Mh Mpendazoe afiwa na mkewe Rosemary

Mola aipumzishe roho ya marehemu mahali pema na awape moyo wa uvumilivu wafiwa wote, Amen
 
pole san mheshimiwa mpendazoe Mungu akufariji katika kipindi hiki kigumu
 
Ndugu,

Tumepoke taarifa za msiba kuwa mke wa Mheshimiwa Mbunge wa Kisapu CCM,Mpendazoe amefiwa na mkewe Rosemary,aliyekuwa ameenda India kwa matibabu jana jioni.

tunakupa pole na mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

Ninampa pole Mheshimiwa kwa kuondokewa na mtu wake wa karibu sana katika maisha yake.

Tukielekea katika matibabu. Mimi huwa najiuliza hivi uwezo wa kufikiri umefikia kikomo?. Kwa nini wananchi wengi wenye uwezo wa fedha hukimbilia nje ya nchi kwa matibabu?. Kitu ambacho hatujajifunza ni kuwa kama hatutaboresha huduma zetu za afya yaani ku-invest heavily on healthcare basi tutarajie kuwa hata kukimbilia nje ya nchi kwa matibabu mara nyingi huwa hakutusaidii hasa linpokuja suala la kuokoa maisha. Sababu ninazo

1. Magonjwa mengi hatari kama cancer et al huwa na chance kubwa ya kudhibitiwa pale yanapokuwa katika stage za mwanzo. Kuna stage yakifikia huwa yanaitwa "terminal" yaani mtu asubiri wakati wake tu. Sisi Tanzania tunaanza kumuuguza mtu muda mrefu kwa kutumia hospitali zetu ambazo ni stone age, vifaa hakuna, madaktari hawalipwi vizuri, kila kitu ni dili. Ikifikia mahali madaktari wakiona majaribio yao yaani "try and error" treating mechanism kwa kuwa hawajui wanatibu nini hasa hayaja zaa matunda ndipo wanapendeleza mtu aende nje ya nchi kwa uchunguzi zaidi.

2. Tukifika nje ya nchi wanagundua kuwa magonjwa yetu yameshakuwa ni "terminal" hawawezi ku-reverse kitu wanaishia kutu-admit na kucharge hela wasituambie kuwa huyu mtu haponi. Mwisho tunawalipa vijisenti vyetu vingine vya misaada ya wananchi kisa tu ipo mikononi mwetu tuanaitumia kuona kama tutapona, ni upotezeji wa rasilimali. Kwa nini Serikali ISI_INVEST? kwenye healthcare? ili watu wawe na ufahamu wa afya zao kabla hazijafikia terminal?

3. Kwa kuwa huu mradi wa kuwapeleka watu nje ya nchi unaratibiwa na wizara ya afya, ni lazima kuna ufisadi. Yaani watu wanatengeneza hela either kwa kupata commission kwenye haya mahospitali ya nje wanaporecommend watu wakatibiwe au kwa kuutumia kujustify matumizi ya pesa za walipa kodi. Serikali ijitoe katika hili na kuwekeza hapa nyumbani.


Umefikia wakati sasa watanzania tuangalie kila sehemu ya maisha yetu kabla ya kuwachagua viongozi. Kwa kuwa wao wanatibiwa nje ya nchi hawana mawazo ya kuwekeza kwenye afya nyumbani tunaoumia ni sisi tusiokuwa na uwezo hata wa kukodi taxi kupelekea mama zetu hospitali wakajifungue.
 
Kila nafsi itaonja mauti, na wote ni marehemu watarajiwa.marejeo ni kwake aliyetuumba...poleni sana wafiwa...
 
Pole sana Mhe. kwa kufiwa na mwenzi wako, lakini yote ni mapenzi ya bwana. Raha ya milele umpe ee bwana, na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani " Amina"
 
POLENI SANA WAFIWA!
mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
tuko pamoja nawe mh mbunge
 
Back
Top Bottom