Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Sober hana moral authority kuzungumzia jambo nyeti kama ili la mafao ya kujitoa kwa kutumia akili ya makamasi.Ni vema akatumia angalau 1/25 ya akili yake kama anayo akajaribu kufanya analysis ya Social security katika Tanzania yetu na mstakabali wake.Ulaya na Amerika social security ndiyo yenye mzizi maana watu wasio na ajira rasmi wanapewa ujira kwa wiki na kama fao la kujitoa litazuiwa bila alertnative solution kwa watu waliokuwa wana ajira na baadae wakakosa basi serikali na mifuko hiyo iandae kanuni za kuwalipa.
Muhimu ni kuwa Sheria mara nyingi utekelezaji wake uko kwenye KANUNI.Bunge alitungi kanuni bali kanuni uandaliwa na waziri mwenye dhamana kwa kushirikiana na ofisi ya mwanasheria wa serikali, ndiyo maana kanuni hii ya kuzuia KUJITOA ambayo SSRA inataka kuweka inapingwa na watu wenye akili TIMAMU. NI ujinga na wendawazimu kama kuna mtu ataunga mkono kanuni ya kuzuia kujitoa na kulipwa mafao yako.
 
Last edited by a moderator:
Everyone has a right to determine his/her destiny! Let pensionable staff determine what is best for them and not SSRA to determine for them.
 
Sober; My brother pole sana; it appears you are living in a bubble! na hili ndio tatizo la wasomi wetu wengi hapa Tanzania; stereo typing! watakusomea a litany of statistics, makabrasha mengi, theories kibao; kwa mfano eti uchumi wa Tanzania umekua consistently for the last 5 - 8 years; when you ask them to explain the discrepancy between that economic growth rate and the level of poverty among the populace; hata wao wanashangaa kama wewe unayeuliza swali!! waulize why now the double digit infalation, hapo wanasingizia world economic trends na sio inhouse poor economic management; majibu rahisi kwa maswali magumu!!
You go further na hapo ndio mtu unataka kupiga ndulu! pale mkuu wa kaya anapotamka kwamba eti anashangaa ni kwa nini Tanzania ina utajiri wa raslimali nyingi lakini wananchi wake ni maskini sana, lol God save our country!

Comrade hizo theories zako za taaluma ya mifuko ya jamii peleka zikusaidie kuandika thesis yako ya Phd; ili uwe a pure academician, completely out of touch with the realities of life in Tanzania, unachofanya ni kujaribu kudurufua hayo uliyaona au kusoma kuhusu mifuko ya jamii katika Welfare societies katika dunia ya Magharibi ambapo welfare payments zinawapa wananchi a bridge gap mechanism ya kuweza kuendesha maisha wakati wanasubiri maturity ya pensheni zao; hapa kwetu je; utakuwa umeshangaa!
In an Ideal scenario unachokisema ni sawa, lakini in the real world, Tanzania halisi hakifai. brother hebu take a fresh breath to reflect kuhusu:
1. Taarifa ya CAG kuhusu jinsi serikali inavyotumia pesa za mifuko hiyo; kiholela na haizirudishi!
2. Culture ya mizengwe, uchakachuaji, ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za umma ambayo watendaji wengi wa Kitanzania tuliyojijengea, 15 - 25 years down the road nani atakulipa mafao yako; wakumbuke wastaafu wa EAC na walimu wetu wanavyodhalilika todate.
3. Kwa kuzingatia point 2 above; Nani ana mkataba na mwenyezi mungu kwamba you will live to see that day at 55 or 60yrs ili ukadai mafao yako au ni kadhia na mateso tu unawaachia wanafamilia yako.
4. Kumbuka hizo pesa ni za mfanya kazi na nyongeza ya mwajiri, serikali ni custodian tu! kwa hiyo wafanyakazi have a right kutengeneza sheria ya mafao inayowafaa wao na sio kushurutishwa na serikali ambayo financial probity yake ni questionable!
5. Usisahau wafanya kazi hawana access na hizo pesa say kwa njia ya mikopo kabla ya kujitoa, na wala hawapati riba yoyote kutokana na investments zinazotokana na mifuko hiyo, so the earlier you withdraw your money so much the better ili unufaike na present value yake, usisahau mla ni mla leo mla kesho kala nini?! again wakumbuke wastaafu wa afrika mashariki!

6. Takwimu za Brela ni fake! ndio wale wale waliosajili makampuni yasiyokuwa na wenyewe wakaishia kutuibia pesa lukuki za EPA, Deep green na Kagoda etc etc; na wala sio kigezo cha kuwanyima wafanyakazi pesa zao eti hawajui kufanya biashara!
Entrepreneurial skills to some are inborn, to some are acquired and more aften than not to some such skills are horned out sheer life challenges; trial and error, wewe au serikali ni nani to usurp madaraka ya kumkatalia mtu huru asijaribu kufanya apendacho using their life time hard earned resources; afterall success or failure sio wajibu wako wewe au wa serikali ambayo inasponsor sheria hii scandalous!

Surely there is something fishy behind this initiative; there is a school of thought kwamba "mtu akijifanya anakupenda sana na kukujali huenda ni mchawi anataka akudhuru mbeleni!!" usilipuuze hili; kusema kwamba serikali yetu hii inajali sana wafanya kazi wake na kwa hiyo inataka wasiteseke sana huko uzeeni is simply foolhardy; again wakumbuke wastaafu wa afrika mashariki na walimu wetu maskini; God shore up their spirits! Then linganisha na culture ya ufahari wa watawala wetu na kushindwa kwake kuchukua hatua madhubuti kudhibiti rushwa, ufisadi, utawala wa kibabe unaoshika kasi kwa sasa nk. nk.

Mkuu nimeku-lecture sana samahani lakini waache hawa wafanyakazi walahoi wachukue chao mapema; hao wabunge unaojaribu kuwaunga mkono na kumkandia JJ mnyika wao wanachukua gratuity kila baada ya miaka 5 probably come 2015 wataibuka na kati ya 50 - 80 milioni; si unajua kwa wabunge gharama za maisha ziko juu sana lakini sio kwa walala hoi wengine; dont get duped and refrain from beig used!! teh teh teh; stay blessed. (Hoja Hai; mtazamo mfu)
 
unachokisema ni sawa lakini bado unatoa ushauri ule ule ambao MNYIKA anataka kuufanyia kazi kwamba angalau mtu aweze kuaccess acount yake pale anapoacha/anapoachishwa kazi. una mawazo mazuri lakini nahisi wewe ndo umepotoka kwa kukosoa kile unachokipendekeza wewe mwenyewe.

Mkuu nahisi unakoelekea siko. Enzi ya mwalimu si enzi hizi, kijana wa leo ana mtazamo mpana sana hutomlinganisha na enzi zile. Mfano mdogo to wale wazee wa Afrika mashariki angalia wanavyoteseka, wataka nasi tupate suluba ile ile???
Nionavyo mimi mnataka nchi iendelee kuwa maskini zaidi sio kujenga bali kubomoa.

Mfano mwingine, Mimi nasomesha wanangu shule za kulipia. Nafukuzwa kazi, watoto wangu hawataendelea kusoma hali pesa yangu ipo yasubiri nizeeke ili imsaidie nani? Serikali kukopesha haitaki, ajira hakuna. Watu wanapenda wakiacha kazi wajiajiri na waajiri wasiokuwa na ajira uli kuinua uchumi wa nchi hii. Unapomnyika si ndo unaongeza wimbi la umaskini, vitendo viovu n.k.
 
Msiwe waoga wa mambo, mtu kuchukua hela yake kabla ya miaka 55 sio ndo atateseka uzeen, vipo vitu ving vya kuinvest mapema na mtu akala faida ya investment yake uzeen. Nyie mnataka achukue hela yake uzeen ili aile kidogo kidogo mpaka iishe, na ikishaisha afanyaje? Au akishazeeka ndo afanye biashara? Namuunga mkono Mh Mnyika na wengine wenye mawazo hayo, watu wawe na option either kuchukua mapema au mpaka uzeen, sio wote watashindwa kuzitumia kufanya mambo mazur, swala kubwa ni watu kuelimishwa mising ya biashara na vitega uchum vingne. Tukifanya mambo mazur kabla ya uzee bas uzeen itakuwa saf sana, kuliko kusubir uzee ndo uanze kukimbizana. TUSIOGOPE, NA TUSIIGE KILA KITU KUTOKA NCHI NYINGINE.
 
Mtoa mada umepotoka ama una maslahi binafsi na sheria hii mpya na kandamizi kwa wanyonge.
 
Nadhani kuna watu wanachanganya mambo. Katika hili suala la Mifuko ya jamii, sherai hiyo mnayopigia s=debe itakandamiza sana watu wa sekta ya madini. Na ndio maana tumekuwawatu wa kwanza kabisa kuipoinga kwa nguvu zetu zote... na kadri siku zinavyoenda itadhihirika ya kwamba, sheia hii kwa ujumla wake haitekelezeki katika sekta hii, na pengine katika sekta binafsi kwa ujumla wake.

Kwa ufupi tu, migodi yote ya TZ ina average life span ya miaka kama 20 hivi, ( GGM, Bulyamhulu na Resolute ) imeshakula nusu au zaidi ya hiyo miaka....ukitilia maanani ya kwamba wafanyakazi wengi katika migodi hiyo ni vijana, na ikatokea migodi ikafungwa sasa..( kitu ambacho ni cha kawaida tu kutokea) au bei kushuka katika soko, na migodi ikalazimika kupunguza wafanyakazi, unataka kutwambia watu wasubiri mpaka miaka 55 ndio wachukue pesa zao? tuwe wakweli jamani ni nani anataka kusema kwa Tz ya leo, ni rahisi kwa mtu kupoteza kazi leo na kupata kesho? Hapo nimejaribu kuonyesha mfano kwa makampuni ambayo tayari yanazalisha , kwa maana ya Mining...

Nikija kwenye mfano mwingine, ambao nina uzoefu nao zaidi. Makampuni ya madini yanayofanya utafiti ( exploration) ambayo inaweza kuchukua miaka 10 mpaka 15, inapofikia kipindi cha uzalishaji (Mining) karibu nusu ya wafanyakazi au zaidi ambao wengi wao ni vijana itawalazimu kuacha kazi ( eg. Geologists, Technicians etc etc..) kuwapisha wataalam wengine kama Mining engineers, Miners etc etc... kuchukua nafasi. Inapofikamhali hiyo... ambayo wengine wetu tuko karibuni kuifikia, mnataka kutwambia tusubiri mika say 15 ijayo ndio tupate pesa zetu? Ikitokea katika kipindi chote hicho hatutapata ajira tutaishi vipi? Nadhani hili suala linahitaji mjadala wa kina na wenye busara nyingi.

Kuna mchangiaji mmoja amesema kuhusu kubaki na 90% au 95% ya mshahara baada ya kukatwa NSSF?PPF uwe wakweli jamani.....hivi huyo bwana hajui dudu linaloitwa PAYE? ambalo linaweza kukufanya ukaanguka kwa mshangao wakati unalinganisha Gross na Net Salary? Nawasilisha....
 
Hivi Mnyika alikuwa wapi wakati mswada unapitishwa bungeni?
swali zuri, lakini labda ni kati ya wale wachache waliosema, siooooooooo, speaker akasema waliosema ndio wameshinda, na muswada ukapita. So kuwepo kwa mnyika hakumaanishi aliunga mkono huu upuuzi
 
Uzoefu wa hii mifuko mingi ni kuwa mwanachama anapochukua mafao ya kujitoa, mwanachama huyuhuyu atarudi kujiunga tena ndani ya miezi 18. Kwa hiyo suala la kusema unafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili na una miaka 30 hivyo utatakiwa usubiri miaka 28 ili upate mafao yako, si sahihi kwa asilimia 100%.

Ila nimefurahi kupitia uzi huu nimeweza kujifunza mambo mengi sana, na kwa kweli inasikitisha kuona elimu ya umuhimu wa kuwa na akiba ya uzeeni inapokosekana kwenye mitaala yetu ya mashuleni.

Naomba niwaulize kitu kimoja tu. Je mmewahi kujiuliza ni kwanini watumishi wa hii mifuko, wao wenyewe wanawaomba waajiri wao wawawekee supplementary schemes kwa ajili ya kupata pension ya ziada? Sababu ni rahisi, wao wanaona jinsi pensheni zinavyowapa wazee nafuu kubwa ya kipato, na wengi wao wanaextra account mfuko wa UTT kwa ajili ya mafao ya uzeeni.


Mh. Mnyika, najua wewe umekomaa kisiasa, chukulia uzi huu kama changamoto za kuboresha utendaji wako na hasa linapokuja suala tata lenye kuhitaji upembuzi wa wataalam.

Niliona kama mtanzania mwenye ufahamu japo kidogo wa haya mambo, nijaribu kushare na wenzangu, ili pengine niwape kidogo cha ziada kufikiri badala ya kushabikia kwa nguvu kila kitu(hasa pesa ya leoleo). Ila kama michango mingi ilivyo, watu wameamua kujinyonga wenyewe kwa kamba zao... Sina la ziada bali ni kuongeza urefu wa hiyo kamba kwa wale watakaotaka kujinyonga.

Kwa wale walionielewa nawasihi sana, tukumbuke fainali uzeeni, hisani za watoto wetu kwa miaka tunayoelekea zitazidi kupungua sababu na wao gharama zitawaelemea... tutajuta na kusaga meno huku nguvu zikiwa zimeisha, nakubaki na msemo wa NINGEJUA!

Namalizia kwa kusema HUTAKI UNAACHA!.... FAINALI UZEENI.
 
Yani serikali hainitafutii kazi, Kazi nimetafuta mwenyewe,
Kwanini inajali maisha yangu baada ya 55?
Je nisingepata kazi hiyo miaka 55 ningefika? Je na matumizi ya hiyo hela ya uzeeni watanipeleka tuition?

Watulipe kwanza mafao ndo tusaini mkataba mpya.
 
Kwa mleta hoja na watetezi wa hoja hii naomba msaada

Shilingi yetu inayumba na kuporomoka thamani kwa kasi ya ajabu, rejea mfumko wa bei.

1. Kanuni zinasemaje (how does this being accounted and evalueted at the final stage) incase has been taken into consideration-fomula please.

2. Nje ya huu mjadala kwa wafanyakazi kupata mafao baada ya 55 ya umri wao ili wasiteseke(huruma ya serikali kwa wafanyakazi) Je? Kunahuruma yoyote kwa kundi la pili wanapozeeka, yaani wakulima wasiteseke uzeen?

3. Kuna huruma yoyote ya kimkakati kuhakikisha watoto yatima na wasiojiweza wanawezeshwa?

Naiona huruma ya serikali kwa walionacho na si kwa maskini. Nahapa ndipo ninapopata mashaka makubwa ya kuibiwa haki yangu.
 
Sober

Aisee!! Najua umeandika kwa kuwa umeamua kuandika. Lakini hali halisi ilivyo najua waijua ila sasa utafanyaje wakati unataka kui-defend hoja yako.

Yanini Malumbano?

SITAKI NA NIMEACHA. FAINALI UJANANI, UZEE NI KIFO.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mtoa mada. kuna tofauti kubwa sana kati ya uhalisia wa mambo na on paper predictions and assumptions. Sheria hii ni kandamizi haifai hata kidogo. Itawaumiza sana watu wanaofanya kazi migodini na wale wengi wa private sector wenye mikataba. Mgodini huwezi kufanya kazi zaidi ya miaka 15 kutokana na nature ya kazi. kama uliajiriwa ukiwa na 24,tunategemea uta retire at 35 to 40. Kwa hiyo ina maana kama hutapata kazi nyingine itabidi usubiri mpaka 55...????. pia kama ulikuwa na kazi ya mkataba let say miaka 5,halafu the same situation inatokea unashindwa kupata kazi sehemu nyingine....... Hapo unafamilia unasomesha watoto huna salary tena..? huoni kama uo ni uonevu...?. Haya una skills za kutosha za ujasiriamali,na pengine pesa iliyoiwekeza ingetosha kabisa ku invest on something e.g kilimo. ukaajiri na watu wengineambapo mwisho wa siku mkaongeza wanachama kwenye mifuko...! Mi namuunga mkono mheshimiwa Mnyika naamini yeye sio mvivu wa kufukiri kama wewe ulietoa hii mada. Kumbuka unaishi leo sio kesho. maisha ya leo ni muhimu zaidi kuliko hayo ya kesho uliyoAHIDIWA. Kwa Tanzania ahadi sio deni...! Nchi za wenzetu wanao implement sheria kama hizi wametengeneza mazingira mazuri ya kuwawezesha waajiriwa wao kufikia huo umri...
 
Nchi kama Kenya na zingine nyingi unapojitoa unapata nusu ya mafao yako yote mpaka kipindi hicho na nusu nyingine mpaka ufikishe 55, bora hii. lakini kutoka bila bila noma!.
 
Mkuu, naona umepotoka kwa asilimia zote!

1) Inabidi ujue jambo hapa, kumwambia Mh. Mnyika akakae na wataalamu wamwelimishe juu hilo analotaka kulifanyia kama private motion, sio sahihi.. kwanza ujue kwamba Serikali ya CCM kwa muda mrefu sasa, haijawahi kuwa na fikra nzuri dhidi ya wananchi wa tanzania, wanachofanya wao na serikali yao ni kuweka viPENYO vya jinsi ya kumwibia mtanzania.

2) Hao walengwa wenyewe wa hao mashirika ya pensheni, hawataki hata kusikia hiyo sheria, na kama ingekuwa na manufaa kwao wasingetaka kugoma, wao wenyewe kama walenga hawakushirikishwa, na jambo lolote lenye heri ni lazima mhusika mkuu ashirikishwe, sio watu wachache kuamua kwa maslahi ya wengi. Ukiona watu wachahce wanakaa kwa kuamua maslahi ya wengi bila kuwashirikisha kuna jambo baya dhidi ya walengwa. Serikali lazima ingekaa na wahusika, sio kupitisha sheria kimya kimya kama mwizi, huo ni wizi wa mchana.

3) Namuunga mh. Mnyika , awatete hao wafanyakazi wanaotaka kuibia na serikali yao, sheria ya zamani ibaki vile vile, tatizo hii mifuko imekuwa ikitumika kisiasa, sasa wanajua ndio mahali pa kupatia hela wakati wa kampeni na upuuzi mwingine, wanajaribu kupitisha sheria ambazo zitalinda hizo pesa... kama ni hivyo na wafanyakazi nao wapunguzwe kazi kwenye hayo mashirika sababu hata wateja watakuwa wamepungua (wale wanaofuatilia madai yao)

4) My take, wataalamu nafikiri wengeza kuja na wazo na kuweka kipengele kinachomfanya mhusika kuweka maagano ya lini ataanza kuchukua mafao yake, mara baada ya kuacha, kufukuzwa, au kustaafu kazi! ajifunge mwenyewe na sio kulazimishwa, ili iwe ni kama "fixed account" !
 
Mkuu mmeshaambiwa kuwa hamna sheria ya mfuko wowote inayoongelea hilo fao la withdrawal. SSRA walichofanya ni kama reglator ni kulipiga stop tu!

Mnyika kakosea kuingilia kitu asichokifahamu kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa. Asione wengine waliokaa kimya kuwa ni wajinga.

Mawazo yako ni ya kizamani sana. Unafikiri kuwa Watanzania wa sasa bado ni wavivu wa kusoma.
Angalia hapa, Hii ni nukuu ya Section 44 ya PPF Act No. 25 ya mwaka 2001. Inasema hivi:-

"Withdraw Benefits"
44.-
(1) Where a member ceases to be benefits employed in circumstances in which he is not
eligible for any pension, gratuity or any other benefit under the provisions of this Act, he shall
be refunded the amount of his own contributions and that of his employer to the Fund.


(2) Where a member has been employed for a period of not less than five years and the
cessation of such employment is not due to dismissal for misconduct the amount of his own
contribution and that of his employer together with a simple interest at that rate to be determined
by the Board of Trustees shall be paid to him.


Mnyika hakukosea hata kidogo.

Pole sana Rejao, maana naona unajaribu kwa nguvu zako zote kutetea udhalimu.
 
....Mimi nafkiri, badala ya kutaka kifungu cha mafao ya kujitoa kirudishwe na hivyo kujihakikishia kuona vurugu za wazee mitaani kama wale wa jumuiya ya afrika mashariki siku za usoni. Ni bora tukaacha sheria ibaki kama ilivyo(kwa maana ya kuzuia mafao ya kujitoa) ILA iongeze kifungu kitakachomtaka mwajiri awe na scheme ya kuchangia wafanyakazi ambayo ni over and above the basic pension scheme, ambayo mtu ataweza kuacess fedha zake pale atakapoacha kazi....
Niishie hapo, naomba tujadili bila matusi.

Nina uhakika utakuwa umetumwa ww si bure, na ufie mbali na upuuzi wako! Mfano mzuri umeutoa ww mwenyewe na bado unatetea upuuzi huo, je Wazee wa Africa Mashariki wanahangaikia fao la kujitoa au pension? na je wanachokiadai kitawasaidia kuwa na maisha bora kwenye umri wao kwa sasa?

Ndio maana nakuambia wewe ni mpuuzi usiyestahili kupuuzwa! Pamoja na point ulizoelezwa huko juu na kujifanya mbishi jaribu kufuatilia yafuatayo pia;

1. Fahamu kwamba sifa ya kupata pension si kufikisha miaka 55 pekee bali kuna sharti ya idadi ya michango ie NSSF ni lazima angalau uchangie michango 180 (miaka 15), je unafahamu kwamba ni chini ya asilimia 20 tu ya watanzania wanaweza kudumu kwenye ajira kwa muda wote huo (hasa sekta ya madini) kwa sababu mbali mbali km vile kampuni kufirisika (maana mdororo wa uchumi ukitokea sekta ya madini ndio ya kwanza kuathirika), madini yenyewe kuisha na mgodi kufungwa, kufukuzwa kazi (kuna sababu nyingi sana huku za kufukuzwa kazi mfano kuangusha gari kama ajali), kupata magonjwa sugu (silicosis, magonjwa ya mapafu kwa watu wa underground, ukimwi nk) na kuwa declared unfit, na mengineyo mengi tu. Na kumbuka ukifukuzwa kazi wana mtandao wao wa kuwasiliana ili usipate kazi kwingine kokote ndani ya tanzania, hili serikali na watu wenye akiri finyu kama wewe hamjawahi kuliona mnafikiri naendekeza mambo ya serikali ya Kuiba mabilioni ya fedha na unahamishwa kituo tu.


2. Kwa kutumia mfano wako huo huo; naweza nikafanya kazi miaka 8 (nikiwa na umri wa miaka 35) nikaachishwa kazi baada ya kukosa nguvu ya kazi kwa sababu ya maradhi, nitalazimika kusubiri kwa muda wa miaka 15 ijayo ndo niweze kupewa michango yangu (maana sina sifa ya kulipwa pension kwa sababu sijafikisha miaka 15), kama nitajikongoja nifike huo umri (maana wengi watakufa kabla ya kufikia umri huo) nitaenda nikapewe vimchango vyangu ambvyo kwa wakati huo vitakuwa havina msaada mkubwa kwangu kwa wakati huo maana mfumuko wa bei utakuwa umetafuna samani yake kwa asilimia kubwa sana.(Mfano ni mzee wa East Africa aliyesafiri kutoka Mwanza hadi Dar kwa gharama ya 35,000/= nauli na alipofika akalipwa penseni ya 1,500)

Naomba niishie hapo maana nadzidi kupata hasira na watu kama ww ambao mnafikiri dunia ya leo bado ni ya wajinga mnaoweza kuwaibia pesa zao mnavyotaka; mmeiba twiga, mmeiba matrilioni ya shilingi na kuweka kwenye mabenki ya nje, mmeiba EPA na mengine mengi bado mnakutaka hata vya mifukoni mwetu...............huo upuuzi hatuutaki Mnyika bravo
 
Mkuu wangu,
Wabunge wetu wengi ni watu wa kuonewa huruma, kwa sababu ukiachilia wachache ambao wana pensheni, wengi wao wanadhani pensheni haiwahusu kwa wao ni waheshmiwa. Mwisho miaka mitano wanavuta cheque wanapeleka kwenye elections(Kosa kubwa!!).

Wako wabunge wengi ambao ukiwaona leo hii walivyopigika na walikuwepo bungeni mpaka 2005 au 2010, hautoamini!. Yote hii ni kukosa uelewa wa nini maana halisi ya pensheni.

Wabunge nao wanapaswa kuwa ndiyo mfano kwa wananchi wanaowaongoza kwa kuwa wa kwanza kujiandikisha kwenye mifuko ya pensheni. Hasa wabunge vijana aina ya Mh. mnyika. Lakini kwa wabunge ambao walishastaafu(miaka 55 au 60), hawatalalizimika tena kujiunga na mifuko hii kwa mujibu wa sheria.

Sober,

Mbona na wewe unavuruga sasa. Ukiangalia post zako zote mimi ndiye nimekupa LIKES nyingi kuliko mtu yeyote humu. NImekupa LIKES kwa sababu unaongea kitaalamu kabisa na uko sahihi kwa kila hoja kiasi kwamba nimelazimika kuamini kwamba wewe ni mmoja wa staff wa PPF maana ungekuwa NSSF usingeongelea ile 5%.

Unachoharibu hapa kuhusu wabunge kuna jambo nilitegemea mtaalamu wewe ulieleze kitalamu kama mengine. Ubunge ni uwakilishi na wala si kazi au ajira. NImeona kuna mahala umembana jamaa aliyekusakama kutumia neno KUPOTOKA. Nakubaliana na wewe uko sahihi lakini pia kuna neno linatakiwa pia kupewa tafsiri sahihi ya kiswahili, nalo ni MSHAHARA WA MBUNGE.

Anachopewa mbunge si mshahara. Wanaobisha basi wanieleze tofauti ya Diwani na Mbunge nini nini? Mimi naona tofauti ni idadi ya wanaowakilishwa lakini concept ni ileile uwakilishi.

Hivyo, tusaidiane kutafuta neno zuri ili anachopewa mbunge kisiitwe mshahara, maana ukikiita kuwa ni mshahara ndipo unakaribisha misconception kwamba kama kuna mshahara wa mbunge basi kuna pension ya mbunge.

Hiki ulichosema kuwa mbunge akimaliza miaka mitano ile hela anapewa anapeleka kwenye kampeni ya uchaguzi hakiitwi PENSION, bali kinaitwa GRATUITY.

Ni hilo tu, otherwise niatendelea kukupa LIKES maana sijaona wa kukuzidi hoja katika unayoeleza. Uko sahihi kabisa endelea kutuelimisha.
 
Back
Top Bottom