Mh. Nyalandu ailaumu CCM kumtega

Wakuu mbona mmekomaa na Seru.Kamba kiasi hicho? Basi kama hafai abaki huko na kamba zake! Ma.Kamba naye nina mashaka naye! Siyo mmoja wa wataka misifa huyu? CDM tuna majembe mengi sana hawa wabaki hukohuko, wasije kutubana tukashindwa na kupumua! Oups!!
 
Ikibidi wote wasije mbona wapambanaji wako wengi, msije mkawa mnawasafishia njia ili waone upepo unavuma je.
Wabaki hukohuko kama wanataka kuja basi iwe mwaka huu, waachie huo ulaji mapema kama alivyofanya mwenzao Mpendazoe
 
Sijui kuhusu hao Filikunjombe ila huyo Nyalandu habari zake nilizozisikia kutoka kwa watanzania wenzake USA alipokuwa anaishi ni balaa, sidhani hata kama anastahili kuwa mbunge wa nyumba kumi...
 
Amesema wamefikia hatua hata ya kumtega kwa kumchomekea wasichana ili akionekana tu yuko naye basi waseme wanachotaka kusema.!!!!

Naona hapo defensive mechanism at its best, kama wewe sio mzinzi huwezi kusema maneno hayo.

Imagine mtu ambaye hana tabia za mambo ya wanawake aseme maneno kama hayo, its impossible huyu jamaa lazima atakuwa mzinzi. Hapo anajaribu kumuweka sawa mke wake siku likibumbuluka ajue anasevu vipi.
 
Wameshosoma alama za nyakati wanatafuta pa kutokea hawana lolote......

Mh. Lazaru Nyalandu(Naibu waziri) ametamka kuwa kuna watu CCM wanampiga kiasi cha kumwekea mitego mbalimbali ili kutimiza malengo yao ya kumchafua kisiasa. Maneno hayo aliyatoa wakati akikanusha shutuma zilizotengenezwa dhidi yake kwamba alitishia kwa bastola na kuvunja vizuizi vilivyokuwa vimewekwa barabara huko Singida katika jimbo lake. Nyalandu alisema hajawahi mtishia mtu kwa Bastola na hajafika jimboni kwake tangu February na kwamba yanayosemwa ni kwa lengo la kumchafua na wanaofanya hivyo ni CCM.
Amesema wamefikia hatua hata ya kumtega kwa kumchomekea wasichana ili akionekana tu yuko naye basi waseme wanachotaka kusema.

Kwa uchambuzi wangu inaonekana vijana walioko CCM wanaona mbali kuliko wazee wao na hii inaondoa status quo ya waasisi kiasi kwamba wazee wanaona vijana wanakosa adabu na kuaza kutumia mbinu chafu kuwanyamazisha.
CCM wako vijana ambao wameamua kutolalia godoro lenye chawa la CCM ya akina Kingunge na wameamua kuwa na mtazamo tofauti na hivyo kuonekana kuwa chukizo kwa wazee. Akina January Makamba, Filikunjombe, Lazaru Nyalandu, Selukamba na wengine wanaonekana kuwa na msimamo ambao utawakera sana CCM kiasi cha kutaka kuwapiga vita na kuzima nyota yao ya kisiasa.

Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!
 
Saaa ya ukombozi ni sasa. kama wanataka kuja waje sasa au wakae uko mlele na milele
 
Huyu Jamaa uwezo wake ni mdogo atasemaje marekani inamtaka agombee Urais, au kwa vile yeye ni Raia wa Marekani?

Watanzania tusiwakubali hivi vipandikiza ndiyo miongoni mwa wale wanaounga mkono kutoa dhahabu na Uranium kwa vyandaruaa vilivyowekwa sumu..

Hakuna kisichosafishika mkuu. Inawezekana alisema hayo kwa sababu mazingira ya magamba yaliruhusu huo ujinga ila akiamua kuongoka inabidi apewe masharti kwanza
 
kijana mwingine asiyetakiwa cdm ni Meela Crispin hana chochote ni mbabaishaji tu. wa kutaka madaraka
 
magamba yameanza kuvimba sasa tunasubiri yapasuke,
moja limeshtuka jana ilmejitakasa tunalikaribisha ndani ya chama la ukombozi na asrudi nyuma tena.

kuhusu suala la wasichana wala asilete zake habari zake tunazijua.

Alaaa kumbe chama cha kupokea magamba kipo sio?ngoja tuwaswage wote waje huko kwenye chama chao
 
Are you really serious na hawa watu kwenye RED? Kama Serukamba ni mzalendo wa nchi hii kwa maana halisi ya neno UZALENDO basi mimi ni Lionel Messi!

Mkuu kwa kifupi kama SERUKAMBA NI MZALENDO basi hii nchi haina mzalengo full stop. Mwanaume mzima unakuwa unaweweseka kwa mwanaume mwenzako? leo mnamwita MZALENDO?
 
Mh. Lazaru Nyalandu(Naibu waziri) ametamka kuwa kuna watu CCM wanampiga kiasi cha kumwekea mitego mbalimbali ili kutimiza malengo yao ya kumchafua kisiasa. Maneno hayo aliyatoa wakati akikanusha shutuma zilizotengenezwa dhidi yake kwamba alitishia kwa bastola na kuvunja vizuizi vilivyokuwa vimewekwa barabara huko Singida katika jimbo lake. Nyalandu alisema hajawahi mtishia mtu kwa Bastola na hajafika jimboni kwake tangu February na kwamba yanayosemwa ni kwa lengo la kumchafua na wanaofanya hivyo ni CCM.
Amesema wamefikia hatua hata ya kumtega kwa kumchomekea wasichana ili akionekana tu yuko naye basi waseme wanachotaka kusema.

Kwa uchambuzi wangu inaonekana vijana walioko CCM wanaona mbali kuliko wazee wao na hii inaondoa status quo ya waasisi kiasi kwamba wazee wanaona vijana wanakosa adabu na kuaza kutumia mbinu chafu kuwanyamazisha.
CCM wako vijana ambao wameamua kutolalia godoro lenye chawa la CCM ya akina Kingunge na wameamua kuwa na mtazamo tofauti na hivyo kuonekana kuwa chukizo kwa wazee. Akina January Makamba, Filikunjombe, Lazaru Nyalandu, Selukamba na wengine wanaonekana kuwa na msimamo ambao utawakera sana CCM kiasi cha kutaka kuwapiga vita na kuzima nyota yao ya kisiasa.

Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!

Hapana, hawa ni myopic ndiyo maana wakasimamia CCM in the first place. Wangekuwa na nia njema kwa taifa hili wangeanza tangu mwanzo kujua kuwa CCM haifai, kwani lilianza kuvuruga nchi zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita, na walaijua hilo lakini walikwenda kugombea huko huko, wakifuata taratibu za ki-CCM za kutoa rushwa nyingi tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom