Mh Mpendazoe afiwa na mkewe Rosemary

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
268
163
Ndugu,

Tumepokea taarifa za msiba kuwa mke wa Mheshimiwa Mbunge wa Kishapu CCM,Mpendazoe amefiwa na mkewe Rosemary,aliyekuwa ameenda India kwa matibabu jana jioni.

Tunakupa pole na Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
 
Dah pole sana Muheshimiwa naona mikasa imekuandama sana upo katika kipindi kigumu. Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu poleni wafiwa poleni wapiga kura wake.
R.I.P Rosemary
 
Ndugu,

Tumepoke taarifa za msiba kuwa mke wa Mheshimiwa Mbunge wa Kisapu CCM,Mpendazoe amefiwa na mkewe Rosemary,aliyekuwa ameenda India kwa matibabu jana jioni.

tunakupa pole na mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

Pole sana Mheshimiwa Mpendazoe kwa kufiwa na mke wako. Sisi tunamwomba Mungu aiweke roho ya marehemu kati ya watakatifu waku. Ukisoma Injili kama ilivyo andikwa na Yohana Mtakatifu sura ya 14: 1-6 Bwana Yesu alisema "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini mungu, niaminini na mimi. Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi; kama sivyo, ningeliwaaambia; maana nakwenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tene niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako;nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba , ila kwa njia ya Mimi".
 
Ni vigumu kusema kitu kwa mtu aliye na majonzi kama haya. Najua ulimpenda mkeo sana, lakini Mungu amempenda zaidi. Pole hatuachi kukupa kwa vile ndio ubinadamu, lakini Mungu anajua namna atakavyokutia nguvu kipindi hiki, mtumaini yeye naye atakusikiliza. Ni haki yake Mungu kuvuna shambani mwake, Jina la Bwana Libarikiwe. Kuna kujifunza nasie hapa kwamba ipo siku, nayo yaja haraka, ttasafiri kwenda huko Rosemary alikoenda. Tumwombe Mungu atuwezeshe kujiandaa kikamilifu.

Leka
 
Pole Mheshimiwa kwa msiba huu mzito,
Mungu akutie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu
Pia aipumzishe roho ya marehemu pema peponi.
 
Ndugu,

Tumepoke taarifa za msiba kuwa mke wa Mheshimiwa Mbunge wa Kisapu CCM,Mpendazoe amefiwa na mkewe Rosemary,aliyekuwa ameenda India kwa matibabu jana jioni.

tunakupa pole na mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

Pole sana Mhe.
 
Mungu aliyetuumba, hutufahamu vema kuliko hata tunavyojifahamu sisi wenyewe, ndio maana ninamuomba huyo (Mungu) akupe faraja yake halisi ambayo itakushikilia katika kipindi hiki chote cha majonzi
 
Pole sana Mheshimiwa Mpendazoe kwa kufiwa na mke wako. Sisi tunamwomba Mungu aiweke roho ya marehemu kati ya watakatifu waku. Ukisoma Injili kama ilivyo andikwa na Yohana Mtakatifu sura ya 14: 1-6 Bwana Yesu alisema "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini mungu, niaminini na mimi. Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi; kama sivyo, ningeliwaaambia; maana nakwenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tene niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako;nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba , ila kwa njia ya Mimi".

nimefarijika na hili neno

poleni sana familia ya marehemu mungu awape faraja yake katika kipindi hiki kigumu
 
Ndugu,

Tumepokea taarifa za msiba kuwa mke wa Mheshimiwa Mbunge wa Kishapu CCM, Mpendazoe amefiwa na mkewe Rosemary, aliyekuwa ameenda India kwa matibabu jana jioni.

tunakupa pole na Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

Mpendwa Mh. Mpendazoe, Pole sana.
Hiyo ndiyo njia yetu sisi wote wanadamu na kiumbe chochote chenye uhai,
Pole sana pamoja na watoto wako na ndugu wote ambao msiba huu unawagusa.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom