Mh Mnyika tuchongee hii barabara

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,876
2,747
Hii barabara inaanzia river side kuelekea jeshini. Leo wakati narudi nyumbani nikitembea kwenye barabara hii, nawaona waenda kwa miguu, pikipiki na magari yanavyopita kwa shida wakati ni jirani kabisa na mandela road. Mbunge wetu nasikia unajenga daraja sijui wapi huko ila ukumbuke na hii njia muhimu sana. Pia kuna kale kakipande kanakochepukia muslim sec. Mh ulituomba kura hadharani na faraghani. Tuchongee hii barabara tafadhali. Ina watumiaji wengi sana! Hivyo usiwaache kutaabika. Ni hayo tu kwa sasa
 
kama itakuwa ya lami tunaomba isijeumuka kama imetiwa hamira kama barabara nyingi zilizojengwa na mchina
 
Hivi ina maana mdau wa jf ni mi pekee ninayeishi kupitia hii njia? Thats ridiculous! Mheshimiwa bado nakungoja useme chochote.
 
dah! Mkuu hujapata wasaa wa kupita hapa? Wadau mwelezeni kuwa anahitajika huku. Au kuna substitute ya jf soon after elections.
 
Hizo ni kazi za tanroads au manispaa ya kinondoni sawa mkuu .......Mbunge kazi yake ni kutuwakilisha bungeni.....kwani kipindi cha kampeni si mlichongewa subirini kipindi kingine cha kampeni....hiyo ndio tz, sana sana Mumtume akashinikize tanroads au manispaa wawajibike.....!
 
Hizo ni kazi za tanroads au manispaa ya kinondoni sawa mkuu .......Mbunge kazi yake ni kutuwakilisha bungeni.....kwani kipindi cha kampeni si mlichongewa subirini kipindi kingine cha kampeni....hiyo ndio tz, sana sana Mumtume akashinikize tanroads au manispaa wawajibike.....!
kha! Atatuwakilishaje bila kuchukua maoni jimboni? Mbona kajenga daraja huko kiyungule. Kawasaidia tanroad? Kwanza hizo fider roads ni za halmashauri/manispaa. Cha msingi pia aongee vizuri na manispaa husika kuhusu hii road
 
siamini mwananchi anataka mbunge amchongee barabara wakati kuna halmashauri, au tanroads (kutegemeana na barabara), kuna juhudi za wananchi wenyewe na donor and then mbunge kwa kushirikiana na wananchi

play your part!!!
 
Mimi namuomba mheshimiwa mbunge wetu ashinikize mambo mawili ya dharura (1) Ratiba ya upatikanaji maji izingatiwe, kwani wakati wa kampeni na uchaguzi mahji yalikuwa yanatoka kila baada ya siku 2 au tatu, lakini kwa sasa ratiba haileweki, maeneo ya Kimara maji hayajatoka kwa ratiba tangu uchaguzi ukamilike. (2) Tanroad/Halmashauri wajenge haraka daraja la Msewe/UDSM ili kupunguza misongamano ya magari ya asubuhi na jioni. Nawasilisha
 
siamini mwananchi anataka mbunge amchongee barabara wakati kuna halmashauri, au tanroads (kutegemeana na barabara), kuna juhudi za wananchi wenyewe na donor and then mbunge kwa kushirikiana na wananchi

play your part!!!
nami siamini kama wabunge hutoa ahadi kama hizi wakati wa kampeni. Lakini ajabu ni ipi kuhitaji huduma ya kijamii toka kwa mbunge? Au mwenzetu lami hadi jikoni. Aliutaka ubunge, kaupata. Cha msingi akabiliane na hizi kero
 
Mpeni muda.....amekuwa mbunge kwa miezi 7 tu hawezi kuwa amemaliza ahadi zote kwa muda huo....ni veme ukawasi;iana nae direct na sio kupitia hapa katika kurahisisha utatuzi
 
mkuu camara, hii ndo maana ya jukwaa. Suala la kumtafuta in person ni ngumu na hakuna tija. Cha msingi akubali hicho kiporo then akiweke kwenye shajara
 
Mnyika anataka kurushiwa makombora ndio aje jukwaani kujitetea? Mbona wakati anausaka ubunge alijileta mwenyewe humu? Anataka mada za aina gani ndo achangie? Mh njoo jf utolee maelezo kwa mara nyingine kero za jimbo lako
 
Back
Top Bottom