Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Katika bunge la mwezi November mwaka jana kama sikosei,mh.Ole sendeka ulitoa ahadi ya kupeleka hoja binafsi bungeni ukitaka nyumba za serikali zilizouzwa zirudishwe.Mh.ulikwenda mbali zaidi na kukiri kuwa ktk mambo ambayo serikali yako ya ccm ilikosea ni kuuza nyumba za serikali.Hata hivyo,nahofia kukubalika na kupitishwa kwa hoja hiyo kwani hata huko bungeni wapo wengi waliofaidika na uamuzi huu.
Ombi langu kwako, timiza ahadi yako na umma wa watanzania walio wengi wako nyuma yako.Itakuwa ni nafasi ya umma kujua ni mbunge yupi yupo kutetea wananchi na yupi yupo kwa maslahi yake binafsi.Pia naamini utaandika historia ktk hili.
Athari ya uamuzi huu ni kumuongezea ugumu wa maisha mtumishi ambaye mshahara wake hautoshelezi mahitaji yake kwa kumlazimisha kupanga mitaani, tena kwa kodi kubwa wakati nyumba zilikuwepo.Uamuuzi huu ulinufaisha wachache kwa gharama ya wengi.