi hii. Hajui hizo nchi nyingine zimeboresha hospital zao? Hajui hizo gharama za kuwapeleka wao nje ndo zinatufikisha kwenye hali ngumu? 50 yrz ct scan moja kwenye mikoa zaidi ya ishirini? Ultrasound nyingi hazifanyi kazi,wao wanashabikia kwenda india? mnh kuna kipindi hata frusemide inakosekana internal medicine,wao wanajitangaza kwa mambo ya kikuda namna hii?
 
Kupeleka wananchi wake ni kupeleka viongozi wake india.
Kiukweli wadosi wako juu kitabibu kuliko tz kwa mbali sana. Hao wanaoenda waende na madaktari ili kuiba ujuzi
 
Nimesikiliza taarifa ya habari ITV jana usiku kweli prof anasikitisha kutamka maneno haya kama sifa kwa wakati ni aibu kubwa kwa huru ya miaka 50, halafu wanaopelekwa na serikali ni vigogo na ndugu wa vigogo maskini kila leo wanahangaika kuomba michango kwenye vyombo vya habari na wengi wao wanaishia kufa hata kabla hawajapata wasamaria wema wa kuwasaidia
 
Ninaonea Huruma hawa wapiga kura wa Rungwe mashariki! Heri huo upupu angeongea mbunge wa Mtera
 
Mie nilimsikia na kumuona live katika ITV...tena ilikua sala ya kumuombea yeye...nilichoshangaa ni hali kuwa dhaifu mno...kiasi kwamba amevaa kitu maalumu mwilini .... kumsapoti..inasikitisha sana..ingawa ni kweli tunapeleka sana wagonjwa INDIA..tukisahau kuimarisha Hospitali zetu
 
Back
Top Bottom