Mh Pinda Acha Uoga!

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
Mh Waziri Mkuu sasa ameanzisha Tabia ya kukimbia Kila alhamis ya week ili kukwepa Maswali ya papo kwa Papo! Ilikuwa kila week akiulizwa maswali lakini kwa sasa amekuwa kila jumatano anaopa ruhusa ya kusafiri, Kama mnakumbuka toka atoe tamko la liwalo na liwe hadi sasa anaogopa kukaa pale alhamis . Tukumbuke week lilopita alikwenda Zanzibar kutoa mkono wa pole, Alhamis iliyopita alikuwa Morogoro kwenye ufunguzi wa maonesho nane nane . Leo hii nimemsikia mama Makinda akisema Mh liwalo na liwe atamuachia Mh Sitta kwakuwa yeye atasafiri.

Hii inaonesha wazi kuwa waziri Mkuu anaogopa kujibu maswali ya liwalo na liwe. Ila ajue wazi kuwa tabia hii si nzuri na aiache.
 
Anajisikia vibaya sana kwa usaliti na uongo wake na anakwepa maswali ya kina dogo janja,Mbowe na wengine kuhusu liwalo na liwe!!!
 
Kweli mkuu, mtoto wa mkulima naona lile wingu jeusi kutokana na kauli yake ya liwalo na liwe bado linamzonga, hajakaa sawa bado. dah! kama hukuzaliwa na roho mbaya huwa ngumu sana ku-pretend. duh!! maliza haraka hang over ya kauli yako ya LIWALO NA LIWE urudi ujibu maswali yetu ya MOJA KWA MOJA.
 
Ukiangalia sura ya Pinda unajua bonge na ngangari, kumbe ana kamoyo kadogoooo, siajabu ndio maana kulia-lia kwake izze tu
 
sasa ataakimbia mpaka lini? mtoto wa mkulima nae kwa matukio!

Ila anaongoza kwa matukio
1. Waziri Mkuu aliyelia Bungeni
2. waziri wa liwalo na liwe
3. Alisema mashangingi hayatanunuliwa leo yananunuliwa ya kumwaga.....
4.........................................
 
na kwa hali ilivyo sasa lazima akimbie madaktari,walimu na sasa bi banda kuvamia nchi hili nafikiri linamchanya zaidi.!
 
Pinda anaonekana kupindapinda kama jina lake. Maana ukitafuta jinsi ya kumchambua unakosa pa kushika. Sumaye pamoja na kasoro zake, alijua alichokuwa akifanya bungeni. Pinda pamoja na elimu yake ya sheria anaonekana kupwaya kama spika ambaye elimu yake ni nusu nusu na ya mashaka.
 
hapo ni kopo na mfuniko
HAPANA aisee , yaani bora fisadi alikuwa hata tunajua ana msimamo gani sio hii lia lia, yaani hajawai kuongea kitu cha mnukuu zaidi ya liwalo na liwe ambayo ni alikuwa ana confess udhaifu wake..kwamba mother nature iamua fate ya masuala magumu na muhimu kwa taifa
 
Back
Top Bottom