Mh. Pinda kwa hili sikubaliani na wewe kamwe!!!

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Majuzi waziri mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda aliwaasa makatibu muhtasi wa serikali na mashirika ya umma kutotoa siri za ofisi zao. Mimi kwa nguvu zote napingana na wito huo wa Mh. Pinda kwa sababu madhambi mengi ya ufisadi tumeyajua kwa msaada wa hawa makatibu muhtasi pamoja na wadau wengine wa maendeleo na wapinga ufisadi.

Baadhi ya nyaraka muhimu ambazo zimewezesha kuibuliwa kwa kashfa/skandali mbali mbali za wizi wa mali ya umma ziliweza kupatikana kwa msaada wa hawa watu. Sasa mimi najiuliza Mh Pinda badala ahimize kila mfanya kazi kwa nafasi yake popote alipo ajitahidi kutoa taarifa zozote za uhujumu uchumi na rushwa inayofanywa na wakubwa kwa kutumia ofisi zao, yeye anakemea watu kutotoa taarifa je hizi nyimbo za kupambana na rushwa hapa nchini zina maana yoyote?

Binafsi natoa wito kwa makatibu muhtasi wote Tanzania kutoijali kauli ya Pinda na kujitahidi kuanika uozo wowote unaotokea ktk ofisi zao.
 
mkuu usijali wataendelea tu. hawapo pale kutekeleza matakwa ya Pinda mbona amewakuta? Na pengine mwaka 2011 hatunaye. Isitoshe makatibu wanatoaga siri kwa sababu wanakerwa. masilahi yao hayazingatiwi kwenye hiyo mikataba ya kilaghai wananajaa. May be wawe sehemu ya deal. Hapo wataficha siri maana na wao watafaidiki. Siyo hii ya mikono mitupu hailambwi.
 
Ni kweli haya maozo kwenye ofisi za umma yataendelea kuvuja manake tunaumizwa sana na mafisadi
 
Kwani siri maana yake nini?,Kwani waziri mkuu alimaanisha taarifa za ufisadi au siri?,Labda kama sijaelewa vizuri,lakini nachojua kila organization ina secret,confidential and top secret informations.Nadhani waziri mkuu hakuwa na maana mbaya.
 
Huko ni kulipereka taifa kubaya sana kwani ni kuficha maovu na kukuza chuki kwa raia sisi kwa sisi itatuletea chukuki na kweli nawambia hizo siri zitapitia kwa njia za Udini, Undugu (Ukabila) hivyo tujue twalitenganisha taifa napenda kuwapa onyo mapema twapaswa kujua nini maaana ya Democrasia jamani na kuwa wazalendo ina maana viongozi wakaapo na kupitisha mikataba yao ya ajabu na kuwa piga mikwara hawa makatibu muhutasari.
 
Kwani siri maana yake nini?,Kwani waziri mkuu alimaanisha taarifa za ufisadi au siri?,Labda kama sijaelewa vizuri,lakini nachojua kila organization ina secret,confidential and top secret informations.Nadhani waziri mkuu hakuwa na maana mbaya.

Let me tell you Mr gun shooter!!!!

Hakuna cha top secret au baba yake na special confidential or top secret informations serikali yetu haijui hilo kwa taaarifa yako kila paper utaikuta confidential ikitoka ofice hii kwenda ofice fulani na hii ndio ilikuwa style yao ya kuutukuza na kuubariki ufisadi kaaa ujue hivyo. Pia hujue serikali yetu haina uzalendo wala ustaharabu wa kujua hayo ya top secret na confidential mkuu.

 
Kwani siri maana yake nini?,Kwani waziri mkuu alimaanisha taarifa za ufisadi au siri?,Labda kama sijaelewa vizuri,lakini nachojua kila organization ina secret,confidential and top secret informations.Nadhani waziri mkuu hakuwa na maana mbaya.

Nakubali kwamba ipo tofauti kati siri na taarifa za ufisadi. Lakini kama hakuwa na maana mbaya kwa nini atamke? After all kuna ile Official Secrecy Act inayokataza watumishi wa umma kutoa siri za serikali. Wangapi wamechukuliwa hatua na kuhukumiwa kutokana na sheria hii?

Bila shaka yoyote Pinda alikuwa na maana ya taarifa za ufisadi, lakini hakuwa na courage ya kutosha kutamka hivyo, kwa sababu naye ni mmoja wao katika jitihada za kufunika maovu ya serikali yake. Ndiyo maana kila mara nasema hafai kabisa kuwa PM.

OH YES! BEING PROLIFIC DOESN'T NECESSARILY MEAN YOU ARE AN ACCOMPLISHED PERSON!
 
Pamoja na maneno yaliyotolewa na Mhe. Pinda kwa nia njema sidhani na sioni sababu kwa nini kila ofisi ya Serikali iwe na 'siri' ambazo inabidi zitunzwe! Wakati mwingine hizo siri ndizo zinazoweza kuangamiza taifa endapo siri hizo hazipo kwa manufaa ya Umma na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom