Mu-Israeli
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 2,454
- 975
Nikusahihishe tu, kuchangia kwa miezi 180 ndio kigezo cha kupata pensheni na siyo kwamba ukishachangia miezi 180 unaweza kuchukua pensheni yako. Miaka ya pensheni inabaki ilele ile 55 voluntary na 60 compulsury!
Pili, unategemea hela za withdrawal ndio ukaanzishie mradi?? Huu ni kama wendawazimu
Hapo juu angalia sana.
Mimi naona huo 'wendawazimu' ni kwa serikali kushindwa kukusanya kodi kwa ajili ya matumizi yake, na badala yake kukimbilia kuchulua pesa kwenye mifuko ya pension.
Mimi nimeshachukua 'withdrawal' yangu mwaka jana, na sasa nimeanzisha mradi unaoniletea mapato ya kutosha tu. Nimejiajiri. Niambie kama kufanikiwa kujiajiri ni 'wendawazimu', au serikali kuogopa kukusanya kodi kwenye makampuni ya madini ndio 'wendawazimu' ???
Humu JF kuna watu wa ajabu sana.