Mh:mnyika fanya hili kabla ya kuwasilisha ushahidi bungeni

MELODY

Member
Apr 6, 2012
23
11
Mh: Kwanza nakufagilia kwa msimamo na uwezo wako. Myika nakushauri kabla ya kuwasilisha ushahidi wa uhusika wa Nchemba kwenye kashfa ya EPA,kwanza mwambie spika aruhusu ushahidi uliowasilishwa na LEMA kuhusu vurugu za Arusha usomwe na ujadiliwe kwanza bungeni.
 
naunga mkono hoja, maana tujadiliane mh spika amepokea ushahidi wa tuhuma nyingi, je mbona hazijadiliwi? Au alikuwa anaomba kuoneshana umwamba? Na kuna miongozo mingi mbona haitolewi majibu, ebu 2kumbushane ushahidi mbalimbali ambao spika amepelekewa na zipi kazifanyia kazi?
 
Wanaweza wakajitetea kuwa Lema sio Mbunge so haina haja ya kuusoma ushahidi wake.
 
Mi kila nikifikiria ushahidi alioambiwa alete Lema kwa jazba na mama Makinda, nakosa hata kujua wapi bunge letu linakwenda. Kama kweli Lema angekuwa amekosea basi ingekuwa I fimbo ya kumchapia. Na Kama ushahidi huo umewekwa kapuni basi kuna uwezekano mkubwa sana aliyokuwa akiyasema Lema yana ukweli
 
Apeleke ushahidi wa plain paper tu, maana huwa hausomwi.

Hizo plain paper iwe rim nzima, zipewe namba moja hadi 500, karatasi ya mwisho ieleze kuwa ushahidi ufuatao una connection na ule wa lema plus ushahidi wa watu na kumtaka spika aamue ataanza kuusoma wa lema ili ufuate wa watu au uanze wa watu amalizie na wa Lema!!
 
Kuna ule ushaidi wa Zitto alitakiwa autoe kwenye Bunge lililopita kusiana na alipolituhumu baraza la mawaziri hivi aliutoaga na ukatolewa majibu?
 
Mh: Kwanza nakufagilia kwa msimamo na uwezo wako. Myika nakushauri kabla ya kuwasilisha ushahidi wa uhusika wa Nchemba kwenye kashfa ya EPA,kwanza mwambie spika aruhusu ushahidi uliowasilishwa na LEMA kuhusu vurugu za Arusha usomwe na ujadiliwe kwanza bungeni.

dah,,,,,siasa hizi
jamaniiiiii
 
Shutuma zimetolewa bungeni,,ushahidi autoe hapo hapo bungeni,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom