Mh Mkapa; Kauli yako inahitaji maelezo ya ziada, otherwise.....!

Kweli yeye (KOKOTO) haoni madhambi yake. Hivi jF haina wachawi wakaroga hawa watu?
 
Makosa ambayo mengine JK anayabeba yametokana na Mkapa kwa asilimia kubwa sana. Kama CCM ikifa au kupoteza mamlaka basi Mkapa indirect anahusika. Yeye ndiye muasisi wa maovu mengi na akatumia ukali na kutokukubali kushaurika kwa manufaa yake binafsi. I hate Mkaa aka Mzee wa Kokoto.

Mkuu hapa nitapingana na wewe, kwani IPTL mkataba ule ulisainiwa na nani? Richmond? je waliofanya madudu haya wamechukuliwa hatua gani? unakumbuka ZAKIA MEGHJI na sakata la bank kuu? alichukuliwa hatua gani.... hawa wote hakuna mwenye nafuu ni wezi wote. Usisahau JK ni raisi wa nchi kwanini asichukue hatua? kama hawezi yupo kwaajiri ya nani?
 
Me bado nina maswali kibao kichwani mwangu, ilikuwaje mwalimu amuite mtu safi??
 
Siku ya ijumaa nilikuwa namuuliza baba yangu je yeye anamuenzi vipi nyerere, alinipa jibu lahisi sana lenye mashiko, jibu lilikuwa hivi ''hakuna mtanzania yeyote anayemuenzi nyerere zaidi wamebaki wanafiki wanaomdhihaki kwa kudai wanamuenzi'' nilivyokuja kumuona mkapa analopoka hizo pumba ilinibidi nifurahi mwenyewe kwa sababu nilikumbuka kile alichokuwa ananiambia baba yangu
 
Kwanza nyani haoni kundule, pili kama kawaida yao wezi wa magamba hufikiria wanaiba gizani kwa sababu wamevaa sun glass wanafikiri hawaonekani na Nzee Nkapa ni mmoja wao!!
Siku watakapopelekwa Kisutu ndio watakapo jitambua
 
Binafsi nimeshangazwa na kauli yake,halafu akaenda mbali kwa kusema sisi(WATANZANIA) eti wavivu wa kufikiri,so yeye m2 wa msumbiji ni mwepec wa kuwaza,hop ana2ng'ong'a tu

Ni kweli sisi ni wagumu kufikiri hajasema uongo! mlaumu kwa mengine.
 
Ni kweli sisi ni wagumu kufikiri hajasema uongo! mlaumu kwa mengine.

Caroline natumai umzima kabisa, Watanzania si wavivu wa kufikiri ndio maana tulipinga ununuzi wa rada, tukapinga Net Group kupewa management positions pale TANESCO, tukapinga uuzwaji wa nyumba za Serikali, tukapinga malipo kwa Dowans, na pia tunapinga mikataba fisadi ya uchimbaji wa madini yetu. Sidhani tungeweza kuyapinga yote haya kama tungekuwa ni wavivu wa kufikiri na kuchanganua mambo mbali mbali labda yeye ndiye mvivu wa kufikiri.
 
Hivi huyu Mkapa anadhani watanzania wooote ni wagojwa wa kusahau? Huyu si ndiyo tuliambiwa tumuache apumzike kwa amani kama mfu, inakuwaje leo anaanza kuongea wakati shida na matatizo ya Taifa ameyachangia yeye?

1.Tukaambiwa tule nyasi ndege yake inunuliwe, Nyerere aliyafanya hoyo?
2. Oooh rada itasaidia kuona mpaka mende kila uvungu, kumbe wanakula dili na Chenge.
3. Akatwambia tusiwabughudhi wawekezaji wa migodi kwani kila penye madini ni mali yao!
4. Netgroup Solution akaingiza ofisini kwa mtutu wa bunduki, kumbe kampuni ni yake, je, Nyerere alifanya hayo.
5. Katuibia akaenda kujenga ghorofa kuubwa kwa Madiba, hapo anamuenzi nani kama siyo Mobutu.

Kakaa Ikulu miaka 10 lakini mali alizonazo zinazidi za Nyerere aliyekaa pale karibu robo karne! Mkapa kaa upumzike kwa amani tutakugeuzia kibao, tuache sisi walala hoi tuikomboe nchi yetu. Uliua Zanzibar na Bulyankulu unatafuta damu nyingine ya kunywa?
 
nimeona kwenye taarifa ya habari jana na leo na pia nimesoma kwenye magazeti kuwa Mh Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekemea wale wote waliojilimbikizia mali wakati wa Kongamano kumbumkuka Mwl nyerere.

naomba ninukuu alichosema ...... Sisi sote ni mashahidi wa baba wa taifa wakati wa uahi wake aliishi maisha ya kawaida, hakuwa na uchu wa madaraka, hakujilimbilikizia mali, na alipenda usawa kwa kila mtu....... ni wakati muafaka kwa watanzania kuendelea kuishi maisha ya kawaida kama alivyoishi Nyerere ambapo alihakikisha anaweka misingi imara ya kuwatetea wanyonge na kuwaunganisha watu wote kwa kuona rushwa ni adui ya haki".

baada ya kunukuu alichosema Mh. Mkapa, naomba niseme kuwa nasikitika kuona kuwa anatambua misingi mizuri aliyokuwa anasimamia baba wa taifa lakini yeye kwa makusudi kabisa akaivunja,. narudia tena kwa makusudi kabisa akaivunja. nasema haya nikiongozwa na matukio yafuatayo:

  1. Mh Mkapa ulianzisha kampuni ya ANABEN ukiwa ikulu na ukanunua kiwanda cha Kiwira kwa bei ya kutupa (nasikia ulikipata kwa bei chee).. sasa hapo kweli ulikuwa umesahau misingi ya mwalimu.. Je kama mwalimu aliishi maisha ya kawaida pasipo kuiba rasilimali za nchi wewe ulishindwa nini.
  2. wakati wa utawala wa mzee Mkapa tulishuhudia nyumba za serikali zikiuzwa kwa bei ya kutupwa. na waliouziwa hizo nyumba wameziuza kwa bei ya kutupa na wengine inawezekana hawakukamilisha malipo. Kama Mwl alijenga hizo nyumba, kwa nini wewe usimamie uporaji wa namna hii. Je mbona watumishi sasa wanahaha kupata mahali pa kuishi. Mfano mzuri na Mh. Nahodha alivyotekekeza mamilioni ya watanzania kuishi hotelini kisa hajapewa nyumba na serikali
  3. Wakati wa utawala wa mkapa tulishuhudia uuzwaji wa makampuni yaliyoanzishwa na Mwl tena kwa bei ya kutupa.. hebu jamani tukumbuke NBC.
  4. wakati wa utawala wako mh. Mkapa tumeshudia, makampuni makubwa yakichukua ardhi kwa ajili ya uchimbaji dhahabu, huku wachimbaji wadogo wadodo wakiachwa hawana kitu. tena wengine nasikia (narudia kusema nasikia kwa sababu sina uhakika 100%) walifukiwa mashimoni. Je hii ndo msingi aliokuachia Mwl Nyereree
  5. Mh Mkapa wakati wa utalawala wako vitendo vya rushwa vilishamiri kwelikweli, nakuimbuka ndo kipindi hiki hata rushwa ndani ya polisi ilishamiri kisawasawa- huku mheshimiwa ukimfumbia macho IGP wa kipindi hicho.
  6. Mh. Mkapa, wakati wa utawala wako ndo kashifa nzito zilitokea zikiwemo EPA, Deep Green, Buhemba etc.
  7. Mh. Mkapa wakati wa kipindi chako ndo tumeshuhudia kampuni ya TIPER ikivunjiliwa mbali kwa hila. sasa matokeo yake tunayaona kwa upande wa mafuta ya petroli, dizeli etc (hapa nakumbuka mchango wa Mbunge wa Muleba alivyolalamika wakati anachangia hotuba ya bajeti ya Mh. Ngeleja).
  8. wakati wa utawala wako, ndo tulishuhudia ukwasi wa kutupa kwa viongozi wetu wakiwemo mawaziiri, makatibu wakuu, wakurugenzi wakipata ukwasi wa ajabu ambao wakati mwingine hauelezekii (ref. kina Balali, Lowasa, etc) . Mbona hukusimama kidete kuwaambia waishi maisha ya kawaida kama ya mwl Nyerere
  9. wakati wa utaawala wako kipato kati ya matajiri na masikiini kilizidi .. mkuuu ina maana haukuyaona haya?
  10. Wakati wa kipindi chako, tulishuhudia wanafunzi vyuoni wakigoma.
ninayomengi ya kueleza lakini, ni vema anaposimama jukwaani na kukemea wanaojilimbikizia mali, ni vema atueleze kwa nini alifanya yaliyobainishwa katika point kumi hapo juu. Asipofanya hivyo mimi nitaona ni kokoto na anasema tu mdomoni na hayatoki moyoni mwake!

Laiti Nyerere angefufuka na kumsikia Mkapa kanena haya maneno na yale mapete yake ya gold aliyoyavaa angemtandika na kale kafimbo kake kwenye mikono mpaka pete za gold zilizomwaga damu ya watanzania zimdondoke then angemuuliza 'kijana uligeuza hekalu kuwa pagari la wanyan'ganyi'?
 
Another controversial statement from Mkapa

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Saturday, 15 October 2011 21:39


By Florence Mugarula
The Citizen Reporter
Dar es Salaam.

Retired leaders yesterday advised Tanzanians to start taking action instead of merely complaining if they wanted to have a better future.

The leaders were contributing to the theme ‘The Tanzania we want’ during a discussion held in Dar es Salaam to commemorate the 12th anniversary of Mwalimu Julius Nyerere’s death and 50 years of independence.

One of the participants, retired President Benjamin Mkapa, emphasized the need for all Tanzanians, especially the youth, to start thinking critically and take action instead of complaining on everything.

He noted that most seminars and workshops held currently to deliberate on the country’s future were characterised by apportioning of blame, anger and complaints, a trend that does not help to get rid of the problems they purport to address.

He warned that if Tanzanians fail to think strategically and remain a complaining lot, there was a danger of foreigners taking advantage of the situation by pushing through unfavourable policies, like the Economic Partnership Agreements (EPA) between East African countries and the European Union.

According Mkapa, the EPA arrangement is meant to benefit the Europeans, and not East African countries.

“The terms of agreement include establishment of industrial partnerships and tax free exportation of goods, among others… However, East Africa cannot compete with European countries in those areas, so we need to think critically to oppose this,” said Mr Mkapa.





Kijana yeyote aliyeipigia kura CCM kwenye uchaguzi wowote ametukanwa na Mkapa hapo kwenye red.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
naungana na BAK, wananchi si wavivu wa kufikiri labda tatizo letu kubwa hatuna vitendo. Ingekuwa sehemu nyingine, nadhani wasikilizaji wa hotuba ya mkapa wangenyanyuka kwenye viti na kutoka nje.
 
Poleni watanzania wenzangu kwa matusi tuliyotukanwa na huyu DUMZI. Napenda kuwakumbusha kuwa wanaume wenye ile sifa ya uha**th, huwa ni wenye jaziba jaziba na husuda husuda. Hupenda sana recognition.
 
Mkapa is a lot of worse things.. Ufisadi... ikiwa moja wapo (thou not yet proven).... But katika Maraisi walopita (Mwalimu pembeni) the most intelligent na the most calculated akijua fika nini anafanya. Jamaa anajua hali ni mbaya ya CCM na siwezi shangaa kama anatafuta upenyo wa kuhemea so that hata Chama kipya kikishinda waone ni mwenzao. Juu ya Mkapa na habari zake yananishangaza mambo mawili:-
  1. Ni kiongozi ambae alikua anakwepa saana vyombo vya habari wakati wa Uraisi na hata baada tu ya kustaafu na hasa pale zilipo rise kashfa juu yake... Kitu gani kimemfanya saizi ghafla bin vuu yupo kwenye Siasa related activities katika sura ya Media... na kwa nini saizi yupo more confident kuongelea Utawala na madhaifu yake.... Very very iff.... (IMO)
  2. Wanahabari wetu wa hapa Tanzania... Kitendo cha kusema wanakutana na the guy face to face na badala ya kumuuliza yale maswali ambayo yana linger katika back of our brains and for long... Wana entertain upuuzi wa kuendelea kuchapisha habari ambazo ni kama anajikosha... Hivi kwamba hawa wanahabari wamenunuliwa na hawana guts ya kuuliza the right questions... AU kwamba anawasiliana tu na wale wana habari ambao wapo katika his back pocket??

Keshaona hawa waliopo wamechemsha kuliko yeye na hivyo amepata uhalali wa kuongea.
 
Hivi huyu Mkapa anadhani watanzania wooote ni wagojwa wa kusahau? Huyu si ndiyo tuliambiwa tumuache apumzike kwa amani kama mfu, inakuwaje leo anaanza kuongea wakati shida na matatizo ya Taifa ameyachangia yeye?

1.Tukaambiwa tule nyasi ndege yake inunuliwe, Nyerere aliyafanya hoyo?
2. Oooh rada itasaidia kuona mpaka mende kila uvungu, kumbe wanakula dili na Chenge.
3. Akatwambia tusiwabughudhi wawekezaji wa migodi kwani kila penye madini ni mali yao!
4. Netgroup Solution akaingiza ofisini kwa mtutu wa bunduki, kumbe kampuni ni yake, je, Nyerere alifanya hayo.
5. Katuibia akaenda kujenga ghorofa kuubwa kwa Madiba, hapo anamuenzi nani kama siyo Mobutu.

Kakaa Ikulu miaka 10 lakini mali alizonazo zinazidi za Nyerere aliyekaa pale karibu robo karne! Mkapa kaa upumzike kwa amani tutakugeuzia kibao, tuache sisi walala hoi tuikomboe nchi yetu. Uliua Zanzibar na Bulyankulu unatafuta damu nyingine ya kunywa?



hapo kwenye red hao ni WADEKEZWAJI, tax holiday, kiburi kwa raia, dharau etc etc
 
Yaani wana CCM wote ni wanafiki,sasa yeye aliongea hivyo ili ajisafishe aonekane ni msafi,bila kujua kwamba uchafu wake ni ukurutu ambao ulikomaa na kuwa kama gamba la mamba,yeye ndio muanzilishi wa UKWAPUZI wa rasilimali zetu,CCM woote ni wezi.
 
Back
Top Bottom