Mh. Nyalandu ailaumu CCM kumtega

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,183
2,304
Mh. Lazaru Nyalandu(Naibu waziri) ametamka kuwa kuna watu CCM wanampiga kiasi cha kumwekea mitego mbalimbali ili kutimiza malengo yao ya kumchafua kisiasa. Maneno hayo aliyatoa wakati akikanusha shutuma zilizotengenezwa dhidi yake kwamba alitishia kwa bastola na kuvunja vizuizi vilivyokuwa vimewekwa barabara huko Singida katika jimbo lake. Nyalandu alisema hajawahi mtishia mtu kwa Bastola na hajafika jimboni kwake tangu February na kwamba yanayosemwa ni kwa lengo la kumchafua na wanaofanya hivyo ni CCM.
Amesema wamefikia hatua hata ya kumtega kwa kumchomekea wasichana ili akionekana tu yuko naye basi waseme wanachotaka kusema.

Kwa uchambuzi wangu inaonekana vijana walioko CCM wanaona mbali kuliko wazee wao na hii inaondoa status quo ya waasisi kiasi kwamba wazee wanaona vijana wanakosa adabu na kuaza kutumia mbinu chafu kuwanyamazisha.
CCM wako vijana ambao wameamua kutolalia godoro lenye chawa la CCM ya akina Kingunge na wameamua kuwa na mtazamo tofauti na hivyo kuonekana kuwa chukizo kwa wazee. Akina January Makamba, Filikunjombe, Lazaru Nyalandu, Selukamba na wengine wanaonekana kuwa na msimamo ambao utawakera sana CCM kiasi cha kutaka kuwapiga vita na kuzima nyota yao ya kisiasa.

Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!
 
magamba yameanza kuvimba sasa tunasubiri yapasuke,
moja limeshtuka jana ilmejitakasa tunalikaribisha ndani ya chama la ukombozi na asrudi nyuma tena.

kuhusu suala la wasichana wala asilete zake habari zake tunazijua.
 
Hivi hao watu waliotajwa hapo mnawafahamu vizuri au ndio mamabo ya kurukia mkokoteni wa bendi?

Inawezekana kabisa watu wote hao waliotajwa hapo juu ni watu wa hovyo haijawahi kutokea!!! Uwezo finyu, wapenda publicity sana hao, na waweza wakawa wanajipendekeza kwa kutumia uwezo wa watu wengine nao kujizolea misifa pasipo kutoa credit where it si due!!

Sam pipo bwana, duuuu!!!
 
Hakuna Mwanasiasa na Mbunge munafiki kama Peter Selukamba hafai kukaa na sisi ni kiongozi anae tarajia kujutia kauli zake pale tutakapo kuwa tunashangilia ukombozi wa mali za wanyonge.
 
Yaliyotakiwa kukanushwa bado hayajakanushwa wala.......hayo ya kisiasa na wanawake ata deal nayo kunakohusika..

Yeye kama mbunge, waziri na mtanzania mwenzetu atuondoe hofu kwa kuweka maelezo kwa mujibu wa hoja husika iliyoletwa hapa

By the way rumours wil fade with time but facts will reamin as a part of history
 
Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!

Huyu hapana hata kwa nini
 
Mtoa maada vipi bwana hivi wewe unamjua Serukamba? Acha kabisa yule mnafiki sana tena kuliko Yuda kwa taarifa yako hata kule Kigoma mjini hakushinda na huu ni mhula wake wa mwisho kwa hiyo anatapatapa
 
Kwenye hiyo list kuna vijana wa mamvi ambao hawaaminiki hata kidogo angalia usichanganye bisuit na mawe itakuwa shida
:ballchain:
 
Huyu Jamaa uwezo wake ni mdogo atasemaje marekani inamtaka agombee Urais, au kwa vile yeye ni Raia wa Marekani?

Watanzania tusiwakubali hivi vipandikiza ndiyo miongoni mwa wale wanaounga mkono kutoa dhahabu na Uranium kwa vyandaruaa vilivyowekwa sumu..
 
Kwa uchambuzi wangu inaonekana vijana walioko CCM wanaona mbali kuliko wazee wao na hii inaondoa status quo ya waasisi kiasi kwamba wazee wanaona vijana wanakosa adabu na kuaza kutumia mbinu chafu kuwanyamazisha.
CCM wako vijana ambao wameamua kutolalia godoro lenye chawa la CCM ya akina Kingunge na wameamua kuwa na mtazamo tofauti na hivyo kuonekana kuwa chukizo kwa wazee. Akina January Makamba, Filikunjombe, Lazaru Nyalandu, Selukamba na wengine wanaonekana kuwa na msimamo ambao utawakera sana CCM kiasi cha kutaka kuwapiga vita na kuzima nyota yao ya kisiasa.

Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!

Are you really serious na hawa watu kwenye RED? Kama Serukamba ni mzalendo wa nchi hii kwa maana halisi ya neno UZALENDO basi mimi ni Lionel Messi!
 
kivuli chake anakikimbia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! watahama sana mpaka 2015 wakati dola inaongozwa na CDM watakuwa wameyasema yote maovu waliokuwa wanatendeana na kuwatendea wapinzani wa nchi hii
 
Mvumbuzi, hiyo list yako ya 'vijana' inatoka moyoni kweli? Serukamba?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom