Mh. Msigwa awekwa kitimoto leo jimboni kwake, yeye alonga ukweli

kamandamakini

Senior Member
Feb 17, 2012
165
137

Mh. msigwa akiwa katika mdahalo leo.​











akizungumza







akisikiliza swali, nakisha kujibu kwa ufasaa

MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amewatakawananchi wa jimbo hilo na watanzania kuendelea kupiga vita vitendo vya ufisadikwa vitendo ikiwa na pamoja na wao wananchi kufanya kazi badala yakuwanyoshea vidole mafisadi wakati na wao wananchi ni mafisadi wa muda.

Alisema kuwa kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni kutokana na hasa wabunge wa chadema kuchukizwa na vitendo vya ufisadi kwa mawaziri waliotemwa katika wizara zao na Rais na kuwa hata baraza jipya lililoteuliwa sasa iwapo litaendeleza vitendo vya ufisadi kama lile lililovunjwa basi watashughulikiwa kama wenzao .

Mbunge Msigwa alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa chuo chamaendeleo ya jamii Ruaha katika mdahalo wa pamoja kati yake na wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini mdahalo ulioandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Iringa na kuratibiwa na asasi ya ICISO .

Akiongea kwa umahiri alisema, jitihada mbali mbali zinazofanywa na wabunge katika kuchukizwa na vitendo vya ufisadi ila bado kwa upande wa wananchi pia wamekuwa wakishiriki kufanya ufisadi ambao ni mkubwa zaidi na wenye kulifanyaTaifa kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo kutoka na tabia ya baadhi yawananchi kuendekeza uvuvi wa kushinda vijiweni bila kazi.

Hivyo alisema kuwa wakati mawaziri na viongozi wanatuhumiwa kwa ufisadi nakuondolewa katika nafasi zao bado wananchi nao wanapaswa kujitathimini kwakufanya kazi kwa bidii badala ya kushinda vijiweni.

Aidha mbunge Msigwa alisema kuwa kamwe hatakuwa tayari kuwatetea wananchiwa jimbo lake ambao wanakiuka sheria za mipango miji kwa kujenga nyumba bilakufuata taratibu za mipango miji.

Kwani alisema kuwa kuendelea kuwatetea wananchi wanaojenga nyumba kiholelakatika maeneo ya hifadhi ya barabara ni sawa na kujipalia makaa ya moto kwa madai kuwa leo ni serikali ya CCM ndio ipo madarakani ila ipo siku serikali ya Chadema itakuwepo madearakani hivyo kama wavunja sheria wataendelea kutetewa nchi haitatawalika pia kwa Chadema.

Mbunge Msigwa aiendeleza falsafa yake kuwa yeye si mbunge wa kugawa samaki kwa wapigakura bali ni mbunge wafundisha wapigakura wake kuvua samaki.

Hivyo lazima ataendelea kuwaongoza wapiga kura wake kufuata sheria na siokuwatetea hata pale wanapokiuka ama kuendelea kuwahonga fedha kama njia ya ushawishi badala ya kuwapa mbinu za kuzifuata.

Aidha aliasema kuwa iwapo utaona mbunge anaendesha jimbo kwa fedha zake za mfukoni basi ujue ni mwizi ama ni mfanyabiashara mkubwa hivyo alisema kuwa hapendi kuwadanganya wapiga kura hao kuwa ataboresha miundo mbinu wakatiserikali yenyewe imekwama kufanya hivyo
Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa mdahalo huo umeonyeshakufana zaidi na kuwa lengo la midahalo hiyo ni kuwakutanisha wapiga kura nawabunge wao ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa matakwa ya wapiga kura .

Hata hivyo alisema midahalo kama hiyo itaendelea katika jimbo la Isimani kwa kumweka kitimoto mbunge wa jimbo hilo Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa nchiofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge , jimbo la Kalenga linaloongozwa na waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa na jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof.Peter Msola na kuwaomba wabunge hao kushiriki midahalo hiyo.

pia aliwaasa vijana kwa jumla kwamba kila kijana anapaswa kuwa na vision, goal, and plans katika maisha yake na kamwa asiwepo mtu anae kubali kutumiwa na mtu yoyote, maana sisi sote ni watu wa muhimu. aliwaasa washiriki wa mdahalo huo kuwa kukubali kutumiwa nikukanbidhi utu wako kwenye rehema na huruma za mtu mwingine, ambako huko nikufilisika kifikra kupita kiasi, alisema mheshimiwa Msigwa.
 
nilitamani sana kuhudhuria mdahalo huo; muda wake ulikuwa mbaya saa 4 asubuhi wakati wa kazi. ushauri: next time tufanye midahalo week ends mpate washiriki wengi zaidi.
 
very attractive speech,

huyu ni kiongozi...ukweli daima!! ''kosoa serikali lakini eleza wajibu wa wananchi''

Impressive na nadra sana kupata utamu huu kwa viongozi wa chadema,

mna hekima humo
 
Haitachukua Muda midahalo hiyo kukwama kufanyika kwenye majibo ya wabunge wa Chama Tawala kama itaendeshwa kwa uhuru, subirini tu muone.
 
CDM wanakuja na style ya ulaya ambayo ccm wakiiga tu majimbo yote wanayapoteza. Mdahalo na ccm ni sawa na paka na panya.ccm wanapendana na pilau tshirt , chachandu na Matusi
 
Back
Top Bottom