Mh. Mwakyembe SUMATRA wanatuumiza sie wajasiriamali wadogo ili kujisafisha kwako

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,696
2,553
Tunajua SUMATRA wanao wajibu wa kuwafurahisha wanasiasa ambao ndio wakubwa wao lakini hili lisiwe kwa gharama ya wamiliki, madereva na makondakta wa daladala. Juzi ijumaa waliendesha kamata kamata ya daladala madai yao ni kutafuta mzizi wa makosa mbalimbali ili kuboresha huduma ya usafiri jijini. Sababu ambazo tunazitilia shaka manake wamekuwepo na bila kumung'unya maneno ni Mh. Mwakyembe ndio amewapa hii wake up call na wapo kwenye kona mbaya na sasa wanahaha kutafuta pakutokea.

Mara zote wadau wao wakubwa ni polisi na wala hawatoi fursa kwa wadau wa daladala wote na inawezekana kabisa maoni ya wamiliki na madereva wa wadaladala sio news na wala haviwezi make headlines katika magazeti ndio maana wahanga siku zote ni wamiliki wa daladala.

Ni masikitiko makubwa mazingira ya kufanya bishara Tanzania yanazidi kuwa magumu uhususani kwa wafanyabiashara wadogo na wazawa. Ripoti ya Word Bank – Doing Business Roadmap inathibitisha hili na mamlaka husika ndio kikwazo SUMATRA wakiwa sehemu ya mamlaka hizo. Daladala zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi hii pamoja na kuchangia kodi mbali mbali pia zimekuwa zikitoa ajira kwa vijana pamoja na changamoto mbali mbali zinazokutana nazo pamoja na :
· Kulipa faini lukuki na kulazimishwa kutoa rushwa kwa traffic.
· Kamata kamata ya SUMATRA na Trafiki polisi
· Wapiga debe
· Gharama kubwa za uendeshaji
· Miundo mbinu mibovu
· Msongamano barabarani
· Magari chakavu na yasiyo na ubora
· Utoaji mgumu wa leseni na kuchaguliwa ruti
. Mishahara midogo kwa madereva na makondakta

Zaidi ya asilimia 90% ya biashara Tanzania ni biashara ndogo, na daladala ni sehemu ya biashara hizo ndogo na kutokana na umuhimu wake zinapaswa kulindwa na sio kukandamizwa, kuonewa na kudhulumiwa ili zieweze kukua. Tunatambua jamii ya watanzania uhususani sekta za umma zinakuwa ngumu sana kutambua sekta binafsi nini na zinaumuhimu gani katika uchumi wa nchi hii na kushindwa kabisa kutoa ushirikiano unaostahili badala yake bishara ya daladala inaonekana adui mbali na kusafirisha mamilioni ya watanzania kila kukicha.

Sinamaana ya kuwatetea wamiliki, madereva na makondakta ni dhahiri yapo ambayo yanapaswa kurekebishwa kutokana ukiukwaji wa sheria za barabarani wanazofanya. Lakini mifumo na kanauni za kutoa haki zinapaswa kuzingatiwa. Haiwezekani kabisa SUMATRA wakukamate, wakushtaki na kukuhukumu wakati waendesha mashitaka na mahakimu ni wao. Trafiki wao pia ni mahakimu wanakamata na kukuhukumu unalipa hapo hapo na wala uruhusiwi kuhoji hizo pesa zimekwenda wapi na risiti hawatoi.

Tulitegemea SUMATRA kama mamlaka zingine wangekuwa watengenezaji wa mazingira mazuri ya kufanya biashara kama ilivyo kwa mamlaka ya mawasiliano ambao pia wanaweka na mazingira mazuri kwa uwekezaji kukua na ubunifu kuongezeka kila kukicha. SUMATRA wao wamewatia kabari wamiliki wa daladala na kuongeza ugumu kila kukicha. Kosa la dereva pia na mmiliki anahukumiwa. Kama huu ni uwajibikaji mbona hatuoni ukifanya kazi sehemu nyingine! Mbunge anakamatwa anakula rushwa mbona hatuoni chama chake na wakuu wake wakiadhibiwa papo kwa hapo kama makosa ya watu wa daladala? Mbunge wa CCM amekamatwa na rushwa anao wakuu wake, mwenyekiti wa kamati yake, spika wa bunge, mwenyekiti wa chama chake mbona na wao hawaadhibiwi?

Wafanyabiashara wakubwa na wakutoka nje wanapendelewa zaidi kwa kupewa mazingira mazuri ya kufanya biashara na watendaji na mamlaka husika wanakandamiza biashara ndogo na za wazawa kwa kuwekewa mazingira magumu ya kufanya biashara. Mgeni hata kama anaharibu mamlaka zitampa kila haina ya sapoti kama TRL ili asishindwe lakini wazawa wakikosea hata kama bahati mbaya ikibidi sheria zitabadilishwa ili waadhibiwe wakome na wasithubutu tena. Wawekezaji wa nje wanasaidiwa kupata mpaka mikopo ya kukuza mitaji na uwekezaji lakini hakuna hata anayetaka kujua daladala wanapata wapi mitaji ya kuanzisha na kuendesha biashara.

Biashara ya waziri au kigogo hao SUMATRA wala hawakamati na ndio maana waziri anamalori 2 anapiga USD 20,000 kwa mwezi. Lakini hakina sisi tunaishia kulipa mikopo na break even mara nyingi hatufikii tukitumaini labda kesho mazingira yanaweza kuwa bora zaidi. Kila waziri anapokuja anakuja jipya na wastani wa muda wa kuja waiziri mpya ni chini ya miaka mitatu anakuja mtu mpya ambaye atataka kuanzisha jipya na kusahau maisha yanaendelea na watangulizi wake kuna kazi walifanya, wamekuwa wakifanya hivyo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.

Nchi hii ni ya kwetu sote kwa pamoja tuwajibike kujenga nchi, mifumo ya kikoloni kuonea sekta binafsi, wafanyabiashara ndogo ndogo na wazawa haina nafasi kabisa kwa dunia ya leo. Mh. Waziri kama umeamua kusafisha fanya utafiti kutosha na kuondoa kero zote SUMATRA wanakuhadaa na operesheni zao mbuzi na wanawalipa waandishi wa habari warushe kazi zao hewani uwaone kuwa wanafanya kazi, mifumo iliyopo inatuumiza tumefanya kazi ya kuwasifirsha watanzania kwa muda mrefu, tunaendelea kufanya hiyo kazi na ndio biashara yetu. Mazingira ya sasa hayaridhishi na sio watu wa daladala ndio waliosababisha, Watunga sera na mamlaka husika zinaowajibu wa kutuwekea mazingira mazuri ya kufanya biashara na sisi tukue na uwekezaji wetu japo ni mdogo uwe wamaana.

SUMATRA tumesikia wamefukuzana kuhusiana na leseni feki lakini wanakamata magari na kuwatuhumu wamiliki kuwa wao ndio watoa leseni wakati wafanyakazi wa SUMATRA ndio wanaotengeza leseni (TLA na TLB) sasa mmiliki anatoa wapi vitabu vya SUMATRA na wametengeneza mazingira ya vishoka ili wawanufaishe wao wenyewe.

Tunaimani kubwa na Mh. Mwakyembe hatuna shaka kwamba anatambua wamiliki wa daladala, madereva na makondakta ni wadau muhimu na wamefanya kazi kubwa kwa muda mrefu, wanastahili kuthaminiwa mchango wao na inefficiency ya SUMATRA na mamlaka nyingine wabebe wao wenyewe sio watu wa daladala. Meli inazama inaangamiza mamia ya watanzania SUMATRA wapo tu wanaendelea na shughuli zao, ingekatisha route daladala mngeona watu wanavyosimamia vidole gumba.
 
Kuna jambo moja waTZ tufanye kuepukana na vitu fake(TLA,Road licence fake) nalo ni kuacha tabia ya kutuma watu wakushughulikie kwa niaba yako! Unamtuma mtu kwenda Sumatra anacolude na mfanyakazi wanatengeneza kitu fake unaletewa gari,,Road licence imeisha badala ya kwenda TRA unamwachia mtu/kishoka docs akate kwa niaba yako,anazama mtaani anatengeneza anaweka kibindoni hela. Mwisho wa siku mwenye gari ndo utasumbuka(umeshikwa na ngozi)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom